KERO Kero ya Uchafu Zanzibar, mkoa wa Mjini Magharibi, Wilaya ya Mjini Jang'ombe - Shehia ya Kidongo Chekundu

KERO Kero ya Uchafu Zanzibar, mkoa wa Mjini Magharibi, Wilaya ya Mjini Jang'ombe - Shehia ya Kidongo Chekundu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kwa shehia ya Jang'ombe, Kidongo Chekundu na Baraza la Manispaa mjini ishughulikie takataka zinazozagaa na kutelekezwa katika jalala la Jang'ombe, Kidongo Chekundu.

Hii hali imekuwepo muda mrefu bila uchafu kuja kuchukuliwa, ukizingatia jalala lipo kwenye makaazi ya watu na karibu na skuli.

Kwa sasa kuna mvua zinanyesha, hali ni mbaya. Tunaomba Manispaa kushirikiana na Ofisi ya Sheha waziondoe kabla hazijaleta madhara makubwa kwa jamii kama maradhi ya kipindupindu na homa ya matumbo.

Ahsante


PXL_20260328_060711562.jpg
PXL_20260328_060603385.jpg
PXL_20260328_060558390.jpg
 
Majina ya MIKOA yenu yamekaa "kimdebwedo" sana

By the way ka nchi mtu akipiga filimbi raia wote mnasikia inakuwaje mnashindwa kukafanyia usafi wa maramoja chap tu?
 
Zanzibar yote ni chafuuuu, huna haja ya kutaja mkoa. Yani kale kakisiwa watu wake hawana kinyaa kabisa. Kwa mnaoendaga mahotelini mnaweza msilijue hili. Ila huko mitaani kumeozaa na sio issue ya serikali, watu wake ni wachafuuu
 
Utaratibu wa kupeleka uchagu,takataka unawezekana hasa awamu hii.
 
Back
Top Bottom