Kwa shehia ya Jang'ombe, Kidongo Chekundu na Baraza la Manispaa mjini ishughulikie takataka zinazozagaa na kutelekezwa katika jalala la Jang'ombe, Kidongo Chekundu.
Hii hali imekuwepo muda mrefu bila uchafu kuja kuchukuliwa, ukizingatia jalala lipo kwenye makaazi ya watu na karibu na skuli.
Kwa sasa kuna mvua zinanyesha, hali ni mbaya. Tunaomba Manispaa kushirikiana na Ofisi ya Sheha waziondoe kabla hazijaleta madhara makubwa kwa jamii kama maradhi ya kipindupindu na homa ya matumbo.
Zanzibar yote ni chafuuuu, huna haja ya kutaja mkoa. Yani kale kakisiwa watu wake hawana kinyaa kabisa. Kwa mnaoendaga mahotelini mnaweza msilijue hili. Ila huko mitaani kumeozaa na sio issue ya serikali, watu wake ni wachafuuu