KERO Responded Kero ya upatikanaji wa maji Kazamoyo, Kirumba, Ilemela – Mwanza

KERO Responded Kero ya upatikanaji wa maji Kazamoyo, Kirumba, Ilemela – Mwanza

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wakazi wa Kazamoyo, Kirumba, Ilemela – Mwanza, tumekuwa tukikabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji kwa muda mrefu, wakati mwingine hupita wiki moja hadi mbili bila kupata maji, na mara nyingi hulazimika kumpigia simu mwenyekiti wa eneo ili awasiliane na mamlaka husika.

Kinachoshangaza ni kwamba tupo karibu na tanki la maji, takribani Mita 600 tu, lakini bado tunapata huduma kwa shida. Zaidi ya hapo, maji yanapotoka mara nyingi hutolewa usiku wa manane badala ya nyakati za mchana ambapo mahitaji huwa makubwa.

Hali hii inawaathiri zaidi wananchi ambao hawana uwezo wa kuhifadhi maji kwenye matanki. Tunaomba mamlaka husika zifanyie kazi changamoto hii ili wananchi wapate huduma ya maji kwa wakati unaostahili.

Pia soma ~ Kukosekana maji Kazamoyo, Kirumba na Ilemela, MWAUWASA yasema "Pole Mdau kwa changamoto iliyojitokeza eneo lako"
 
Habari.

Sisi wakazi wa Kazamoyo, Kirumba, Ilemela – Mwanza, tumekuwa tukikabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji kwa muda mrefu. Wakati mwingine hupita wiki moja hadi mbili bila kupata maji, na ili huduma ipatikane hulazimika kumpigia simu mwenyekiti wa eneo ambaye naye huwasiliana na wahusika.

Cha kushangaza ni kwamba tupo karibu sana na tanki la maji, takribani mita 600 tu, lakini bado tunapata shida ya huduma hiyo. Pia, maji yanapotoka mara nyingi hutolewa usiku sana wa manane badala ya asubuhi au mchana ambapo mahitaji huwa makubwa.

Hali hii ni changamoto hata kwa wale wenye matanki ya kuhifadhia maji, sembuse wananchi ambao hawana uwezo wa kuhifadhi maji. Tunaomba mamlaka husika zisaidie kutatua tatizo hili ili wananchi wapate huduma ya maji kwa wakati unaofaa.

Asante.
 
Back
Top Bottom