Habari.
Sisi wakazi wa Kazamoyo, Kirumba, Ilemela – Mwanza, tumekuwa tukikabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji kwa muda mrefu. Wakati mwingine hupita wiki moja hadi mbili bila kupata maji, na ili huduma ipatikane hulazimika kumpigia simu mwenyekiti wa eneo ambaye naye huwasiliana na wahusika.
Cha kushangaza ni kwamba tupo karibu sana na tanki la maji, takribani mita 600 tu, lakini bado tunapata shida ya huduma hiyo. Pia, maji yanapotoka mara nyingi hutolewa usiku sana wa manane badala ya asubuhi au mchana ambapo mahitaji huwa makubwa.
Hali hii ni changamoto hata kwa wale wenye matanki ya kuhifadhia maji, sembuse wananchi ambao hawana uwezo wa kuhifadhi maji. Tunaomba mamlaka husika zisaidie kutatua tatizo hili ili wananchi wapate huduma ya maji kwa wakati unaofaa.
Asante.