Kero za madereva wengi hapa Dar es Salaam

Kero za madereva wengi hapa Dar es Salaam

Mukulu wa Bakulu

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2014
Posts
4,051
Reaction score
12,954
Kwa watu ambao tumewahi kuendesha gari nchi zaidi ya moja, ukija kuendesha hapa nyumbani hasa Dar es Salaam unaweza kutamani kupiga watu makofi.

Madereva wengi wa Dar hawana rush hour, sa 2 asubuhi ama sa 1 asubuhi wakati watu wana haraka ya kufika kazini unakuta mtu anaendesha gari kama vile amelazimishwa kutoka nyumbani kwake, yaani kama vile hapendi ama hataki, unajiuliza huyu ameingia barabarani kufanya nini?

Kutokujua matumizi ya barabara, unakuta dereva yuko kwenye right lane, ule ni upande wa kutembea kama huwezi weka gari kwenye left lane, lakini ajabu unakuta mtu kang'ang'ania kwenye right lane huku ana mwendo wa kobe, unajiuliza huyu alipita kweli driving school.

Kuingiza learners barabarani wakati wa rush hour, hua sielewi hawa wenye vyuo vya udereva kuamua kuingiza wanafunzi wao barabarani wakati wa rush hours, unakuta sa 2 ama 1 asubuhi wakati unawahi kibaruani eti kuna kigari cha driving school kuna mtu anafundishwa, kwa nini usimfundishe wakati wa mchana ambapo hakuna rush hours?

Madereva wenzangu, kama huna haraka, toka nyumbani sa 4 ama sa 5 usiingie barabarani kusumbua watu na kuwapotezea muda kushikilia barabara wakati wenzako wana haraka.

Nashukuru sana.
 
Kuna dereva anajua atatakiwa kupinda kulia, unamkuta yupo kushoto anaanza kuhangaika kuhama.
Dereva anakuzuia kuingia na hivyo kusababisha msongamano upande mwingine.
Dereva anaziba makutano ya barabara huku upande wake ukiwa umejaa.
 
Huyu wa kulia anaenda kushoto ndio mataahira kabisa.

Kuna mwingine anaonyesha indicator wakati ameshafika anapoenda.
 
Dar Tanzania yetu sehemu kubwa hii hakuna barabara std bali kuna sehemu ya kunyooshea magari au kupita magari
 
Wapo wale ambao kupisha wenzao ni mtihani ili hali na yeye kuna mahali ataomba apishwe........
 
Hakuna madereva TZ, kuna watu wenye poor driving skills. Alafu ni wajuaji.
 
Hapo bado wale wanaohama lane anatoka kulia kwenda kushoto au kushoto kwenda kulia hangalii vizuri kioo anahama tu huku spidi yake ndogo kuliko ya gari linalokuja huko anapohamia
 
Kwa watu ambao tumewahi kuendesha gari nchi zaidi ya moja, ukija kuendesha hapa nyumbani hasa Dar es Salaam unaweza kutamani kupiga watu makofi.

Madereva wengi wa Dar hawana rush hour, sa 2 asubuhi ama sa 1 asubuhi wakati watu wana haraka ya kufika kazini unakuta mtu anaendesha gari kama vile amelazimishwa kutoka nyumbani kwake, yaani kama vile hapendi ama hataki, unajiuliza huyu ameingia barabarani kufanya nini?

Kutokujua matumizi ya barabara, unakuta dereva yuko kwenye right lane, ule ni upande wa kutembea kama huwezi weka gari kwenye left lane, lakini ajabu unakuta mtu kang'ang'ania kwenye right lane huku ana mwendo wa kobe, unajiuliza huyu alipita kweli driving school.

Kuingiza learners barabarani wakati wa rush hour, hua sielewi hawa wenye vyuo vya udereva kuamua kuingiza wanafunzi wao barabarani wakati wa rush hours, unakuta sa 2 ama 1 asubuhi wakati unawahi kibaruani eti kuna kigari cha driving school kuna mtu anafundishwa, kwa nini usimfundishe wakati wa mchana ambapo hakuna rush hours?

Madereva wenzangu, kama huna haraka, toka nyumbani sa 4 ama sa 5 usiingie barabarani kusumbua watu na kuwapotezea muda kushikilia barabara wakati wenzako wana haraka.

Nashukuru sana.
Unaweza kuwa uko sahihi lakini hujaangazia ubora miundo mbinu yetu.

Hizi haraka ndio zinasababisha ajali kila kukicha, Mfano. Juzi maeneo ya Bucha, Kimara, taa za barabarani zilikuwa haziwaki, na hivyo ikawa kila mtu anawahi kupita! ghafla akaja jamaa na lori akiwa na haraka kama usemavyo, kilichotokea ni ajali mbaya na watu kupoteza maisha.

Pili, kwanini katikati ya mji wenye miundo mbinu mibovu ya barabara kama hii ya Jiji la Dar, ukimbie kwa speed ya 120?? na wakati ukijua watembea kwa mguu wapo kila mahali, na mbaya zaidi hawajatengewa vivuko vinavyowaepusha kugongwa na magari kama cha Kimara mwisho na Manzese!

Tatu, Kwanini kwenye maeneo ya Taa kunapotokea kukatika kwa umeme, kunakosekana njia mbadala kuwawezesha watumiaji wa vyombo vya usafiri kubaki salama (mfano halisi ni Kimara Bucha) na kila kukicha watu wanagongwa!

Nimalize kwa kusema, kama unaharaka sana usemavyo wewe (Rush hours) kwanin usiamke mapema kabla ya msongamano wa magari kuanza? unapoona mtu anatembea kwa avarage speed, tambua huyo anathamini maisha yake na maisha ya wengine kama watembea kwa mguu, boda boda na hata bajaji!

Punguzeni mwendo kasi barabarani ,ajali zinatuteketeza watanzania. Miundo mbinu yetu ya barabara ni duni kulinganisha na ya huko ulipotolea mfano (Nchi za nje)
 
Back
Top Bottom