Kero za Muungano, waandishi wa habari wamelala!

Kero za Muungano, waandishi wa habari wamelala!

Tigershark

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2018
Posts
7,051
Reaction score
12,566
Habari wanajamvi?

Kuna hili suala la Kero za Muungano zilizogonga mwamba kutatuliwa Kwa awamu nyingi zilizopita!Lakini awamu hii ilipoingia tulitangaziwa kero hizo zilizosumbua sana zimetatuliwa chini ya SSH ndani ya muda mfupi!

Ajabu ni kwamba waandishi wa habari wakabeba taarifa kama walivuopokea na kuileta Kwa wananchi!Hawakuhoji kero hizo zilikuwa zipi na zimetatuliwa vipi na Nini kilishindikana awamu zilizopita na ikawezekana Kwa muda mfupi awamu ya 6!!

Mpaka sasa walioko jikoni ndio wanazijua hizo kero zilizotatuliwa, wananchi hatuzijui ni zipi!

Binafsi kero yangu Bado ipo kuhusu huu Muungano, ndio maana nawauliza waandishi waliolala, hawaoni ni jukumu lao kufuatilia na kutuhabarisha kero hizo ni zipi?

Isije ikawa kampa, kampa tena!
 
Mtoa mada nadhani siyo mfuatilaji wa some articles hapa JF hasa kupitia kurasa tofauti na hii ya Jukwaa la siasa.
 
Wengine unatuonea bure!. Umewahi kukutana na bandiko hili?
Kasome baadhi ya kero zilizo tatuliwa.
Pasco
Sijui ilikuwaje sikuusoma huu uzi wako! Au niliusoma, lakini NILIUSAHAU! Linakuja jambo lile lile, we Mkuu, ni kama NABII FULANI! Una MAONO!
Tukisubiri UFE ndipo tukupe sifa zako, tutakuwa HATUKUTENDEI HAKI!
 
Wengine unatuonea bure! Umewahi kukutana na bandiko hhili


Kasome baadhi ya kero zilizo tatuliwa.
Pasco
Mkuu naomba utusaidie Wana JF kama unazijua kero alizoagizwa Dr Philip Mpango akazitatue na utupe namna alivyozitatua kama tulivyotangaziwa!
 
Wengine unatuonea bure! Umewahi kukutana na bandiko hhili


Kasome baadhi ya kero zilizo tatuliwa.
Pasco
huyu mama ana kauli tofauti alipokuwa vc president na alipokuja kuwa president. Alipokuwa makamu wa rais alipokutana na wanawake wenzie aliwasisitiza wawe na heshima kwa waume zao bila kujali mafanikio yao kwani hata yeye anamnyenyekea mme wake lakini alipoapishwa kuwa rais alisema wanawake ndio zaidi kwani kazi ya wanaume ni kutia mbegu tumboni . Hana tofauti na wanasiasa wengine wanaobadilisha kauli kutokana na mazingira.
 
Waandishi wa habari hawamsaidiii Rais na serikali yake.

Ukiangalia vichwa vya habari vya magazeti karibia yote yamejaa sifa tu kwa karibia kila jambo.

Kitu ambacho kwa hali ya kawaida hakina afya sana kwa ustawi wa Taifa letu.
 
Tanzania wandishi wa habari hakuna, imejaa makanjanja.
Mfano majuzi Gavana wa BOT alikuwa anahojiwa pale Clouds Media, sikusikia akiulizwa usahihi wa kiwango cha deni letu ni Trillion 70 kama alivyonukuliwa spika au Trillion 82 kama wasemavyo wengine humu JF?
 
Hizi kero zilizotatuliwa majuzi hazijawahi kuwekwa hadharan acha uongo.
We ndo mgonjwa wa akili kweli kweli, nimeandika wapi kuwa kuna kero iliwahi kutatuliwa na himo humu jf..?


👉🏾 Skuli siyo lazima ufaulu hata kuwa na uelewa wa unachosoma nao ni ufaulu.
 
Nipe link!

Tafuta mwenyewe kupitia jukwaa la siasa, nowdays mmekuwa watu wa kutafuniwa kila kitu 🙁!.

That why unakuta mnaanzisha mada moja watu sita, sababu hamna muda wa story search!.
 
Mojawapo ni suala la ajira, 21% kwa wazanzibar na 79% kwa wabara japo hiyo 79% pia kuna wazanzibar waliopo bara wanaruhusiwa kugombania
Huu ni unyonyaji na uonevu dhahiri Kwa Watanganyika..
21% Kwa watu 1,3m na 79% Kwa watu 60m?!!!
Hakuna uwiano
 
Back
Top Bottom