ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 21,643
- 51,642
Bongo hii usiwe mtumishi serikalini yaani ni zaidi ya kero kila ikifika tarehe 22 Na 23 nyumbani huko simu zinaita wanataka uwagaie Na wenyewe posho ebu fikiria kwa mfano umekaa bench mwezi wote hujapata activity ya kufanya unatoka mshahara kalaki saba hakohako unadaiwa madeni karibia laki tatu. Je, kwa Salio linalobaki utaweza kuendesha maisha kwa mwezi mzima assume hujapata safari hata moja katikati ya mwezi na upo mkoa wa ugenini.
Sitaki kuutetea uchoyo ila jamani wazazi muwe mnaangaliwa ndo kwanza watoto wenu wanaanza maisha ya utumishi bado hawajajipanga kimaisha hawana miradi yoyote..unakuta Mzee ana Nyumba ana mashamba analima bado anataka atumiwe 50000 kila mwezi na mwanae na badala asubiri atumiwe mwenyewe yeye anafanya kama formula kabisa kwamba kila siku za mshahara anapiga simu kuomba.