Kero za tarehe ya Mshahara kufahamika na ndugu

Kero za tarehe ya Mshahara kufahamika na ndugu

Ila niwape tu pole wale ambao wanakuwa wa kwanza kwenye ukoo kupata hela unakuta inatakiwa ajenge mpaka kwao [emoji34][emoji34]

Kuna dogo napiga nae job take home ni kama 2.3 mpaka 2.8 milioni huyo dogo ana wadogo 13 na yeye ndio wa kwanza ana wadogo 3 wamefaulu form four walipata division 3 inatakiwa awasomeshe vyuo

Pia dingi wake anataka ajengewe nyumba bad enough baba yake ana wake 3

Hao wadogo zake 13 anachangia nao baba na mama bado wale anaochangia nao baba tu [emoji21]

Huwa ananipa simu nisome meseji za wanaukoo wake huwa nacheka saana unakuta mtu anajitambulisha yeye ni nan end of the day anaomba hela
Nimeelewa unavyojihisi. Ila kaka, kama ana ndugu 13 asipowasaidia yeye ndugu zake nani aende akawasaidie ?
Tusifundishane uchoyo, hela zipo tu, weka hakiba yako kias kdg, kingine asaidia wadogo zake.

Mtoto wa kwanza wazaz wanatumia nguvu nyingi kumsomesha kwa lengo la kwamba akifanikiwa atakuja kusaidia wazaz wake. Na ni wajib wetu kuwasaidia wadogo zetu bro. Sikatai tuna mitazamo tofuat na tumeumbwa tofaut kwaio mtu ni maamuzi yake kusaidia wadogo zake wasome waje wafanikiwe kama yeye au awa ache wadhalilike na kuishia njiani kimasomo.
 
Bongo hii usiwe mtumishi serikalini yaani ni zaidi ya kero kila ikifika tarehe 22 Na 23 nyumbani huko simu zinaita wanataka uwagaie Na wenyewe posho ebu fikiria kwa mfano umekaa bench mwezi wote hujapata activity ya kufanya unatoka mshahara kalaki saba hakohako unadaiwa madeni karibia laki tatu. Je, kwa Salio linalobaki utaweza kuendesha maisha kwa mwezi mzima assume hujapata safari hata moja katikati ya mwezi na upo mkoa wa ugenini.

Sitaki kuutetea uchoyo ila jamani wazazi muwe mnaangaliwa ndo kwanza watoto wenu wanaanza maisha ya utumishi bado hawajajipanga kimaisha hawana miradi yoyote..unakuta Mzee ana Nyumba ana mashamba analima bado anataka atumiwe 50000 kila mwezi na mwanae na badala asubiri atumiwe mwenyewe yeye anafanya kama formula kabisa kwamba kila siku za mshahara anapiga simu kuomba.
Kama ni mzazi mtumie tu hakuna namna
 
Pole kwa mitihani hiyo
Mimi nashukuru wazazi hawajawahi kuniomba hata senti yangu moja
Ila nalazimisha tu kuwapa kama Asante kwa kunizaa

Kuna wakati nilikosa kazi kwa mda na niko ugenini walikuwa wananitumia hela wao ingawa nilikuwa nakataa ila wanatuma tu

Wavumilieni wazazi wenu kama hawana kitu kwani ni mipango ya Mungu
Usimlalamikie mzazi hata siku moja bali Omba wakuombee sana na hutakosa kitu duniani

Ila ukiwa wa lawama hata kwa wazazi basi ni mtihani mkubwa
Jitume hata kibiashara kidogo after work ikuingizie cha ziada ili uwakumbuke zaidi
Amini hili ukiwatunza vizuri wazazi hutakosa kitu
Punguza matumizi yasio ya lazima pia
 
50k mbona hela ndogo Sana hiyo Mimi bro wangu anamtumia Mama laki mbili kila wiki na sisi wadogo zake bado tunatuma si haba then sio Kwamba Mama yetu ana shida , yupo vizuri tu well financially stable

Vijana tafuten Blessings kutoa ndo kupata
 
Mzazi unabidi kumpatia mahitaji yote ya msingi na Pesa kila wiki umtumie

Kama hautoi wewe ni bahili huwezi kufanikiwa hata siku moja.
 
Pole kwa mitihani hiyo
Mimi nashukuru wazazi hawajawahi kuniomba hata senti yangu moja
Ila nalazimisha tu kuwapa kama Asante kwa kunizaa

Kuna wakati nilikosa kazi kwa mda na niko ugenini walikuwa wananitumia hela wao ingawa nilikuwa nakataa ila wanatuma tu

Wavumilieni wazazi wenu kama hawana kitu kwani ni mipango ya Mungu
Usimlalamikie mzazi hata siku moja bali Omba wakuombee sana na hutakosa kitu duniani

Ila ukiwa wa lawama hata kwa wazazi basi ni mtihani mkubwa
Jitume hata kibiashara kidogo after work ikuingizie cha ziada ili uwakumbuke zaidi
Amini hili ukiwatunza vizuri wazazi hutakosa kitu
Punguza matumizi yasio ya lazima pia
Mkuu umeongea ukweli..
 
Shida ya watanzania kwa wingi ni Uvivu. Uvivu wa akili na mwili.

Nakumbuka kuna kipindi kigumu sana nilipitia, nilikula msoto sana nikawa alosto nikawa naishi maisha ya kubet kesho itakuwaje nilikuwa sina hata wallet maana nabeba ya nini sasa na hela nikiipata natumia instantly haikai mfukoni.

Sasa ndugu zetu hawa, wazee wa kupiga majungu na kusema negative ikawa wanapiga sana majungu hadi ya wazi wazi. Dharau hadi wanawafundisha watoto kuleta dharau yaani mtoto uliyemuona anazaliwa na umempakata leo kanakuletea dharau ya wazi.

Unamuomba mtu akutoe kitu kidogo uweke mishe zako sawa mtu anakupiga madongo kuwa kama unataka pesa kapige kazi, sio kutegemea kupewa, imagine hapo umeomba labda 5,000 au 10,000 au hata 2000 tu. Na sio kwamba hawezi kukupa au hana anayo ila ameshajiwekea kuwa yeye tu ndie huwa anashida na anatakiwa kusaidiwa ila sio wewe. Wewe upambane ndio umsaidie yeye.

Nikaona haina shida. Nikakaza akili yangu nikaanza jitafuta. Picha linaanz anilipotea miaka kama miwili hivi hakuna mtu anajua nilipo ila napatikana hewani. Wakiuliza nilipo nakata simu sitaki story ziendelee maana itakuwa unafiki sasa. Watu ambao mlinikataa na kutokuwa tayari kunisapoti kwenye hali ngumu mnataka kujua nafanya nini ili iweje sasa?

Fast Forward today. Hawa ndugu na jamaa anaweza kukuona upo somewhere umetulia na Vijana, unasikia anapiga simu kwa bi mkubwa kulalamika mbona fulani siku hizi hata hanitafuti.

Kuna m'moja juzi kati nikampa kubwa kwa njia ya sms. Siku kadhaa nyuma kabla ya juzi aliniomba kwa utani 2000 ya umeme nikamnunulia wa wa 5,000 makusudi nikamtumia tokens zake. Sasa juzi hapa akanitumia gazeti la sms kunielezea hali yake anahitaji nimsaidie 50,000/= nikamwambia tafuta shughuli ya kufanya pesa zipo kwa wanaotafuta usipende kupewa mbona kazi zipo.

Ule ujumbe niliukuta kwa bi mkubwa na sista wakaniambia. Nikawaambia hayo ndio majibu yangu. Nilipokuwa nimekwama nawaomba hata buku wakawa wananiona mvivu wao wanavyoniomba hizo kubwa kwann wasifanye kazi wapate hela wanarudia kosa lile lile walilosema nafanya. Waache upuuzi.

Usiwaendekeze hao omba omba. Maana hata ukikwama au ukirudi chini hao hao watakuwa ndio wakandiaji namba moja. Hali yako ya kiuchumi ikiboreka ukaanza ona visimu vya watu ambao hawakuwa na mazoea ya kukutafuta wape tu salamu na buku za vocha acha kuendekeza kusaidia watakufilisi ukianguka wanakugeuka na hawatakusaidia hata nauli watakusema tu kuwa wewe ni mvivu, mzembe, hauna direction na kila neno la hovyo watakutupia.
 
Mkono WA mtoaji ni Bora zaidi.

Jifunze kutoa kidogo ulicho nacho ukiwa kijana
 
Ila niwape tu pole wale ambao wanakuwa wa kwanza kwenye ukoo kupata hela unakuta inatakiwa ajenge mpaka kwao [emoji34][emoji34]

Kuna dogo napiga nae job take home ni kama 2.3 mpaka 2.8 milioni huyo dogo ana wadogo 13 na yeye ndio wa kwanza ana wadogo 3 wamefaulu form four walipata division 3 inatakiwa awasomeshe vyuo

Pia dingi wake anataka ajengewe nyumba bad enough baba yake ana wake 3

Hao wadogo zake 13 anachangia nao baba na mama bado wale anaochangia nao baba tu [emoji21]

Huwa ananipa simu nisome meseji za wanaukoo wake huwa nacheka saana unakuta mtu anajitambulisha yeye ni nan end of the day anaomba hela
Kwanini aliwaambia anafanya kazi mbaya zaidi kuna uwezekano wanajua makadirio ya mshahara wake.

Familia kama hizo kama uko mbali usiwaambie unafanya kazi au unadanganya mshahara tu.
 
Nimeelewa unavyojihisi. Ila kaka, kama ana ndugu 13 asipowasaidia yeye ndugu zake nani aende akawasaidie ?
Tusifundishane uchoyo, hela zipo tu, weka hakiba yako kias kdg, kingine asaidia wadogo zake.

Mtoto wa kwanza wazaz wanatumia nguvu nyingi kumsomesha kwa lengo la kwamba akifanikiwa atakuja kusaidia wazaz wake. Na ni wajib wetu kuwasaidia wadogo zetu bro. Sikatai tuna mitazamo tofuat na tumeumbwa tofaut kwaio mtu ni maamuzi yake kusaidia wadogo zake wasome waje wafanikiwe kama yeye au awa ache wadhalilike na kuishia njiani kimasomo.
kuna majukumu ambayo kama mzazi inabidi uyabebe ... usiache kiporo kwa ajiri ya mtu mwingine yeyote yule .... labda itokee umefariki/umelemaa before watoto wajitegemee.

Ukitaka kujua kwanini hatuendelei .. ni tunarithishana majukumu ya mtu mwingine ... kusomesha wadogo zako siyo jukumu lako ... itokee tu mzazi amefariki au amelemaa lakini siyo fair mzazi kujivua jukumu lako eti kwa sababu first born kapata kazi...
 
Walimu wanatokea maisha duni
Mishahara yao duni

Niliwai kuwa na demu mwalimu alikuwa ni single mother nikamtafutia kazi ya ualimu salary laki 3 akawa anatuma kwao kila mwezi 70K
Analipa ada ya mtoto wake 35K
Boda boda 20K
Anakoishi yeye alipe kodi avae
Pia atume hela ya matibabu kwa mwanae na nguo muda huo huo akawa anamsomesha mdogo wake pharmacy ada 1.4 kwa mwaka [emoji23][emoji23][emoji23]

Yote haya hakuwai kuniambia ila nikawa nashangaa ananiomba hela saaana

Nikamtoa kwenye hiyo shule nikamtafutia nyingine ambayo ipo wilaya ya jirani na kwao mshahara pale ukawa ni laki 5
Sasa alivyoona mshahara ni laki 5 akaona ni nyingi saana akawatangazia ndugu zake
Now day mama yake akaanza kudai ajengewe [emoji23][emoji23]

Pale kwao kulikuwa kuna nyumba kubwa inajengwa ikaishia msingi akaja kuniambia nimkopeshe milioni 5 aimalizie ile nyumba (msingi wa vyumba 4 kigoma mjini alafu yeye anataka aumalizie kwa milioni 5 [emoji3])

Nikamwita fundi kupiga hesabu mpaka nyumba kukamilika bila finishing ni milion 22 plus finishing 30+ akawa mpole

Akaamua kujenga vyumba viwili mama yake akafyumu (anadhani laki 5 ni pesa nyingi) so nyumba now ipo kwenye lenta mwalimu na laki 5 tano zake yupo anajichanga aweke bati

NADHANI KUTAJA PIA MISHAHARA KUNACHANGIA KUOMBWA PESA AU KUFANYA KAZI ZINAZOJULIKANA saana mfano
Polisi
Jwtz
Ualimu
Dr
TRA
Bank

Kuna fanya wanandugu wajue mzunguko wenu tofauti na watu wanaofanya kazi ambazo sio maarufu kama
Tpdc
Tbs
NGOs

Mkuu watu wametoka familia duni wana kiu na ndoto ya kufanya angarau kakitu ili waonekane wamefanya kitu majumbani mwao,hongera kwa kumvuta mkono kwa kadri ulivyoweza.

Bahati mbaya ana mama mzazi mpuuzi,anayeweza kumponza hata akaingia kwenye madeni na matatizo makubwa ili amridhishe mama asiye na shukrani wala imani ya kumtia moyo binti yake.

Ukute kila wakati huwa anampogia simu anataka hela mbali na huo ujenzi.
 
Back
Top Bottom