Kero za tarehe ya Mshahara kufahamika na ndugu

Nimeelewa unavyojihisi. Ila kaka, kama ana ndugu 13 asipowasaidia yeye ndugu zake nani aende akawasaidie ?
Tusifundishane uchoyo, hela zipo tu, weka hakiba yako kias kdg, kingine asaidia wadogo zake.

Mtoto wa kwanza wazaz wanatumia nguvu nyingi kumsomesha kwa lengo la kwamba akifanikiwa atakuja kusaidia wazaz wake. Na ni wajib wetu kuwasaidia wadogo zetu bro. Sikatai tuna mitazamo tofuat na tumeumbwa tofaut kwaio mtu ni maamuzi yake kusaidia wadogo zake wasome waje wafanikiwe kama yeye au awa ache wadhalilike na kuishia njiani kimasomo.
 
Kama ni mzazi mtumie tu hakuna namna
 
Pole kwa mitihani hiyo
Mimi nashukuru wazazi hawajawahi kuniomba hata senti yangu moja
Ila nalazimisha tu kuwapa kama Asante kwa kunizaa

Kuna wakati nilikosa kazi kwa mda na niko ugenini walikuwa wananitumia hela wao ingawa nilikuwa nakataa ila wanatuma tu

Wavumilieni wazazi wenu kama hawana kitu kwani ni mipango ya Mungu
Usimlalamikie mzazi hata siku moja bali Omba wakuombee sana na hutakosa kitu duniani

Ila ukiwa wa lawama hata kwa wazazi basi ni mtihani mkubwa
Jitume hata kibiashara kidogo after work ikuingizie cha ziada ili uwakumbuke zaidi
Amini hili ukiwatunza vizuri wazazi hutakosa kitu
Punguza matumizi yasio ya lazima pia
 
50k mbona hela ndogo Sana hiyo Mimi bro wangu anamtumia Mama laki mbili kila wiki na sisi wadogo zake bado tunatuma si haba then sio Kwamba Mama yetu ana shida , yupo vizuri tu well financially stable


Vijana tafuten Blessings kutoa ndo kupata
 
Mzazi unabidi kumpatia mahitaji yote ya msingi na Pesa kila wiki umtumie


Kama hautoi wewe ni bahili huwezi kufanikiwa hata siku moja.
 
Mkuu umeongea ukweli..
 
Shida ya watanzania kwa wingi ni Uvivu. Uvivu wa akili na mwili.

Nakumbuka kuna kipindi kigumu sana nilipitia, nilikula msoto sana nikawa alosto nikawa naishi maisha ya kubet kesho itakuwaje nilikuwa sina hata wallet maana nabeba ya nini sasa na hela nikiipata natumia instantly haikai mfukoni.

Sasa ndugu zetu hawa, wazee wa kupiga majungu na kusema negative ikawa wanapiga sana majungu hadi ya wazi wazi. Dharau hadi wanawafundisha watoto kuleta dharau yaani mtoto uliyemuona anazaliwa na umempakata leo kanakuletea dharau ya wazi.

Unamuomba mtu akutoe kitu kidogo uweke mishe zako sawa mtu anakupiga madongo kuwa kama unataka pesa kapige kazi, sio kutegemea kupewa, imagine hapo umeomba labda 5,000 au 10,000 au hata 2000 tu. Na sio kwamba hawezi kukupa au hana anayo ila ameshajiwekea kuwa yeye tu ndie huwa anashida na anatakiwa kusaidiwa ila sio wewe. Wewe upambane ndio umsaidie yeye.

Nikaona haina shida. Nikakaza akili yangu nikaanza jitafuta. Picha linaanz anilipotea miaka kama miwili hivi hakuna mtu anajua nilipo ila napatikana hewani. Wakiuliza nilipo nakata simu sitaki story ziendelee maana itakuwa unafiki sasa. Watu ambao mlinikataa na kutokuwa tayari kunisapoti kwenye hali ngumu mnataka kujua nafanya nini ili iweje sasa?

Fast Forward today. Hawa ndugu na jamaa anaweza kukuona upo somewhere umetulia na Vijana, unasikia anapiga simu kwa bi mkubwa kulalamika mbona fulani siku hizi hata hanitafuti.

Kuna m'moja juzi kati nikampa kubwa kwa njia ya sms. Siku kadhaa nyuma kabla ya juzi aliniomba kwa utani 2000 ya umeme nikamnunulia wa wa 5,000 makusudi nikamtumia tokens zake. Sasa juzi hapa akanitumia gazeti la sms kunielezea hali yake anahitaji nimsaidie 50,000/= nikamwambia tafuta shughuli ya kufanya pesa zipo kwa wanaotafuta usipende kupewa mbona kazi zipo.

Ule ujumbe niliukuta kwa bi mkubwa na sista wakaniambia. Nikawaambia hayo ndio majibu yangu. Nilipokuwa nimekwama nawaomba hata buku wakawa wananiona mvivu wao wanavyoniomba hizo kubwa kwann wasifanye kazi wapate hela wanarudia kosa lile lile walilosema nafanya. Waache upuuzi.

Usiwaendekeze hao omba omba. Maana hata ukikwama au ukirudi chini hao hao watakuwa ndio wakandiaji namba moja. Hali yako ya kiuchumi ikiboreka ukaanza ona visimu vya watu ambao hawakuwa na mazoea ya kukutafuta wape tu salamu na buku za vocha acha kuendekeza kusaidia watakufilisi ukianguka wanakugeuka na hawatakusaidia hata nauli watakusema tu kuwa wewe ni mvivu, mzembe, hauna direction na kila neno la hovyo watakutupia.
 
Mkono WA mtoaji ni Bora zaidi.

Jifunze kutoa kidogo ulicho nacho ukiwa kijana
 
Kwanini aliwaambia anafanya kazi mbaya zaidi kuna uwezekano wanajua makadirio ya mshahara wake.

Familia kama hizo kama uko mbali usiwaambie unafanya kazi au unadanganya mshahara tu.
 
kuna majukumu ambayo kama mzazi inabidi uyabebe ... usiache kiporo kwa ajiri ya mtu mwingine yeyote yule .... labda itokee umefariki/umelemaa before watoto wajitegemee.

Ukitaka kujua kwanini hatuendelei .. ni tunarithishana majukumu ya mtu mwingine ... kusomesha wadogo zako siyo jukumu lako ... itokee tu mzazi amefariki au amelemaa lakini siyo fair mzazi kujivua jukumu lako eti kwa sababu first born kapata kazi...
 

Mkuu watu wametoka familia duni wana kiu na ndoto ya kufanya angarau kakitu ili waonekane wamefanya kitu majumbani mwao,hongera kwa kumvuta mkono kwa kadri ulivyoweza.

Bahati mbaya ana mama mzazi mpuuzi,anayeweza kumponza hata akaingia kwenye madeni na matatizo makubwa ili amridhishe mama asiye na shukrani wala imani ya kumtia moyo binti yake.

Ukute kila wakati huwa anampogia simu anataka hela mbali na huo ujenzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…