Kero za tarehe ya Mshahara kufahamika na ndugu


Huyu watamuua kama si kwa mawazo basi tunguli.

Kwanini watu wanaruhusu vipato vifahamike na ukoo mzima??mimi hata mzazi anajua sababu kazi aliyoifanya ina asili hii ya kwangu,lakini si baba mdogo wala shangazi.

Nimekaa na watu kazini mtu anakwambia bro kwetu hata nikienda na gari nimejiharibia[emoji23][emoji23][emoji23],ntapata tabu sana.
 
Kuna maisha ambayo tunayapitia ni kipindi cha mpito kwa vizazi kama vitatu hivi alafu hii hali itapotea yenyewe tu!!
Hata huko kwa wenzetu walipitia hivi vipindi na kuna baadhi ya nchi Bado inaendelea!!
Ila kila rizki na urefu wake,,,,, mwambie asifanye lolote na abaki na fedha zake alafu mcheki kitakachokuwa kinaendelea kwake!!!
 
Nlitaka nikucriticize lkn nlipoona neno la.mwisho kabisa nkasizi..broo utashangaa hata hako ka akiba unaliliwa shida na mtu ambae hafanyi kazi yupo Bush halimi hana asset yyte ya mfugo si mbuzi kuku wala ng'ombe anasubir tareh za mshahara zimekarbia akupige kibomu,inakera mtu na nguvu zake timamu hataki kujishighulisha...kwa changamoto ya kimasomo ruksa kusaidia maana itapuguza chain ya dependants na umaskini utapungua Ila asotaka kufanya kazi makusudi asaidiwe mpaka lini hao ndo kero zenyew
 
Ndio shida watu kuzoeana zoeana....
Ukishatangaza una kazi kwanini usiombwe...
Mimi kuna anko mmoja alisikia kuna marekebisho makubwa nilifanya home..
Akaanza kunipangia watoto wake nimuitikia tu poa tutacheki ile muda umepita ananikumbusha nikajibu tu simple " Anko nilikula mtaji shida zilizidi nikafunga biashara sasa napambana na mkopo wa benki" hakunichek tena na alienda kutangaza kote kwamba nina mkopo benki na wamenifilisi...
Mimi ndugu zangu wote hata wazazi wanajua sina kazi ni misheni town tu😆😀
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…