Kesho (30-03-2021) ninaenda kufanya "Oral Interview" kwenye N.G.O huku Dar. Niombeeni kwa Mungu ndugu zangu, mtaani maisha ni magumu sana

Kesho (30-03-2021) ninaenda kufanya "Oral Interview" kwenye N.G.O huku Dar. Niombeeni kwa Mungu ndugu zangu, mtaani maisha ni magumu sana

O
Habari zenu ndugu zangu wa jamiiforums.

Kesho (30-03-2021) saa 4 asubuhi ninaenda kufanya "Oral Interview" kwenye N.G.O moja huku Dar. Niombeeni kwa Mungu ndugu zangu mtaani maisha ni magumu sana.

Tulifanya written Interview tukiwa watu 20, tumechujwa na kubaki 9 ambao kesho ndio tunapambania kombe ili wawili waibuke kidedea na 7 watakaobaki warudi tena mitaani kupambana na maisha. Je, Infantry Soldier atavuka Interview hii na kuachana na biashara yake ya kuendesha Taxi Bubu?

Mwambie Mungu anisaidie nivuke salama challenge hii kwa maana mshahara wa hawa jamaa zangu ni mnono kweli kweli.

Na sisi utukumbuke kwenye mshahara wako!
 
Back
Top Bottom