Kesho nafungua kesi dhidi ya Tigo Tanzania

Kesho nafungua kesi dhidi ya Tigo Tanzania

The Saver

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2014
Posts
202
Reaction score
651
TAARIFA KWA UMMA

Kesho natalajia kufungua kesi dhidi ya Tigo Tanzania kwa kukiuka haki za mlaji/mteja wake.

Tokea jana tarehe 6/04/2021 saa 11.15 jioni miamala ya tigo ilikuwa haitoki wala huwezi kuangalia salio niliwapigia simu 3.30 usiku wakasema ndani ya masaa 24 huduma itakuwa imerudi, Leo tarehe 7/06saa 3.04usiku bado.

Biashara yangu inategemea 100%online payment na mimi nafanya kazi kwa online business kwa kutumia tigopesa.

Pamoja kuwa wamepata tatizo la kiufundi au wamezima system kufanya marekebisho bado hawajatoa taarifa kwa umma taarifa inakuja baadae.

Mamlaka za serikali TCRA wapo kimya upuuuzi huu.

Wizara ya habari wapo kimya upuuuzi Mwananchi anaumia.
 
Una haki kabisa lakini ukienda kiwepesi hivi watakushinda vibaya sana. Kwanza kabisa hapo wenye makosa siyo huu mtandao wa TiGO Tanzania peke yao, bali hata mamlaka za usimamizi za kiserikali nazo inabidi zishitakiwe. Hivyo itakubidi ushitaki wahusika wengi kidogo.

Pia, hutakiwi kufungua hii kesi ukiwa peke yako, itakuwa haina uzito sana maana walioumia ni watu wengi zaidi yako, hivyo mahakama inaweza kukutaka kuthibitisha kwamba wewe ndiyo umeumia zaidi kuliko wateja wengine wote nchini Tanzania. Hivyo hili litakueletea changamoto, labda utufahamishe zaidi unataka kufungua kesi ya aina gani.

Binafsi nadhani kesi kama hizi, ili kuwashinda hawa maharamia wa mali zetu, inabidi utumie mwanya wa KIKATIBA hasahasa chini ya kipengele cha Haki za Binadamu (Basic Rights and Duties), tena ikiwezekana utafute wateja wenzako waliopata hasara halafu mnafungua kesi ya pamoja (A Representative Suit).

Ukijipanga na kutulia, unaweza kufungua kesi nzuri sanaa.
 
Una haki kabisa lakini ukienda kiwepesi hivi watakushinda vibaya sana. Kwanza kabisa hapo wenye makosa siyo huu mtandao wa TiGO Tanzania peke yao, bali hata mamlaka za usimamizi za kiserikali nazo inabidi zishitakiwe...
Asante mkuu hii kesi sitakuwa peke yangu tupo wafanyabiashara 25 bado wanaongezeka na nakusanya ushahidi kupitia maelekezo ya mwanasheria
 
Cha kushangaza ujumbe wa "tigo inakutakia heri ya Karume day" kwanini ujumbe wa taarifa haujatumwa?

Binafsi mimi sitegemei kuwa mtumwa wa mtandao mmoja, kwa hiyo hii kero nawachora tu
 
Una haki kabisa lakini ukienda kiwepesi hivi watakushinda vibaya sana. Kwanza kabisa hapo wenye makosa siyo huu mtandao wa TiGO Tanzania peke yao, bali hata mamlaka za usimamizi za kiserikali nazo inabidi zishitakiwe. Hivyo itakubidi ushitaki wahusika wengi kidogo...

Afuate huu ushauri apige pesa ya usumbufu kama kina Mwana FA na AY.
 
Asante mkuu hii kesi sitakuwa peke yangu tupo wafanyabiashara 25 bado wanaongezeka na nakusanya ushahidi kupitia maelekezo ya mwanasheria
Tafuta watu ambao wamepeta hasara ambayo inaoneka na inawezekana kuthibitishwa kirahisi mahakamani: Lakini kabla ya kufungua kesi hebu jaribu kwanza kuwaandikia barua ya malalamikona madai kwenye mamlaka husika za TiGO na TCRA, ukiwaeleza kinagaubaga hasara uliyoipata na kuwaomba wakulipe fidia.

Hili lifanywe na kila mfanyabiashara ambaye unamfahamu kwamba amepata hasara (aandike barua binafsi), wekeni viambatanisho vyote vya mihamala. Wapeni muda wa kujibu na kujitetea, huku mkiwajulisha nia yenu ya kufungua kesi mahakamani endapo watakaidi kulipa fidia ya hasara mliyoipata kutokana na uzembe wao.

Muwaambieni dhahiri, mbali na kulipa fidia itabidi waombe msamaha kwa wateja wao wote kwa uzembe ambao wameufanya, kwa kushindwa kutoa taarifa kwamba kuna hitilafu kwenye mfumo hivyo wateja wasifanye mihamala ya kifedha kwa siku kadhaa.

Nenda taratibu, wageuzie kibra halafu shusha kisu...
 
TAARIFA KWA UMMA

Kesho natalajia kufungua kesi dhidi ya Tigo Tanzania kwa kukiuka haki za mlaji/mteja wake...
Sidhani kama kuna kampuni inayotoa huduma za miamala ya fedha ambayo imewahi kufanya kituko kama hiki cha tigopesa. Kuanzia leo nimeamini hoja ya jamaa yangu kuwa hii kampuni ni incompetent na haifai kuaminiwa. Jana nilikuwa kwenye biashara zangu alamanusura niaibike sababu ya hawa tigiopesa.

Poor tigopesa. Siwezi kuwaamini tena
 
Tafuta watu ambao wamepeta hasara ambayo inaoneka na inawezekana kuthibitishwa kirahisi mahakamani: Lakini kabla ya kufungua kesi hebu jaribu kwanza kuwaandikia barua ya malalamikona madai kwenye mamlaka husika za TiGO na TCRA, ukiwaeleza kinagaubaga hasara uliyoipata na kuwaomba wakulipe fidia...
TCRA wameishapata barua hawakujibu lolote wameniambia nifuate majibu kesho
 
TIGO WAHUNI SANA HAWAHESHIMU MAONI YA RAIS LEO WAMEWEKA WHATSAPP YA WIKI 3000sh badala ya 2000sh l na leo siku ya pili tigo pesa yao imefungwa wanasema wanaifanyia matengenezo
 
Una haki kabisa lakini ukienda kiwepesi hivi watakushinda vibaya sana. Kwanza kabisa hapo wenye makosa siyo huu mtandao wa TiGO Tanzania peke yao, bali hata mamlaka za usimamizi za kiserikali nazo inabidi zishitakiwe. Hivyo itakubidi ushitaki wahusika wengi kidogo...
Naomba awe mteja wako, kama ni wakili una maandishi yenye kueleweka kabisa.
 
Back
Top Bottom