Kesho ndo utekelezaji wa mtaala mpya kwa kidato Cha kwanza unaanza: vitabu havijafika mashuleni, mafunzo kwa walimu yametolewa wakati likizo na Bure..

Kesho ndo utekelezaji wa mtaala mpya kwa kidato Cha kwanza unaanza: vitabu havijafika mashuleni, mafunzo kwa walimu yametolewa wakati likizo na Bure..

Dr wa Manesi

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2024
Posts
997
Reaction score
1,220
Zilipita wiki 2 Hadi 3 ndipo yakatangazwa mafunzo ya walimu kwa ajili ya kuuanza mtaala mpya!

Walimu wengi hawakuhudhuria sababu walikuwa likizo (waliyoipata kisheria kabisa kwenye ess). Waliohudhuria, walilazimika kugharamika kidogo kinauli pamoja na muda wao wa kupumzika.

Mafunzo yalikuwa yanaanza saa 1 asubuhi Hadi saa 6 mchana.....HUKU YAKIWA HAYANA POSHO WALA NAULI WALA CHAKULA KWA WALIMU WALIOHUDHURIA. Dah, hii Dunia hii!!!!!

Mind you, 95% hata hawajaelewa.....si kwa kukurupushwa Huku na njaa hii.

Wabunge wakiupata tu ubunge, wanaenda kupigwa mafunzo ya pengine mwezi mzima, ya namna ya kupiga makofi bungeni Huku yakishereheshwa na maposho mengi na mavyakula ya kufa mtu.


Vitabu ndo hata haijulikani vitafika lini.....walimu tupo tunang'aang'aa sharubu tukivisubiri.

NB:
Tarehe 18 unaanza usaili wa ajira za walimu 14,000 wa msingi na sekondari wasambazwe kwenye shule zaidi ya 6000 zilizopo nchini hapa Huku 90%+ ya shule hizo zikiwa Zina wastani wa walimu wa3 kati ya 20 wanaohitajika.

Nawatakia muangalio mwema wa mpira!!!
 
Back
Top Bottom