Kesho ni mkutano mkuu wa Simba ajenda kuu ni Katiba

Mzee Chacha atawasumbua sana
 
Huu mkutano unaenda kuivuruga Simba upyaaa.

Shida kubwa kwenye hili suala zima ni kuwa Mo hawaamini waswahili katika uendeshaji wa timu na kusimamia kwa uaminifu rasilimali na pesa za klabu ndiyo maana anahakikisha ana nguvu au ushawishi fulani ndani ya klabu. Ukweli ni kuwa Simba bado haijajipambanua kuwa ina watendaji wenye weledi kiasi cha mtu kukubali kuweka mabilioni yake alafu kuwa tu mwekezaji wa 12%.

Mo mwenyewe siyo kwamba mchakato ukiisha hizo 49% atakaa nazo ndani, naye ataenda kuzigawa vipande vipande na kuziuza kwa wawekezaji wengine wakubwa.
 
Ivi yanga wametumia model gani katika katiba yao?
 
Mkutano Mkuu wa mwaka wa Wanachama wa klabu ya Simba utafanyika Jumapili, Januari 21 kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere

Mkutano huo utakaofanyika kuanzia saa 3 asubuhi, utahusisha Wanachama HAI wa klabu (waliolipa ada ya uanachama ya mwaka)

Miongoni mwa ajenda zitakazojadiliwa kwenye Mkutano huo ni kupitisha maboresho ya Katiba ya Simba ili mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji uweze kukamilika

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limeridhia maboresho muhimu yaliyofanyika kupitia Kamati ya maboresho ya Katiba iliyoongozwa na Hussein Kitta

Jumapili Wanachama wa Simba watapitisha maboresho hayo ili klabu ikamilishe mchakato wa uendeshaji kwa mfumo wa hisa
 
Wenye pesa kwanini wasiige mfano wa Bakrhes waanzishe timu zao badala ya kudandia tre
Mzee Chacha atawasumbua sana
Sio chacha wako wengi tatizo tumeingiza siasa kwenye mpira Ila kitakachotokea Leo ni aibu.
 


Kuna sehem moja inaonyesha pia bado wewe unaweza kuwa sehem tatizo.. unaposema kuwa unaona vingoz watataka watu wajadili katiba huku ukisema kuna jambo la kujadili ikiwemo goli 5 walizofungwa..

Yaan unataka mkutano mkuu wa club ujadili ilikuwaje kufungwa goli tano?

Kufunhwa lilikuwa swala kiufundi ambacho technical bench walitakiwa na naamin walishapeleka majibu..

Wanachama wanatakiwa kujadili
Mazingira bora ya uendeshwaji wa team ili kuhakikisha kunakuwa na maslah bora ya wachezaj na recruitment nzuri..

Sio wajadili matokeo ya uwanjan huko ni kupoteza mda..

Mkiacha siasa za mafanikio ni kumfunga yanga mtasogea ( yanga wanaonekana walishatoka huko)
 
Uongozi unapimwa mafanikio take kutokana na mafanikio ya uwanjani na nje ya uwanja, matokeo waliyopata Simba kiasi kikubwa yalichangiwa na uongozi lakini hakuna aliyewajibika zaidi ya kuwatupia lawama makocha na wachezaji. Usajili ulifanywa na viongozi hivyo so sahihi wanachama wasijadili kwanini Simba inabaki na wachezaji wazee Kama Boko au Saidoo badala ya kusajili wachezaji wazuri ambao wapo wengi.
 
Aliyeandika hivyo ni Yanga......
Ameandika kutroll na wewe umejaa mazima.
 
Mkutano unaendelea Sasa hivi CEO anaongea
KWA KIFUPI YALIYOJIRI KWENYE KIKAO CHA VIONGOZI WA MATAWI MAKAO MAKUU YA CLUB NI KAMA IFUATAVYO.

1. Tupunguze utitiri wa matawi ili kuunganisha nguvu ya kupata matawi mengi.

2. Kila mwanachama alipie kadi kwa mujibu wa katiba ya klabu. Wanachama wote ambao hawajalipa ada ya mwaka 2022/23 kadi zao zimekufa.

3. Tawi ambalo halina wanachama hai ni tawi mfu sambamba na wanachama wasiolipa ada kwa mujibu wa katiba.

4. Inaanzishwa kadi ya Tsh. 1'000'000/- kwa mwaka

5. Kadi za benki zitaanza kutoka ndani ya siku 3 kwa Dar es Salaam na siku 5 kwa wanachama wa mikoani

6. Matawi yote makubwa yatatumika kama mawakala wa benki ya CRDB

7. Kadi zote za benki zina bima ya maisha

8. Rais wa klabu ya Yanga Mhandisi Hersi Said yupo nchini China kushughulikia mchakato wa ujenzi wa uwanja

9. Wiki ijayo timu itacheza mechi mbili za Kimataifa

10. Idara ya Masoko, matawi, wanachama na mashabiki inazunguka mikoa yote kuhamasisha ulipaji wa ada na usajili wa wanachama na mashabiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…