Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mnooo. Kama enzi zile za wastaarabuIla kunakuwa kunapendeza kweli😂
Yaani Mshana Jr umenichekesha sana 🤣 kumbe wewe ni zaidi ya uchawi 🤣🤣🤣!!Mliokimbizwa kea nguvu na mliokimbia kwa hiari karibuni tena.. Najua mlipamisi sana hasa pale kati.. Leo mitaa ilikuwa tupu na barabara hasa za kuelekea na kutoka Airport ilikuwa raha tupu
Hakuna watu
Hakuna bodaboda
Hakuna gari za mizigo
Na kama vilikuwepo ilikuwa kwa uchache mno
Wendawazimu wote walikuwa wamefungiwa ndani.. Waliojaribu kuleta fyoko walikiona cha mtema kuni
Maaskari wa usalama barabarani na FFU na magereza nadhani walikuwa kwenye mpangilio mzuri... Nguo mpya safi na nadhifu haswa..
Kwa namna walivyokuwa wamesimama, kushika doria na kuongoza magari kwa weledi mkubwa nilitamani kila siku iwe hivyo
Yale madifenda chakavu, mabaya na machafu yasiyo na plate number, au plate number nusu na robo hayakuonekana popote.. Au wale maaskari wao kama wavuta mjani na mibunduki yao mibaya hawakuonekana kabisa
Yaliyokuwa yanaringa mitaani ni pickup nzuri nyeupe safi na mpya kabisa(pickup zile za mvimba macho) na askari waliokuwa wameoga, Ku shave au kusuka nywele.. Na mavazi pamoja na kofia bunduki buti na vyeo vyote brand new kabisa.. Nimesahau na soksi na gloves
Yaani ukiwaangalia tu walivyopendeza na kukaa kwa utulivu hata hofu inakutoka na kutamani kupiga nao selfie😂
Sasa wageni wameondoka .. Vyote vipya ghalani..vichafu vichakavu mtaani.. Machizi mateja, chinga na kila aina ya binadamu turudini kwenye maisha yetu tuliyozoea sana.. Najua wote tuliyamiss sana
Dar hapapendezi kabisa pakiwa pasafi patulivu na ukimya.. Welcome back home wandewa wote.
Hata joto lilipungua mjue😂😂😂
View attachment 3216578
View attachment 3216578
Aisee dar ni nzuri bila watuNimetumia takriban dakika 35 kutoka Quality Plaza mpaka Gongolamboto.
Mfugale nilikuwa peke yangu.
Yaani kama nimepata ganzi.zimeletwa kwa shughuli hii au zilikuwepo? Halafu wasafi Kwanza wamejipanga kama wambele huko.😂😂😂😂
Mnashangilia magari makari ya Polisi, huku wama wajawazito wanaambiwa kama hawana 50,000 wakajifungulie nyumbaniNimekutana na gari moja Kali ya polisi yaani nilivowashangaa kidogo wanikamate
Wameazima au ?