KESHO YA SIMBA NI BORA KULIKO LEO YA YANGA

Upo sahihi..simba wanajitafuta...ila wakati wanajitafuta kuna mwenzie anatumia hali yenu ya kujitafuta kujitengenezea ufalme wa vikombe na heshima juu yenu..sasa miaka miwili ijayo wachezaji mliowatengemeza wataamza kusambaa kwingine kwa mikataba kuisha au kudakwa na timu zingine..mana mikataba mingi ni miaka 2 au 3..wakati huo nao washajanjaluka kiwango kizuri..kwahiyo future ya club zetu hizi ni uimara kiuchumi na kiuongozi kisha kupata wachezaji wazuri na wazoefu..timu hizi kubwa hazilei sana vijana, hapa mashabiki wanataka mchezaji avumiliwe msimu mmoja au awe vema mwanzoni kabisa
 
Endeleeni tu kujiliwaza kila msimu Yanga wachezaji bora wanaingia. Yanga haijakalili kukaa na wachezaji kama Simba. Msimu ujao kuna maingizo mapya kama kawaida. Mtasubiri sana na hao under 17 wenu.
 
Mimi ni simba ila ukweli ni kwamba timu ni dhaifu,uongozi ni dhaifu.Hakuna uimara nje na ndani ya uwanja kwa Simba.
Na yanga ataendelea kutufunga.
Simba uhuni, ujanja ujanja mwingi
 
Kwakweli inabidi nijitafakari kwanini Simba wanafungwa mara 4 mfululizo wakati Yanga ikiwa unga na wanajitafuta kipindi hicho hakuwa wanyonge kiasi cha kukubali kiwa wateja wa kufungwa tu kila mchezo na Simba. Najitafakari sana mkuu huyu Gamondi
🚮
 
Kaka Yanga wapo smart sana kwenye kujenga timu. Angalia replacements za wachezaji zinavyofanyika.

Sitegemei Yanga kushuka kiwango miaka ya karibuni ila nategemea kuwa na Simba imara na Yanga imara miaka ya karibuni.

Japo wanaonitia wasiwasi hapo Simba ni aina za viongozi walionao, wanamanage timu kisela sana. Imagine mpo kwenye kipindi cha kujenga timu na kuleta umoja anajitokeza kiongozi tena anapost hadharani kabisa akimtumuhumu Kipa amehujumu mechi.
 
Kesho yake wachezaji wazuri watachukuliwa na timu bora na Simba watasubiri wanaomaliza mikataba!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…