Kesho yenye uwajibikaji inahitaji Citizen journalism (Uandishi wa Umma)

Kesho yenye uwajibikaji inahitaji Citizen journalism (Uandishi wa Umma)

OLS

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2019
Posts
426
Reaction score
685
Tasnia ya Habari imeonekana kama moja ya muhimili wa serikali hata hivyo tasnia ya habari imeonekana kupoteza uwezo wake wa kuibua mambo na kuleta uwajibikaji kwa mihimili mingine ya serikali.

Waandishi huripoti matukio na press hali inayofanya stori ziwe hazina maajabu ya kutosha kwenye kuleta uwajibikaji.

Halkadhalika kutokana na maisha yaliyopo ni ngumu kwa mtu kuacha elfu 10 kwa jina la maadili ya kazi hali inayozidi kufifisha ubora wa tasnia ya habari, bila shaka mnakumbuka tukio la waandishi kuvunjiana kamera walipotupiwa hela na wasanii wa bongo movies.

Hali ni tofauti kwa Waandishi wa Umma, Citizen Journalists ambao hawana taaluma rasmi ya kuandika lakini huweza kufichua uovu na uozo unaoendelea kwenye jamii.

Hapa JamiiForums watu wengi wamekuwa wakiweka vitu mbalimbali kuhusu mambo mengi tofauti tofauti hali inayofanya kuchukiwa kwa namna fulani kwa kuwa kimsingi ni ngumu kumpata member wa kumrubuni ili aandike kitu unavyotaka.

Mbali na uwepo wa watu wanaoleta habari za ukasuku bado JamiiForums ina maudhui mengi yanayoangukia kwenye citizen journalism hali inayoipa nguvu kwenye kuiwajibisha serikali. Waandishi wana safari ndefu ya kutoboa ni nafasi ya citizen journalism ili kufanya vitu viende.

Signed OLS
 
Back
Top Bottom