Kesi inakuzwa;inapotoshwa

Mtu katolewa jicho huko unasema hakuna bifu?

Tuhuma za hongo, magari, pesa na ukiritimba zimejaa kibao kwa pande zote, uongozi wa CHADEMA unaoburuzana na Zitto, na Zitto mwenyewe.

Unasema hakuna bifu?

Mipasho mpaka Facebook, mtu mzima anasema "I will not die" kama Farao wa zama hizi.

Halafu unasema hamna bifu?

Wewe kama vegetarian sema tu, lakini usiseme hamna bifu.
 
Je,kama sio mistake aliyoifanya Kibatala kama ilivyogunduliwa na Jaji na sio kupanguliwa na Msando ina maana rufani ya Zitto isingesikilizwa?yaani Kamathj Kuu ingeruhusiwa kumjadili uanachama wake?
 

Kesi inafaa isomeke "Zitto Vs Kamati kuu ya Chadema" na si "Zitto Vs Chadema"
 
Kwa hilo bw petro,umenrna jambo la msingi sna.tatizo letu wabongo ni kukuza mambo ya kizushi na kutashabikia.
 

hatuwezi kukwepa ukweli,hiyo ndio hali halisi.kwa yeyote yule atakayeshinda ushindi utashangiliwa kama vile mechi ya yanga na simba,hata kama ni mechi ya mtani jembe bado maudhui yake na mihemuko itasimama na kuleta hisia zilezile
 
Mbona kuna wanaosema kuwa chadema imeshindwa katika kesi mahakamani leo?ebu tujuzeni mliopo mahakamani.

Mkuu ni mitizamo tuu...kiukweli zit to kashinda,kapewa Nafasi ya kusikilizwa na baraza kuu...pia chadema imeamriwa kufuata huo utaratibu,ikumbukwe kuwa sio kuwa cdm imeshindwa ila imeamriwa kufuata utaratibu iliouweka yenyewe....pia kesi imekuwa based kwenye makosa ya wakili ambaye pia ni afisa wa iyo mahakama,vivo basi zit to kashinda ,kapewa haki ya kusikilizwa!,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…