unataka kusema nini labda? kwamba kila mtu ajenge au? wewe umejenga? alafu hapa swala sio kujenga au kupanga, ila pale mtu alipopanga apaiteje, jibu anapaita kwake, binafsi nimepanga na nikitoka kzn naenda nyumbani kwangu, sio kwa mwenye nyumba, nikipata mgeni namwambia karibu nyumbani kwangu hapa ndipo napoishi simpeleki kwa mwenye nyumba ndio amkaribishe, mwenye nyuma nikishampa kodi yake anapita hivi, akija kwangu shurti abishe hodi na nimkaribishe kwanza ndio aingie.HARUHUSIWI kuingia kwangu bila ruhusa yangu. kwa kifupi aliyejenga nyumba ni mmiliki wa nyumba mimi niliyepanga ndie mwenye nyumba. kujenga nyumba ni hatua tu za maisha na sio wote wenye uwezo huo.