Kesi namba 456 ya 2016 JamiiForums vs Jamhuri, Kisutu: Maxence Melo ahukumiwa Mwaka jela au faini ya Tsh. Mil 3. Mwenzake aachiwa huru

Kesi namba 456 ya 2016 JamiiForums vs Jamhuri, Kisutu: Maxence Melo ahukumiwa Mwaka jela au faini ya Tsh. Mil 3. Mwenzake aachiwa huru

Pole sana MAX,hii ndio maana ya ukubwa umeonyesha kwa vitendo kile unachokifanya,

hujakubali kuuza utu wako kwa vipande, najua ahadi nyingi na vitisho vingi ulipewa ili utoe na uwauze watoa taarifa lakini ulisimama wima na kidete.

hii inazidi kutupa imani ya kuwa tupo salama nyuma ya keyboards zetu,manake........!.
 
Bora kesi ilivyoisha....Tugange yajayo
 
Wana Jamii Forum,

Wengi mtakuwa mmeshasikia au kusoma juu ya hukumu katika kesi ya Jamii Forum, ambapo Maxence Mello amehukumiwa kulipa faini ya Tshs 3m au kifungo cha mwaka mmoja. Faini imelipwa.

Wengi wameshindwa kuelewa athari za hii hukumu, na wanaiona katika mapana ya hukumu au faini ya Stsh 3 tu, ambayo hata wengine wameita pesa ya mfukoni.

Lakini suala la kujiuliza ni kama tunaelewa athari za hukumu hii kwa JF hapo mbeleni. Kimsingi, hukumu hii inaweza kuweka precedent kwamba kila wakati serikali isipofurahishwa na thread au post ya mwana JF, inawataka JF kutoa taarifa za mtu aliyeanzisha hiyo thread au kuweka hiyo post.

Sasa najua JF ilianzishwa kwa namna ambayo ilitaka kuzuia suala la JF kulazimishwa kutoa taarifa binafsi za wana JF. Lakini hukumu haitambui hili, kitu ambacho kinamweka Maxence na Jamii Forums katika hali mbaya sana.

Sasa hii ni vita ya Watanzania waote katika kupigania uhuru wa kutoa maoni, hatupaswi kuwaachia JF na Mexence peke yao. Kama kuna uwezekano wa kuikatia rufaa hii hukumu tufanye hivyo, na ikiwezekana utaratibu uwekwe wale wote wenye mwamko wa uhuru wa kutoa maoni tuchangie gharama za kuhakikisha uhuru wa Watanzania kutoa maoni kupitia JF haukomeshwi na watawala wachache wanaopenda kukandamiza uhuru wa kutoa maoni.

JF imekuwa mwiba mchungu sana kwa nia dhalimu za wale wote wenye mwelekeo wa kufinya haki za binadamu, unyanyasaji wa watu, utawala wa mabavu na kutofuata sheria, ufisadi, dhuruma na ukandamizaji wa uhuru wa kujieleza. Hatuwezi kukaa kimya dhidi ya vita hii, ni vita yetu, sio vita ya Macence Mello na JF, ni vita ya Watanzania wote wenye kupenda maendeleo na utandawazi. Hii ndio nafasi nzuri ya kuonyesha loyalty yetu kwa JF. IKiwezekana, tungependa kupata mwongozo toka JF wa nini wana JF tunaweza kufanya kusaidia katika hili.
 
Una hoja ya maana sana
Nafikiri kama wenyewe hawa walioimshitaki walivyompa shitaka la kuwekea ngumu upelelezi usifanyike kama kifungu cha 22(1)Cyber crimes Act,2015.

Members wawe wanatoa taarifa za ukweli hasa wanapokuwa wanafichua madudu yanayohusu maslahi ya umma.
 
Back
Top Bottom