Kesi namba 456 ya 2016 JamiiForums vs Jamhuri, Kisutu: Maxence Melo ahukumiwa Mwaka jela au faini ya Tsh. Mil 3. Mwenzake aachiwa huru

Wana Jamii Forum,

Wengi mtakuwa mmeshasikia au kusoma juu ya hukumu katika kesi ya Jamii Forum, ambapo Maxence Mello amehukumiwa kulipa faini ya Tshs 3m au kifungo cha mwaka mmoja. Faini imelipwa.

Wengi wameshindwa kuelewa athari za hii hukumu, na wanaiona katika mapana ya hukumu au faini ya Stsh 3 tu, ambayo hata wengine wameita pesa ya mfukoni.

Lakini suala la kujiuliza ni kama tunaelewa athari za hukumu hii kwa JF hapo mbeleni. Kimsingi, hukumu hii inaweza kuweka precedent kwamba kila wakati serikali isipofurahishwa na thread au post ya mwana JF, inawataka JF kutoa taarifa za mtu aliyeanzisha hiyo thread au kuweka hiyo post.

Sasa najua JF ilianzishwa kwa namna ambayo ilitaka kuzuia suala la JF kulazimishwa kutoa taarifa binafsi za wana JF. Lakini hukumu haitambui hili, kitu ambacho kinamweka Maxence na Jamii Forums katika hali mbaya sana.

Sasa hii ni vita ya Watanzania waote katika kupigania uhuru wa kutoa maoni, hatupaswi kuwaachia JF na Mexence peke yao. Kama kuna uwezekano wa kuikatia rufaa hii hukumu tufanye hivyo, na ikiwezekana utaratibu uwekwe wale wote wenye mwamko wa uhuru wa kutoa maoni tuchangie gharama za kuhakikisha uhuru wa Watanzania kutoa maoni kupitia JF haukomeshwi na watawala wachache wanaopenda kukandamiza uhuru wa kutoa maoni.

JF imekuwa mwiba mchungu sana kwa nia dhalimu za wale wote wenye mwelekeo wa kufinya haki za binadamu, unyanyasaji wa watu, utawala wa mabavu na kutofuata sheria, ufisadi, dhuruma na ukandamizaji wa uhuru wa kujieleza. Hatuwezi kukaa kimya dhidi ya vita hii, ni vita yetu, sio vita ya Macence Mello na JF, ni vita ya Watanzania wote wenye kupenda maendeleo na utandawazi. Hii ndio nafasi nzuri ya kuonyesha loyalty yetu kwa JF. IKiwezekana, tungependa kupata mwongozo toka JF wa nini wana JF tunaweza kufanya kusaidia katika hili.
Wameomba rufani. Hii itakwenda mpaka CA maana hgh court sioni jaji mwenye ujasiri wa kutoa hukumu ya haki!
 
Mbona unaniuliza maswali ya kizushi? Mimi sina nakala ya hukumu. Subiri tuipate. Ila nilisoma kwenye gazeti moja ishu ilikuwa ni ip adress ya mtoa mada. Sasa sina uhakika kama Jf walikataa kutoa au vipi.Na wala sina uhakika kama walikuwa nayo au vipi.
Maswali yangu ni katika ku-expose uhalali au kukosekana kwa uhalali wa hukumu.
 
IKiwa watu ambao wanaikosoa serikali Bungeni wanawekewa kila aina ya vizuizi, na ikiwa serikali imefunga uwanja wa wana siasa kuikosoa serikali kwnye mikutano ya siasa, na ikiwa magazeti yakiandika habari za kuikosa serikali yanafungiwa, ni wapi pengine Watanzania wanaweza kuikosoa serikali yao?

CAG alikosoa serikali ikawa shida, sembuse mimi na wewe? Tutapata wapi uwanja wa kumkosoa Magufuli na serikali yake maka sio JF?

KUmbuka kwamba serikali haipo pale kwa ajili ya mambo yao wenyewe, ipo pale kwa ajili ya wananchi. Kwa hiyo inapaswa kuruhusu wananchi waikosoe kwa uhuru kama kulingana na mtazamo wao,
Huu ni thread muhimu sana kwa leo labda na miaka ijayo mapaka hii hukumu ibatilishwe. Maxence Melo
 
Hukumu za kipuuzi tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Hizi kesi zenye flavor ya kisiasa Mahakimu wanaosimamia sheria siku hizi ni wachache sana. Wengi wanatoa hukumu kwa uoga au kujipendekeza kwa serikali. Hata mwanasheria Mkuu siku hizi anakuwa guarded sana kwenye kuongelea ukweli pale haki isipotendeka. Anaongea kama anaibembeleza serikali imsikilize. Just call a spade spade.

Kwa mfano akiongelea suala la ukosefu wa haki katika kuwanyima dhamana watu. Aliongea utafikiri anaiposa serikali.
 
... mnatakiwa kuwa smart kweli kweli Mkuu. Otherwise hoja zikiwa dhaifu bora msiende maana High Court ikienda kukazia hukumu imekula kwetu mazima.
Majaji wenyewe wapo humu,watasaidia kuiweka vizuri.
 
Kweli waweke namba tuchangie hata kwa visent vyetu tulivyopata kwa kuuza alkasusu.

idumu jf.

Naunga mkono hoja.Huwa tunachangia wanasiasa tu,tunaacha huyu anayetoa mchango mkubwa huo.Ilitakiwa tumsadie hats gharama za mawakili
 
Wana Jamii Forum,

Wengi mtakuwa mmeshasikia au kusoma juu ya hukumu katika kesi ya Jamii Forum, ambapo Maxence Mello amehukumiwa kulipa faini ya Tshs 3m au kifungo cha mwaka mmoja. Faini imelipwa.

Wengi wameshindwa kuelewa athari za hii hukumu, na wanaiona katika mapana ya hukumu au faini ya Stsh 3 tu, ambayo hata wengine wameita pesa ya mfukoni.

Lakini suala la kujiuliza ni kama tunaelewa athari za hukumu hii kwa JF hapo mbeleni. Kimsingi, hukumu hii inaweza kuweka precedent kwamba kila wakati serikali isipofurahishwa na thread au post ya mwana JF, inawataka JF kutoa taarifa za mtu aliyeanzisha hiyo thread au kuweka hiyo post.

Sasa najua JF ilianzishwa kwa namna ambayo ilitaka kuzuia suala la JF kulazimishwa kutoa taarifa binafsi za wana JF. Lakini hukumu haitambui hili, kitu ambacho kinamweka Maxence na Jamii Forums katika hali mbaya sana.

Sasa hii ni vita ya Watanzania waote katika kupigania uhuru wa kutoa maoni, hatupaswi kuwaachia JF na Mexence peke yao. Kama kuna uwezekano wa kuikatia rufaa hii hukumu tufanye hivyo, na ikiwezekana utaratibu uwekwe wale wote wenye mwamko wa uhuru wa kutoa maoni tuchangie gharama za kuhakikisha uhuru wa Watanzania kutoa maoni kupitia JF haukomeshwi na watawala wachache wanaopenda kukandamiza uhuru wa kutoa maoni.

JF imekuwa mwiba mchungu sana kwa nia dhalimu za wale wote wenye mwelekeo wa kufinya haki za binadamu, unyanyasaji wa watu, utawala wa mabavu na kutofuata sheria, ufisadi, dhuruma na ukandamizaji wa uhuru wa kujieleza. Hatuwezi kukaa kimya dhidi ya vita hii, ni vita yetu, sio vita ya Macence Mello na JF, ni vita ya Watanzania wote wenye kupenda maendeleo na utandawazi. Hii ndio nafasi nzuri ya kuonyesha loyalty yetu kwa JF. IKiwezekana, tungependa kupata mwongozo toka JF wa nini wana JF tunaweza kufanya kusaidia katika hili.
kama una hukumu tuwekee hapa tutoe maoni ya rufaa
 
Maswali yangu ni katika ku-expose uhalali au kukosekana kwa uhalali wa hukumu.
Utaratibu hauko hivyo. Subiri hukumu itoke maadam inatuhusu sote wana Jf utaisoma alafu utatapa uhalali gani huyu hakimu alitumia kumhukumu jamaa yetu.
 
Hukumu ya subordinate court siyo precedent
Wana Jamii Forum,

Wengi mtakuwa mmeshasikia au kusoma juu ya hukumu katika kesi ya Jamii Forum, ambapo Maxence Mello amehukumiwa kulipa faini ya Tshs 3m au kifungo cha mwaka mmoja. Faini imelipwa.

Wengi wameshindwa kuelewa athari za hii hukumu, na wanaiona katika mapana ya hukumu au faini ya Stsh 3 tu, ambayo hata wengine wameita pesa ya mfukoni.

Lakini suala la kujiuliza ni kama tunaelewa athari za hukumu hii kwa JF hapo mbeleni. Kimsingi, hukumu hii inaweza kuweka precedent kwamba kila wakati serikali isipofurahishwa na thread au post ya mwana JF, inawataka JF kutoa taarifa za mtu aliyeanzisha hiyo thread au kuweka hiyo post.

Sasa najua JF ilianzishwa kwa namna ambayo ilitaka kuzuia suala la JF kulazimishwa kutoa taarifa binafsi za wana JF. Lakini hukumu haitambui hili, kitu ambacho kinamweka Maxence na Jamii Forums katika hali mbaya sana.

Sasa hii ni vita ya Watanzania waote katika kupigania uhuru wa kutoa maoni, hatupaswi kuwaachia JF na Mexence peke yao. Kama kuna uwezekano wa kuikatia rufaa hii hukumu tufanye hivyo, na ikiwezekana utaratibu uwekwe wale wote wenye mwamko wa uhuru wa kutoa maoni tuchangie gharama za kuhakikisha uhuru wa Watanzania kutoa maoni kupitia JF haukomeshwi na watawala wachache wanaopenda kukandamiza uhuru wa kutoa maoni.

JF imekuwa mwiba mchungu sana kwa nia dhalimu za wale wote wenye mwelekeo wa kufinya haki za binadamu, unyanyasaji wa watu, utawala wa mabavu na kutofuata sheria, ufisadi, dhuruma na ukandamizaji wa uhuru wa kujieleza. Hatuwezi kukaa kimya dhidi ya vita hii, ni vita yetu, sio vita ya Macence Mello na JF, ni vita ya Watanzania wote wenye kupenda maendeleo na utandawazi. Hii ndio nafasi nzuri ya kuonyesha loyalty yetu kwa JF. IKiwezekana, tungependa kupata mwongozo toka JF wa nini wana JF tunaweza kufanya kusaidia katika hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata kama amelipa, kuna ubaya gani tukimrefund jamaa yetu?
Ili kuonyesha solidarity ni vizuri hiyo pesa ikachangwa na kuziba pengo la ilikotoka kulipa faini. Tupe account number au namba ya simu haraka.

Tiba
 
Wekeni utaratibu michango ianze. Mil tatu si kitu tuko wengi sana humu.

Shida sio m3 shida ni jamaa kukutwa na hatia so bila kukata rufaa itamaanisha amekubali so faini ni kama onyo kwa hio from here onwards mko open to the world
 
Kichekesho hata mawaziri wanalitumia ili jukwaa kutukanana na raia wa kawaida.

Ukiwa kiongozi lazima uwe tayari kukosolewa ni wajibu hata kukashifiwa ni kawaida Trump watu wanamkashifu hata wa nje ya marekani pale twitter lakini hajamkamata mtu yeyote

Bongo kuna uchochezi gani? unaweza kuchochea nini hapa wakati nchi haina ugaidi wala haujamtishia rais au raia yeyote? kama kweli serikali ipo serious iwe inawakamata hata wanaowakashifu wapinzani na kuandika uzushi juu yao upinzani kama ni usalama uwe pande zote.

Ukiwa hauna kifua ni bora usiwe kiongozi uzuri jf wameshaweka utalatibu habari ikiwa haieleweki uwa wanafuta faster sasa tatizo lipo wapi mnataka mfanye ufisadi mkwepe kodi tunyamaze?

Rufaa inahitajika
Naanza kutia shaka kama kweli kama akili zako ziko timamu!
 
IKiwa watu ambao wanaikosoa serikali Bungeni wanawekewa kila aina ya vizuizi, na ikiwa serikali imefunga uwanja wa wana siasa kuikosoa serikali kwnye mikutano ya siasa, na ikiwa magazeti yakiandika habari za kuikosa serikali yanafungiwa, ni wapi pengine Watanzania wanaweza kuikosoa serikali yao?

CAG alikosoa serikali ikawa shida, sembuse mimi na wewe? Tutapata wapi uwanja wa kumkosoa Magufuli na serikali yake kama sio JF?

KUmbuka kwamba serikali haipo pale kwa ajili ya mambo yao wenyewe, ipo pale kwa ajili ya wananchi. Kwa hiyo inapaswa kuruhusu wananchi waikosoe kwa uhuru kama kulingana na mtazamo wao,
Beware mkuu. Hali ni tete, maoni sahv tunawambia tu baadhi ya marafiki, tena kwa kuangalia kama anaaminika. Usithubutu kukosoa au kulaumu publicly.
 
Back
Top Bottom