Kesi namba 456 ya 2016 JamiiForums vs Jamhuri, Kisutu: Maxence Melo ahukumiwa Mwaka jela au faini ya Tsh. Mil 3. Mwenzake aachiwa huru

Kesi namba 456 ya mwaka 2016 inawakabili Mkurugenzi wa Jamii Media Ndg. Maxence Melo na mwana hisa mwenzake Mike William itasomwa leo Aprili 08, 2020 mbele ya Hakimu Thomas Simba kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.

Hukumu hii awali ilipangwa kutolewa Novemba 26, 2019 lakini iliahirishwa mara nne (4) kwa kigezo kwamba Hakimu alikuwa hajamaliza kuandika hukumu hiyo. Tarehe nyingine ilizoahirishwa ni Desemba 06, 2019, Januari 22, 2020, Februari 19, 2020, Machi 19, 2020 na Aprili 02, 2020

Historia ya kesi hii

Kampuni ya Oilcom iliandikwa katika mtandao wa Jamii Forums ikidaiwa kukwepa kulipa kodi na kuchakachua mafuta kwenye bandari ya Dar es Salaam.

Baada ya taarifa hizo kuandikwa kwenye mtandao wa Jamii Forums, Polisi waliandika barua kwenda kwa “Mkurugenzi wa Jamii Forum” kuomba taarifa za mtu aliyeandika ujumbe kuhusu Oilcom. Polisi wanadai hawakufanikiwa kupata taarifa hizo ndipo walipoamua kumkamata na kumuhoji Ndg. Maxence Melo na kumfungulia shitaka la kuzuia upelelezi kwa kutokutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi alipotakiwa kutoa taarifa za aliyeandika kuhusu Oilcom kwenye mtandao wa Jamii Forums kinyume na kifungu namba 22(1) cha Sheria ya Makosa ya Mitandaoni ya Mwaka 2015.

Ndg. Maxence Melo alikamatwa mnamo Desemba 13, 2016 na alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Desemba 16, 2016 na kufunguliwa kesi tatu (3) tofauti zenye shitaka moja la kuzuia upelelezi kwa kutokutoa ushirikiano kwa Polisi juu ya taarifa za walioandika kwenye mtandao wa Jamii Forums. Hata hivyo, alijikuta analazimika kupelekwa gereza la Keko kwa siku 3 baada ya kuchelewa kupewa dhamana.

Mapema mwaka 2017 upande wa Jamhuri ulimuongeza Micke William (Mushi) kwenye kesi hizo kama mmoja wa wanahisa wa kampuni ya Jamii Media.

Kuhusu kesi zilizofunguliwa mahakamani

Kesi 3 zilizofunguliwa ni zifuatazo:

Mosi, Kesi namba 456 ya mwaka 2016 ambapo Ndg. Maxence Melo alishtakiwa kama Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Jamii Media kwa kosa la kuzuia upelelezi kwa kutokutoa ushirikiano kwa polisi juu ya taarifa za aliyeandika kuhusu Oilcom kwenye mtandao wa Jamii Forums. Katika nyakati tofauti za usikilizwaji wa kesi hii namba 456 upande wa Jamhuri umewahi kukiri kwamba Micke William aliingizwa kimakosa kwenye kesi hiyo. Aidha, upande huo wa mashtaka mashahidi wote walikiri watuhumiwa walijibu barua zote za polisi wakisema wapo tayari kutoa ushirikiano endapo jinai ya mwanachama wao itabainishwa na jeshi la Polisi.

Pili, Kesi namba 457 ya mwaka 2016 ambapo washitakiwa walituhumiwa kwa kosa la kuzuia upelelezi wa Polisi kwa kutokutoa ushirikiano juu ya taarifa za aliyeandika kuhusu kampuni za CUSNA Investment na Ocean Link kudaiwa kukwepa kulipa kodi kwenye Bandari ya Dar es Salaam na kunyanyasa wafanyakazi wa kitanzania.

Uamuzi wa shauri hilo (shauri namba 457) ulitolewa Juni 01, 2018 ambapo Hakimu Godfrey Mwambapa aliamua kwamba Washitakiwa hawakuwa na kesi ya kujibu na hivyo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliwaachia huru.

Katika kesi hiyo pia, Polisi walitaka JamiiForums iwapatie taarifa za mwanzisha mada KWAYU na mchangiaji mmoja AMRISHIPURI ili waweze kuwakamata na kuwahoji kutokana na ukiukwaji wa taratibu. JamiiForums haikutoa taarifa binafsi za wanachama wake kwa kuamini kuwa chanzo hiki cha taarifa kilikuwa na nia njema hivyo kutaka kwanza iwepo Hati ya Mahakama inayoridhia kukamatwa kwa mhusika na kuelezwa kosa lake.

Tatu, Kesi namba 458 ya mwaka 2016 ambapo washtakiwa wanatuhumiwa kwa kosa la kuzuia upelelezi kwa kutokutoa ushirikiano kwa Polisi kuhusu Benki ya CRDB ambapo Polisi ilimtaka Mkurugenzi wa “Jamii Forum” kutoa taarifa kuhusu Wanachama wawili wa Mtandao wa JamiiForums walioandika kuhusu Benki ya CRDB.

Taarifa zilizotakiwa ni za Wanachama walioanzisha mijadala iliyosomeka "Charles Kimei (CRDB) jiuzulu, kashfa ya kontena, tiketi TFF, wanafunzi na ujambazi CRDB" mjadala unaodaiwa kuanzishwa tarehe 18 Januari 2016 pamoja na "Wizi wa Benki ya CRDB - Part II" unaodaiwa kuanzishwa Machi 11, 2015.

Taarifa za Wanachama ambazo zilitakiwa kutolewa ni IP-Address, barua pepe, Majina Halisi ya Wanachama hao. Kesi hii bado inaendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Huruma Shaidi na haijawa na shahidi tangu Novemba 2018.

=======

UPDATES:

========
View attachment 1412705
KESI NAMBA 456 (JAMHURI v JAMIIFORUMS): MELO AKUTWA NA HATIA HUKU MIKE AKIACHIWA

Maxence Melo amekutwa na hatia na kuhukumiwa faini ya milioni 3 au kifungo cha mwaka 1 jela
View attachment 1412852
Aidha Mike Mushi amekutwa hana hatia na kuwa aliungwa kwenye kesi kimakosa

Mahakaka ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu, Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa JamiiForums, Maxence Melo(40) kulipa faini ya Sh3 milioni au kwenda jela mwaka mmoja, baada ya kutiwa hatiani katika shitaka moja la kuzuia jeshi la polisi kufanya uchunguzi.

Pia mahakama hiyo imemuachia huru Mike Mushi ambaye ni mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo ya jinai namba 456/2016.

Mushi ameachiwa huru baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha shtaka dhidi yake.

Uamuzi huo umetolewa leo Jumatano Aprili 8, 2020 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakamani hiyo, Thomas Simba.

UPDATE:
Tayari faini imeshalipwa na Maxence Melo ameachiwa huru.

Hukumu dhidi yangu: Shukrani kwa watanzania – Maxence Melo - JamiiForums

Kujua kesi Zilizoisha na zile zinazoendelea JamiiForums dhidi ya Jamhuri, soma;

Muendelezo wa Kinachojiri Kisutu: Kesi za Jamhuri dhidi ya JamiiForums - JamiiForums
View attachment 1412640
Huyo sajenti anayemueskot Mello hapo mahakamani(aliyepo mbele ya Mello) na huyo Koplo aliyepo nyuma ya Mello ni member wazuri tu humu, utekelezaji tu wa majukum ya kazi(Maelekezo) ya viongozi, ila wanatamani Sana kumwambia Mello akaze kamba asirudi nyuma, JF mbele kwa mbele
 
Katukanwa matusi gani?Who is him by the way?
Tuache na Jf yetu kama unaona mambo ya ukweli wanayoandika watu ni matusi.Una bahati mie si moderator ningekupiga life ban

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio ujue hao vikaragosi wana anakili za sisimi, wanaponda halafu bado wanashinda humuhumu, halafu huyo kibwengo hajui hata kesi inahusu nini
 
nahofia hii hukumu inaweka precedent ya kufungua pandora box kwa serkali dhidi ya uhuru wa kutoa na kupata habari. ukubwa wa tatizo utakuwa pale hii njia rafiki ikiachwa, haijuliukan itabuniwa inayodhibitiwa kias gani. isije kuwa yale ya paka kumbana chumban ukiwa humo humo!
 
Tutachanga tu hata buku buku kuliko kuharibu image ya jf.Hizo kesi ndizo zimeifanya jf kuwa maarufu zaidi
 
Kesi namba 456 ya mwaka 2016 inawakabili Mkurugenzi wa Jamii Media Ndg. Maxence Melo na mwana hisa mwenzake Mike William itasomwa leo Aprili 08, 2020 mbele ya Hakimu Thomas Simba kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.

Hukumu hii awali ilipangwa kutolewa Novemba 26, 2019 lakini iliahirishwa mara nne (4) kwa kigezo kwamba Hakimu alikuwa hajamaliza kuandika hukumu hiyo. Tarehe nyingine ilizoahirishwa ni Desemba 06, 2019, Januari 22, 2020, Februari 19, 2020, Machi 19, 2020 na Aprili 02, 2020

Historia ya kesi hii

Kampuni ya Oilcom iliandikwa katika mtandao wa Jamii Forums ikidaiwa kukwepa kulipa kodi na kuchakachua mafuta kwenye bandari ya Dar es Salaam.

Baada ya taarifa hizo kuandikwa kwenye mtandao wa Jamii Forums, Polisi waliandika barua kwenda kwa “Mkurugenzi wa Jamii Forum” kuomba taarifa za mtu aliyeandika ujumbe kuhusu Oilcom. Polisi wanadai hawakufanikiwa kupata taarifa hizo ndipo walipoamua kumkamata na kumuhoji Ndg. Maxence Melo na kumfungulia shitaka la kuzuia upelelezi kwa kutokutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi alipotakiwa kutoa taarifa za aliyeandika kuhusu Oilcom kwenye mtandao wa Jamii Forums kinyume na kifungu namba 22(1) cha Sheria ya Makosa ya Mitandaoni ya Mwaka 2015.

Ndg. Maxence Melo alikamatwa mnamo Desemba 13, 2016 na alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Desemba 16, 2016 na kufunguliwa kesi tatu (3) tofauti zenye shitaka moja la kuzuia upelelezi kwa kutokutoa ushirikiano kwa Polisi juu ya taarifa za walioandika kwenye mtandao wa Jamii Forums. Hata hivyo, alijikuta analazimika kupelekwa gereza la Keko kwa siku 3 baada ya kuchelewa kupewa dhamana.

Mapema mwaka 2017 upande wa Jamhuri ulimuongeza Micke William (Mushi) kwenye kesi hizo kama mmoja wa wanahisa wa kampuni ya Jamii Media.

Kuhusu kesi zilizofunguliwa mahakamani

Kesi 3 zilizofunguliwa ni zifuatazo:

Mosi, Kesi namba 456 ya mwaka 2016 ambapo Ndg. Maxence Melo alishtakiwa kama Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Jamii Media kwa kosa la kuzuia upelelezi kwa kutokutoa ushirikiano kwa polisi juu ya taarifa za aliyeandika kuhusu Oilcom kwenye mtandao wa Jamii Forums. Katika nyakati tofauti za usikilizwaji wa kesi hii namba 456 upande wa Jamhuri umewahi kukiri kwamba Micke William aliingizwa kimakosa kwenye kesi hiyo. Aidha, upande huo wa mashtaka mashahidi wote walikiri watuhumiwa walijibu barua zote za polisi wakisema wapo tayari kutoa ushirikiano endapo jinai ya mwanachama wao itabainishwa na jeshi la Polisi.

Pili, Kesi namba 457 ya mwaka 2016 ambapo washitakiwa walituhumiwa kwa kosa la kuzuia upelelezi wa Polisi kwa kutokutoa ushirikiano juu ya taarifa za aliyeandika kuhusu kampuni za CUSNA Investment na Ocean Link kudaiwa kukwepa kulipa kodi kwenye Bandari ya Dar es Salaam na kunyanyasa wafanyakazi wa kitanzania.

Uamuzi wa shauri hilo (shauri namba 457) ulitolewa Juni 01, 2018 ambapo Hakimu Godfrey Mwambapa aliamua kwamba Washitakiwa hawakuwa na kesi ya kujibu na hivyo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliwaachia huru.

Katika kesi hiyo pia, Polisi walitaka JamiiForums iwapatie taarifa za mwanzisha mada KWAYU na mchangiaji mmoja AMRISHIPURI ili waweze kuwakamata na kuwahoji kutokana na ukiukwaji wa taratibu. JamiiForums haikutoa taarifa binafsi za wanachama wake kwa kuamini kuwa chanzo hiki cha taarifa kilikuwa na nia njema hivyo kutaka kwanza iwepo Hati ya Mahakama inayoridhia kukamatwa kwa mhusika na kuelezwa kosa lake.

Tatu, Kesi namba 458 ya mwaka 2016 ambapo washtakiwa wanatuhumiwa kwa kosa la kuzuia upelelezi kwa kutokutoa ushirikiano kwa Polisi kuhusu Benki ya CRDB ambapo Polisi ilimtaka Mkurugenzi wa “Jamii Forum” kutoa taarifa kuhusu Wanachama wawili wa Mtandao wa JamiiForums walioandika kuhusu Benki ya CRDB.

Taarifa zilizotakiwa ni za Wanachama walioanzisha mijadala iliyosomeka "Charles Kimei (CRDB) jiuzulu, kashfa ya kontena, tiketi TFF, wanafunzi na ujambazi CRDB" mjadala unaodaiwa kuanzishwa tarehe 18 Januari 2016 pamoja na "Wizi wa Benki ya CRDB - Part II" unaodaiwa kuanzishwa Machi 11, 2015.

Taarifa za Wanachama ambazo zilitakiwa kutolewa ni IP-Address, barua pepe, Majina Halisi ya Wanachama hao. Kesi hii bado inaendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Huruma Shaidi na haijawa na shahidi tangu Novemba 2018.

=======

UPDATES:

========
View attachment 1412705
KESI NAMBA 456 (JAMHURI v JAMIIFORUMS): MELO AKUTWA NA HATIA HUKU MIKE AKIACHIWA

Maxence Melo amekutwa na hatia na kuhukumiwa faini ya milioni 3 au kifungo cha mwaka 1 jela
View attachment 1412852
Aidha Mike Mushi amekutwa hana hatia na kuwa aliungwa kwenye kesi kimakosa

Mahakaka ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu, Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa JamiiForums, Maxence Melo(40) kulipa faini ya Sh3 milioni au kwenda jela mwaka mmoja, baada ya kutiwa hatiani katika shitaka moja la kuzuia jeshi la polisi kufanya uchunguzi.

Pia mahakama hiyo imemuachia huru Mike Mushi ambaye ni mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo ya jinai namba 456/2016.

Mushi ameachiwa huru baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha shtaka dhidi yake.

Uamuzi huo umetolewa leo Jumatano Aprili 8, 2020 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakamani hiyo, Thomas Simba.

UPDATE:
Tayari faini imeshalipwa na Maxence Melo ameachiwa huru.

Hukumu dhidi yangu: Shukrani kwa watanzania – Maxence Melo - JamiiForums

Kujua kesi Zilizoisha na zile zinazoendelea JamiiForums dhidi ya Jamhuri, soma;

Muendelezo wa Kinachojiri Kisutu: Kesi za Jamhuri dhidi ya JamiiForums - JamiiForums
View attachment 1412640
POLEMKUU SIJUU HUYU ALIEKUJA NA KUTOKA KILASIKU AKAACHIWA HURU NAE ANALIPWA.AMA
 
Tutachanga tu hata buku buku kuliko kuharibu image ya jf.Hizo kesi ndizo zimeifanya jf kuwa maarufu zaidi
Naunga Mkono iwekwe a/c tuchangie jamani hata hizo milioni 3 zilizolipwa kwenye faini
au urudi ule utaratibu wa kupewa beji, za Diamond, Platinum nk
Jf inaendeshwa kwa pesa la sivyo isingekuwepo hewani, au hata malipo ya Mawakili kutetea hiyo kesi
 
Milioni 3 ni watu elf 3 wakichanga buku buku yatosha.Jf pekee ndo platform huru angalau wawezapata habari kamili zisizochujwa unachuja mwenyewe tofauti na huko kwingine unapata cooked information
 
Hivi kwa kesi hii Melo anaweza kugombea ubunge na uraisi?
Kisheria Mtu aliyefungwa zaidi ya miezi 6 hawezi gombea Uongozi kisiasa Udiwani, Ubunge nk
Max amelipa faini badala ya kifungo lkn amekata rufaa huenda ikaclear hilo la adhabu na akawa huru
Maxcense asigombee uongozi wa kisiasa kwani JF itasambaratika, tumewaona wengi walioingia huko wamezimika kutetea ukweli
 
Naamini ipo siku udhalimu na ukandamizaji huu utafika mwisho. Mungu akiwa upande wetu wanaJF ni nani aliye juu yetu? Hakuna.
 
Back
Top Bottom