Kesi ya Abdallah Zombe: Mashitaka, hatia, hukumu na yanayojiri

Kesi ya Abdallah Zombe: Mashitaka, hatia, hukumu na yanayojiri

Jamani any update?
Wazee wa mahakama wameitaka mahakama kutomtia hatiani na achiliwe huru Zombe, kwa kile walichodai kuwa Zombe hakuwa eneo la tukio la mauhaji.
 
Wazee wa mahakama wameitaka mahakama kutomtia hatiani na achiliwe huru Zombe, kwa kile walichodai kuwa Zombe hakuwa eneo la tukio la mauhaji.

Huu ni upuuzi, ripoti ya marehemu Lema ilimtaja Zombe kabisa jinsi alivyohusika! bado wanamtetea nini huyu?
 
Huu ni upuuzi, ripoti ya marehemu Lema ilimtaja Zombe kabisa jinsi alivyohusika! bado wanamtetea nini huyu?

unajua kisheria Coplo Lema alitakiwa kuutoa ushahidi ule NDANI YA MAHAKAMA,ndipo ungetambulika.sasa wakati anajiandaa kwa hilo WAKAMUWEKA SAWA-akakata kauli,hakutamka lolote mpaka alipokutwa na mauti!
 
Leo asubuhi nimesoma Gazeti la habari leo na kukuta kichwa cha habari kinasema ''Zombe Apumua'' nilipoingia ndani zaid ya habari hiyo nikaona jinsi wazee wa baraza walivyosema juu ya zombe na mshitakiwa wa 13 kuwa hawana hatia ila wengine saba wana hatia. sasa hapa wana jf wenzangu hasa mlioko huko nyumbani napenda kujua kama wazee wa baraza wana influence kubwa ya kufanya zombe aachiwe huru. na pia jaji aanaweza kupuuza waliyosema wazee?
 
Kesi zingine huwa hatusikii sana ushawishi wa hao wazee. Lakini kwa vile hukumu inategemea ushahidi uliotolewa, basi judge atahukumu kutokana na huo ushahidi na siyo ushauri wa wazee wa mahakama.

Mimi naamini hukumu itafuata misingi ya sheria na siyo 'sympathy' ya watu fulani. Na judge atakapohukumu pia ata'cite' kesi kadhaa ambazo ziliamriwa katika mazingira kama hayo ya mauaji.
 
Wazee hao wababaishaji na inaelekea wana tegemea zaidi sentiments zao kuliko ushahidi uliotolewa.
Ni wazi kuwa msukumo wa mauaji ni kunyakua pesa, kitu ambacho ni sawa sawa na umamluki wa kuwa timia askari wadogo kwa faida yake.
Kwamba Zombe hakuwa na habari kwa mauaji yaliyofanyika ni ukwepaji wa ukweli.
 
Tatizo ni mfumo mbovu wa mahakama zetu au wanasheria wetu.Waendesha mashtaka wamefanya kusudi kutomuhusisha Zombe na mauaji kwani kila walipokuwa wanaendesha kesi walikuwa wakitumia neno 'inaonekana Zombe amehusika'.Katika kiswahili neno Kuonekana inamaanisha ni kwa macho lakini kimazingira Zombe hakuwepo kule polini yalipofanyika mauaji hivyo dhana ya inaonekana inatoweka kabisa na kufanya wazee wa baraza watoe hekima yao.Walimu wa sheria waelekezeni vizuri vijana wenu jinsi ya kutunga na kutetea kesi mahakamani ndio maana tunasikia eti waendesha mashitaka wamekosea jinsi ya kumfungulia kosa Amartus LIUMBA na kusababisha kuachiwa huru na mahakama,kama si polisi kumkamata tena na kumfungulia kesi nyingine LIUMBA angekuwaa anapeta uswahilini.Kazi tunayo!
 
Kuhusu Wazee wa Baraza, Tazama Sheria mbili hapo chini zinasemaje:
Magistrate's Courts Act, Cap. 11, R.E. 2002.
6. Constitution of magistrates' courts
(1) Subject to the provisions of section 7, a magistrates' court shall be duly constituted when held by a single magistrate, being–
(a) in the case of a primary court, a primary court magistrate;
(b) in the case of a district court, a district magistrate resident or a magistrate;
(c) in the case of a court of a resident magistrate, a resident magistrate.
(2) Notwithstanding the provisions of subsection (1), where jurisdiction is conferred on a district court only when held by a magistrate of a particular description, such court shall not be duly constituted for the exercise of such jurisdiction unless held by a magistrate of that description.
(3) Where two or more magistrates of the same description are assigned to a particular magistrates' court each may hold sittings of the court concurrently with the other or others.
(4) Notwithstanding the foregoing provisions of this section, the Chief Justice may direct two or more magistrates of the same or other appropriate description to sit for the hearing and determination of any proceeding or any category thereof, and in any such case the court shall not be duly constituted for such proceeding nor any proceeding of such category, unless it is composed of the number and description of magistrates so directed.
(5) In any case where any proceeding is directed to be heard and determined by two or more magistrates, the same shall be determined in accordance with the opinion of the majority and if the court is equally divided the proceedings shall be dismissed.
[PCh11s7]7. Assessors
(1) In every proceeding in the primary court, including a finding, the court shall sit with not less than two assessors.
(2) All matters in the primary court including a finding in any issue, the question of adjourning the hearing, an application for bail, a question of guilt or innocence of any accused person, the determination of sentence, the assessment of any monetary award and all questions and issues whatsoever shall, in the event of difference between a magistrate and the assessors or any of them, be decided by the votes of the majority of the magistrates and assessors present and, in the event of an equality of votes the magistrate shall have the casting vote in addition to his deliberative vote.
(3) In any proceeding in any other magistrates' court in which any rule of customary or Islamic law is in issue or relevant the court may, and when directed by an appropriate judicial authority shall, sit with an assessor or assessors; and every such assessor shall be required, before judgment, to give his opinion as to all questions relating to customary or Islamic law in issue in, or relevant to, the proceeding; save that in determining the proceeding the court shall not be bound to conform with the opinion of the assessors.

The Criminal Procedure Act, Cap. 20, R. E. 2002.
298. Delivery of opinion by assessors and giving of judgment
(1) When the case on both sides is closed, the judge may sum up the evidence for the prosecution and the defence and shall then require each of the assessors to state his opinion orally as to the case generally and as to any specific question of fact addressed to him by the judge, and record the opinion.
(2) The judge shall then give judgment, but, in doing so, shall not be bound to conform to the opinions of the assessors.
(3) If the accused person is convicted, the judge shall pass sentence on him according to law.
(4) Nothing in this section shall be construed as prohibiting the assessors, or any of them, from retiring to consider their opinions if they so wish or, during any such retirement or at any time during the trial, from consultation with one another.
 
ALELUYA!

JE HILI LA WAZEE WA BARAZA TUNALITAFAKARI VIPI? HOFU YANGU NI PALE HAWA WATU WATAKAPO KUWA HURU URAIANI ITABIDI WAWE NA ULINZI WA MASAA 24. KWANI MAMBO HAYA YAMEFANYIKA KIMWILI

Kiroho jambo hili linahitaji zaidi roho ya msamaha kama vile Yesu alivyotusamehe sisi na sisi ambao misiba hii ilitugusa sana kwa namna moja au nyingine tuwe tayari kusamehe na tumwachie mfalme wa haki afanye hukumu ya kweli peke yake.
N mara nyingi pigania haki kwa akili zetu na tumeishia kuzikosa, lakini pale tu unapoamua kusamehe na kumruhusu Mungu yeye anafanya maamuzi kwa jinsi ya tofauti na tunavyofikiri.
Ebu Huyu Roho Mtakatifu atusaidie atupe ufahamu wakutatua mambo na jina la bwana lihimidiwe!
Mbarikiwe na bwana.
 
Tatizo ni mfumo mbovu wa mahakama zetu au wanasheria wetu.Waendesha mashtaka wamefanya kusudi kutomuhusisha Zombe na mauaji kwani kila walipokuwa wanaendesha kesi walikuwa wakitumia neno 'inaonekana Zombe amehusika'.Katika kiswahili neno Kuonekana inamaanisha ni kwa macho lakini kimazingira Zombe hakuwepo kule polini yalipofanyika mauaji hivyo dhana ya inaonekana inatoweka kabisa na kufanya wazee wa baraza watoe hekima yao.Walimu wa sheria waelekezeni vizuri vijana wenu jinsi ya kutunga na kutetea kesi mahakamani ndio maana tunasikia eti waendesha mashitaka wamekosea jinsi ya kumfungulia kosa Amartus LIUMBA na kusababisha kuachiwa huru na mahakama,kama si polisi kumkamata tena na kumfungulia kesi nyingine LIUMBA angekuwaa anapeta uswahilini.Kazi tunayo!

'Inaonekana Zombe amehusika' - it seems Zombe has fully participated or it appears that Zombe has fully participated. Yaani, kwenye ushahidi ambao siyo 'direct' kwa vile yeye hakuua kwa kushika silaha, upande wa mashtaka hauwezi kuepa kutumia lugha ya namna hiyo kwa vile ushahidi unaomhusisha Zombe na kosa lenyewe siyo 'direct' bali 'circumstancial'.

'Circumstancial evidence' ni pale mshitakiwa anapokuwa ameshiriki kutenda kosa bila yeye mwenyewe kuonekana ametenda ila mazingira kwa jinsi gani kosa limetendeka yanamhusisha moja kwa moja. Hii ni pamoja na nia ya kutenda kosa, mipangilio yake nk.

Askari wa cheo cha juu anapomwamru aliye chini yake kutekeleza amri fulani, kama ikitokea kuwa haikuwa amri halali naye anashiriki kutenda hilo kosa kwa vile bila amri yake kwa wakati huo kusingetendeka kosa hilo kwa namna lilivyotendeka.

Mimi sitaki kukata tamaa kabla mahakama haijamua kesi hii na hata kama mahakama itamua kitu ambacho Jamhuri haitaridhika nacho bado kuna nafasi ya kukata rufaa.
 
ALELUYA!

JE HILI LA WAZEE WA BARAZA TUNALITAFAKARI VIPI?
Na inabidi kulitafakari wka makini sana kwani kuna tofauti kubwa kati ya ushahidi uliotolewa mahakamani na ushabiki unaendelea kwenye mahakama zetu huku mitaani
 
Leo asubuhi nimesoma Gazeti la habari leo na kukuta kichwa cha habari kinasema ''Zombe Apumua'' nilipoingia ndani zaid ya habari hiyo nikaona jinsi wazee wa baraza walivyosema juu ya zombe na mshitakiwa wa 13 kuwa hawana hatia ila wengine saba wana hatia. sasa hapa wana jf wenzangu hasa mlioko huko nyumbani napenda kujua kama wazee wa baraza wana influence kubwa ya kufanya zombe aachiwe huru. na pia jaji aanaweza kupuuza waliyosema wazee?

Kwa mtazamo wangu mimi, naona Zombe hawezi kukosa hatia wakati inasemakena ndiye aliyekuwa anatoa maagizo kwa Bageni nini kifanyike. Huwezi kumtia hatia Bageni, na wakati huo huo unamwachia Zombe... Zombe hakuhusika moja kwa moja katika Kesi. HAkushika silaha na kuwaua washitakiwa, bali aliwauwa kwa kuamrisha wauae. Na kwenye jeshi swala la amri ndiyo kazi za kila siku. Bageni hakuwa na sababu ya kutotekeleza maelekezo ya Kamishna Msaidizi wa Polis kwa kipindi hicho (Bwana Zombe).

Kwa mfumo wetu wa Mahakama, sidhani kama WAZEE WA BARAZA wanaweza kutengua ukweli huu (kwamba Zombe ni mshitakiwa namba 1, na ana HATIA).... Nafasi kubwa bado anayo MHESHIMIWA JAJI MASATI, ambaye ndio anasikiliza kesi hii.... Anaweza akakubaliana na baraza, au akaamua tofauti vile vile...

MAMA NASALI NA KUMWOMBEA JAJI, ATOE MAAMUZI YA HAKI NA SI KUSIKILIZA UPANDE MMOJA. WALIOUWA MASKINI HAWAKUWAHI KUWA MAJAMBAZI NA WAKAZI WALIO WENGI WA MAHENGE/ULANGA AMBAKO MAREHEMU WATOKA WAMETHIBITISHA NA WATAENDELEA KUTHIBITISHA....

HAPO KWA KWELI LAZIMA HAKI ITENDEKE KWA KWELI.......
NINAOMBA WANA JF MNIUNGE MKONO KWA HILO..........
 
wauaji wa kimbari kule rwanda waliohukumiwa si wale tu walioshika mapanga hata akina Akayesu, mameya.
 
Hata mimi ningekuwa Mzee wa baraza ningetoa ushauri huo huo. Upande wa mashtaki ulishindwa kabisa kuthibitisha kwamba Zombe alihusika kwa namna yeyote. Summary ya upande wa Jamhuri umekuwa na hoja moja tu kwamba Zombe alihusika kama mshirika wa mauaji yaliyopangwa na kundi (jama). Hata hivyo walishindwa kuthibitisha juu ya hiyo jama.

Maeneo ambayo yangemfunga Zombe ni:-

a) kuwapongeza askari wauaji:
Hata hivyo suala la Askari kupongezwa ni la kawaida, upande wa Serikali umeshindwa kuthibitisha pasipo shaka kwamba pongezi hizo hazikuwa za kawaida.

b) kuwanyanyasa ndugu wa marehemu walipoenda kutambua miili mhimbili na polisi kati:
Hapa Serikali imeshindwa kujenga hoja inayoeleweka na kuonyesha unyama alioufanya Zombe ili kuunganisha kwamba alitaka kuficha ukweli kwa kuwanyamazisha ndugu. Ushahidi wa jambo hili haukupewa uzito kabisa.

c) Zombe kutoa amri ya kuua:
Shahidi mzuri wa Serikali ktk hili alikuwa ni Afande Bageni (wa Osterbay), Marehemu Lema na wale wawili waliokimbia (nasikia aliwachinyia baharini). Hivyo, Serikali kukosa ushahidi mzuri wa hawa jamaa, unamuondoa Zombe kwenye kesi.

d) Kuwafundisha askari wauaji namna ya kujieleza na kuficha ukweli
Pia ushahidi wa vikaratasi alivyo andika Zombe ulikuwa mhimu, hao askari wanaposema Zombe alitufundisha namna ya kujitetea bila kutoa vikaratasi husika au ushahidi mwingine, unaweza kuwa ni uongo.

Kinachobaki sasa ni Afande Bageni kuwa ndo alikuwa key player wa movie nzima. Hata hivyo Zombe hawezi kuishi kwa raha uraiani, atakuwa mzee wa mikosi tu, damu nzito kuliko maji. Labda atubu na kuokoka.
 
Naona muelekeo ni kama wa kesi ya O. J. Simpson kwa tuhuma za mauaji ya mke wake Nikole mwaka 1994. Simpson alishinda kesi ile nzito japo rufaa ilimtia hukumu ndogo.

Sina kumbukumbu nzuri wanaokumbuka wanaweza kunisaidia.
 
True hapa kukiwa na kesi ndogo inayohusika maybe na uzembe wa zombe alipokaimu u-RPC na kusababisha mauaji husika atapatwa na kosa tu. Kama RPC alipaswa kujiridhisha kama tukio hilo limeandikishwa katika kituo cha polisi na alipokwenda Urafiki kushughulikia upotevu wa fedha, alipaswa kujua watuhumiwa wako wapi. Alipaswa kujua mazingira ya vifo pale alipoambia (Sinza posta) na juu ya hali za maiti. So, kuna makosa mengi ya kiutendaji ambayo anaweza kutiwa hatiani.
 
Mambo ya Zombe kwa mujibu wa sheria yetu bado ni mazuri tuu.
Ili utiwe kosa litendeke, lazima kuwepo kwa mambo mawili, 1 'mens reus.'- nia ya kutenda koso na 2.'actus reus' -kitendo chenyewe cha kutekeleza kosa.
Kwa sheria yetu ni jukumu la jamuhuri kuthibitisha hayo mawili bila mashaka, kitu ambacho hakikuthibitishwa kwa Zombe.
 
Inawezekana hayo mawili hayakuthibitishwa kwa 'direct evidence'. Lakini kwa jinsi episode nzima ilivyoenda ni dhahiri Zombe alikuwa na nia mbaya ya kuwamaliza hao wafanyabiashara na alishiriki vizuri katika kupanga na kuhakikisha huo mpango unafanikiwa.

Kama kwa yote hayo hatakuwa na hatia, ina maana kesi hiyo itakuwa 'precedent' kwa kesi zingine kama hiyo na itaweza kuongeza maovu nchini kwa jeshi hilo kuliko kutoa ulinzi kwa raia na mali zao.

By the way, hivi kuna shahidi yeyote aliweza kumtetea Zombe kwa kusema, mfano, siku hayo yote yanatokea Zombe alikuwa amelazwa au hakuwepo nchini na hivyo hakushiriki kosa kwa namna yoyote ile?
 
Back
Top Bottom