Kesi ya Abdallah Zombe: Mashitaka, hatia, hukumu na yanayojiri

Wengi hawataki kujua hili!
 
i nadhani wamevuna walichopanda na waandishi wa TZ ni wa hovyo hovyo
 
Maneno yako yapo juu ya mstari, aidha Watz wengi nao ni wavivu wa kusoma mambo kwa kina.
 
Hapa TZ hakuna waandishi wa habari ila wapo wambea na wazandiki,wadaku wa mambo ya watu tuu.Hawajuhi lolote katika uandishi isipokuwa kuomba tips kila waitwapo na mafisadi,hata maudhui ya taaluma wameipotosha kwa kupewa rushwa ndogondogo.Yaani imefikia mmbea wa habari wa TZ hasipopewa hongo basi atakuchukia na kukuharibia jina lako kwa kila jamii kisa choo hajakiona.Adhabu kubwa itawafikia waandishi na mafarisayo kwa kuaharibu habari njema na kutia utumbo wao ili waweze kwenda ******,aibu kubwa.Angalia habari zao nyingi ni kusikia mtu kamchungulia mwenzie ******,kakamatwa ugoni,kavunja yai la kuku yaani utumbo mtupu,hakuna waandishi hapa ila uozo tuu.
 
zombe ana nafasi kubwa sana kuyashitaki magazeti yote yaliyokuwa yanaandika upendeleo katika kesi yake

Zombe yashitaki magazeti uyadai fidia ya mamilioni ya fedha kwa kosa la kukukashifu na kukudhalilisha katika jamii iwe fundisho kwao na upate kiinua mgongo chako. Na umaarufu ulioupata ugombee ubunge.
 
zombe ana nafasi kubwa sana kuyashitaki magazeti yote yaliyokuwa yanaandika upendeleo katika kesi yake

Zombe yashitaki magazeti uyadai fidia ya mamilioni ya fedha kwa kosa la kukukashifu na kukudhalilisha katika jamii iwe fundisho kwao na upate kiinua mgongo chako. Na umaarufu ulioupata ugombee ubunge.
 
Bwana Barubaru ebu nimnukuu Judge Masatu kwenye The Citizen ya leo. "In the absence of the actual perpetrators, the case against the accused remains that of strong suspicion, which is not sufficient to obtain a conviction". Haina maana kwamba washitakiwa hawakuhusika na mauaji ya wafanyabiashara na teksi dreva ila ushahidi haukutosha. Tena Judge Masatu anaendelea kusema; " The circumstantial and direct evidence, of course, do not link the second accused (Mr. Bageni) with the actual killings of the victims. What is clear is that it establishes that he was present at Pande Forest and might have been privy to the killings and knew who commited them. Anaedelea " I have established that the second accused (Bageni) was present at the scene of the crime but did not prevent the commission of the crime but there is no evidence that he procured, aided or abbeted any of the other accused persons in committing the murders". Oh lala! Kina Zombe wameshinda kesi ya mauaji kwa vile hakuna ushaidi wa kutosha kwamba walihusika lakini hata Judge mwenyewe anakiili kwamba wengine kama Bageni walikuwepo na walishuhudia tukio hilo! Kushinda kesi mahakamani ni jambo moja. Kushinda kesi mioyoni mwa umma (hearts and minds) ni jambo lingine. Kuna mtu/watu waliwauwa kina Chigumbi na wenzake na Zombe na genge lake walihusika kwa namna moja au nyingine.
 
Kwa bahati mbaya mi si mwanasheria wala si mwandishi wa habari. Najiuliza Nikitarajia jibu lenu wanajamii. Hivi ile tume ya rais chini ya jaji Kipenka ilimdananya rais? Manake nahisi waandishi wetu inawezekana walimhukumu Zombe na wenzake kwa kuwa tayari Tume ya jaji Kipenka ilishawahukumu kiaina. Kipenka ni Jaji, na Masati ni Jaji. Jaji na Jaji wanapotofautiana, kwanini waandishi wetu wasikengeuke? Tusiwalaumu bure waandishi wetu! Natoa hoja!
 
.

ByaseL,

Mimi sipingani kabisa na hukumu ya Jaji. kwa bahati mimi nina taaluma zote mbili za Sheria na uandishi wa habari.

Nilichobainisha mimi ni kuwa WAANDISHI WA HABARI WA MAGAZETI YA HUKO TANZANIA YALISHA MUHUKUMU ZOMBE NA ENZAKE KUWA NI WAUAJI NALAZIMA WAFUNGWE, NA WALITAKA JAJI AWE KAMA RUBBER STAMP TU. SASA HIYO NI KINYUME CHA MAADILI YA UANDISHI.

Mwandishi anatakiwa kuripoti au kuandika kitu vile kilivyo bila kuongeza au kupunguza au kueleza yale matakwa yake. sasa waandishi wa huko Tanzania waliya muhukumu. sasa nikizungumza kisheria. Zombe ana nafasi nzuri sana kuyashitaki magazeti hao na kudai fidia.

hakika sheria inataka uthibitisho pasipo shaka yoyote kuwa walifanya tendo hilo. Na kwa maamuzi ya jaji kutokana na ushahidi ulioletwa na serikali walishindwa kuthibitisha ushiriki wao katika mauaji hayo.
 
Let hope that God will do something on this. If its true they didnt kill anyone. Damu ya mtu haiendi hivi hivi.

These guys will regret to free him with confindence that he is clean while not.
 
wabongo bwana mara wote sasa mnamshabikia ZOMBE?kazi ipo tanzania yani huu usingizi sijui kama tutaamka,ngoja nikatandike box langu mie nshachoka na hizi blaah blaaaah.
 


wewe inaonekana hujui hata nini maana ya mwenendo wa kesi na mashtaka. Waandishi wa habari hawana kosa na wako sahihi kwa sababu walikuwa wanaripoti case proceedings (mwenendo wa kesi) na siyo mashtaka. kama wangeandika mashtaka, hapo kuna cha kuwalaumu lakini walikuwa wanaandika ambacho hata wewe ukiwa unapita barabarani unakisikia jaji akiongea tena kwenye vipaza sauti.

Kingine nikushauri tu kwamba, wakati haya yanajiri sisi tulio majirani tunajua nini kilitokea, kwa hiyo mshangao wa jamii ni kuona uamuzi wa mahakama unakuja kinyume, ingawa hakuna anayeweza kupingana na uamuzi wa mahakama, labda kukata rufaa.

Kwa hiyo ndugu yangu, waandishi hawana hatia, walichokuwa wanakiandika ni sahihi kwa ni ni kile kinachotamkwa hadharani pale mahakamani na waandishi wanakaribishwa ili kuelewesha umma mwenendo wa kesi. Na wala siyo kesi ya zombe tu ambayo waandishi wamekuwa wakiifuatilia kila hatua, kuna ile ya Kasusura na zingine.
 
wabongo bwana mara wote sasa mnamshabikia ZOMBE?kazi ipo tanzania yani huu usingizi sijui kama tutaamka,ngoja nikatandike box langu mie nshachoka na hizi blaah blaaaah.

hapo ndo utajua watanzania halisi waliyo. Siku zote kila mtu alikuwa ansema oh..zombe haponi...lakini leo eti wanajifanya...oh...zombe hakuwa na hatia....oh..mara jaji sijui katenda haki...na ushenzi mwingine mwingi.

Nadhani watanzania walio wengi wenye mawazo ya kinafiki na kigeu geu kama wanaomsapoti zombe leo humu JF ni punguani.
 

Jamani acha kuwa na mawazo potofu, nani kakwambia mwandishi wa habari ni mahakama?? Wao wameandika mwenendo wa kesi na siyo kutoa hukumu...ebo!!!

Muache unafiki..... kwani angehukumiwa kunyongwa wewe hapa ungetapika vingine na siyo hayo unayo sema leo, pumbafu kabisa nyie!!
 

naomba ujue kuwa tume yoyote inayoundwa lazima ie na ADIBU ZA REJEA. na kwa tume kama hio nafikiri ilikua na malengo yafuatayo: 1. kujuwa kama kweli waliouwawa walikuwa majambazi au wafanyabiashara? 2.kujuwa mazingira yaliowafanya wauwawe ( je walipambana na polisi au walikamatwa na kuuwawa) 3.maoni ya tume.

sasa naomba ujuwe kuwa maoni haya au hata taarifa ya tume hii haiwezi hata kidogo kutumika kama ushahidi au hata kielelezo mahakamani.

Ili kesi iweze kusimama lazima polisi wafanye uchunguzi wao, kisha ushahidi huo uwakilishwe ofisi ya DPP. nae akikubali basi kesi inafunguliwa.

aandishi inawabidi waandike kile kinachosemwa na sio kuongeza au kupunguza jambo. Suala la maamuzi katika habari linabaki kwa msomaji au msikilizaji wa habari hiyo.

Mwandishi aruhusiwi hata kidogo kuiamulia jamii. Kwa kufanya hivyo ni kinyume cha Katiba ya Tanzania ( uhuru wa kupata habari) na kinyume cha maadili a uandishi.
 
[quoteJamani acha kuwa na mawazo potofu, nani kakwambia mwandishi wa habari ni mahakama?? Wao wameandika mwenendo wa kesi na siyo kutoa hukumu...ebo!!!

Muache unafiki..... kwani angehukumiwa kunyongwa wewe hapa ungetapika vingine na siyo hayo unayo sema leo, pumbafu kabisa nyie!!] [/quote]


Sheria ni msumeno. unakata pande zote.

Hebu pata nakala ya hukumu ya Jaji masati ya jana kisha soma magazeti yameripoti nini kwa jamii utaona ninachobainisha.

Pole sana
 
inawezekna tunakuwa na ujinga wa kufikiri, mimi sioni ni wapi hao waandishi wa habari walipoumbuka, hata kama wewe ulikuwa hujuhi kufanya uchunguzi wa haya mambo ya mahuaji, hii kwsi ilikuwa hiko open kabisa kwa ushahidi wa kimazingira na kivitendo, waandishi walikuwa wakiriport kilichokuwa sahihi kabisa kwamba zombe. lema na wengineo wamehusika kwa asilimia 100, kuwaua hao wafanya biashra wa madini, labda swali la kujiuliza hao jamaa walikuwa Sinza na waliondoka na polisi, walifikaje pale kwenye msitu wa pande na kupata mahuti huko
tatizo lililojitokeza sio waandishi bali ni serikali yako ya Kikwete na utendaji wake mbovu, uwezi kugharamia mamilioni ya pesa za walipa kodi kisha unapeleka kesi mahakamani isiyokuwa na ushahidi wa kutosha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…