Kesi ya Abdallah Zombe: Mashitaka, hatia, hukumu na yanayojiri

Kesi ya Abdallah Zombe: Mashitaka, hatia, hukumu na yanayojiri

Siri zafichuka kesi ya Zombe

na Asha Bani

SHAHIDI wa 14 katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara watatu na dereva teksi inayomkabili aliyekuwa Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abdallah Zombe na wenzake, Sajenti mstaafu D 6829 Constantino, ameiambia mahakama kuwa risasi alizowakabidhi askari hao wanaodai kuzitumia siku ya tukio zilirudishwa kama zilivyokuwa.

Shahidi huyo ambaye ni mtunza silaha katika Kituo cha Polisi Chuo Kikuu Dar es Salaam, alidai usiku wa Januari 14 mwaka 2006 aliwakabidhi askari waliokuwa zamu siku hiyo risasi 68 na bunduki tatu aina ya SMG, na kwamba zote zilirudishwa zikiwa hazijatumika, licha ya askari hao kudai kulikuwa na kurushiana risasi baina yao na majambazi siku hiyo.

Sehemu ya mahojiano kati ya shahidi huyo na wakili wa Serikali, Angaza Mwaipopo, yalikuwa kama ifuatavyo:

Wakili: Shahidi hebu ielezee mahakama kuwa unaitwa nani na unafanya kazi gani.

Shahidi: Naitwa Costantino nilikuwa nafanya kazi katika Kituo cha Polisi Chuo Kikuu kama msaidizi wa mkuu wa kituo. Nilikuwa na namba D 2829 kwa sasa nimestaafu.

Wakili: Unakumbuka Januari 14 kuamkia 15 mwaka 2006 kulitokea nini kituoni kwako?

Shahidi: Siku hiyo nilikuwa zamu kituoni na nilitakiwa kuwakabidhi silaha askari waliokuwa zamu (lindo) siku hiyo, ikiwa ni moja ya majukumu yangu ya kawaida.

Aliendelea kueleza kuwa aliwakabidhi silaha tatu ikiwa ni bastola moja na bunduki aina ya SGM mbili, zikiwa na risasi 68 ambazo alidai hazikutumika.

Constantino alidai silaha hizo aliwakabidhi askari D 1406 Koplo Emmanuel, F 5612 PC Noel, na D 901 Lema, ambao aliwatambua mahakamani. Wengine ni Koplo James na Sajenti Alawi, ambao hawakuwapo mahakamani.

Alidai asubuhi ya Januari 15 aliingia ofisini kwa mkuu wa kituo (OSS) Sebastian Masinde na kukuta Polisi zaidi ya 10 wakiwa wanapongezwa kwa kazi nzuri waliyofanya ya kuua majambazi usiku uliopita.

Alinukuu maneno ya Masinde: "Hongereni sana vijana wangu mmejitahidi kupambana na majambazi, hongereni sana, mmefanya kazi nzuri." Alidai baada ya kusikia hivyo aliuliza kuna nini? Akaambiwa kuwa askari hao wamefanikiwa kupambana na majambazi na kwamba wameua majambazi wanne, na yeye akadai kuanza kuwapongeza pia.

Aliendelea kuidai kuwa baada ya hapo hawakuandika ripoti yoyote ya tukio kama kawaida yao na badala yake askari hao waliitwa Kituo cha Polisi Oysterbay na hakujua kilichoendelea.

Naye shahidi wa 12 katika kesi hiyo, Zainabu Hashim (33), mfanyakazi katika Hoteli ya Bondeni, alidai siku ya Januari 18 wakiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili walifika askari polisi zaidi ya 10 waliokuwa wamefuatana na Zombe huku wakiwa wamevalia soksi usoni na kubakisha macho (mask).

Alidai askari hao waliokuwa wameambata na Zombe waliruka kwenye gari la Polisi la wazi walilokuwa wamepanda na kuvamia msikitini wakati wa ibada ya mwisho ya kumuombea marehemu Juma Ndugu, ambaye ni dereva teksi ikiwa inaendelea.

Alidai watu waliokuwepo katika eneo la tukio walishangaa na wengine kuanza kukimbia kwa kuwa si tukio la kawaida.

Sehemu ya mahojiano kati ya Zainabu na wakili Angaza Mwaipopo yalikuwa kama ifuatavyo:

Wakili: shahidi hebu iambie mahakama kuwa unajishughulisha na nini.

Shahidi: Najishughulisha na shughuli za uhudumu katika Hoteli ya Bondeni iliyopo Magomeni.

Wakili: Unaweza ukawakumbuka wateja waliokuja kwako siku ya Januari 13 na 14 mwaka 2006?

Shahidi: Nawakumbuka na niliwarekodi katika kitabu cha kumbukumbu nikiwa kama mhudumu (receptionist).

Wakili: Unaweza ukawataja ni kina nani waliokuja siku ya Januari 13 na kulala hadi 14 mwaka 2006?

Shahidi: Nawakumbuka kwa kuwa walikuwa wateja wetu tangu mwaka 2003 ambao ni Sabinus Chigumbi, Ephraim Lunkombe na Mathius Lunkombe.

Wakili: Unakumbuka nini siku ya Januari 15 mwaka 2006?

Shahidi: Nakumbuka siku hiyo nikiwa hotelini nilipokea simu kutoka kwa Ngonyani ambaye ni ndugu wa marehemu na alinitaarifu nifunge chumba cha marehemu, ikiwa ni pamoja na kunitaarifu kuwa kina Jongo wamekamatwa na Polisi.

Alidai wakati anakwenda kufunga chumba na kutoa vitu vya marehemu hao alimkuta msichana aliyemtaja kwa jina la Stella ambaye alidai kuwa na uhusiano wa kimapenzi na marehemu Jongo.

Alieleza alimtaka Stella atoke ili afunge mlango sambamba na kukusanya vitu vya marehemu na kuvihifadhi hadi watakapojua kinachoendelea.

Alieleza baada ya kukusanya vitu hivyo na kuvitunza alipiga simu kwa askari Polisi Mbaraka Kituo cha Urafiki, ambaye mke wake anafanya naye kazi na kumuuliza kama anafahamu lolote kuhusiana na kukamatwa kwa watu hao.

Alidai Mbaraka alimwambia awaambie ndugu wa marehemu kwenda nyumbani kwake kwa ajili ya mazungumzo na wakafanya hivyo, baada ya kufika nyumbani kwa Mbaraka aliweza kuzungumza nao na kuwataarifu kwamba wale watu waliokamatwa wameuawa kwa tuhuma za ujambazi.

Kwa upande wake, shahidi wa 11, Jaffer Amir Jaffer (3 ambaye ni mfanyabiashara katika duka la kuuzia vito vya thamani eneo la Mkunguni, Kariakoo, aliiambia mahakama kuwa waliouawa hawakuhusika na wizi katika duka lake, Januari 14 mwaka 2006.

Jaffer alidai kuitwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kuwatambua majambazi hao ambao aliwaona wakiwa wanne, lakini hakuweza kuwatambua.

Alidai anakumbuka Januari 14 mwaka 2006 akiwa dukani kwake walifika watu wawili na kuulizia mkufu wa dhahabu na alipowatajia bei walitaka wapunguziwe.

Alidai baada ya kuomba kupunguziwa bei, ghafla aliingia mwanamke ambaye pia aliulizia mkufu huo na ghafla aliondoka akaingia tena mwanamume mmoja ambaye alimuonyesha silaha kichwani na kuchukua vito alivyokuwa anaviuza.

Shahidi huyo alieleza wakati ameinama kutaka kuchukua silaha walimvamia na kumkandamiza kiunoni na kushindwa kuichukua na kisha kumnyang'anya silaha hiyo.

Alidai kufanikiwa kuchukua vito hivyo na wakati wanaondoka walikuwa wanarusha silaha na pia kumjeruhi mlinzi wake aliyekuwa mlangoni.

Alidai kuwa wale aliowaona mochwari wakiwa wamehifadhiwa hawahusiani na waliokuwa wamemuibia dukani kwake, na kwamba hata akiwaona leo atawafahamu.

Shahidi mwingine wa 12 Koplo John katika Kituo cha Msimbazi anayejishughulisha na kupokea simu za matukio mbalimbali na kusambaza katika vituo vingine (control room), alidai siku ya Januari 14 -15 mwaka 2006 hapakuripotiwa tukio lolote la ujambazi linalohusiana na kurushiana risasi kati ya askari na majambazi.

Alidai tukio ambalo liliripotiwa ni la ujambazi wa Kampuni ya mafuta ya BIDCO OIL, ambalo lilitokea siku hiyo na unyang'anyi wa gari, lakini majambazi hao hawakufanikiwa kunyang'anya gari hilo.

"Siku hiyo hakuna simu yoyote au taarifa kupitia chumba cha mawasiliano (control room), zilizokuwa zinasema kulikuwa na majibizano ya risasi au kuna majambazi maeneo ya Sam Nujoma yalirushiana risasi na Polisi,"alieleza Koplo John.

mbali na Zombe, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni ASP Christopher Bageni, ASP Ahmed Makelle, Konstebo Noel Leonard, Kontebo Jane Andew, Koplo Nyangerela Moris, Konstebo Emanuel Mabula, Koplo Felix Sedrick, Konstebo Michael Shonza na Koplo Abeneth Salo.

Wengine ni Koplo Rashid Lema, Koplo Rajabu Bakari na Koplo Festus Wabisabi.

Washitakiwa hao wanadaiwa kuwa Januari 14 mwaka 2006 waliwaua kwa makusudi wafanyabiashara watatu na dereva teksi mmoja katika msitu wa Pande uliopo Mbezi Luis.
 
Kesi ya Zombe, wenzake: Shahidi adai kulazimishwa kufyatua risasi

Na Grace Michael

SHAHIDI wa 15 wa upande wa mashitaka katika kesi inayowakabili askari Polisi akiwamo aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Abdallah Zombe na wenzake, C 7521 Sajini Joseph (49) amedai mahakamani kuwa alishinikizwa kutoa bunduki na risasi kwa ajili ya kufyatuliwa ili kumnusuru Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya, Bw. Christopher Bageni katika janga zito lililokuwa likimkabili.

Wakati shahidi huyo akidai hivyo jana, shahidi wa 16 Bw. Ramadhan Mfaume, alidai wakati wakiaga mwili wa marehemu Juma Ndugu, Bw. Zombe aliingia msikitini na kuwatangazia kuwa waliouawa ni majambazi na wala hawawasingizii.

Hayo yalijitokeza katika Mahakama Kuu ya Tanzania mbele ya Jaji Salum Masati wakati mashahidi wa upande wa mashitaka wakitoa ushahidi wao kuhusiana na tukio la mauaji ya wafanyabiashara wa madini kutoka Mahenge, Morogoro, ambao wanadaiwa kuuawa na polisi hao.

Shahidi wa 15 aliongozwa na wakili wa Serikali, Bw. Jasson Kaishozi na hali ilikuwa kama ifuatavyo:

Wakili: Unafanya kazi gani?

Shahidi: Nafanya kazi ya askari Polisi na niko kitengo cha kutunza silaha katika ghala la kituo cha Oysterbay, Dar es Salaam.

Swali: Upo tangu lini na unafanya kazi zipi?

Jibu: Tangu mwaka 1992 na kazi zangu ni kutoa silaha na kupokea wakati zikirejeshwa.

Swali: Mko wangapi katika kitengo hicho?

Jibu: Tuko wawili na huwa tunaingia kwa saa 48 kila mmoja.

Swali: Unakumbuka nini Januari 14, 2006?

Jibu: Nilikuwa kazini kwangu mpaka Januari 15, 2006 ambapo siku hiyo nikuwa nikipokea silaha zinazorejeshwa.

Swali: Je unawafahamu Koplo Saad, Konstebo Jackson, Konstebo Joseph, Konstebo Rashid na Koplo Rajab?

Jibu: Nawafahamu na baadhi yao wako hapa mahakamani.

Swali: Uliwapa silaha gani siku hiyo?

Jibu: Koplo Rajab (mshitakiwa) alichukua bastola aina ya chinese ambayo ilikuwa na risasi nane, Koplo Saad (hajapatikana mpaka sasa) alichukua SMG ikiwa na risasi 30 na Konstebo Rashid naye alichukua SMG ikiwa na risasi 30.

Swali: Je wote walirudisha na zilikuwaje?

Jibu: Ndiyo, asubuhi yake walirejesha silaha hizo, lakini SMG aliyokuwa nayo Koplo Saad ilikuwa na upungufu wa risasi tisa.

Swali: Kwa nini kitabu kinaonesha kuwa Bw. Rashid naye alikuwa na upungufu wa risasi tatu, ilikuwaje na wakati mahakama umeieleza kuwa alirudisha zote?

Jibu: Baada ya siku tatu lilitokea shinikizo kutoka kwa uongozi wa juu kituoni hapo, ukimshinikiza Rashid kwenda kufyatua risasi ili kujinasua na janga.

Swali: Hayo maneno wewe uliyasikia wapi?

Jibu: OC CID Bw. Bageni aliniita na kunitaka nitoe silaha aliyokuwa nayo Rashid siku ya tukio, ili aende kufyatua risasi ili kuwaokoa na janga zito walilonalo.

Naye wakili wa utetezi, Bw. Gaudioze Ishengoma, alimhoji ifuatavyo:

Swali: Uliripoti kwa nani kuwa umeshinikizwa kutoa silaha?

Jibu: Mkuu wa kituo alikuwa anafahamu suala hilo la mauaji na mimi nilipewa amri ya kutoa silaha, ili waweze kujiokoa na janga kubwa hivyo amri hiyo ilikuwa ni halali, kwani ni ya mkubwa wangu, nisingeweza kukataa amri hiyo na niliogopa sana.


Alidai kuwa amri ya Polisi ni kutekeleza kwanza ndipo uhoji.

Aidha, shahidi huyo alidai kuwa wakati anatoa maelezo yake Polisi, alikuwa bado hajawa huru na kulikuwa bado kuna shinikizo hivyo aliyoyaeleza mahakamani ndiyo sahihi.

"Hili shinikizo sikulisema, kwani wale wote ni polisi na leo nasema kwani mahakama ni ya haki na kuna Jaji," alidai.

Alidai kuwa siku anapewa shinikizo hilo, alikuwapo mmoja wa washitakiwa ambaye ni Bw. Rashid.

Shahidi wa 16 Bw. Mfaume ambaye ni ndugu wa marehemu Ndugu, alieleza kuwa baada ya tukio hilo walifuatilia mochari ambapo siku ya mwisho ambayo walikuwa wakiaga mwili wa marehemu msikitini, Bw. Zombe alitokea na kutangaza kuwa waliouawa ni majambazi na hawasingiziwi.

Alidai kuwa wakiwa hapo, lilitokea gari la Polisi likiwa na askari waliofunika nyuso zao akiwapo Bw. Zombe aliyewatangazia hayo.

Shahidi wa 17 Bw. Emmanuel Ikonga (5 naye alihojiwa na wakili wa Serikali Bw. Alexander Mzikila kama ifuatavyo:

Swali: Unakumbuka nini Januari 7, 2006?

Jibu: Siku hiyo nilikuwa safarini kutoka Mahenge kuelekea Arusha kupitia Dar es Salaam na nilikuwa na Bw. Sabinus Chigumbi, Ephraim Chigumbi, Protas Lukombe, Theopister Chigumbi na Bernadeta Ephraim.

Swali: Mlifikia wapi?

Jibu: Hawa wote walifikia hoteli ya Bondeni na mimi nilifikia Keko na Januari 9, 2006 tuliondoka kwenda Arusha ambako tuliwapeleka watoto shule na baadaye tulielekea kwenye soko la kuuza madini na tuliporudi hotelini niliona Sabinus ana fedha nyingi kwenye begi lake.


Swali: Mlirejea lini?

Jibu: Januari 12, 2006 tulirudi na wenzangu kama kawaida walifikia hotelini kwao na mimi Keko, kesho yake nilipeleka gari gereji ambalo Januari 14, 2006 tuliendelea kulifuatilia gari hilo na siku hiyo tulishinda na marehemu gereji.

Swali: Baadaye nini kiliendelea?

Jibu: Kesho yake tulipata taarifa kuwa wenzetu wameuawa hivyo tuliamua kwenda Muhimbili mochari kwa ajili ya kutambua jamaa zetu.

Tukiwa Mochari ghafla walivamia watu wakiwa na silaha na nyuso zao wameziziba na walitupandisha kwenye gari na kutupeleka Kituo cha Kati cha Polisi.

Swali: Baada ya kufika ilikuwaje?

Jibu: Tulipofika hapo wale askari walianza kumtafuta Zombe na tuliingizwa kwenye chumba kimoja ambamo Zombe na maofisa wengine wa Polisi walikuwa.

"Tulipoingia tu Zombe alisema kuwa 'nyie ndio majambazi mliotukimbia jana hivyo nanyi lazima muuawe'.

"Baada ya kusema hivyo mmoja wa maofisa waliokuwapo alishauri tuhojiwe ili wajue tuna uhusiano gani na marehemu.

"Tukiwa tunahojiwa mimi nilisema marehemu ni wapwa zangu na ndipo Zombe aliponiambia kuwa 'wewe ndio mjomba wao mwanajeshi mstaafu, ndiye mwalimu wa majambazi huko Mahenge?'," alidai shahidi.

Alidai kuwa baada ya kuchuliwa maelezo yao waliwekwa mahabusu kila mtu chumba chake na walitolewa mahabusu Jumatatu jioni wakiwa wamefungwa pingu.

Wakiwa nje ya kituo cha Kati na Bw. Zombe kuwaona wamefungwa pingu, alifoka na kuhoji sababu ya kufungwa pingu na wakati si majambazi wala watuhumiwa, kitendo kilichomshangaza shahidi huyo na kumfanya asielewe kilichokuwa kikiendelea.

Alidai kuwa aliamuru wapelekwe kituo cha Oysterbay kwa Bw. Bageni ili awape dhamana, ambako walidhaminiwa.

Naye shahidi wa 18 ambaye ni E 5448 Sajini Nasib (43) wa Makao Makuu ya Polisi, alidai kuwa Februari 22, 2006 alipewa maelekezo na bosi wake ASP Mkumbi ya kuongozana naye eneo la tukio, ambalo lilidaiwa kutokea mashambulizi ya majambazi na polisi.

Alidai kuwa walikwenda mpaka Sinza C ambako walipiga picha na kuelekea katika ukuta wa Posta ulioko maeneo hayo, ambako nako walipiga picha za tukio hilo.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali Bw. Angaza Mwipopo, alidai kuwa baada ya kupiga picha hizo aligonga mhuri wake nyuma na kuziweka kwenye albamu na alizikabidhi kwa timu aliyokuwa ameongozana nayo.

Swali: Kitabu hiki unakikumbuka?

Jibu: Ndiyo ni albamu ya zile picha ambazo nilitengeneza mimi.

Swali: Ungependa zitolewe kama sehemu ya kielelezo?

Jibu: Ndiyo.

Bw. Mwipopo aliiomba mahakama kupokea albamu hizo kama kielelezo, hoja iliyopingwa na upande wa utetezi ambao ulidai kuwa kielelezo hicho hakiko kwenye orodha waliyonayo hivyo kisipokewe.

Jaji alisikiliza malumbano ya kisheria ya pande zote mbili na kukubaliana na upande wa utetezi.

Baada ya pingamizi hilo kukubaliwa, Bw. Mwipopo aliiomba mahakama kuahirisha kesi hiyo mpaka kesho ili kuwapa nafasi upande huo wa kuwasilisha notisi ya kuomba kuwa na kielelezo cha nyongeza.

Hoja hiyo pia ilipingwa na kudai kuwa upande wa mashitaka haujatoa hoja ambayo inaweza kuishawishi mahakama kuahirisha kesi hiyo, hivyo upande wa utetezi uruhusiwe ili uendelee kumhoji shahidi.

Uamuzi wa Jaji ulikubaliana na upande wa Serikali na kuahirisha kesi hiyo ambayo inaendelea leo saa 3 asubuhi.

Washitakiwa katika kesi hiyo wanadaiwa kuwa Januari 14 mwaka juzi wakiwa katika msitu wa Pande Luisi Mbezi, Dar es Salaam, waliwaua kwa makusudi Bw. Ephraim Chigumbi, Bw. Sabinusi Chigumbi, Bw. Juma Ndugu na Bw. Mathias Lukombe.

Washitakiwa hao ni Bw. Zombe, Bw. Bageni, Bw. Ahmed Makele, F5912 Noel Leonard, WP4513 Jane Andrew, D6440 Nyangerella Moris, D1406 Mabula, E6712 Felix, D8289 Michael, D2300 Abeneth, B1321 Rashid Lema, D4656 Rajab Bakari na D1367 Festus Gwabisabi.
Source: Majira, Jumatano 04.06.2008 0115 EAT
 
Kesi ya Zombe : Wafanyabasha walipigwa risasi wakiwa wamekaa pamoja

James Magai na Nora Damian

SHAHIDI wa 19 katika kesi ya mauaji ya kukusudia ya wafanyabiashara watatu madini kutoka Mahenge Morogoro na dereva teksi wa Manzese jijini Dar es Salaam, waliouawa na askari polisi wakidhaniwa ni majambazi, Dk Martin Phillip Mbonde, amedai mahakamani kuwa inaonekana wafanyabiashara hao, walikalishwa sehemu moja na kupigwa risasi kwa pamoja.

Dk Mbonde alitoa madai hayo jana, wakati akitoa ushahidi katika kesi hiyo inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam, ACP Abdallah Zombe na wenzake 12, katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam baada ya kuulizwa swali na Naibu Kiongozi wa Waendesha Mashtaka wa Serikali, Jasson Kaishozi.

Daktari huyo ambaye ni Muhadhiri Chuo Kikuu cha Muhimbili na mfanyakazi Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Kitengo cha Uchunguzi wa Chanzo cha Vifo vya Binadamu (Pathology), alikuwa ni mmoja ya watu waliochunguza maiti za wafanyabiashara hao.

Mahojiano kati ya wakili huyo, mshauri wa mahakama na shahidi huyo, yalikuwa kama yafuatavyo.

Kaishozi: Shahidi, hebu ieleze mahakama hii je, ni nini ?Pattern? ya majeraha uliyoyaona kwa marehemu hao?

Dk Mbonde: Hali ya majeraha hayo inaonesha kuwa ni kama vile marehemu walikalishwa mahali pamoja na wote kuanzwa kupigwa risasi.

Alipoulizwa na Mshauri wa Mahakama Magreth Mosi kuwa alijuaje au ni nini ambacho kinamfanya aseme kuwa marehemu walikalishwa sehemu moja na kupigwa risasi, shahidi huyo alisema majeraha yaliyokuwa sehemu moja tu katika miili ya marehemu hao, yalionyesha kuwa walikalishwa sehemu moja.

"Hii ni kwa sababu kuwa mahali risasi zilipoingilia na mahali zilipotokea ni sehemu moja tu. Kama kungekuwa na mapambano ya kurushiana risasi basi risasi hizo zingekuwa zimeingilia katika sehemu tofauti tofauti katika miili," alidai Dk Mbonde.

Awali akiongozwa na Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Kaishozi kutoa ushahidi huo wake mbele ya Jaji Salum Masatti anayesikiliza kesi hiyo, Dk Mbonde alidai marehemu wote walikuwa na majeraha ya risasi walizopigwa shingoni kwa nyuma na kutokezea mbele.

Dk Mbonde alifafanua kuwa marehemu Ephraimu Chigumbi alikuwa na majeraha matatu, sehemu za usoni, mkononi, kifuani na lilikuwa shingoni.

Alidai Chigumbi alipigwa risasi shingoni kwa nyuma ambayo iliacha jeraha lenye ukubwa wa sentimita moja kwa moja na kutokea mbele mdomoni sehemu ya kulia na kuacha jeraha lenye ukubwa wa sentimita nane kwa nane.

Shahidi huyo, alidai risasi hiyo ilimvunja taya na baadhi ya meno na kupasua mishipa ya damu na kusababisha damu nyingi kuvuja na kwamba chanzo cha kifo chake ni majeraha ya risasi hiyo.

Aliongeza kuwa marehemu Sabinus Chigumbi (Jongo) alipigwa risasi mbili, moja shingoni kwa nyuma na kuacha jeraha lenye ukubwa wa sentimita moja kwa moja na kutokea mbele karibu na taya la chini na kuacha jeraha la ukubwa wa sentimita sita kwa nne.

Alidai risasi ya pili alipigwa katika mkono wa kushoto na kutokea kwa nyuma na kwa mbele, hivyo kuacha jeraha la ukubwa sentimita sita kwa sita na ilivunja mifupa na kupasua mishipa ya damu na kusababisha damu nyingi kuvuja na kwamba risasi hizo, zilikuwa chanzo cha kifo chake.

Kuhusu marehemu Mathias Lunkombe, Dk Mbonde alidai marehemu huyo alikuwa na majeraha matatu ya risasi na kwamba risasi moja ililengwa kwenye taya la kulia na kuacha jeraha kubwa la sentimita moja kwa moja na kutokea kushoto chini ya taya.

"Risasi nyingine mbili alipigwa shingoni katika pingili ya nne ya mfupa wa shingo na kuvunjika mataya na ubongo kuathirika pamoja na mishipa ya damu kupasuka na kusababisha damu nyingi kuvuja. Hivyo chanzo cha kifo hicho kilikuwa ni majeraha ya risasi za bunduki," alidai Dk Mbonde.

Akisimulia sababu za kifo cha dereva teksi, Juma Ndugu, Dk Mbonde alidai alikuwa na jeraha moja la risasi iliyoingilia ilivunja pingili ya sita ya mfupa wa shingo kwa nyuma na kuacha jeraha lenye ukubwa wa sentimita moja kwa moja na kutokea mbele na kuacha jeraha lenye ukubwa wa sentimita sita kwa sita.

Aliongeza kuwa risasi hiyo, ilivunja pingili ya sita ya shingo ya marehemu Ndugu na kuumiza uti wa mgongo jambo lililosababisha kuvuja kwa damu nyingi na hatimaye kufariki dunia.

Baadaye alipoulizwa na wakili wa upande wa utetezi, Jerome Msemwa iwapo marehemu walikuwa na majeraha mengine katika miili yao kama vile kukatwa sehemu za viuongo vyao Dk Mbonde alidai hakuwahi kuona.

Alieleza kuwa kama mtu angeliangalia kwa haraka jeraha hilo, angedhani marehemu Juma alikatwa shingoni kwa kitu chenye ncha kali kwa kuwa risasi ilichana ngozi ya sehemu ya shingoni.

Mbali na wakili Msemwa, Dk Mbonde alihojiwa na mawakili wengine wa upande wa utetezi na sehemu ya mahojiano yao ilikuwa kama ifuatavyo:

Wakili Gaudioz Ishengoma: Shahidi ulipoulizwa na msomi mwenzangu, ulisema hujawahi kuwa askari polisi na wala huna utaalamu wa risasi je, majeraha yale kwa asili hakuna kitu kingine kinachoweza kusababisha majeraha yale?

Dk Mbonde: Hakuna

Ishengoma: Je ulifanya upasuaji wa miili ya wale marehemu?

Dk Mbonde: Ndio.

Ishengoma: Je, ulikuta risasi ndani?

Dk Mbonde: Hapana.

Ishengoma: Sasa ulijuaje kuwa hayo ni majeraha ya risasi?

Dk Mbonde: ?Kuna tofauti kubwa sana kati ya jeraha la risasi na jeraha la mshale au kitu chochote chenye incha kali. Kwanza, risasi ikiingia mwilini inapenya na kutokeza nje tofauti na vitu vingine vyenye ncha kali, lakini pia risasi inapoingia mwilini inavunjavunja mifupa, lakini vitu vyenye ncha kali kama kisu haviwezi kuvunja mfupa?.

Mbali na Dk Mbonde, shahidi mwingine namba 18, E.5448 Sajenti Nasibu Masoud anayefanya kazi Makao Makuu ya Polisi kitengo cha picha aliiambia mahakama kuwa siku chache baada ya tukio la mauaji hayo, aliagizwa na mkuu wake wa kazi, SP Hamis kwenda kupiga picha Sinza C mahali ambako wafanyabiashara hao walikamatwa.

Shahidi Masoud akiongozwa na PP Angaza Mwipopo, alidai akiwa Sinza C alipiga picha zisizopungua nane katika maeneo tofauti tofauti ikiwemo iliko nyumba ya Ngonyani ambaye ni shahidi wa kwanza kwenye kesi hiyo, ambako marehemu walikamatwa.

Alidai picha nyingine alipiga sehemu ya ukuta wa kibanda walikokuwa wamekaa akina Mjatta ambaye ni shahidi wa sita katika kesi hiyo na nyingine alipiga eneo lilipopaki gari la marehemu na eneo lingine ambako Mama Ngonyani (shahidi namba mbili) na marehemu Jongo walikokuwa wamekwenda kuzungumza.

Masoud alidai mbali na eneo hilo la Sinza C pia alikwenda kupiga picha eneo la ukuta wa Posta ambako ilisemekana kuwa ndiko marehemu alikouawa wakati wakijibizana na askari polisi.

Alidai alipiga picha hizo akiongozwa na mkuu wake wa kazi aliyeambatana naye, Kaimu Kamishna Msaidizi Mkuu wa Polisi (SACP) Mkumbi na kwamba, katika ukuta huo kulikuwa na matundu manne madogo ambayo yalidaiwa kuwa ni ya risasi zilizotokana na mapambano.

Alifafanua kuwa hakuwa na uhakika kama matundu hayo yalikuwa ni risasi ila yalionekana kwamba yalikuwa matundu madogo yaliyozungushiwa alama ya duara kwa kutumia chaki.

Alidai matundu hayo yalionekena kupishana, lakini kwa umbali mfupi na kwamba alisafisha picha hizo na kuziweka katika albam na kuzikabidhi makao makuu.

Naye shahidi wa 20 katika kesi hiyo, Issa Salum (52) aliieleza mahakama kuwa wakati akiwa mlinzi katika gereji iliyoko Sinza C, hakuwahi kusikia milio ya risasi wala bunduki.

Shahidi huyo alidai alikuwa mlinzi kwenye gereji hiyo kwa muda wa miaka mitatu na kwamba, kipindi cha mwezi Januari mwaka 2006 hakuwahi kusikia milio yoyote ya risasi ama kuona tukio lolote la ujambazi katika eneo hilo.

Kesi hiyo namba 26 ya mwaka 2006 kwa mara ya kwanza, Zombe na wenzake 12 walifikishwa mahakamani Septemba 28, mwaka juzi mbele ya aliyekuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Laurian Kalegeya ambaye sasa ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa.

Zombe alipandishwa katika mahakama hiyo kwa mara ya kwanza Juni 9, saa 4.00 asubuhi na Juni 15 mchana alifutiwa shtaka la mauaji lilokuwa likimkabili peke yake mbele ya Kaimu Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi Addy Lyamuya na kuunganishwa na wenzake 12 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi, Sivangilwa Mwangesi.

Jaji Masati anayesikiliza kesi hiyo aliahirisha kesi hiyo hadi leo itakapoendelea tena.

http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=6029

Kesi inaendelea: Huo ni unyama, polisi aibu kubwa kwenu.
 
loh lakini tusije shangaa sikia kina zombe wameshinda kesi wako huru na anarudi kwenye post yake
 
Kesi ya Zombe, wenzake.. Shahidi adai waliouawa hawakuiba

*Adai yeye na wenzake ndio walistahili kifo
*Alishiriki kupora fedha za Bidco barabarani

Na Grace Michael

SHAHIDI wa 25 katika kesi ya mauaji inayomkabili aliyekuwa Ofisa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Bw. Abdallah Zombe na wenzake; Bw. Shabaan Manyanya amedai kuwa wafanyabiashara wa Mahenge hawakustahili kuuawa bali yeye na wenzake ndio waliostahili kifo hicho.

Alidai mahakamani jana kuwa yeye na wenzake walistahili kuuawa kutokana na kushiriki tukio la uporaji fedha katika gari la kampuni ya Bidco katika barabara ya Sam Nujoma, Dar es Salaam.

Bw. Manyanya alidai hivyo katika Mahakama Kuu ya Tanzania mbele ya Jaji Kiongozi Salum Masati, wakati akitoa ushahidi katika kesi hiyo yenye washitakiwa 13.

Shahidi huyo aliongozwa na wakili wa Serikali Bw. Alexander Mzikila kama ifuatavyo:

Swali: unaishi wapi?
Jibu: Kwa sasa naishi Songea, lakini kipindi cha nyuma nilikuwa naishi Mwananyamala, Dar es Salaam.

Swali: Mwanzoni mwa Januari 2006 kilitokea nini?
Jibu: Nakumbuka kipindi hicho nilifuatwa na rafiki yangu Bw. Grayson na kuniambia kuwa ana biashara fulani ambayo tungeifanya na rafiki yake, Bw. Ally.

Swali: Ulimjibuje?
Jibu: Nilimwambia amlete huyo Ally nijue hiyo biashara na alifanikiwa kumleta na kuzungumza naye, lakini tena niligundua kuwa mhusika mkuu ni dereva wa Bidco anayeitwa Mashaka.

Swali: Nini kiliendelea?
Jibu: Niliongea na Mashaka moja kwa moja na kunieleza kuwa gari lao hufanya biashara ya mafuta na sabuni, ambazo huzisambaza sehemu mbalimbali na jioni hupitia makusanyo ya fedha hivyo alitaka tuibe fedha hizo.

Swali: Mlikubaliana nini?
Jibu: Mimi nilimwambia kuwa huwa situmii silaha ya aina yoyote bali mdomo tu ndiyo silaha yangu, hivyo tulikubaliana tukutane kesho yake ili niwatafute watendaji wangu watakaofanikisha kazi hiyo.

Swali: Uliwapata hao watendaji?
Jibu: Ndiyo niliwapata, akina Kiwalaka, Ramadhan na Mawenga na tulimwita dereva wa gari hilo, ili atoe maelezo ya mwisho na eneo zuri la kufanyia kazi hiyo ambayo alituambia kuwa ni barabara ya Sam Nujoma.

Swali: Mlifanya kazi hiyo?
Jibu: Kazi hiyo ilikwama kama siku mbili mfululuzo, kwani siku ya kwanza dereva alitufahamisha kuwa mzigo wote wamekopesha na siku ya pili mzigo ulipelekwa Zanzibar nako ulikuwa mkopo vilevile.

Swali: Je, Januari 14, 2006 nini kilifanyika?
Jibu: Siku hiyo pia nilijipanga na watu wangu na Mashaka alipiga simu na kutujulisha kuwa mzigo wa siku hiyo ulikuwa wa cash (taslimu) hivyo tujipange kukamilisha kazi hiyo.

Swali: Je mlifanya?
Jibu: Niliwapanga vijana wangu na aliongezeka kibarua mmoja wa Bidco ambaye alikuwa kwa ajili ya kulinda maslahi ya dereva wake, lakini mimi na Bw. Grayson hatukwenda eneo la tukio.

Swali: Nini kiliendelea?
Jibu: Ilipofika jioni nilisikia mlango unagongwa na nilipofungua, niliwakuta wenzangu waliokuwa eneo la tukio na kusema wamemaliza biashara, lakini imekuwa ndivyo sivyo, kwani zilipatikana sh. milioni sita badala ya sh. milioni 36 ambazo waliahidiwa.

Swali: Mlifanya nini?
Jibu: Hapo tulianza 'karata' (kugawana fedha) na tuligawana kulingana na ugumu wa kazi, hivyo mimi nilipata sh. 400,000 tu.

Swali: Nini kiliendelea tena?
Jibu: Kwa upande wangu ilipofika saa mbili tu nilikwenda zangu baa kujipongeza na nikiwa hapo baa alikuja askari Polisi wa Oysterbay kwa jina anaitwa Kulwa Wafoo ambaye aliniuliza kama nimeiba na nilimjibu, ndiyo.

Baada ya hapo nilirudi zangu kulala, lakini alfajiri yake nilisikia mlango ukigongwa, na mke wangu alitoka na kukuta askari ambao walimwambia wananihitaji mimi.

"Niliamka na kuwakuta askari wa Oysterbay ambao ni Henjewele, Gallus, Kulwa na mwingine simjui kwa jina na muda huo walikuwa na Grayson na Mawenga na kunitaka nitoe zile fedha, kwani ametumwa na bosi wao anaitwa Madaraka," alidai.

Swali: Uliwapa hizo fedha?
Jibu: Niliwapa sh. 350,000 na wenzangu walinijulisha kuwa tayari wameshawapatia fedha hizo, hivyo Henjewele alinitaka kuondoka Dar es Salaam mara moja na kwenda mkoani mpaka tukio hilo litakapopoa.

Swali: Uliondoka?
Jibu: Ndiyo nilikwenda zangu Zanzibar na kukaa huko, lakini baada kama ya siku nne hivi, nilimwona afande Zombe akitangaza kuua majambazi waliopora Bidco, tukio ambalo lilinishangaza sana, lakini nilinyamaza tu kwani nilishangaa kwa nini askari hao hao wameua na hao hao wamechukua fedha zetu!

Swali: Ulifanya nini?
Jibu: Nilirudi Dar es Salaam na Rais alipounda Tume ya Mauaji hayo nilikwenda na kutoa maelezo kama haya.

"Nilikwenda kutoa maelezo Tume kutokana na uchungu wa kuuawa watu ambao hawakustahili, kwani tuliotakiwa kuuawa ni mimi na wenzangu tuliochukua fedha hizo," alidai.

Akihojiwa na mawakili wa utetezi ilikuwa kama hivi:

Maira: Kwa nini uko hapa badala ya kuwa gerezani?
Jibu: Waulize polisi kwa nini siko gerezani.

Magafu: Huogopi kukamatwa kwa sasa?
Jibu: Siogopi kwani nilishakamatwa na kunyang'anywa fedha zangu na mimi ni mwizi kama miaka 10 iliyopita na sitaacha mpaka kufa.

Magafu: Ulishawahi kukamatwa?
Jibu: Huwa nakamatwa, lakini namalizana na askari lakini kuhusiana na tukio la Bidco, askari wa Oysterbay walikuwa wanalifahamu.

Shahidi wa 26 Bw. Ramadhan Said (32) aliongozwa na wakili wa Serikali Bw. Angaza Mwipopo na ilikuwa ifuatavyo:

Swali: Unaishi wapi?
Jibu: Mwananyamala Kisiwani.

Swali: Januari 14, 2006 ulikuwa wapi?
Jibu: Nilikuwa nyumbani kwangu na ilipofika saa tano nilifuatwa na Bw. Manyanya na kuniambia ule mpango tayari umekamilik, hivyo tuliondoka hadi Mwenge kituo cha daladala, tukisubiri maelekezo kutoka kwa watu walioko ndani ya gari.

Swali: Nini kiliendelea?
Jibu: Tulipata taarifa kuwa gari hilo linakwenda kushusha mzigo Mabibo hivyo sisi tulipanda teksi na kufuatilia gari hilo mpaka liliposhusha mzigo, baada ya hapo tulielekezwa kulifuata gari hilo mpaka Ubungo, ambako nako lilishusha mzigo.

Swali: Nini kiliendelea?
Jibu: Mmoja wetu aliwasiliana na Mashaka ambaye alisema anaelekea kiwandani na fedha iliyoko ndani ya gari ni sh. milioni sita tu.

"Gari hilo liliondoka na kupitia barabara ya Sam Nujoma ambapo sisi tulifuata na kumpigia honi akasimamisha gari ghafla na sisi tukashuka na kugawanyika, mimi nikiwa kwa 'cashier'ambaye nilimwambia atupe chetu, kutokana na uoga wao walitupa mfuko tukaondoka zetu," alidai.

Swali: Mlielekea wapi?
Jibu: Tulielekea Mwananyamala, tukakutana na wenzetu tukagawana hizo fedha na mimi nilichukua sh. 1,070,000 nikaachana na wenzangu,

Swali: Nini tena kiliendelea?
Jibu: Nilikuja kukamatwa na askari wa Oysterbay ambao ni Madilu na Abeya, ambao mwisho wao walitaka niwape sh. 200,000 lakini sikuwapa, kwani tayari Henjewele alishachukua sh. 400,000 hivyo niliwabembeleza mpaka sh. 40,000.

Shahidi wa 26 Mrakibu Mwandamizi Masinde Sebastian (54) ambaye alikuwa Mkuu wa Kituo cha Chuo Kikuu aliongozwa na Mugaya Mutaki na ilikuwa ifuatavyo:

Swali: Januari 14, 2006 ulikuwa wapi?
Jibu: Nilikuwa Chuo cha Diplomasia na nilirudi saa mbili usiku.

Swali: Ulipata taarifa gani?
Jibu: Nilipewa taarifa na Koplo Omary kuwa kuna majambazi wamekamatwa wakiwa na bastola na sh. milioni tano.

Swali: Januari 15, 2006 ulikuwa wapi?
Jibu: Nikiwa kazini kwangu nilipata taarifa kutoka kwa Afande Zombe kupitia 'radio call' ambayo ilinitaka kwenda na vijana wangu.

Swali: Je, ulikwenda nao?
Jibu: Ndiyo nilikwenda nao na tulipofika tulimkuta Zombe katika ofisi ya Tibaigana (Alfred) na wakuu wa vituo wote walikuwapo.

Swali: Nini kiliendelea?
Jibu: Alitueleza kuwa vijana wamepambana na majambazi na kuwakamata wakiwa na bastola na sh. milioni tano, hivyo akatutaka kuandika mapendekezo ya kupandishwa vyeo vijana hao.

Swali: Je mlifanya hivyo?
Jibu: Tuliweka kama rekodi tu ili siku kikitokea kitu cha namna hiyo, tuangalie ni kijana gani anatakiwa kupanda cheo kutokana na alichokifanya.

Swali: Nani mwingine alikuwa na vijana wake?
Jibu: Christopher Bageni wa Oysterbay alikuwa na vijana wake na Ahmed Makele naye alikuwa nao na mimi.

Washitakiwa katika kesi hiyo wanadaiwa kuwa Januari 14, mwaka juzi wakiwa katika msitu wa Pande Luisi ulioko Mbezi, Dar es Salaam, walimuua kwa makusudi Bw. Ephraim Chigumbi, Bw. Sabinus Chigumbi, Bw. Juma Ndugu na Bw. Mathias Lukombe.

Washitakiwa hao ni Bw. Zombe, Bw. Bageni, Bw. Makele, F5912 Noel Leonard, WP4513 Jane Andrew, D6440 Nyangerella Moris, D1406 Mabula, E6712 Felix, D8289 Michael, D2300 Abeneth, B1321 Rashid Lema, D4656 Rajab Bakari na D1367 Festus Gwabisabi.
 
NB: Kwa kuwa kila mwandishi anauwezo tofauti na mwingine hii hapa ya Zombe jana.

Shahidi adai Zombe aliwapongeza polisi wauaji
*Aliagiza wapelekwe kwake awapongeze
*Alitaka wapandishwe vyeo kwa kazi nzuri
*Mwingine adai waliouawa hawakustahili
*Yeye ndiye alitakiwa kuuawa kwa ujambazi

James Magai na Nora Damian

SHAHIDI wa 24 katika kesi ya mauaji ya kukusudia ya wafanyabiashara watatu wa madini kutoka Mahenge mkoani Morogoro na dereva wa teksi, amedai mshitakiwa wa kwanza katika kesi hiyo, Abdallah Zombe aliagiza askari waliowaua wafanyabiashara hao wapandishwe vyeo, wakati shahidi mwingine ameibuka na kudai wafanyabiashara hao hawakuwa na kosa badala yake alistahili kuuawa yeye.

Shahidi wa 24 katika kesi hiyo, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP), Sebastian Masinde ambaye wakati huo alikuwa Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alidai katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam jana kwamba siku moja baada ya mauaji ya wafanyabiashara hao aliagizwa na Zombe awapeleke askari hao, ofisini kwa Zombe ili awape mkono wa pongezi kwa kazi waliyokuwa wameifanya.

''Asubuhi ya Januari 15, mwaka 2006 nilipokuwa nikijiaandaa kwenda chuoni ambako nilikokuwa nikisoma nilipata taarifa kwa njia ya 'Radio Call' kutoka kwa aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Dar es Salaam na Kaimu Kamanda ACP Zombe kuwa niwapeleke vijana wangu ofisini kwake ili awape mkono wa pongezi kwa kuua majambazi na kukamata pesa na silaha,'' alidai SSP Masinde.

Alidai taarifa hiyo ya Zombe iliwahusisha wakuu wa vituo vingine ambao askari wao walishiriki katika tukio hilo na kwamba aliwataka Makamanda wa Polisi wa Wilaya (OCD) na wakuu wengine wa vituo vya polisi kutoka sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam, kufika ofisini kwake kwa ajili ya hafla ya kuwapongeza askari hao.

SSP Masinde alidai baada ya kupata taarifa hiyo alimwita dereva, Koplo Noel ambaye ni mshitakiwa wa nne na kumwagiza awakusanye wenzake wengine na kuingia ndani kwa ajili ya kuwapeleka kwa Zombe kupongezwa.

''Niliwapeleka askari wangu wote waliokuwa wameshiriki katika tukio hilo kasoro Koplo James ambaye hakuwepo kazini na kwa sasa sijui aliko,? alieleza SSP Masinde.

Alidai walipofika ofisini kwa Zombe katika Kituo Kikuu cha Polisi (Central), walimkuta Zombe katika ofisi ya Kamishna Tibaigana akiwa pamoja na maofisa wengine wa Polisi.

''Zombe aliwapongeza vijana wale akisema wamefanya kazi nzuri sana kuwakamata majambazi na pesa pamoja na bastola. Alioonesha pesa zile zikiwa kwenye mfuko pamoja na bastola ile na akaagiza tufanye utaratibu wa kuwapandisha vyeo,'' alisisitiza SSP Masinde.

Alipoulizwa na Kiongozi wa waendesha Mashtaka (PP) Revocatus Mtaki ambaye ni Wakili wa Kujitegemea kama walitekeleza agizo hilo, SSP Masinde alisema hawakutekeleza na badala yake waliwaweka katika kumbukumbuku wakisubiri taratibu nyingine za kuwapandisha vyeo askari.

Alidai katika utaratibu wa kuwapandisha vyeo askari, huwezi kuandika mara moja tu bali unapaswa kuweka kumbukumbu na kusubiri maagizo kutoka makao makuu.

SSP Masinde aliiambia mahakama kuwa wakati wa tukio hilo alikuwa akisoma katika Chuo cha Polisi Kurasini na kwamba siku ya tukio, Januari 14, mwaka 2006 alikuwa chuoni ambako kulikuwa na kikao cha wanafunzi na walimu (School Baraza).

Alidai baada ya kikao hicho aliondoka kurudi kituoni na alipofika katika kituo hicho, saa 2:00 usiku alipata taarifa kutoka kwa Koplo Omar kuwa askari wake walikuwa wamewakamata majambazi wakiwa na Sh5milioni pamoja na bastola moja.

Aliwataja askari hao ambao siku hiyo walikuwa zamu na ambao walishiriki katika tukio hilo kuwa ni Koplo Moris, Koplo Felix Nyangelela, Koplo Festus ambaye ni mshitakiwa wa 13 na Koplo Michael, Koplo Emmanuel Mabula na Staff Sajenti James ambaye hadi sasa hajulikani aliko.

Alidai askari hao, waliondoka kuelekea eneo la tukio wakiwa na gari aina Toyota Isuzu lenye namba za usajili SU 29363.

Pesa hizo zilipelekwa katika Kituo cha Polisi cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na ASP Ahmed Makelle ambaye wakati huo alikuwa Mkuu wa Upelelezi katika kituo hicho (OC-CID) na ambaye ni mshtakiwa wa tatu katika kesi hiyo.

SSP Masinde alidai katika msafara huo, Koplo Noel na Koplo Festus hawakuwa na silaha kwa kuwa walikuwa madereva na kwamba kazi yao ilikuwa ni kuwasindikiza wenzao.

Alidai wakati akienda kwa Zombe, alimwagiza Mtunza ghala la silaha akague silaha na risasi lakini aliporudi alipewa taarifa kuwa silaha zote tatu walizokuwa wamepewa askari zikiwemo SMG mbili na risasi 30 kila moja na bastola moja na risasi nane, zote zilirejeshwa salama na kwamba hakuna hata moja iliyokuwa imetumika.

Naye Shahidi wa 25 Shabani Saidi Manyanya aliiambia mahakama hiyo kuwa aliumia sana aliposikia Zombe akitangaza kwenye luninga kwamba askari polisi wamewaua majambazi wanne Sinza, jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kuhusika katika tukio la uporaji wa pesa za Kampuni ya Bidco.

Manyanya alidai katika mahakama hiyo kuwa kilichosababisha hadi aumie ni kuuawa kwa wafanyabiashara hao na kwamba walionewa kwa kuwa siyo wao waliokuwa wamehusika katika tukio hilo la uporaji lililotokea katika barabara ya Sam Nujoma bali yeye na wenzake ndiyo waliohusika katika uporaji huo.

Manyanya alidai alipaswa auawe yeye na wenzake kwa kuwa wao ndio waliofanya uporaji huo si wafanyabiashara hao ambao hawakuwa na hatia yoyote.

Manyanya alidai kutokana na kuumia kupita kiasi baada ya wafanyabiashara hao kuuawa, alikwenda kutoa maelezo yake katika Tume ya Rais ya kuchunguza mauaji hayo iliyoongozwa na Jaji Kipenka.

Manyanya alidai yeye na wenzake wengine wanne, waliohusika katika uporaji huo kwa kushirikiana na baadhi ya wafanyakazi wa kampnuini hiyo.

Akielezea mipango ya uporaji huo, Manyanya ambaye wakati huo alikuwa mkazi wa Mwananyamala alidai siku moja alifuatwa na rafiki yake mmoja, Grayson na kumwambia kuwa kulikuwa pesa za Kampuni ya Bidco ambazo wanapaswa wazipore.

Alidai baada ya kuelezwa hivyo, alimuuliza Grayson nani alimwambia kuhusu kuwepo kwa fedha hizo, naye alimjibu kuwa aliambiwa na Ali (kibarua wa zamani wa kampuni hiyo) na kwamba mpango kamili alikuwa akiujua Mashaka ambaye alikuwa ni dereva wa magari ya kampuni hiyo yanayokusanya mauzo ya bidhaa mbalimbali kutoka maduka ya kampuni hiyo.

Alidai baada ya kupata taarifa hizo aliwaandaa wenzake na kupanga jinsi ya kupora fedha hizo, wakishirikiana na dereva wa Bidco Mashaka, lakini mara ya kwanza na ya pili mpango wao ulishindikana na kwamba walikuja kufanikiwa mara ya tatu.

Manyanya alidai siku ya tatu hakwenda eneo la tukio na badala yake alibaki nyumbani kwake Mwananyamala na wenzake wakaenda kuzivizia pesa hizo.

Alidai walipokwenda kwenye tukio walikodi gari ndogo teksi iliyokuwa ikiendeshwa na dereva ambaye naye alijulikana kwa jina la Mashaka na kwamba siku hiyo walifanikiwa kupora pesa hizo na bila kutumia silaha yoyote.

Aliongeza kuwa akiwa nyumbani kwake jioni hiyo wenzake walimwambia tayari wamefanikiwa kupora pesa hizo lakini wakadai kuwa zilikuwa ni Sh.6milioni tu badala ya Sh36milioni kwa kuwa duka lingine ambako walitarajia kupata makusanyo ya Sh30milioni lilikuwa limefungwa.

Aliendelea kudai baada ya wenzake kufika waligawana pesa hizo na kupewa Sh 400,000 na jioni hiyo kwenda kujipongeza katika baa moja.

Alidai akiwa katika baa ambayo hakuitaja jina alifuatwa na askari mmoja aliyeitwa Kulwa akamwambia kuwa amesikia wamepora pesa naye alikubali.

Alieleza mahakama kuwa alimfukuza askari huyo huku akimwambia asimletee njaa zake.

Alidai saa 10:00 usiku alifuatwa na askari wengine aliowatambua kwa majina ya Enjewele na mwenzake kutoka Kituo cha Polisi Oysterbay wakiwa wamewakamata wenzake aliokuwa ameshiriki nao katika uporaji huo.

Alidai Enjewele alimuuliza kama alikuwa anawafahamu wale aliokuwa nao na Manyanya alisema anawafahamu na kwamba walipora nao fedha hizo huku askari Enjewele akimwambia kuwa alikuwa ametumwa na mamlaka kuchukua fedha hizo.

''Nilikuwa nimezitumia na zimebakia Sh350,000, hivyo nilimpa zote akaniachia na akaniambia inabidi nihame Dar es Salaam na ndipo nilipokwenda Zanzibar,'' alidai.

Alidai akiwa Zanzibar aliona kwenye luninga wakitangaza kuwa kuna majambazi wanne wameuawa kwa tuhuma za kupora pesa za Kampuni ya Bidco.

''Iliniuma sana kwani waliouawa siyo waliokuwa wamepora hizo pesa bali ni mimi na wenzangu. Kwa hiyo kama ni kufa mimi ndio nilitakiwa niuawe lakini si wale waliouawa,'' alidai Manyanya na kuongeza kuwa alishangaa kusikia kuwa pesa zilozoporwa ni Sh.5milioni wakati wao walipora Sh.6milioni.

Akijibu maswali kutoka kwa mawakili wa upande wa utetezi, Manyanya alidai amekuwa akifanya kazi hiyo ya wizi kwa muda wa miaka 10 sasa na kwamba hatarajii kuacha hadi atakapokufa jambo ambalo liliwaacha wasikilizaji kuvunjika mbavu.

Yafuatayo ni maswali na majibu kutoka kwa mawakili wa utetezi na shahidi wa 25 Shaban Manyanya.

Maira: Shahidi, leo umetokea wapi kuja hapa mahakamani, nyumbani kwako au gerezani?

Manyanya: Nimetokea nyumbani kwangu.

Maira: Kwa nini siyo gerezani wakati wewe umeiambia mahakama kuwa ni mwizi na ulistahili uwe gerezani?

Manyanya: Kwani polisi hakuna?

Maira: Si ndio waliokuachia?

Manyanya: Waulize wao.

Maira: Umesema wenzako walipokwenda kupora walikuwa na teksi, je kama polisi wa doria, badala ya kufuata teksi ya majambazi wenzako na kwa bahati mbaya wakafuata teksi nyingine wakidhani ndio kundi lako walifanya makosa?

Manyanya: Mimi sikuwepo.

Majura Magafu: Shahidi kutokana na ushahidi wako umekiri kushiriki katika uporaji wa pesa za Bidco kwa kushiriki katika kufanikisha mipango hiyo?

Manyanya: Sawa kabisa.

Majura: Baada ya kuona taarifa za tukio la mauaji kwenye TV. je ulijitokeza kwenye chombo chochote kama vile polisi kuwa waliouawa walionewa au kwa bahati mbaya au nyie ndio mliopora?

Manyanya: Sikufanya hivyo kwa sababu siwezi kujishitaki.

Majura: Umesema uliogopa kukamatwa, je leo hii uko hapa na unajitangaza hivyo, huogopi kukamatwa?

Manyanya: Nilikamatwa na walichukua pesa zote.

Majura: Kwa hiyo unadhani kunyang?anywa hizo pesa ndio ulikuwa adhabu yako?

Manyanya: Unavyojua wewe.

Magafu: Nikisema hujawahi kuwa mwizi na kwa tabia ya mwizi hawezi kujitangaza hivi, utasemaje?

Manyanya: Siyo kweli.

Majura: Wizi ulianza lini?

Manyanya: Miaka 10 iliyopita.

Majura:
Na mpaka sasa leo hii unaendelea?

Manyanya: Bado naendelea.

Majura: Ni lini unategemea kuacha?

Manyanya: Sitegemei kuacha mpaka kufa kwangu.

Majura:Ulishawahi kupatikana na matatizo ya ugonjwa wa akili?

Manyanya: Sijawahi.

Myovela: Mbali na hizo pesa za Bidco unazodai mlipora, je ni wizi gani mwingine huwa unaufanya?

Manyanya: Kuwauzia watu madini hewa.

Mshauri Magreth Mosi:
Hilo group (kundi ) lenu la wizi linafahamika Oysterbay?

Manyanya: Wanalifahamu sana.

Mosi: Enjewele na wenzake alipokuja kwako uliwapa nini hadi wakakuachia na kuwambia mtoroke?

Manyanya: Zile pesa walizochukua.

Sehemu ya maswali na majibu kutoka kwa mawakili hao upande wa utetezi na majibu kutoka kwa shahidi wa 24, SSP Masinde.

Wakili Moses Maira: Shahidi, hebu tusaidie,ulipofika ofisini kwa Zombe ulikuta maofisa wangapi?

Shahidi SSP Masinde: Sikumbuki.

Maira: Umesema Zombe alizungumzia suala la kuwapandisha vyeo je, hiyo imo kwenye PGO? (utaratibu wa maagizo ya utendaji kazi wa jeshi la polisi)

SSP Masinde: Ni maagizo ya mara kwa mara.

Maira: Kwa hiyo Zombe hakuwa nje ya utaratibu kuagiza hivyo??

SSP Masinde: Hakuwa nje ya utaratibu.

Maira: Umesema mkiwa ofisini kwa Zombe, Zombe alionesha fedha na bastola je hizo pesa zilikuwa shilingi ngapi?

SSP Masinde: Sijui kwa sababu hazikuhesabiwa ila alisema tu ni Sh5milioni.

Wakili Gaudioz Ishengoma: Shahidi, umesema taarifa za askari wako kukamata majambazi uliambiwa na Koplo Omary na hukusikia wakati Makelle na Bageni wakiwasiliana, kwani huna ?Radio Call??

SSP Masinde: Ninayo lakini nimesema siku hiyo nilikuwa niko shuleni hivyo huko sikuwa nayo.

Wakili Rongino Myovela: Shahidi, umesema Noel na Felix wao huwa ni wasindikizaji tu wa askari wanaopewa silaha kwenda kazini, je utakubaliana nami kuwa siku hiyo hakuna silaha waliyochukua kwa sababu ni wasindikizaji tu?

SSP Masinde: Ni kweli.

Mshauri wa Mahakana, Nicolas Kimolo: Shahidi, hebu ifahamishe mahakama, ulipopata taarifa kwa Omary kuwa askari wako wamekamata majambazi alikwambia wamewapeleka wapi?

SSP Masinde: Hakusema hilo na kwa kuwa alikuwepo Mkuu wa Upelelezi (OC-CID) wa Wilaya ya Kinondoni na OC-CID wa Kituo cha Urafiki ambao wote ni viongozi mimi sikutaka kufuatilia zaidi niliwachia tu wafanye kazi.

Mshauri Magreth Mosi: Je, Zombe alisema majambazi waliokamatwa wako wapi?

SSP Masinde: Hilo hakulisema.

Mosi: Ulipoambiwa kuwa silaha hazikuitumika lakini majambazi wamekamatwa wakiwa na silaha, je taarifa hizo uliichukuliaje?

SSP Masinde: Niliichukulia kwamba hapakuwa na mapambano ya kurushiana risasi maana kama kungekuwa na kurushiana risasi ingekuwa ni ua nikuue hivyo risasi zingekuwa zimetumika.

Naye shahidi wa 26 katika kesi hiyo, Ramadhan Said Tupa (32) jana aliieleza Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam jinsi alivyowatuliza polisi na pesa alizopora kwenye tukio la ujambazi.

Shahidi huyo ambaye ni mfanyabishara ndogondogo na mkazi wa Mwananyamala kabla ya kuanza kutoa ushahidi wake alinyoosha kidole na kumuomba jaji amlinde kutokana na ushahidi atakaoutoa.

Alidai katika mahakama hiyo kuwa mwanzoni mwa mwezi Januari mwaka 2006 akiwa Dar es Salaam alifuatwa na marafiki zake wawili Italaka na Kei na kumweleza kuwa kuna ?dili? la pesa.

Alidai baada ya marafiki zake kumueleza ?dili? hilo aliwataka aonane na muhusika mkuu ambaye ni dereva wa kampuni ya Bidco aliyemtaja kwa jina moja la Mashaka.

''Tulikutana na Mashaka Mwananyamala B. Januari 14, mwaka 2006 nikiwa nyumbani nilifuatwa na Italaka na aliniambia mipango iko tayari na tukaenda barabarani kusubiri gari lipite ili tupore pesa,'' alidai Tupa.

Tupa alieleza walipora fedha hizo za Bidco katika eneo la barabara ya Sam Nujoma na kwamba zilikuwa kwenye mfuko wa rambo wa rangi ya bluu.

''Lile gari lilipofika pale tulilisimamisha tukamwambia dereva tupe chetu akatoa mfuko wenye hela, sisi huwa hatutumii silaha ya aina yoyote bali ni maneno tu,'' alieleza Tupa.

Shahidi huyo aliyeonekana kujiamini wakati wa kutoa ushahidi wake aliendelea kuieleza mahakama kuwa baada ya uporaji huo walikwenda baa.

Alidai kuwa baada ya kutoka baa waliondoka kwenda kwa rafiki yao mmoja aliyemtaja kwa jina moja la Lunje ambako huko walihesabu fedha walizopora na kupata Sh6milioni.

Alidai waligawana na alipata Sh1.7 milioni na Lunje alipata Sh3milioni na kwamba waligawana viwango tofauti kutokana na ugumu wa kazi.

Alidai Januari 16, mwaka 2006 majira ya saa 4:00 asubuhi alikutana na Koplo Joel wa Kituo cha Polisi cha Oysterbay ambaye alimuuliza kuhusu wizi huo na kwamba yeye alikataa.

''Baada ya kuona askari wananisumbua Januari 17, mwaka 2006 niliamua kwenda nyumbani kwa mke wa askari Enjewele wa Kituo cha Polisi cha Oysterbay ili kumuomba namba ya mumewe nimpigie tumalizane,'' alisema Tupa .

Alidai alipewa namba hiyo ya simu na kumpigia Enjewele na kwamba walikutana usiku wa Januari 17, mwaka 2006 na kumpa Sh 400,000.

Alidai baada ya kumpa fedha hizo, Enjewele alimtaka atoe hela nyingine na kwamba alimuagiza aende Kituo cha Mwananyamala A.

''Nilipofika pale nilivamiwa na maaskari wawili Hadilu na Mabela wote wa Kituo cha Polisi cha Oysterbay wakanionyesha kitambulisho na bastola na kunipeleka Kituo cha Polisi cha Mwinyijuma CCM kilichoko Mwananyamala,'' alieleza Tupa.

Shahidi huyo alidai alipofika katika kituo hicho Hadilu alimwambia kuwa anataka Sh 200,000 na kwamba yeye alimjibu kuwa ameshawapa askari wenzake.

Alidai baada ya kuona wanamsumbua aliagiza mtu aende kumuita dada yake aliyemtaja kwa jina moja la Tausi na kwamba kabla hajafika polisi walimfundisha aseme uongo kwamba amekamatwa kwa wizi wa simu ili dada yake amuwekee dhamana.

Alidai dada yake alipofika alitoa Sh 40,000 na kwamba polisi walimuachia.

Shahidi huyo pia aliieleza mahakama kuwa aliamua kwenda kutoa taarifa za uporaji huo kwenye tume iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete kutokana na uchungu alioupata wa kusikia roho za watu ambao hawana hatia wameuawa.

''Niliamua kwenda kule tume kwa sababu wale waliouawa sio majambazi kama kuuawa ilikuwa tuuawe sisi, nilisikia uchungu sana halafu polisi walizidi kunifuata fuata kila siku na kuchukua hela zangu,'' alieleza Tupa.

Baadhi ya mahojiano na mawakili yalikuwa kama ifuatavyo:

Wakili Nsemwa: Shahidi kutokana na ushahidi ulioutoa hapa utakubaliana nami kuwa wewe ni mwizi?

Shahidi: Ndio.

Nsemwa: Je unafahamu kama wizi ni kosa la jinai?

Shahidi: Ndio.

Nsemwa: Katika matukio ya uhalifu je umeiba mara ngapi?

Shahidi: Hili la Bidco ni tukio langu la pili ila nimezoea wizi wa 'nyatunyatu' (kibaka).

Nsemwa: Huo wizi wa 'nyatunyatu' umekuwa ukiufanya wapi?

Shahidi: Uswahilini.

Wakili Magafu: Je, katika matukio yako ya wizi uliwahi kushikwa na polisi?

Shahidi: Ndio nashikwa halafu tunamalizana.

Magafu: Tangu ulipofanya uporaji wa hela za Bidco uliwahi kufikishwa mahakamani?

Shahidi: Sijawahi.

Magafu:
Wewe polisi ni marafiki zako?

Shahidi: Hapana ila nawapenda kama wakiwa wakweli.

Magafu:
Uchungu unaousema ni uchungu gani hasa?

Shahidi: Baada ya kusikia Zombe anatangaza kwenye vyombo vya habari kuwa wamewaua majambazi wa Bidco wakati ni uongo nilisikia uchungu sana.

Magafu:
Utakubaliana nami kuwa kuombwa ombwa hela na polisi ndiko kumekufanya usikie uchungu na kwenda kutoa taarifa kwenye tume?

Shahidi: Ndio lakini mbali ya hela ni uchungu wa Watanzania wenzangu waliouawa bila hatia.

Kesi hiyo namba 26 ya mwaka 2006 kwa mara ya kwanza, Zombe na wenzake 12 walifikishwa mahakamani Septemba 28, mwaka juzi mbele ya aliyekuwa Jaji Mfawidhi wa mahakama hiyo, Laurian Kalegeya ambaye sasa ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa.

Kesi hiyo inaendelea tena leo katika mahakama hiyo.
 
loh dis kesi is very interestin na hapo zombe alijibuje???maana maovu yao yooote yanazidi fichuliwa tuuuu lakini kwa vile ni tz mie yangu macho tu,watu wanaweza wasifungwe hapo
 
Hivi mwizi akikiri mahakamani kwamba yeye ni mwizi, amekuwa akiiba mara kadhaa na ataendelea kuiba maisha yake yote, anaachiwa tu? au anakamatwa mara tu baada ya kutoka mahakamani ili kumhoji na ushahidi ni yeye mwenyewe! loh hao jamaa kweli ni machizi.

Hao akina Enjewele (askari wa Osterbay) bado wapo hapo Osterbay? au hawa washikaji wametumwa! hii haiingii akilini!
 
Natumaini huyo shahidi amepewa protection / immunity baada ya kujitokeza ahojiwe na tume ya Jaji Kipenka; na hivyo hawezi kukamatwa!!!
 
Imetolewa mara ya mwisho: 11.06.2008 0150 EAT

•
Kesi ya Zombe, wenzake: Shahidi hakuamini kuwapo majibizano ya risasi

sogeza Habari Zinazoshabihiana
• Kesi ya Zombe na wenzake Tume yasisitiza Polisi ilidanganya 05.08.2006 [Soma]
• Kesi ya Zombe yanguruma ... Shahidi akana kuona majibizano ya risasi 30.05.2008 [Soma]
• Kesi ya Zombe, wenzake. Mtaalamu athibitisha silaha zinazodaiwa kuua 06.06.2008 [Soma]

Na Grace Michael

SHAHIDI wa 27 wa Upande wa Mashitaka katika kesi ya mauaji inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Abdallah Zombe na wenzake, Bw. Maxminus Ubisimbai (61) amedai kuwa hakuamini maelezo aliyopewa na OC CID Bw. Christopher Bageni, kuhusiana na majibizano ya risasi.

Amedai kuwa alishindwa kuamini maelezo hayo kutokana na kwamba katika eneo la tukio hakukuta alama yoyote ya damu.

Majibizano hayo ya risasi yalidaiwa kutokea Sinza katika ukuta wa Posta kutokana na majambazi hao kujeruhiwa na kupoteza maisha muda mfupi wakipelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Hayo yalidaiwa jana na Bw. Ubisimbai katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam, mbele ya Jaji Kiongozi Salum Masati, wakati akitoa ushahidi wake kuhusiana na tukio na wafanyabiashara wa madini kutoka Mahenge, Morogoro, wanaodaiwa kuuawa na askari Polisi.

Akiongozwa na wakili wa Serikali, Bw. Jason Kaishozi, ilikuwa ifuatavyo:

Swali: Unafanya kazi gani?
Jibu: Nafanya kazi ya upolisi makao makuu ya Polisi kitengo cha kushughulikia makosa ya wizi wa kalamu.

Swali: Unakumbuka nini Januari 19, 2006?
Jibu: Nakumbuka nilikuwa ofisini kwangu na ilipofika saa mbili usiku, niliitwa na MrakibuMwandamizi wa Polisi (SSP) Mgawe, aliyekuwa hoteli ya Movenpick na nilikwenda nikakutana naye.

Swali: Je alikupa taarifa?
Jibu: Aliniambia kuwa anatakiwa kufanya uchunguzi wa tukio la mauaji ya Sinza, hivyo alinitaka tuwe pamoja katika uchunguzi.

Swali: Mlifanya nini?
Jibu: Tuliondoka mpaka kituo Kikuu cha Kati na kuonana na aliyekuwa Kaimu Kamanda, Bw. Zombe, ambaye ofisini kwake alikuwa na Mrakibu wa Polisi (SP) Mkumbo, SP Masawe na Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Bageni.

Swali: Nini kiliendelea?
Jibu: SSP Mgawe alimpa taarifa Bw. Zombe kuwa ameagizwa kufanya uchunguzi wa mauaji ya Sinza na atasaidiana na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Mgasa na mimi.

Swali: Ulifanya nini wewe?
Jibu: Nilimuuliza Zombe kama eneo la tukio tayari amelikagua na yeye alijibu bado hajafika eneo hilo, hivyo tulikubalina kesho yake tuanze kulikagua.

Swali: Je mlikwenda?
Jibu: Kesho yake tuliondoka mpaka Oysterbay kwa Bageni na tukiwa pale, alikuja Bw. Zombe na kuongozana naye Sinza ambako kulidaiwa kufanyika majibizano ya risasi, hivyo Bageni alipanda gari la Zombe.

Swali: Mlipita maeneo gani?
Jibu: Aliyekuwa akituongoza ni Bageni hivyo alitupeleka mpaka barabara ya Sam Nujoma ambako alitueleza kutekwa kwa gari ya BIDCO na majambazi waliokuwa na bastola.

Swali: Yeye alitoa amri gani baada ya tukio hilo?
Jibu: Baada ya kupata maelezo kuwa majambazi wamekimbia alitoa amri kwa askari wake kufuatilia gari la majambazi na wakiwa kwenye safari hiyo maeneo ya ukuta wa Posta, walikuta magari mawili, moja likiwa la rangi nyeusi na lingine nyeupe.

Swali: Nini kilifuata?
Jibu: Kilichofuata, baada ya maelezo hayo tulipanda kwenye magari na kuelekea ukuta wa Posta ambapo ni kama kilometa moja hivi.

Tukiwa hapo Bageni alitueleza kuwa siku ya tukio akiwa na askari wake, waliingilia njia ya uchochoro wa Posta na kukuta hayo magari, lakini ghafla watu waliokuwa kwenye gari jeusi, mmoja wao alirusha risasi kwa askari.

Swali: Alifanya nini?
Jibu: Alisema baada ya kurushiwa risasi, alitoa amri kwa vijana wake kujibu mashambulizi na muda huo majambazi hao walikuwa wakijaribu kutoroka kwa kuruka ukuta huo.

Walijeruhiwa na askari hao kwa risasi hivyo wakakamatwa na kupandishwa kwenye gari ili wapelekwe Muhimbili, lakini Bageni aliokota bastola pembeni mwa majeruhi hao.

Swali: Walikwenda Hospitali?
Jibu: Wakiwa njiani kuelekea Hospitali walipita kwanza eneo lilipofanyika tukio la BIDCO ambapo waliovamiwa waliweza kuwatambua majeruhi hao.

Swali: Mkiwa eneo hilo mliokota nini?
Jibu: Yaliokotwa maganda mawili ya risasi ambayo awali Bageni alikuwa amedai kuwa ni ya SMG, lakini baada ya kuyaona yalikuwa ni ya bastola.

Swali: Je ukuta huo ulikuwa na nini?
Jibu: Kwenye ukuta huo kulikuwa na matundu ambayo yanasemekana kuwa ni ya risasi, lakini kitu ambacho kilinifanya nipate shaka na hilo tukio, ni kukosekana kwa damu eneo hilo.

"Kwa kweli niliingiwa shaka, kwani kama kweli watu wanne wote wamejeruhiwa haiwezekani damu ikosekane na kwa uzoefu nilionao, ilinipa shaka kubwa," alidai shahidi.

Swali: Je uliuliza kwa nini hapakuwa na damu?
Jibu: Niliuliza lakini nilijibiwa kuwa jana yake mvua ilikuwa imenyesha na kutokana na shaka hiyo, nilizungumza na majirani wengi, lakini walijibu kuwa hapakuwa na tukio la aina yoyote ile.

Swali: Baada ya hapo nini kiliendelea?
Jibu: Tulirudi hadi makao makuu ya Polisi.

Akihojiwa na mawakili wa utetezi ilikuwa ifuatavyo:

Maira: Kwa nini hukuendelea na uchunguzi wako?
Jibu: Sikuendelea kutokana na kuundwa kwa Tume, lakini ripoti yangu ilipelekwa kwa Tume pia.

Maira: Je ungependa itolewe kama kielelezo?
Jibu: Hapana, kwani mimi si Mwenyekiti wa timu yetu, hivyo itatolewa na Mwenyekiti.

Baada ya jibu hilo, Bw. Maira aliomba ripoti hiyo ipokewe kama sehemu ya kielelezo, ambayo ilikuwa imesema kuwa waliouawa ni majambazi.

Jaji alikubaliana na ombi hilo na kutupilia mbali pingamizi la upande wa mashitaka, lakini shahidi huyo alidai kuwa ripoti hiyo iliandikwa kutokana na maelezo yaliyokuwa yametolewa na OC CID Bageni, ambaye alikuwa eneo la tukio.

Akihojiwa na Wakili Gaudioze Ishengoma kuhusiana na wasiwasi wake katika majibizano ya risasi, alidai kuwa hakuamini maelezo yote aliyopewa kutokana na kukosekana kwa damu eneo la majibizano na hakuridhika na jibu la kunyesha kwa mvua.

Akihojiwa na Mzee wa Baraza, Bw. Nicholaus Kimolo, kuhusiana na marehemu walikopelekwa, alidai kuwa kwa mujibu wa maelezo ya Bageni, marehemu hao walifia eneo la tukio la wizi wa BIDCO kabla hawajafika hospitali.

Swali: Kielelezo gani kinaonesha hao walikuwa ni majambazi?
Jibu: Kwa mujibu wa maelezo ya Bageni.

Upande wa mashitaka uliiomba mahakama kuahirisha kesi kutokana na kuwa na shahidi mmoja.

Washitakiwa katika kesi hiyo wanadaiwa kuwa Januari 14 mwaka juzi, katika msitu wa Pande Luisi, Mbezi, Dar es Salaam walimuua kwa makusudi Bw. Ephraim Chigumbi, Bw. Sabinus Chigumbi, Bw. Juma Ndugu na Bw. Mathias Lukombe.

Washitakiwa hao ni Bw. Zombe, Bw. Bageni, Bw. Ahmed Makele, F5912 Noel Leonard, WP4513 Jane Andrew, D6440 Nyangerella Moris, D1406 Mabula, E6712 Felix, D8289 Michael, D2300 Abeneth, B1321 Rashid Lema, D4656 Rajab Bakari na D1367 Festus Gwabisabi.

Source: Majira
 
Kesi ya Zombe, wenzake..Tume ya Rais yapingana na ya Polisi

Na Grace Michael

MKURUGENZI wa Mashitaka Nchini, Bw. Eliezer Feleshi ambaye ni shahidi wa 28 katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara wa madini kutoka Mahenge, Morogoro amedai mahakamani kuwa Tume iliyoundwa na Rais haikuafikiana na ripoti iliyotolewa na Tume ya Jeshi la Polisi, ambayo iliundwa kuchunguza tukio hilo.

Mbali na kutoafikiana na taarifa hiyo, alidai kuwa pia Tume ya Rais ilibaini kutokuwapo uhalali wowote wa nguvu kutumika kuua wafanyabiashara hao, kwani bastola waliyokuwa nayo tayari ilikuwa imeshachukuliwa na askari wakati wanawakamata Sinza, Palestina.

Hayo yalisemwa jana katika Mahakama Kuu ya Tanzania, mbele ya Jaji Kiongozi Salum Masati, wakati Bw. Feleshi akitoa ushahidi wake kuhusiana na kesi inayowakabili askari Polisi akiwamo aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Abdallah Zombe.

Bw. Feleshi ndiye alikuwa Katibu wa Tume ya Rais na jana alitoa ushahidi wake akiongozwa na Wakili wa Kuteuliwa, Bw. Mugaya Mutaki na ilikuwa kama ifuatavyo:

Mutaki: Unafanya kazi gani?
Feleshi: Nafanya kazi Wizara ya Katiba na Sheria kama Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP).

Swali: Januari 23, 2006 ulipata taarifa gani?
Jibu: Siku hiyo nilipata taarifa ya kuteuliwa kuwa Katibu wa Tume ya kuchunguza vyanzo, mazingira na sababu za vifo vya marehemu wanne waliouawa Sinza.

Swali: Wenzako walikuwa ni akina nani?
Jibu: Jaji Issa Kipenka kama Mwenyekiti, Bibi Mwantumu Malale, Profesa Ibrahim Juma, Bw. Aford Mwaipenga na wengine.

SWali: Mlikuwa na hadidu za rejea?
Jibu: Ndiyo tulikuwa nazo ambazo ni kuchunguza vyanzo, mazingira na sababu za vifo, kuchunguza ukweli wa maelezo ya polisi ambayo yalidai kuwa waliouawa ni majambazi, kutambua uhalali wa nguvu iliyotumika kuua na kutambua kazi, majina na wanakoishi marehemu.

Swali: Ni muda gani mlitakiwa kumaliza kazi hiyo?
Jibu: Tume ilipewa siku 21 za kufanya kazi hiyo na ilianza rasmi Januari 26, 2006 katika ukumbi wa Karimjee na mashahidi walitumiwa samansi, lakini wengine walijitokeza kutokana na tangazo tulilolitoa kupitia vyombo vya habari.

Swali: Mlianza vipi kazi hiyo?
Jibu: Kwa kuwa barua ya uundwaji Tume ilikuwa ikijieleza na ikitaka waitwe askari wote waliohusika na tukio hilo, tuliwaita askari hao.

Swali: Walikuja hao askari?
Jibu: Januari 26, 2006, Bw. Christopher Bageni, alikuja na askari wake aliokuwa nao kwenye tukio, Bw. Zombe naye alikuja pamoja na watu wengine ambao walikuwa wamejitokeza kwa siku hiyo na Tume iliamua kuwachanganya na tulianza na raia watatu, ndipo tulipomhoji Bw. Zombe.

Swali: Mlitumia utaratibu gani?
Jibu: Utaratibu uliotumika ulikuwa ni wa kisheria, ikiwamo kuapishwa.

Swali: Je Dar es Salaam mlitumia siku ngapi?
Jibu: Kulingana na wingi wa mashahidi waliokuwa Dar es Salaam, tulikaa mpaka Februari mosi, 2006 ambapo jumla ya mashahidi 69 walikuwa wamehojiwa wakiwamo wawili kutoka Arusha.

Swali: Ushahidi huo mlikuwa mnaurekodi vipi?
Jibu: Tuliuchukua kwa maandishi, lakini pia tulitumia kinasa sauti.Baada ya hapo tulilazimika kutembelea maeneo matatu ambayo tuliongozwa na Bw. Bageni aliyekuwa kwenye tukio hilo na tulianzia Sam Nujoma kulikodaiwa kutokea tukio la uporaji wa BIDCO.

Eneo lingine tulikwenda ukuta wa Posta, ambapo palidaiwa kufanyika majibizano ya risasi kati ya askari na marehemu hao.

Swali: Mlipofika hapo, Bageni alieleza nini?
Jibu: Bageni na askari wenzake waliokuwa kwenye tukio siku hiyo walikiri kufika eneo hilo wakifukuza majambazi na kutuonesha mahali walipofyatua risasi dhidi ya majambazi hao.

Swali: Tume iliona viashiria vyovyote vya mapambano?
Jibu: Kwenye ukuta kulikuwa na matundu lakini cha ajabu hapakuwa na viashiria vyovyote kama damu na hii ndiyo iliyowafanya makamishina wangu kuhoji sana suala hili na walihoji namna askari hao walivyokuwa wamekaa wakati wa kufyatua risasi. Tume ilihoji sana uwezekano wa watu wanaoruka ukuta kupata majeraha sehemu moja.

Swali: Kwa nini mlihoji uwezekano huo?
Jibu: Tulihoji kwani tayari tulikuwa na ripoti ya daktari aliyewafanyia uchunguzi wa vifo hao, marehemu ambao risasi zilionesha kuingilia pingili ya sita ya shingo na kutokea nyuma.

Swali: Je hao askari waliwapa hayo majibu?
Jibu: Hapana, hawakuweza kutupa majibu zaidi ya kushikilia msimamo wao kuwa walifyatua risasi wakati marehemu wakiruka ukuta, hali iliyoifanya Tume kubaki na maswali mengi juu ya hilo.

Swali: Mlifanya nini baada ya kukosa ukweli?
Jibu: Tuliamua kupata maelezo kutoka kwa watu mbalimbali wanaozunguka eneo la ukuta wa Posta, ambao wote walikana kuona au kusikia tukio lolote la ujambazi likitokea.

Swali: Mlielekea wapi tena?
Jibu: Katika eneo la tatu, tuliamua kuachana na hawa askari na kubaki peke yetu ambapo tulielekea Sinza Palestina na kukutana na watu walioshuhudia namna marehemu wakikamatwa na askari hao mpaka kufungwa pingu na kupandishwa gari wakiwa wazima.

Swali: Je Bageni na wenzake waliwaambia tukio hilo lilitokea muda gani?
Jibu: Walisema tukio hilo lilikuwa saa 12 hadi saa 12.30 hivi za jioni. Baada ya kutoka Sinza Palestina, tulielekea White Sands ambako Tume ilikuwa na ukumbi mdogo wa mashahidi, ambao hawakutaka kufika katika ukumbi mkubwa wa Karimjee.

Swali: Mliishia hapo?
Jibu: Februari 2, 2006 tulisafiri kwenda Mahenge ambako kesho yake tulihoji watu zaidi ya 12 na kwenda kijijini kwao marehemu, Ipango, ambako tulifika kwa shida sana.

Ipango ilikuwa ni kutaka kujua uhalali wa kazi za marehemu na majina yao, lakini pia walijitokeza watu wengi sana kuelezea kazi za marehemu na wachimbaji wadogo wadogo ambao walikuwa kwenye mgodi wa marehemu.

Tukiwa Mahenge mjini alijitokeza Inspekta wa Polisi Maganga na kueleza namna marehemu Jongo alivyofuata taratibu za kupata bastola na hawakuwa na kumbukumbu yoyote kuhusiana na matukio ya ujambazi hivyo walikuwa ni watu safi.

Tukiwa Ipango tulizungumza na baba wa marehemu Mathias, pamoja na baba yao akina Chigumbi, ambao walieleza kazi walizokuwa wakifanya marehemu.

Swali: Mlifika kwenye migodi yao?
Jibu: Ndiyo tulifika na kuambiwa kuwa marehemu Jongo alikuwa amepata jiwe la mwaka ambalo ni kubwa sana na jiwe hilo lilichukuliwa na marehemu kwa ajili ya kufanyiwa biashara huku Arusha na Dar es Salaam.

Swali: Mlirudi lini?
Jibu: Tuliondoa huko Februari 4, 2006 na kesho yake tuliendelea na uchunguzi hapa Dar es Salaam ambapo tulipigiwa simu na Bw. Shabaan Manyanya, ambaye alidai yuko Zanzibar, lakini alituhoji usalama wake.

Baada ya kutuhoji usalama wake, ilibidi tumuulize kwa nini anasema hivyo, ndipo aliposema kuwa anatafutwa na Polisi na yeye ndiye aliyeshiriki wizi wa BIDCO, hivyo tulimwelekeza namna ya kufanya hadi kufika kwetu.

Swali: Je, askari waliwaambia marehemu wakiwa majeruhi walipelekwa wapi?
Jibu: Walisema waliwapeleka Muhimbili na hakuna aliyesema walifia wapi mbali na ripoti iliyotolewa hospitalini hapo.

Swali: Je Tume ilihoji mashahidi wangapi?
Jibu: Jumla ya mashahidi 90 na wengine 31 tuliwakataa kutokana na ushahidi wao kujirudiarudia, na wengine kuelezea matukio mengine tofauti na hilo.

Swali: Baada ya hapo Tume iliona nini?
Jibu: Haikuridhika na maelezo ya Polisi kuhusu marehemu kuhusika na tukio la BIDCO, kwani muda huo walikuwa maeneo mengine.

Kitu kingine, Tume haikuridhika na kuwapo majibizano ya risasi na iliona kuwa waliohusika kuwakamata watu hao wakiwa wazima na kuwapeleka Muhimbili, ndio wanawajibika kueleza kilichotokea.

Baada ya kuona hivyo, Tume ilipendekeza kuwa sheria ichukue mkondo wake kwa wahusika wa vifo vya marehemu na ripoti ilikabidhiwa kwa Rais Februari 17, 2006.

Akihojiwa na mawakili wa upande wa utetezi, ilikuwa kama ifuatavyo:

Msemwa: Unamfahamu mshitakiwa wa kwanza na alikamatwa lini?
Jibu: Namfahamu na sikumbuki alikamatwa lini.

Swali: Sasa mshitakiwa huyo ana malalamiko kuwa alipokamatwa ofisini kwake Juni 9, 2006 na kupelekwa mahakamani, hakuwa amehojiwa maelezo yake. Je ukiwa kama DPP ni halali kufanya hivyo?

Swali: Mimi ni shahidi na sikuwa mpelelezi wa kesi hiyo lakini si lazima kuchukuliwa maelezo, kitu cha muhimu kama upo ushahidi wa kutosha na mchakato wa sasa, ni mahakama kusikiliza na kuthibisha makosa.

Swali: Je hiyo ripoti ya Tume unayo hapo?
Jibu: Ripoti iko kwa Rais na kwa mujibu wa sheria mwenye mamlaka ya kuitoa ni yeye.

Swali: Ripoti ilisemaje kuhusu Zombe?
Jibu: Ilipendekeza kuwa achukuliwe hatua za kinidhamu lakini hakuwa miongoni mwa askari 15 waliotakiwa kufikishwa mahakamani.

Swali: Nani alitoa amri ya kushambulia?
Jibu: ASP (Mrakibu Msaidizi wa Polisi) Bageni alitoa amri hiyo na askari wengine walieleza namna walivyosimama na kushiriki.

Swali: Mligundua ni kitu gani mmedanganywa?
Jibu: Ni kurushiana risasi na kujeruhi watu bila kuwapo damu wala majirani kusikia mlio wowote wa risasi.

Magafu: Majina ya watuhumiwa mliyapata wapi?
Jibu: Tuliyapata kupitia taarifa ya Polisi.

Swali: Mlikuwa mkiwahoji mara ngapi?
Jibu: Tulikuwa tukiwahoji kulingana na utata wa kila mtu, hivyo Bw. Zombe tulimhoji mara mbili kuhusiana na tukio.

Swali: Je Bageni hakuwa na maelezo kuhusu kukosekana kwa damu?
Jibu: Alidai kuwa yawezekana kwa sababu ya mvua.

Myovela: Ripoti ilikuwa na kurasa ngapi?
Jibu: Ilikuwa na kurasa 69 na tape recorders 36.

Swali: Kazi ya Tume ilikuwa na kusudi lipi?
Jibu: Kumwezesha mwenye mamlaka kutoa maelekezo, lakini mahakama ni kusikiliza na kufikia uamuzi.

Swali: Kwa nini hukuamini kama kulikuwa na majibizano?
Jibu: Siamini mpaka leo, kwani marehemu watatu risasi ziliingilia sehemu moja na ni maajabu kwa watu wanaoparamia ukuta kuwa hivyo na nilitarajia kukuta chochote ukutani au chini walipodondoka marehemu, lakini maelezo yote ya akina Bageni hatukuyaamini na ndiyo maana tuliendelea kutafuta ushahidi mwingine.

Akiohojiwa tena na Bw. Mutaki ilikuwa hivi:

Swali: Aliyekuwa na mamlaka ya kumshitaki Zombe ni nani?
Jibu: Alikuwa ni DPP na si aliyekuwa DCI Adadi Rajab kama alivyonukuliwa na gazeti la Mwananchi, akisema kuwa Zombe hawezi kushitakiwa.

Swali: Nini kiliwafanya kumwita Zombe mara mbili?
Jibu: Ni kutokana na utata wa taarifa, kwani taarifa ya kwanza ilisema marehemu hao walipigwa risasi wakiwa ndani ya gari na taarifa nyingine ilisema kuwa walipigwa risasi wakiwa katika ukuta wa Posta.

Wakihoji wazee wa baraza ilikuwa kama hivi:

Kimolo: Je ni askari wangapi walikuwa eneo la tukio na wangapi walirusha risasi?
Jibu: Askari 15 walikuwa eneo la tukio, wakiwamo wa Urafiki, Oysterbay na Chuo Kikuu, lakini ni wawili ndio waliorusha risasi.

Swali: Kitu gani Bageni kilimfanya atoe amri hiyo?
Jibu: Kwa maelezo yao walidai kuwa Bageni naye alikuwa akiwasiliana na wengine ambapo na yeye alipata amri kutoka ngazi ya juu.


Swali: Je Tume ilibaini nini kuhusu nguvu iliyotumika?
Jibu: Tume ilibaini kuwa hapakuwa na uhalali wa nguvu iliyotumika, kwani marehemu tayari walikuwa wameshachukuliwa bastola yao wakati wanakamatwa.

Mosi: Kwa nini Tume ilibaki na maswali mengi?
Jibu: Tume ilibaki na maswali kutokana na kukosekana viashiria vyoyote vya majibizano ya risasi na watu kujeruhiwa, lakini pia Tume kuridhika na ushahidi wa kukamatwa kwa marehemu wakiwa hai na bila kuwapo purukushani ya aina yoyote.

Swali: Marehemu waliuawa katika eneo lipi?
Jibu: Tume haikubaini ni mahali gani marehemu waliuawa mbali ya kutilia shaka eneo lililodaiwa kuhusika na Tume iliridhika, kuwa askari waliokamatwa ndio waliohusika na nguvu hiyo.

Swali: Je mlikubaliana na taarifa ya Tume ya Polisi?
Jibu: Taarifa ya Tume ya Polisi hatukuafikiana nayo kwani haikuhusisha watu wa Sinza na majirani wa ukuta wa Posta na baada ya kufika hapo, hatukuweza kuamini kabisa.

Upande wa mashitaka haukuwa na shahidi mwingine hivyo uliomba kuahirisha kesi ambapo Jaji Masati alisema itaendelea leo saa 5 asubuhi.

Washitakiwa katika kesi hiyo wanadaiwa kuwa Januari 14, mwaka juzi wakiwa katika msitu wa Pande Luisi,Mbezi, Dar es Salaam, walimuua kwa makusudi Bw. Ephraim Chigumbi, Bw. Sabinus Chigumbi, Bw. Juma Ndugu na Bw. Mathias Lukombe.

Washitakiwa hao ni Bw. Zombe, Bw. Bageni, Bw. Ahmed Makele, F5912 Noel Leonard, WP4513 Jane Andrew, D6440 Nyangerella Moris, D1406 Mabula, E6712 Felix, D8289 Michael, D2300 Abeneth, B1321 Rashid Lema, D4656 Rajab Bakari na D1367 Festus Gwabisabi.

Source: Majira, Alhamis Juni 12, 2008
 
Kwa kweli ninaingia wasiwasi pale mkuu wa polisi anaposema wanahitaji ushirikiano na wananchi ili wafanikiwe kuwakamata wananchi.hapo kwa kiasi fulani nakubaliana nae ,ila kuzuia uhalifu na kuumaliza sidhani kama kunahitajika ushirikiano na wananchi kwani Jeshi la polisi limefundishwa njia na njama za kuwajua na kuwakamata wahalifu sasa unaposema mwananchi nae ashiriki umekusudia kitu gani ?

Mwananchi ambae amekudiwa ni raia wa kawaida kabisa hana himaya ya ulinzi wowote ,iwe anawajua wahalifu kwa majina bado hatokuwa na ulinzi pindipo akiwataja na kuwaripoti wahalifu hao ambao inawezekana kabisa kwa jinsi ya aina ya wahalifu tulio nao wanamawasiliano ya namna fulani na polisi ,na ripoti iliyopelekwa juu yao inaweza kirahisi ikajulikana ni nani aliepeleka ripoti hiyo na hapo ndipo anapoanzwa kuandamwa na si ajabu hata maisha yake yakakatishwa na wale polisi waliokuwa wakisisitiza ushirikiaji hawaonekani katika kusaidia zaid watakuwa hata hawajihusishi au kusema kilichomuua mtoa ripoti ni sababu ya yeye kupeleka habari kituoni.
Kazi ya kuwafichua wahalifu ni kazi ya Polisi tena inatakiwa raia asihushwe kabisa kuna njia za askari kanzu na nyingi nyenginezo ambazo zikitumika ipasavyo basi wahalifu hawatakuwa na pahala pa kujificha ,inawezekana kabisa polisi wa kituo kingeni kwenda kufanya uchunguzi mbali kabisa na maeneo yao na wakishagundua wanaweza kupeleka ripoti katika kituo husika ,mkuu tumegundua selo ya wahalifu katika maeneo yako sehemu fulani na sehemu fulani hukusanyika na kupanga maangamizi saa fulani na hulewa na kulala bar na guest fulani.

Sasa kumtuma mwananchi afanye kazi hiyo ni kumpoza ,kwani wananchi wengi wana imani wahusika wa ujambazi huwakusanya pia wenye kazi ya upolisi pengine huyo huyo unaemshitakia ndie jambazi wenyewe hapo si utakuwa umeshajichora.

Hii ni kazi ya polisi fedha wanayolipwa ni hutokana na kodi za hao wananchi hivyo kamati za ulinzi za vituo zipanue wigo na kuchunguza sehemu ambazo hata hawajulikani kama wao ni polisi, waweke rasta ,wavae kihuni huni tu ,wavute bangi wapulize na unga huku wakipatiwa treatment bila ya kuathiri afya zao ndivyo tuonavyo kwenye nchi nyengine jinsi wachunguzi wa polisi wanavyojichanganya na majambazi na wavuta bangi. Sio hapo mnarudi eti mwananchi shirikianeni naona mnataka kuwajua wale wanaotoa habari na waliowasitukia maficho yenu.Akina Zombe mko wengi ndani ya jeshi la Polisi.
 
Wana JF, kesi hii ni ya kipee sana, inatuonesha namna ufisadi ulivyokuwa unaendelea kulivamia Taifa kila kona yaani BOT, TANESCO, ATCL, hadi POLISI nk. Kesi hii imeanza tena baada ya kuahirishwa kwa muda wa miezi kadhaa. Haya ndo yaliyoendelea jana.


Katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, mahakama hiyo ilielezwa na upande wa mashtaka kuwa mshitakiwa wa 11 Koplo Rashidi alishinikizwa na wakuu wake wa kazi, Zombe na Bageni, kutoa maelezo ya uongo kwenye tume ya Polisi na ya Jaji Kipenka.

Shahidi huyo, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Edson Mmari (55) kwa sasa ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora na wakati wa tukio hilo alikuwa Mpelelezi wa Makosa ya Kuwania mali, Makao Makuu ya Upelelezi.

ACP Mmari aliieleza mahakama kuwa alikuwa ni mmoja wa maofisa walioteuliwa kuchunguza kesi ya mauaji inayomkabili Zombe na polisi wenzake.

"Baada ya kuteuliwa tuliambiwa washitakiwa wamekamatwa na wako Kituo cha Polisi Kati (Central) hivyo tuliwahoji,"alisema ACP Mmari.

Mmary alikuwa akihojiwa na wakili wa Serikali Alexander Mzikila na shahidi huyo aliieleza mahakama hiyo kuwa Machi 6, mwaka 2006 majira ya asubuhi aliitwa makao makuu ya upelelezi.

Alidai baada ya kufika ofisini na mshitakiwa wa 11 Koplo Rashidi kutoka kituo cha Polisi cha Kati (Central) alifikishwa ofisi hiyo ya upelelezi. Baada ya maelezo hayo majadiliano yalikuwa kama ifuatavyo:-

Wakili Mzikila: Baada ya mshitakiwa huyo kuletwa makao makuu ya upelelezi mlifanya nini?

Shahidi: SSP Mkumbi alimuuliza jinsi anavyofahamu tukio hilo na mshitakiwa alisema maelezo yote aliyoeleza tume ya polisi na ile ya Jaji Kipenka yalikuwa ni ya uongo na kwamba angetueleza ukweli wa tukio lilivyotokea.

Wakili: Alieleza ni sababu zipi zilizomfanya atoe maelezo ya uongo?

Shahidi: Alidai maelezo ya uongo aliyoyatoa, alishinikizwa na viongozi wake wa kazi yaani Zombe na Christopher Bageni (mshitakiwa namba mbili) na alionyesha kikaratasi kilichoandikwa maelezo aliyotakiwa kujibu kwenye tume hizo.

Wakili: Baada ya hapo mlifanya nini?

Shahidi: Mimi na afisa mwingine wa polisi Inspekta Omar tulimpeleka mshitakiwa katika mahakama ya Mwanzo Kinondoni kwa ajili ya kutoa maelezo ya ungamo.

Wakili: Wakati anatoa maelezo ya ungamo kwa mlinzi wa amani wewe na afisa mwenzako mlikuwa wapi?

Shahidi: Tulikuwa nje.

Wakili: Katika upelelezi wenu mlifanya nini tena?

Shahidi: Machi 6, mwaka 2006 mshitakiwa PC Rashidi alitueleza kuwa yuko tayari kutuonyesha eneo halisi la tukio.

Wakili: Tukio lipi hilo?

Shahidi: Tukio la majambazi ambao walidaiwa kuuawa katika msitu wa Pande huko Mbezi Luis.

Wakili: Je mlikwenda huko?

Shahidi: Machi 7, mwaka 2006, saa 4 asubuhi tuliondoka mimi na maafisa wengine tuliokuwa tukifanya upelelezi na kwenda huko katika msitu wa Pande.

Wakili: Je ni nani alikuwa akiwaonyesha njia?

Shahidi: Mshitakiwa ndiye alikuwa akituonyesha njia.

Wakili: Eneo hilo likoje?

Shahidi: Ndani ya msitu wa Pande hakuna makazi ya watu lakini kuna barabara inayofika eneo hilo.

Wakili: Nyie kama timu ya upelelezi mlifanya nini?

Shahidi: Katika msitu ule yalipatikana maganda mawili ya risasi yanayoweza kutumika kwenye bunduki aina ya SMG na SAR na pia tuliona damu iliyokuwa imeganda na kuchanganyika na udongo.

Wakili: Baada ya hapo mlifanya nini?

Shahidi: Tulichukua sampuli ambayo ilipelekwa kwa Mkemia Mkuu wa serikali kwa ajili ya kubaini kama damu ile ni ya binadamu au ya mnyama.

Wakili: Nini matokeo ya uchunguzi huo wa Mkemia Mkuu?

Shahidi: Matokeo yalionyesha kuwa ile ilikuwa ni damu ya binadamu.

Wakili: Katika upelelezi wenu mlifanya kitu gani tena?

Shahidi: Tulipiga picha za video na za kawaida na pia tulichora ramani ya eneo lile.

Wakili: Mshitakiwa alieleza nini zaidi ya hayo?

Shahidi: Alieleza kuwa yeye binafsi hakuhusika kuwapiga marehemu risasi bali Koplo Saad ambaye bado hajakamatwa ndiye aliyehusika.

Pia alidai marehemu hao walikuwa wakitolewa mmoja mmoja kutoka kwenye gari na kulazwa kifudifudi na kupigwa risasi.

Wakili: Baada ya kumaliza mlielekea wapi?

Shahidi: Mshitakiwa alidai kwamba katika ya Januari 17 na 18 mwaka 2006 waliagizwa na Bageni (Mshitakiwa wa pili) waende Bunju wakafyatue risasi na kumletea maganda ya risasi na alienda huko akiwa na Koplo Saad.

Wakili: Je mlienda huko?

Shahidi: Tulienda na mshitakiwa alituonyesha walikofyatulia risasi.

Wakili: Je walifyatua risasi ngapi?

Shahidi: Rashidi alidai walifyatua risasi 3 na mwezake Koplo Saad alifyatua risasi 6.

Wakili: Nyie kama timu mlifanya nini zaidi ya hayo?

Shahidi: Pia tulipiga picha za video na za kawaida.

Wakili: Baada ya shughuli hiyo mlifanya nini tena?

Shahidi: Tulienda Makao Makuu ya Upelelezi na kuandika tena maelezo ya Rashidi ili kueleza aliyokwenda kutuonyesha.

Wakili: Nyie kama wapelelezi mlifanya nini tena?

Shahidi: Tulienda kuangalia kitabu cha kumbukumbu za silaha kuona kama bunduki hizo zilichukuliwa kihalali na kwamba risasi ngapi zilitumika.

Wakili: Kitabu hicho ni cha kituo kipi?

Shahidi: Ni cha kituo cha polisi cha Oysterbay.

Wakili: Katika kitabu hicho mliona nini?

Shahidi: Tuliona kuwa Januari 14, mwaka 2006 Rashidi alipewa silaha na risasi 30 na alirejesha Januari 15 mwaka 2006 na alirudisha risasi zote lakini kulionekana kumefutwafutwa na kuandikwa risasi 27. Kwa Coplo Saad ilionyesha zilipungua risasi 9.

Wakili: Rajabu alikamatwa lini na alipelekwa lini mahakamani?

Shahidi: Alipelekwa Machi 8, mwaka 2006.

Wakili: Shahidi ulisema mliandika maelezo ya mshitakiwa wa pili SSP Bageni, je alisema nini kuhusu shitaka linalomkabili?

Shahidi: Bageni hakukiri kosa moja kwa moja bali alidai kulikuwa na mapambano kati ya polisi na majambazi na yeye alitoa maelekezo majambazi hao wauwawe.

Wakili: Bageni alikueleza matokeo yoyote ya mapambano hayo na majambazi?

Shahidi: Alidai mapambano hayo, yalitokea katika ukuta wa posta Sinza na baada ya mapambano hayo waliokuwa wakidaiwa ni majambazi walijeruhiwa.

Wakili: Kilifuata nini baada ya maelezo hayo?

Shahidi: Februari 20, mwaka 2006 tuliwafikisha washitakiwa mahakamani.

Wakili: Siku hiyo washitakiwa walikuwa wangapi?

Shahidi: walikuwa washitakiwa 8.

Wakili: Februari 22 ulikuwa wapi?

Shahidi: Nilikuwa ofisini na tuliondoka na maafisa wengine kwenda eneo la tukio Sinza block C Palestina karibu na maduka.

Wakili: Kwanini ulienda Sinza Block C badala ya kule alikosema Bageni?

Shahidi: Tulienda huko baada ya kupata maelezo ya mashahidi kwamba wanaodaiwa kuwa ni majambazi walikamatwa eneo la Sinza C.

Wakili: Madhumuni ya kwenda huko yalikuwa nini?

Shahidi: Tulienda huko kwasababu hao marehemu walidaiwa kuwa walifika kwa mama Bernadetha Lyimo (shahidi wa 2) kumpelekea fedha na huko tulimkuta pia Majatta Kayamba (shahidi wa 6).

Wakili: Baada ya hapo kilifuata nini?

Shahidi: Mjatta alituonyesha mahali ambapo marehemu walikuwa wamepaki gari lao na nyumba ambayo marehemu Sabinus alikwenda kukabidhi fedha kwa mama Bernadetha.

Wakili: Nyie kama wapelelezi mlifanya nini?

Shahidi: Tulipiga picha za video na za kawaida pamoja na kuchora ramani ya eneo lile.

Wakili: Baada ya hapo kilifuata nini?

Shahidi: Tulienda eneo la Sam Nujoma mahali ambako kunadaiwa gari la kampuni ya Bidco liliporwa fedha.

Wakili: Katika upelelezi wenu mlifanya nini hapo?

Shahidi: Tulichora ramani na baada ya hapo tuliondoka kwenda posta kulikodaiwa kuwa kulitokea tukio la mapambano kati ya majambazi na polisi.

Wakili: Eneo hilo likoje?

Shahidi: Pembeni yake kuna nyumba na gereji.

Wakili: Kutoka ukuta wa posta hadi gereji kuna umbali gani?

Shahidi: Kwa kukisia ni kati ya hatua 10 hadi 15?

Wakili: Je urefu wa ukuta wa posta ukoje?

Shahidi: Ukuta ni mrefu kiasi kwamba huwezi kuchungulia upande wa pili.

Wakili: Katika ukuta huo, mliona nini?

Shahidi: Tuliona matundu manne yanayodaiwa kuwa yalipigwa na bunduki aina ya SMG.

Wakili: Matundu hayo yalikuwa na umbali gani?

Shahidi: Hayakupishana sana.

Wakili; Ulivyoyaona yalipigwaje?

Shahidi: Yalipigwa kwa usawa.

Wakili: Kitu gani kingine uliona.

Shahidi: hakukuwa na kitu kingine.

Wakili: Je mlihoji majirani?

Shahidi: Tulihoji na walisema hawakuwahi kusikia milio ya risasi siku ya Januari 14, mwaka 2006.

Wakili: Je mlifanya uchunguzi kujua silaha zilizotumika?

Shahidi: Zilitumika SMG.

Wakili: Mlijua zilitoka kituo kipi na zilitumika ngapi?

Shahidi: Zilitoka kituo cha polisi cha Oysterbay Dar es Salaam na zilitumika SMG mbili.

Wakili: Mlipeleleza kujua walikabidhiwa askari gani?

Shahidi: Moja alipewa Coplo Saad na nyingine alipewa Constebo Rashidi (mshitakiwa wa 11).

Baada ya mahojiano hayo wakili Mzikila aliiomba mahakama iende maeneo mbalimbali ya tukio ambayo shahidi huyo, ameyazungumzia katika ushahidi wake yakiwemo msitu wa Pande ulioko Mbezi Luis ambako wafanyabiashara hao, wanadaiwa kuuawa.

Kutokana ombi la wakili Mzikila, kesho Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, mawakili na waandishi wa habari watakwenda kutembelea maeneo ambayo, shahidi huyo, amezungumzia jana mahakamani.

Jaji Kiongozi Salum Massati alikubali na kuahirisha kesi hiyo hadi leo itakapoendelea tena.



Source: Mwananchi
 
Ofisi zafungwa kusikiliza kesi ya Zombe, Koplo akiri uongo kwa Jaji Kipenka

Mshtakiwa wa kwanza katika mauaji kwa kukusudia ya wafanyabiashara ya madini,Mkuu wa Upelelezi wa zamani wa mkoa wa Dar es Salaam ACP, Abdallah Zombe, enzi zake akiwa ofisini.
Na Nora Damian

SHAHIDI wa 30, Edson Mmari katika Kesi ya mauaji ya wafanyabiashara wa madini wa Mahenge inayomkabili Mkuu wa Upelelezi wa zamani wa mkoa wa Dar es Salaam ACP Abdallah Zombe na wenzake jana, imeendelea kuwa kivutio kikubwa huku baadhi ya wafanyakazi karibu na Mahakama Kuu wakifunga ofisi zao ili kufuatilia mwenendo wa kesi hiyo.

Kesi hiyo, ilianza saa 4.30 na Jaji Salum Massati alipoingia katika chumba namba moja, watu waliokuwa wakisubiri kesi hiyo kwa hamu, walikimbilia katika chumba hicho huku wakipigana vikumbo kutafuta nafasi za kukaa.

Baadhi ya makarani katika mahakama hiyo, walionekana wakiingia katika chumba namba moja ambako kesi hiyo, inasikilizwa na kutoka na kurudi kwenye chumba hicho kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo.

Karani mmoja alisikika akisema kesi hiyo ni ya aina yake na kwamba hawezi kuacha kuifuatilia licha ya kuwa alikuwa na kazi nyingi wakati kesi hiyo, ikiendelea.

Watu wengine wakazi wa jijini Dar es Salaam waliohojiwa kwa nyakati tofauti na kuomba kutotajwa majina yao, walisema wametoroka kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo na moja kati yao, alisema anafanya kazi Wizara Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Mkazi wingine wa Kiwalani ambaye pia hakutaka kutaja jina lake, alisema anafanya kazi Kampuni ya ulinzi ya Armor Group (Tz) Ltd) ya jijini Dar es Salaam.

"Sijatoroka kazini, leo niko ‘off' lakini jioni nitaingia kazini nimekuja kuisikiliza hii kesi kwani nimekuwa nikisoma kwenye magazeti tu, sasa leo nimekuja kabisa ili nijue kinachoendelea," alisema mfanyakazi wa Armor group.

Naye Athumani Mussa mkazi wa Temeke aliyekuwa nje ya mahakama hiyo, alisema tangu kuanza kwa kesi hiyo, hajawahi kukosa kuisikiliza kwa kuwa ina mvuto na pia kiongozi wa cheo cha juu kufikishwa mahakamani.

Nje ya chumba namba moja ambako kesi hiyo, inasikilizwa kabla ya kesi kuanza, watu wengi walikuwa wamekusanyika ili kusubiri kuanza kwa kesi hiyo huku wengine wakiulizana mwisho wa kesi hiyo, itakuwaje.

Katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, mahakama hiyo ilielezwa na upande wa mashtaka kuwa mshitakiwa wa 11 Koplo Rashidi alishinikizwa na wakuu wake wa kazi, Zombe na Bageni, kutoa maelezo ya uongo kwenye tume ya Polisi na ya Jaji Kipenka.

Shahidi huyo, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Edson Mmari (55) kwa sasa ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora na wakati wa tukio hilo alikuwa Mpelelezi wa Makosa ya Kuwania mali, Makao Makuu ya Upelelezi.

ACP Mmari aliieleza mahakama kuwa alikuwa ni mmoja wa maofisa walioteuliwa kuchunguza kesi ya mauaji inayomkabili Zombe na polisi wenzake.

"Baada ya kuteuliwa tuliambiwa washitakiwa wamekamatwa na wako Kituo cha Polisi Kati (Central) hivyo tuliwahoji,"alisema ACP Mmari.

Mmary alikuwa akihojiwa na wakili wa Serikali Alexander Mzikila na shahidi huyo aliieleza mahakama hiyo kuwa Machi 6, mwaka 2006 majira ya asubuhi aliitwa makao makuu ya upelelezi.

Alidai baada ya kufika ofisini na mshitakiwa wa 11 Koplo Rashidi kutoka kituo cha Polisi cha Kati (Central) alifikishwa ofisi hiyo ya upelelezi. Baada ya maelezo hayo majadiliano yalikuwa kama ifuatavyo:-

Wakili Mzikila: Baada ya mshitakiwa huyo kuletwa makao makuu ya upelelezi mlifanya nini?

Shahidi: SSP Mkumbi alimuuliza jinsi anavyofahamu tukio hilo na mshitakiwa alisema maelezo yote aliyoeleza tume ya polisi na ile ya Jaji Kipenka yalikuwa ni ya uongo na kwamba angetueleza ukweli wa tukio lilivyotokea.

Wakili: Alieleza ni sababu zipi zilizomfanya atoe maelezo ya uongo?

Shahidi: Alidai maelezo ya uongo aliyoyatoa, alishinikizwa na viongozi wake wa kazi yaani Zombe na Christopher Bageni (mshitakiwa namba mbili) na alionyesha kikaratasi kilichoandikwa maelezo aliyotakiwa kujibu kwenye tume hizo.

Wakili: Baada ya hapo mlifanya nini?

Shahidi: Mimi na afisa mwingine wa polisi Inspekta Omar tulimpeleka mshitakiwa katika mahakama ya Mwanzo Kinondoni kwa ajili ya kutoa maelezo ya ungamo.

Wakili: Wakati anatoa maelezo ya ungamo kwa mlinzi wa amani wewe na afisa mwenzako mlikuwa wapi?

Shahidi: Tulikuwa nje.

Wakili: Katika upelelezi wenu mlifanya nini tena?

Shahidi: Machi 6, mwaka 2006 mshitakiwa PC Rashidi alitueleza kuwa yuko tayari kutuonyesha eneo halisi la tukio.

Wakili: Tukio lipi hilo?

Shahidi: Tukio la majambazi ambao walidaiwa kuuawa katika msitu wa Pande huko Mbezi Luis.

Wakili: Je mlikwenda huko?

Shahidi: Machi 7, mwaka 2006, saa 4 asubuhi tuliondoka mimi na maafisa wengine tuliokuwa tukifanya upelelezi na kwenda huko katika msitu wa Pande.

Wakili: Je ni nani alikuwa akiwaonyesha njia?

Shahidi: Mshitakiwa ndiye alikuwa akituonyesha njia.

Wakili: Eneo hilo likoje?

Shahidi: Ndani ya msitu wa Pande hakuna makazi ya watu lakini kuna barabara inayofika eneo hilo.

Wakili: Nyie kama timu ya upelelezi mlifanya nini?

Shahidi: Katika msitu ule yalipatikana maganda mawili ya risasi yanayoweza kutumika kwenye bunduki aina ya SMG na SAR na pia tuliona damu iliyokuwa imeganda na kuchanganyika na udongo.

Wakili: Baada ya hapo mlifanya nini?

Shahidi: Tulichukua sampuli ambayo ilipelekwa kwa Mkemia Mkuu wa serikali kwa ajili ya kubaini kama damu ile ni ya binadamu au ya mnyama.

Wakili: Nini matokeo ya uchunguzi huo wa Mkemia Mkuu?

Shahidi: Matokeo yalionyesha kuwa ile ilikuwa ni damu ya binadamu.

Wakili: Katika upelelezi wenu mlifanya kitu gani tena?

Shahidi: Tulipiga picha za video na za kawaida na pia tulichora ramani ya eneo lile.

Wakili: Mshitakiwa alieleza nini zaidi ya hayo?

Shahidi: Alieleza kuwa yeye binafsi hakuhusika kuwapiga marehemu risasi bali Koplo Saad ambaye bado hajakamatwa ndiye aliyehusika.

Pia alidai marehemu hao walikuwa wakitolewa mmoja mmoja kutoka kwenye gari na kulazwa kifudifudi na kupigwa risasi.

Wakili: Baada ya kumaliza mlielekea wapi?

Shahidi: Mshitakiwa alidai kwamba katika ya Januari 17 na 18 mwaka 2006 waliagizwa na Bageni (Mshitakiwa wa pili) waende Bunju wakafyatue risasi na kumletea maganda ya risasi na alienda huko akiwa na Koplo Saad.

Wakili: Je mlienda huko?

Shahidi: Tulienda na mshitakiwa alituonyesha walikofyatulia risasi.

Wakili: Je walifyatua risasi ngapi?

Shahidi: Rashidi alidai walifyatua risasi 3 na mwezake Koplo Saad alifyatua risasi 6.

Wakili: Nyie kama timu mlifanya nini zaidi ya hayo?

Shahidi: Pia tulipiga picha za video na za kawaida.

Wakili: Baada ya shughuli hiyo mlifanya nini tena?

Shahidi: Tulienda Makao Makuu ya Upelelezi na kuandika tena maelezo ya Rashidi ili kueleza aliyokwenda kutuonyesha.

Wakili: Nyie kama wapelelezi mlifanya nini tena?

Shahidi: Tulienda kuangalia kitabu cha kumbukumbu za silaha kuona kama bunduki hizo zilichukuliwa kihalali na kwamba risasi ngapi zilitumika.

Wakili: Kitabu hicho ni cha kituo kipi?

Shahidi: Ni cha kituo cha polisi cha Oysterbay.

Wakili: Katika kitabu hicho mliona nini?

Shahidi: Tuliona kuwa Januari 14, mwaka 2006 Rashidi alipewa silaha na risasi 30 na alirejesha Januari 15 mwaka 2006 na alirudisha risasi zote lakini kulionekana kumefutwafutwa na kuandikwa risasi 27. Kwa Coplo Saad ilionyesha zilipungua risasi 9.

Wakili: Rajabu alikamatwa lini na alipelekwa lini mahakamani?

Shahidi: Alipelekwa Machi 8, mwaka 2006.

Wakili: Shahidi ulisema mliandika maelezo ya mshitakiwa wa pili SSP Bageni, je alisema nini kuhusu shitaka linalomkabili?

Shahidi: Bageni hakukiri kosa moja kwa moja bali alidai kulikuwa na mapambano kati ya polisi na majambazi na yeye alitoa maelekezo majambazi hao wauwawe.

Wakili: Bageni alikueleza matokeo yoyote ya mapambano hayo na majambazi?

Shahidi: Alidai mapambano hayo, yalitokea katika ukuta wa posta Sinza na baada ya mapambano hayo waliokuwa wakidaiwa ni majambazi walijeruhiwa.

Wakili: Kilifuata nini baada ya maelezo hayo?

Shahidi: Februari 20, mwaka 2006 tuliwafikisha washitakiwa mahakamani.

Wakili: Siku hiyo washitakiwa walikuwa wangapi?

Shahidi: walikuwa washitakiwa 8.

Wakili: Februari 22 ulikuwa wapi?

Shahidi: Nilikuwa ofisini na tuliondoka na maafisa wengine kwenda eneo la tukio Sinza block C Palestina karibu na maduka.

Wakili: Kwanini ulienda Sinza Block C badala ya kule alikosema Bageni?

Shahidi: Tulienda huko baada ya kupata maelezo ya mashahidi kwamba wanaodaiwa kuwa ni majambazi walikamatwa eneo la Sinza C.

Wakili: Madhumuni ya kwenda huko yalikuwa nini?

Shahidi: Tulienda huko kwasababu hao marehemu walidaiwa kuwa walifika kwa mama Bernadetha Lyimo (shahidi wa 2) kumpelekea fedha na huko tulimkuta pia Majatta Kayamba (shahidi wa 6).

Wakili: Baada ya hapo kilifuata nini?

Shahidi: Mjatta alituonyesha mahali ambapo marehemu walikuwa wamepaki gari lao na nyumba ambayo marehemu Sabinus alikwenda kukabidhi fedha kwa mama Bernadetha.

Wakili: Nyie kama wapelelezi mlifanya nini?

Shahidi: Tulipiga picha za video na za kawaida pamoja na kuchora ramani ya eneo lile.

Wakili: Baada ya hapo kilifuata nini?

Shahidi: Tulienda eneo la Sam Nujoma mahali ambako kunadaiwa gari la kampuni ya Bidco liliporwa fedha.

Wakili: Katika upelelezi wenu mlifanya nini hapo?

Shahidi: Tulichora ramani na baada ya hapo tuliondoka kwenda posta kulikodaiwa kuwa kulitokea tukio la mapambano kati ya majambazi na polisi.

Wakili: Eneo hilo likoje?

Shahidi: Pembeni yake kuna nyumba na gereji.

Wakili: Kutoka ukuta wa posta hadi gereji kuna umbali gani?

Shahidi: Kwa kukisia ni kati ya hatua 10 hadi 15?

Wakili: Je urefu wa ukuta wa posta ukoje?

Shahidi: Ukuta ni mrefu kiasi kwamba huwezi kuchungulia upande wa pili.

Wakili: Katika ukuta huo, mliona nini?

Shahidi: Tuliona matundu manne yanayodaiwa kuwa yalipigwa na bunduki aina ya SMG.

Wakili: Matundu hayo yalikuwa na umbali gani?

Shahidi: Hayakupishana sana.

Wakili; Ulivyoyaona yalipigwaje?

Shahidi: Yalipigwa kwa usawa.

Wakili: Kitu gani kingine uliona.

Shahidi: hakukuwa na kitu kingine.

Wakili: Je mlihoji majirani?

Shahidi: Tulihoji na walisema hawakuwahi kusikia milio ya risasi siku ya Januari 14, mwaka 2006.

Wakili: Je mlifanya uchunguzi kujua silaha zilizotumika?

Shahidi: Zilitumika SMG.

Wakili: Mlijua zilitoka kituo kipi na zilitumika ngapi?

Shahidi: Zilitoka kituo cha polisi cha Oysterbay Dar es Salaam na zilitumika SMG mbili.

Wakili: Mlipeleleza kujua walikabidhiwa askari gani?

Shahidi: Moja alipewa Coplo Saad na nyingine alipewa Constebo Rashidi (mshitakiwa wa 11).

Baada ya mahojiano hayo wakili Mzikila aliiomba mahakama iende maeneo mbalimbali ya tukio ambayo shahidi huyo, ameyazungumzia katika ushahidi wake yakiwemo msitu wa Pande ulioko Mbezi Luis ambako wafanyabiashara hao, wanadaiwa kuuawa.

Kutokana ombi la wakili Mzikila, kesho Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, mawakili na waandishi wa habari watakwenda kutembelea maeneo ambayo, shahidi huyo, amezungumzia jana mahakamani.

Jaji Kiongozi Salum Massati alikubali na kuahirisha kesi hiyo hadi leo itakapoendelea
 
Mwema kuna haja ya kuwa na nyangau kama huyu


kweli mwema unampa ukamanda wa mkoa????????????


R u serious??????????????????????

katika mahakama kuu ya tanzania, kanda ya dar es salaam, mahakama hiyo ilielezwa na upande wa mashtaka kuwa mshitakiwa wa 11 koplo rashidi alishinikizwa na wakuu wake wa kazi, zombe na bageni, kutoa maelezo ya uongo kwenye tume ya polisi na ya jaji kipenka.
 
Hili ni jeshi la polisi au jeshi la manyang'au. Mheshimiwa Masha, safisha hilo jeshi la majambazi.

Kuna jamaa aliniambia mauaji ya namna hii yako mengi tu na huko nyuma raia wengi walikuwa wanauawa kwa njia kama hizi na mapolisi fisadi.

Huyo Zombe sio tu afungwe lakini wataifishe hata mali zake zote.

Pia inaelekea jeshi letu la polisi halina maadili kabisa. Mkuu anakuambia kaue na unaenda kweli kuua, kwanini? Je hakuna sehemu kwa kwenda kutoa siri kimya kimya na kuokoa maisha ya raia wema?
 
Mkulu Zombe hili kalikoroga kisawa sawa hapa alinywe tu yaani noma tupu!
 
Back
Top Bottom