Kesi ya Abdallah Zombe: Mashitaka, hatia, hukumu na yanayojiri

Kesi ya Abdallah Zombe: Mashitaka, hatia, hukumu na yanayojiri

Hivi kumbe hata mahakama kuu zina wazee wa baraza? Mimi nilifikiri ni kwa mahakama za mwanzo tu?
 

By the way, hivi kuna shahidi yeyote aliweza kumtetea Zombe kwa kusema, mfano, siku hayo yote yanatokea Zombe alikuwa amelazwa au hakuwepo nchini na hivyo hakushiriki kosa kwa namna yoyote ile?
Hiyo inaitwa 'alibi' inatamkwa 'alabai' Zombe hakuhitaji ushahidi huu kwa sababu hakuna ushahidi wa yeye kuwepo eneo la tukio.
Ushahidi wa alibi unahitajika pale tuu kinapofanyika kitendo cha mauaji'first degree murder' mwili ukapatikana na mshukiwa ni fulani. Baada ya taarifa ya uchunguzi wa forensic, inayohusisha na muda sahihi wa tukio, mshukiwa anatakiwa kuthibitisha alikuwa wapi muda huo. Kama kesi ya OJ. Simpson.
Zombe hakuwepo, ila ushahidi wa circumstancial utamtia hatiani kwa negligence kama kesi ya Kombe.
Kwa vile aliyepiga risasi hajapatikana, mbele ya wanasheria mahiri, jamaa wote wanashinda kesi.
 
"Abdallah Zombe, mtuhumiwa aliyehukumiwa kabla ya hukumu"

Kosa kubwa, Media inaripoti Zombe tu kana kwamba hakuna washtakiwa wengine. Hii inawapotosha wananchi wengi hasa wasiopenda kufuatilia kwa undani juu ya kesi hii. Kuna baadhi hawajui kabisa kama Zombe anakabiliwa kesi hii pamoja na askari wengine kadhaa. Media zimeharibu mwendo mzima wa kesi kwa kuiita 'kesi ya Zombe'
 
Hiyo inaitwa 'alibi' inatamkwa 'alabai' Zombe hakuhitaji ushahidi huu kwa sababu hakuna ushahidi wa yeye kuwepo eneo la tukio.
Ushahidi wa alibi unahitajika pale tuu kinapofanyika kitendo cha mauaji'first degree murder' mwili ukapatikana na mshukiwa ni fulani. Baada ya taarifa ya uchunguzi wa forensic, inayohusisha na muda sahihi wa tukio, mshukiwa anatakiwa kuthibitisha alikuwa wapi muda huo. Kama kesi ya OJ. Simpson.
Zombe hakuwepo, ila ushahidi wa circumstancial utamtia hatiani kwa negligence kama kesi ya Kombe.
Kwa vile aliyepiga risasi hajapatikana, mbele ya wanasheria mahiri, jamaa wote wanashinda kesi.

Pasco,
Nadhani Magobe anahitaji sana kuangalia zile CSI au Forensic Files zinaweza kumpa mwanga zaidi
 
"Abdallah Zombe, mtuhumiwa aliyehukumiwa kabla ya hukumu"

Kosa kubwa, Media inaripoti Zombe tu kana kwamba hakuna washtakiwa wengine. Hii inawapotosha wananchi wengi hasa wasiopenda kufuatilia kwa undani juu ya kesi hii. Kuna baadhi hawajui kabisa kama Zombe anakabiliwa kesi hii pamoja na askari wengine kadhaa. Media zimeharibu mwendo mzima wa kesi kwa kuiita 'kesi ya Zombe'
Mkuu,
Taarifa zisizo rasmi zinasema kuwa ukiachana na hawa wafanyabiashara wa madini,ZOMBE AMETUMIA VIBAYA SANA MADARAKA YAKE KWA KUUA WATU WENGI MNO KWA MTINDO HUOHUO,ndio maana wamemuandama sana.na huwezi amini,presha yote inaanzia eneo lake la kazi
 
Kwa ushahidi wa mazingira Zombe anaweza tiwa hatiani kwa Accessory to Murder kwa sababu kwa nini afundishe wengine jinsi ya kujibu! Ina maanisha alikuwa anajua nini kimetokea ila alikuwa anawalinda wauaji
 
Muda umebakia mfupi sana mbivu na mbichi tutajizijua...tuachie jaji na wazee wake wa baraza then mpira atakuwa nao jaji ataamua.....tutaitafakari tena umamuzi wake...kama rufaa zitakatwa...zitasikilizwa tena na tena hadi tutajua mwisho wa mwisho kabisa....kama kesi ya babu seya...ila haki haitapotea ya marehemu na ya hao washitakiwa.....kwenye ukweli na haki ....uongo utajitenga tu....damu ya watu mbaya sana haipotei hv hv...
 
Wana JF,

Nakumbuka tangu siku ile alipouwawa mbwa wa polisi kule Kawe na majambazi (sikumbuki tarehe), lilitokea wimbi la mauaji ya ajabu kwa watu wote waliotuhumiwa kuwa majambazi. Kulikuwa na case nyingi za mauaji ya majambazi ambazo kama ungefuatilia undani wake kwa karibu ungegundua kwamba kulikuwa na uongo mwingi na wakati huo ukitangazwa na Kamanda Mstaafu Tibaigana. Kwa mfano kuna siku alishawahi kutangaza kuwa kuna majambazi yalikuwa yanafuatiliwa na askari na walipofika eneo ninaloishi (samahani sitalitaja) majambazi yaligundua kwamba yanafuatwa na polisi na kuamua kusimamisha gari lao na kuwatupia askari risasi kabla ya kuanza kukimbia na wananchi kuwafukuza, kuwakamata na kuwaua. Hii taarifa ulikuwa ni uongo mtupu kwani katika eneo hilo hakukuwa na mlio wa risasi kwa mwezi ule mzima achilia mbali siku hiyo. Ukweli ni kwamba watu wale waliuwawa na polisi sijui wapi na katika mazingira gani lakini eneo la nyumbani kwangu likasingiziwa.

Zombe na kundi lake walitaka kufuata mkondo huo huo na walitaka kuchukua advantage ya ujambazi waliofanyika katika barabara ya Sam Nujoma kama kinga ingawaje marehemu walikuwa watu safi kabisa. Mimi sio mwana sheria lakini nimesoma sheria kidogo. Nimefuatilia kesi hii kwa karibu na niliishafikia hatua ya kusema itakuwa ngumu kumtia Zombe kwenye hatia, ikitiliwa maanani kwamba yeye kama acting Kamanda anapokea taarifa kutoka kwa watendaji wake na kuuarifu umma kupitia vyombo vya habari. Inwezekana kabisa alipewa taarifa za uongo na wasaidizi wake au alijua kinachoendelea remotedly na ushahidi uliotolewa umeshindwa kuonyesha yeye alihusika vipi na hayo mauaji. Hivyo vikaratasi alivyowaandikia washitakiwa wenzake akiwafundisha jinsi ya kujieleza kwa nini havikutolewa kama ushahidi mahakamani? Hii ingemmaliza kabisa.

Tusubiri uamuzi wa mahakama kama ilivyosemekana.

Tiba
 
Ipo mizigo miwili mikubwa juu ya mabega ya Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali (IGP), Said Mwema. Hii ni askari wake watatu wanaotuhumiwa kuua raia watatu, mkoani Arusha na jijini Dar es Salaam.
Tayari kamati mbili tofauti, yaani ile iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Isdore Shirima na ile iliyoundwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Kandoro, zilikwisha kutoa ripoti juu ya mauaji haya na kueleza wazi kwamba waliouawa hawakuwa majambazi.

Mjini Arusha waliuawa vijana wawili Machi mosi mwaka huu, Goodluck Olais Motika (22) na Eward Joseph Mtui (36), wakati jijini Dar es Salaam eneo la Kimara Stopover, kijana Lazaro Mwapi (34) aliuawa kwa kupigwa risasi na polisi Aprili. Kote huko polisi walizusha kwamba waliouawa walikuwa ni majambazi.

Matukio haya yanafanana na lile la Januari 14, 2006 lilitokea jijini Dar es Salaam ambalo wafanyabiashara watatu na dereva teksi mmoja, waliuawa na polisi na kusingiziwa kwamba walikuwa ni majambazi.

Tunajua kwamba kwa sasa ipo kesi ya mauaji Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam ikiwakabili polisi tisa, akiwamo aliyekuwa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam pia akiwa ni Mkuu wa Upelelezi wa mkoa huo, Abdallah Zombe. Kesi hii bado inaendelea na hatuna sababu ya kuingia uhuru wa mahakama kwa kuwa tunaamini kwamba haki itatendeka.

Lakini kilio chetu leo ni kuona jinsi suala zima la polisi wanaotuhumiwa kuua vijana wawili mjini Arusha na mmoja jijini Dar es Slaam, linavyoendeshwa.

Taarifa ambazo zimezagaa mitaani na ambazo hatuna sababu za kuzipuuza kwa sababu zinaeleza undani wa matukio haya mawili, polisi waliohusika na mauji haya bado wako kazini, wanaendelea na kazi kana kwamba hakuna kilichotokea.

Kila mmoja kwa nafasi yake, yaani Kandoro ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, na mwenzake wa Arusha, walipotangaza ripoti za kamati zao, walisema wazi kwamba imethibitika vijana waliouawa hawakuwa majambazi na kwamba taarifa zimepelekwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa ajili ya taratibu zaidi za kisheria.

Tunajiuliza kwamba hadi sasa umma haujui kinachoendelea juu ya hatua hizi za kisheria; wananchi wanataka kujua ni lini askari polisi waliohusika katika kadhia hii watafikishwa mahakamani ili walau imani ya wananchi kwa chombo hiki chenye dhima ya kulinda maisha na mali zao irejee?

Swali hili tunaliuliza si kwa sababu polisi hawa wakifikishwa mahakamani uhai wa waliouawa utarejeshwa, ila wazazi na marehemu wote walau wataona kwamba kweli nchi hii inaendeleshwa kwa utawala wa sheria na si kwa matakwa na hisia za watendaji ndani ya serikali hasa polisi wanaotumia sihala za kuwalinda raia kuwaua wananchi wasio na hatia.

Tunatambua kwamba zipo taratibu za kufuata kabla ya kumfungulia mtu mashitaka mahakamani na hasa inapokuwa ni ya jinai, pamoja na kutambua hatua hizo, lakini tunahisi kwamba kasi si nzuri katika kutekeleza hayo; la muhimu zaidi ni kwamba hatuioni mantiki ya watuhumiwa wa mauaji kuendekea na kazi ya upolisi wakati suala lao likiwa katika mkondo wa sheria. Hawa wakae kando wasubiri hatima yao.

Ni utaratibu wa kisheria kwamba mtu anayetuhumiwa kwa kesi kubwa kama mauaji hukaa kando wakati suala lake likishughulikiwa. Ndiyo maana tunasema IGP Mwema ana mzigo begani mwake, tunadhani ni vema polisi hawa wakawekwa pembeni wakati taratibu nyingine za kisheria zikisubiriwa kutoka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
CHANZO: NIPASHE
 
Verdict in Zombe case out Monday

By Bernard James

The judgement in the murder case facing former Dar es Salaam Crime Officer ACP Abdallah Zombe and his co-accused will be pronounced on Monday, The Citizen has exclusively learnt.

Justice Salum Massati will deliver the eagerly awaited verdict against Mr Zombe and eight other police officers who have been on trial for brutal murder of three gemstone dealers and a taxi driver in 2006 in Dar es Salaam.

Apart from Zombe, others whose fate will be known on Monday are SSP Christopher Bageni , WP Jane Andrew, Assistant ASP Ahmad Makelle, corporals Emanuel Mabula, Michael Shonza, Ebeneth Saro and Corporal Rajabu Bakari.

The Citizen has exclusively established that Justice Massati will wrap-up the marathon trial of the law enforcers, who are accused of murdering businessmen Sabinus Chighumbi, Ephraim Chighumbi, Mathias Lukombe and taxi driver Juma Ndugu at Pande Forest in the outskirts of the city.

The District Registrar of the High Court (Dar es Salaam Zone), Mr Saul Kinemela confirmed the date when reached for an official comment. He, however, declined to divulge any further details.

But highly placed sources within the judiciary said security arrangements were being made to ensure more policemen and prison warders are deployed around the court premises on Monday.

"The judiciary is not taking any chances due to sensitivity of the case," the source said. It is expected that many people including victims' residents will turn out to hear the High Court?s conclusion of the case that dominated media headlines.

While the officers have been maintaining that the four men were killed during a shootout with the police after they robbed a Bidco oil company delivery lorry, the prosecution insists that the robbery incident was staged and that the four were murdered in cold blood at Pande forest.

The deceased were gemstone businessmen from Mahenge, Ulanga district in Morogoro region who had travelled to Dar es Salaam in pursuit of a good market for their gemstone.

It is alleged that at the time of their unwarranted arrest at Dar es Salaam's Sinza suburb, the four men had just sold part of their gemstone in Arusha and had millions of shilling as well as unspecified quantity of gemstone.

It was further alleged that the police officers converged at the scene of the crime and organised the murder of the four men. The prosecution alleged that the officers, with their eyes on gemstone and money, made false claims that the four were bandits who had robbed Bidco sales lorry and Al-mar Jewellers Mkunguni Street in Kariakoo.

According to the prosecution, on the night of January 14, 2006, under the command and coordination of Mr Zombe but direct supervision of SSP Christopher Bageni, the police officers headed the victims to Pande forest at Mbezi Louis, where they executed them.

A pathologist had told the court that the victims' death was due to gun shot wounds. After the murder, the officers shared the victims' belongings at Urafiki police station in the presence of Mr Zombe, it was alleged.

Initially 13 officers were charged in the case but later the prosecution managed to prove their case against nine suspects and three were acquitted in February for lack of evidence and one officer died in hospital.

At the conclusion of the hearing of the trial on June 26, Zombe had all the reasons to smile after court assessors opined that he should be set free for lack of evidence.

The assessors, Mr Nicolous Kimolo and Ms Margareth Mosi, told the court that Zombe and another officer Festus Gwabisabi Should be acquitted because prosecution had failed directly or circumstantially to link them with the murder.


Source: http://thecitizen.co.tz/newe.php?id=14369
 
Hapa kazi ipo. Hao policemen na prison warders watakuwepo ili kuchukua share yao ya wafungwa out of this case au ni nini?? Tusubiri ukweli wenyewe on Monday. May the Allah give me a favor to live till Monday to hear fair judgement from Hon. Masati!!!
 
J3 jiji lote litakuwa na ganzi kusubiria hukumu hiyo....maana itakuwa hukumu ya kihistoria....ktk tanzania...kazi kwake mh jaji masati
 
Kama Babu sea alifungwa kwa haki na huyu atafungwa kwa haki,
 
The clock is ticking and let us wait for the judgement day. it is Judge Masati's show!
 
MAHAKAMA Kuu Tanzania kesho inatarajiwa kutoa hukumu ya kesi ya mauaji inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam, Abdallah Zombe, na wenzake 10.

Zombe na wenzake wanatuhumiwa kuwaua wafanyabiashara watatu wa madini kutoka Mahenge mkoani Morogoro na dereva wa teksi aliyekuwa anaishi Dar es Salaam.

Washitakiwa hao wanadaiwa kuua kwa kukusudia Januari 14, 2006 kwenye msitu wa Pande, Mbezi Luis jijini Dar es Salaam.

Jaji Kiongozi, Salum Massati, anatarajiwa kutoa hukumu hiyo inayosubiriwa kwa hamu hasa ikizingatiwa kuwa kesi hiyo ilikuwa na mvuto wa aina yake.

Mahakama ilimtaka Zombe na wenzake wajibu mashitaka yanayowakabili, walipewa nafasi ya kutoa ushahidi. Mahakama pia ilichambua ushahidi wa upande wa mashitaka na ule wa utetezi uliokuwa na mashahidi 37.

Awali, washitakiwa katika kesi hiyo walikuwa ni Abdallah Zombe, Christopher Bageni, Ahmed Makele, F 5912 Noel Leonard, na WP 4513 Jane Andrew.

Wengine ni D6440 Nyangerella Moris, D1406 Mabula, E6712 Felix, D 8289 Michael, D 2300 Abeneth, B 1321 Rashid Lema, D 4656 Rajab Bakari na D1367 Festus Gwabisabi.

Baada ya uchambuzi baadhi ya washitakiwa waliondolewa katika kesi hiyo wakabaki Zombe, Bageni, Makele, WP 4513 Jane, D1406 Mabula, D8289 Michael, D2300 Abeneth, B1321 Rashid, D4656 Rajab na D1367 Philipo.

Mshitakiwa Lema amefariki dunia hivyo mashitaka dhidi yake yamefutwa.

Kesi hiyo ilianza 2006 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji ilihamishiwa Mahakama Kuu.
http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=3226
 
sie wengine tupo chanika huku,sasa ukisema kesho unatupa kazi ya kujua siku,you mean jumatatu sio?
 
mr kiroboto Una maanisha wewe unataka kwenda kusikiliza kesi ya Zombe Mahakamani?Mimi nimenukuu kwenye gazete lipo hapo chini nimetowa kopi sijazidihsa kitu mr kiroboto jaribu kuifuatilia kwenye Magazeti kesi ya Zombe utapata Latest zote mr kiroboto upende sana kusoma magazeti ndugu mr kiroboto hapa mimi nimekurahishia wewe ujuwe kuwa hata wakubwa wa serikali wanapofanya makosa na kila afanyae makosa hukumu inamhusu Mahakamani ndipo penye haki upo na mimi ndugu mr kiroboto ?
 
Zombe, mtuhumiwa aliyehukumiwa nje ya mahakama kabla ya kesi kusikilizwa.
 
Wanaachi na ndugu wamefurika mahakama kuu nje. Ndani hakuingiliki bila kibali maalum!!! Security is very tight nje na ndani!!!! Inaashiria nini hapo jamani?? Tusubiri, hukumu ndefu ambayo itachukua hours kuisoma, je yatajiri yapi??? Je hukumu hii itakuwa fundisho kwa wasio waaminifu jeshi la polisi au itawapa mwanya zaidi wa kudhulumu mali za wasiokuwa na hatia kwa kuwabambikizia kesi na pengine kuwaua kabisa????.
 
Back
Top Bottom