Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma imekataa ombi la kusaini malalamiko yaliyotolewa na Paul Kisabo dhidi ya Fatma Kigondo maarufu kama Afande, baada ya kubaini kuwa malalamiko hayo yana dosari mbalimbali ikiwemo kutofuata taratibu za kisheria.
Uamuzi huu wa Mahakama uliotolewa siku ya Ijumaa Oktoba 18, 2024 unamaanisha kuwa Fatma Kigondo hatokabiliwa na shitaka lolote dhidi yake.
Pia soma: Mahakama yatupilia mbali ombi la Afande Fatma kusomewa mashtaka popote alipo
Paul Kisabo alikuwa amefungua malalamiko akimlalamikia Fatma Kigondo kwa kosa la kubaka kwa kundi, na Oktoba 15, 2024, Wakili wake Peter Madeleka aliiomba mahakama kusaini malalamiko hayo ili yawe hati ya mashtaka rasmi na mshitakiwa asomewe makosa popote atakapokuwa.
Hata hivyo, uamuzi uliotolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Dodoma, Nyambuli Tungaraja, umesema kuwa kutokana na dosari mbalimbali zilizojitokeza kwenye malalamiko hayo, hayakidhi vigezo vya kusainiwa kuwa hati ya mashtaka.
Jambo TV