Kesi ya Babu Seya na wanae - Ukweli ni upi haswa?

Ulikuwepo wapi wakati wa kesi si ungemtetea na hizi porojo zako? Hivyo tumesahau vile Hakimu aliemuhukumu alikuwa JK vile enhe!
 
no comment nalia-probably coincidence yote mawili yanauma.
 
ndugu zangu ni kweli familia nzima ya nguza vikingi ilifanya tendo la kuzalilisha watoto wa shule ya fulani ya msingi au kunamkono wa mtu ulitumika kuisambaratisha familia hii kongwe yenye mafanikio ya kimuziki? ni kweli baba na watoto wanaweza wakawa wanapeana zamu ya kuchangia tendo la ngono kwa kuwabaka watoto wadogo takribani darasa zima?
 
Kesi ya Babu Seya inanikumbusha kesi ya OJ Simpson, tofauti ni kuwa OJ aliachiwa. Watu huwa wana-sympathize sana na watu maarufu wanapopata matatizo ya kisheria (kumbuka pia R. Kelly) hivyo sishangai nikiona watu wakisema kuwa kina Nguza wameonewa tatizo ni kuwa hakuna aliye na ushahidi kuwa wameonewa zaidi ya maneno ya mitaani.
 
watu wa bagamoyo na msata msata hivi watakuwa wanamnyaka huyu jamaa 😛opcorn::roll:
 

watz wengi hawalioni hilo,je unaweza kushawishi familia 11 zenye baba na mama wenye itikadi tofauti wakubaliane na kisasi chako?watu wangapi wanahukumiwa life sentence lakini kwa sababu sio maarufu no body cares!
Vuta picha kama wewe ni mmoja wa wazazi wa watoto waliotendwa ungecomment nini?
Jaribu kufikiria future ya hao watoto na athari za kiafya na kisaikolojia zilizowapata zimewaathiri kwa kiasi gani
Mambo ya kushobokea watu maarufu yanatugharimu sana,tubadilike!!
 
Jalada anayeandika ni watoto au ni hakimu........ushahidi wa kusema inawezekana ukawa si wa kuandikwa kwenye jalada. lisemwalo lipo......kwamba walibambikizwa kesi inawezekana, tusubiri kuna siku ukweli utajulikana. Ouko wa Kenya aliwawa 1990 lakini ukweli umejulikana mwaka jana mwishoni...........ni baada ya miaka 20 wauaji wajulikana.
 
Binafsi toka mwanzo wa kuifahamu kesi hii iliyojaa kila aina ya mbwembwe na umaarufu kwa sababu ya washtakiwa wenyewe siku zote na kwa mtazamo wangu na upande wa pili unisamehe ila imani yangu ni kwamba pale hakuna kesi zaidi ya siasa chafu na visasi vya kila aina,chuki na ubinafsi wa nafsi ndio vilivyofanya paka leo hii familia ya Nguza Viking ikiteseka bila sababu.Yashasemwa mengi sana kuwa kuna mlono wa mtu pale na hata ukiangalia mwenendo mzima wa kesi utakubaliana nami pasipo shaka kuwa pale kuna ujanja unaofanyika ingawa ni ngumu na siwezi kutibitisha moja kwa moja ila rai yangu na maombi yangu juu yao waweze kuwa huru tena na kama walifanya kweli basi uhuru wao hakika hautadumu huku uraiani...Mtazamo wangu binafsi.
 
Ni kweli mkuu kwani kesi yenyewe ilihusisha watoto wa shule wa miaka 7 ambapo inasemekana Babu Seya na Watoto wake walijamiiana na hao watoto zaidi ya mara moja lakini cha ajabu wazazi hawakuweza kugundua kuwa watoto wao wameingiliwa na mijibaba kama hiyo kwani walikuwa wanacheza na kwenda shule kama kawaida.
 
Uonevu mkubwa sana...viongozi wengi watatupwa jehanam
 
kweli naamini yataisha tu kwani hata wao hawapo salama tofauti na wanavyodhani ipo siku maumivu ya ile familia yatarudi kwao kwa nyakati na mda wasiojua kwani hakuna aliye salama chini ya jua..
 
Kaka huu sio mtazamo wako binafsi:Niukweli usiopingika.MUNGU WANGU NYOSHA MKONO WAKO UMKOMBOE NGUZA VIKIG NA MWANAE.
 
Ipo siku yatawashukia wale wote waliofanya haya,MUNGU WEWE WAJUA,NA OKOA WAJA WAKO
 
Yaani huwa nikiona thread inayomhusu Babu seya huwa nasikitika sana. Lkn naamini kabisa mtu aliyewafanyia kitendo hicho hakika kuna siku atapigwa mapigo ya kutosha na Mungu. Mtu mnyonge siku zote mtetezi wake ni Mungu.
 
Nasita kuomba kwa Mungu kwa sababu najua Mungu hujibu sara na vilio vya watu wake ila, kila mwenye kumjua Mungu basi na aseme Amen kwani yu aja na Ole wake yule....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…