Kesi ya Babu Seya na wanae - Ukweli ni upi haswa?

mmenikumbusha ndugu zangu wa mahenge.sio mahakama za tanzania.
 

Hospital watoto walipimwa ikaonekana hawajaingiliwa kwa vyovyote dokta akatimuliwa akaitwa mwingine kuandika PF3 kuwa waliingiliwa akafanya hivyo muziki usio na mchezaji ukaendelea.

Naomba nikanushe kwa herufi kubwa 'UWONGO' huu hata kama nitakuwa nimeenda kinyume na taaluma na maadili yangu kama Daktari. Sentensi niliyonukuu hapo juu ni UONGO mkubwa! Wakati inatokea hii issue nilikuwa bado nafanya kazi Muhimbili National Hospital, watyoto hawa walichunguzwa katika kitengo cha upasuaji watoto (Paeditric Surgery) chini ya Daktari ambaye namfahamu sana...na ni 'very senior' na anaheshimika Muhimbili kimaadili na mshika dini.

Kwa kesi ya kubaka, details zinakuwa kwenye faili na si PF3 kama muandishi anavyotaka kutuaminisha, PF ni Police Form inayomsaidia mtu kupata matibabu hospitali na haina details za nini amegundulika nacho mgonjwa. Details za kwenye faili ndio hutumika mahakamani wakati wa kutoa ushaidi (na sio PF3).

Daktari aliyewachunguza watoto ndiye yeye aliyeawapokea walipoletwa hospitali, aliyejaza faili, na ndiye aliyetoa ushahidi mahakani. With my own eyes, nilimuona akilia wakati alipokuwa anachunguza wale watoto kwa extent ya UHARIBIFU ambao baadhi ya watoto walipata kwa kuingiliwa over and over again..

Watoto dhahiri kwa ripoti ya Daktari walibakwa...nani aliwabaka? Hilo ndilo swali la kujiuliza!
 
Ooh Lord,have mercy!
 

Nakubaliana nawe......lkn kumbuka ya kuwa mahakama pamoja na sheria hutegemea sana umejieleza vipi juu ya kesi unayoiendesha.....plus ushahidi uliopo juu yako....hivyo kama unatoa maelezo/utetezi ambao kila msikilizaji akiupima anajiridhisha ya kuwa umefanya kosa je unataka mahakama ifanye nini juu ya mtu huyo?.......Ushahidi uliletwa mahakamani......Maelezo yao yanaonyesha walitenda kosa.........Mazingira nayo yanathibitisha..........Watoto wamebakwa...........Mahakama ifanye nini?.....Labda kwa hiki kinachoendelea sasa kitawanusuru Nasikia wametubia na kumuomba mkulu awahurumie kama mkuu wa Anga na si vinginevyo kama mnavyotaka kupotosha.........ndipo mahakama imeagizwa ipitie upya kuwanunusuru...........Nelly nely upo mkuuuuuuu..........
 
Akili mbovu hata humu Jf wamo.....Maamuzi ya Mahakama zote siyo ushahidi tuu?.........mna matatizo gani nyie Someni mwenendo wa Kesi ndio mutajua mbivu na mbichi.............!!!!!!!!

Unapigwa nao na banyamulenge weee ....lione hata aibu mbele za mungu huna ??kipi uteteacho kuhusu unyanuasaji wafanyiao kina babu seya ?????gamba mkuu wewe na mtetee hta shetan coz nyi ni mashetan pia watu wa mtazamo huu !!!kaa kimya usilete ungese hpa kma huna cha kuchangia !!!!
 

thats why i like Jf,ukiujua huu,mwenzio anaujua ule
 
Yaani huwa nikiona thread inayomhusu Babu seya huwa nasikitika sana. Lkn naamini kabisa mtu aliyewafanyia kitendo hicho hakika kuna siku atapigwa mapigo ya kutosha na Mungu. Mtu mnyonge siku zote mtetezi wake ni Mungu.

Inasemekana aliyeamuru wafungwe anaamini katika kulipa visasi! Ni mtu wa aina gani anayependa visasi? Umwonapo akicheka mwogope, moyoni amejaa visasi! Hapendi kuchunguza ili kubaini ukweli na mara nyingi hupenda kuambiwa au kupewa taarifa mara kwa mara na matokeo yake mtu huyu kama atakuwa ni kiongozi, uongozi wake huwa dhaifu!
 
wacha tusubiri mkuu japo naamini hawatatoka zaid ya kupunguziwa adhabu,km tetes zilizopo ni za kweli basi kaz ipo!kuna wa2 wako juu ya sheria nchi hii,japo na hili unaweza kupinga
 
yaani sungura anamuomba fisi amsaidie kuwaokoa wanae mikonon mwa simba??
 
Riwa je kama ndio walibakwa au walidanganywa, je nani aliwabaka?

Huyo Dr alifanya DNA akakuta ya hao wanaume ndani ya watoto?
Au wengine waliwatenda kama rituals au paedo. Na wakawasingizia hawa?

Sababu ni kwamba y wengi TZ haijawaingia kuwa wapo guilty?
I hope siku moja tutajua ukweli.

Hivi huyo rafiki Dr ulikuwa nae alipokuwa anawachunguza?
Alisema wazazi wa watoto walikuwepo nao?
Je wapo wapi sasa? Walirudi check-up kuona kama wapo wanapona vizuri?
Je ni wewe unaamini kila kitu alichokuambia, embu weka story hapa alisema ilikuwaje nataka nijue as wengi hatukuwa kotini?
Kwa hiyo walikuta evidence wakapima dna na ndio kuwakamata? Thank you
 
Last edited by a moderator:
hilo nalo neno
 
Last edited by a moderator:
yanayo mkuta babu seya yanaweza kumkuta yoyote anaye angalia na kusoma uzi huu. familia nzima kulala na wadodo wa sehemu moja hainiingi akilini. mia
 
wacha tusubiri mkuu japo naamini hawatatoka zaid ya kupunguziwa adhabu,km tetes zilizopo ni za kweli basi kaz ipo!kuna wa2 wako juu ya sheria nchi hii,japo na hili unaweza kupinga

Unaweza kupinga??!!!!.......kuna Wa2 wako juu ya sheria??!!!!........Umefikiria nini?........Sheria ni Msumeno hukata mbele na nyuma........Nawasikitikia wale watoto maana baadhi yao wamepata maambukizi ya vvu.....Fidia ya 2M si chochote....Fikiria mmoja wao angekua ni ndugu yako wa Damu.......
 

Labda kama MUNGU hayupo jamani,lakini ile kesi ina mlolongo ambao siyo kabisa, ile kesi ukiipitia kwenye ukarasa wa kwanza hadi wa nne utagundua uongo wa hali ya juu katika hilo,haiwezakani mtoto wa miaka sita na miaka saba wafanyiwe unyama kama huo kwa muda mrefu bila mzazi kujua,siku ya kwanza ilitosha sana kwa mzazi kugundua kuwa kuna tatizo kwa mtoto wake,
MUNGU BABA WEWE NDO MWENYE KUTENDA HAKI DUNIANI NA MBINGUNI
 
mzurimie..

Kwanza ujue...DNA si evidence pekee katika kesi ya kubaka, hasa kubaka au kunajisi watoto. DNA ni 'supportive evidence' tu..kwa sababu ili upime DNA ya manii lazima mbakaji akojoe..na kubaka si lazima ukojoe ndio kitendo kiitwe 'umebaka'..hata ukichomeka mara moja ukachomoa bila 'consent' ni kubaka. Kwa hiyo usilazimishe kuwa kutiwa hatiahani kwa kesi ya kubaka basi DNA ithibitishe.

Victim wa kesi ya kubakwa anapochunguzwa na Daktari kwa ajili ya matibabu na ushahidi..kuna procedure za kufuatwa, na issue za 'privacy, confidentiality' ni muhimu sana ili victim ajenge trust na kuweza kuopen-up kuhusu tukio husika. Sio tukio la 'kimaonyesho' kwamba yoyote atakaye basi anakuwepo kushuhudia mbakwaji akichunguzwa. Lakini rekodi hutunzwa kwenye faili, na rekodi hizo ni 'legal documents', hata Daktari hasipokuwepo bado zitatumika kama ushahidi mahakamani.

Kwa taratibu za kesi za kubaka watoto mara nyingi 'identity' ya mtoto victim hufichwa kumpunguzia unyanyapaa na kuathirika kisaikolojia..wale watoto waliendelea na follow up kwa afya zao kimwili na kisaikolojia Muhimbili, ulitaka watangaze na hilo!?

Kuhusu waTanzania wengi 'haijawaingia' kuwa kina Seya wako guilty mimi sijui..kwani kuna waTanzania wengi tu pia imewaingia kuwa wako guilty. Kinachonishangaza, umeshasikia wanaharakati wa haki za binadamu (taasisi, vikundi au mtu mmoja mmoja) wajuzi wa sheria wakiwatetea kina babu Seya (zaidi ya mwanasheria wao Mabere Marando, ambaye yeye ni wajibu wake kuwatetea hata kama anajua walitenda kosa)? Jiulize kwa nini kwani hawa ni wajuzi wa sheria na watetezi wa haki za binadamu!

Hizo stori sijui wanafanyiziwa na bwana mkubwa sijui eti walimfanya nini mama mkubwa 'ni stori za vijiwe vya kahawa tu', nani ana evidence?! Miaka nenda miaka rudi stori hizo zinapigwa hakuna aliyethibitsha, stori pekee inayothibitishika ni kuwa wamebaka 'wanetu'. Sheria ibebe mkondo wake.
 
Last edited by a moderator:
sidhan km unazungumza toka moyoni mwako mjini chai,hivi hata km n mwanao kafanyiwa hvyo na akapatkana m2 wa kusingiziwa kesi ndo utamalzia hasira kwake?kwann uctafte muhusika?otherwise uwe umechonga kesi!!!
 

Hebu pitia hiyo attachment
 
Yaani huwa nikiona thread inayomhusu Babu seya huwa nasikitika sana. Lkn naamini kabisa mtu aliyewafanyia kitendo hicho hakika kuna siku atapigwa mapigo ya kutosha na Mungu. Mtu mnyonge siku zote mtetezi wake ni Mungu.

kama wengi wanavyoamini... pia hata muumba naye yupo pamoja nao ila isiwe ni ubatiri/ au kwaajiri ya dhambi.

hakuna marefu yasiyo na ncha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…