Janjaweed
JF-Expert Member
- Jan 20, 2010
- 13,153
- 10,670
Naomba nikanushe kwa herufi kubwa 'UWONGO' huu hata kama nitakuwa nimeenda kinyume na taaluma na maadili yangu kama Daktari. Sentensi niliyonukuu hapo juu ni UONGO mkubwa! Wakati inatokea hii issue nilikuwa bado nafanya kazi Muhimbili National Hospital, watyoto hawa walichunguzwa katika kitengo cha upasuaji watoto (Paeditric Surgery) chini ya Daktari ambaye namfahamu sana...na ni 'very senior' na anaheshimika Muhimbili kimaadili na mshika dini.
Kwa kesi ya kubaka, details zinakuwa kwenye faili na si PF3 kama muandishi anavyotaka kutuaminisha, PF ni Police Form inayomsaidia mtu kupata matibabu hospitali na haina details za nini amegundulika nacho mgonjwa. Details za kwenye faili ndio hutumika mahakamani wakati wa kutoa ushaidi (na sio PF3).
Daktari aliyewachunguza watoto ndiye yeye aliyeawapokea walipoletwa hospitali, aliyejaza faili, na ndiye aliyetoa ushahidi mahakani. With my own eyes, nilimuona akilia wakati alipokuwa anachunguza wale watoto kwa extent ya UHARIBIFU ambao baadhi ya watoto walipata kwa kuingiliwa over and over again..
Watoto dhahiri kwa ripoti ya Daktari walibakwa...nani aliwabaka? Hilo ndilo swali la kujiuliza!
thanks Dr....
naona watu wanashambulia bila kuona context ya hoja yako