Kesi ya Babu Seya na wanae - Ukweli ni upi haswa?


thanks Dr....

naona watu wanashambulia bila kuona context ya hoja yako
 

Thanks Riwa.
Watu wanachukulia suala hili kiushabiki.
Wewe umetoa mwanga !
 
Last edited by a moderator:
Ni mpaka siku watoto wao watakwenda majumbani makalio (mik......ndu) yao inachirizika damu ndio watajua adha ya kulawitiwa watoto wao. kwani babu seya alikuwa mwanasiasa hata useme ni mambo ya kisiasa siasa tu. ingekuwa amri yangi ningewahukumu wakatwe hiyo miboriti yao.
 
Watu tunaropoka sana. Ukiambiwa ulete ushahidi kuwa babu seya alisingiziwa huna,unabaki kuokoteza maneno ya mitaani eti jk anahusika. Kina babu seya sio malaika mjue. Tunaongozwa na hisia tu. Kama kweli waliwabaka watoto.waozee huko huko ndani

Hata mimi mwanzoni nilipatwa na hisia mbaya sana juu ya hukumu hiyo, lakini kwa bahati nzuri mwezi mmoja uliopita nilipata habari kutoka kwa mmoja wa watu waliokuwa wanafanya upelelezi wa kesi hiyo, ambaye alikuwa upande wa usalam wa Taifa akaniambia kiunaga ubaga kwamba mzee alihusisika kwa 100%.

Sababu alizonipa ni kwamba wakongo kihistoria wanaimani sana za kishirikina katika muziki, kwa hiyo kuhusika kwao babu seya na wanawe katika sakata hilo kulitokana na shinikizo kutoka kwa mganga wao ambaye aliwaambia ili wapate umaarufu ilibidi wajamiiane na watoto wadogo.

Akaendelea kusema hata wanamuziki nguli wa kongo mnaowajua leo hii kama kina koffi, Werason, Jb mpyana na wengi kila mmoja ana mganga wake ambaye ndiye wanamtegemea katika kufanya mambo yao yaende sawa, akasema hata huyo mganga naye aliwekwa ndani lakini cha ajabu watu wanamjadili babu seya as if yeye ni malaika jamani, ondoeni ushabiki katika mambo ya kisheria .

Ukweli ndio huo ushirikina ndio uliomsukuma mzee wa watu afanye makosa yale kwa lengo la kupanda chati kimuziki na sio vinginevyo wabongo achene unazi, we unathubutu kumuomba mungu amwachie babu seya vipi ingekuwa watoto wale wale ni wako, ama wa nduguyo???
 
ni hisia zao hata km n za mitaani,na we toa hisia zako kwa kufuata story za chumbani,shida iko wapi hapo?heshimu hisia za watu!

unapotaka hisia zako ziheshimiwe na wewe huna budi kuheshimu hisia za wengine! aliyeleta hoja(rudia kuisoma) anasema kesi imetokana na 1. SIASA CHAFU-hivi hao akina nguza walikuwa wanasiasa? 2. VISASI-baina ya nani na nani? 3.CHUKI-kwa sababu gani? 4.UBINAFSI- wa nini? 5. MKONO WA MTU-mtu gani? mbona watuhumiwa walishindwa kujitetea kwa misingi hiyo na matokeo yake nyie ma-bush lawyers mnapayukapayuka bila vigezo! acheni mahakama ifanye kazi yake na msilete hisia za ovyo ovyo kwenye mambo yanayotaka misingi ya sheria itende haki! By the way, what is '' kuna mkono wa mtu''? kama sio uzushi ni nini? kama mlikuwa na ushahidi kwa nini hamkujitokeza mahakamani na badala yake mna lalama baada ya hukumu! huu ni unafiki uliopitiliza mipaka ya unafiki!
 
Tatizo ni kwamba sheria yenyewe haifati mkondo wana nchi hawana imani na mamlaka sheria zinakuwa flexible zinapindwa according to the need of country owners hatuna jinsi acheni tuumie mpaka tuje tupate viongozi wenye uchungu na raia wao
 
How sure ur kama kweli walipewa hayo masharti na mganga wa kienyeji?na je ww ulikuwepo wakati wanapewa hilo sharti?

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 

wkt fulani nilikuwa nafanya field pale COA, kati ya mwishoni mwa 2009 na mwanzoni mwa 2010, kilikuwa ni kipindi APPEAL ya hii kesi ikiendelea! Nilikuwa napata fursa ya kuingia ktk zile courts na nikawa nanasa kwa ufasaha mabishano kati ya MABERE MARANDO (wakili wa kina babu seya kipindi hicho) na mawakili wa serikali/Jamhuri! Kuna quote 1 ya mabere pale court kuhusu PAPII "haiwezekani mtu awe amesafiri kufanya show za muziki Mwanza na wakati huo huo aka-commit crime DSM" hii ilijibiwa na m1 wa mawakili wa Jaamhuri kuwa: mtu kusafiri kwenda Mwanza ama popote pale hakumzuii mtu huyo kufanya uhalifu DSM!
Pia kulikuwa na hoja mabere alitoa kuwa m1 wa watoto wa nguza alikuwa under 18, m1 wa mawakili wa Jaamhuri alisema mahakama haijaonyeshwa BC ya huyo mtoto mpaka hukumu inatolewa! Na hoja kuwa alikuwa anasoma (pale walitaja Mbezi Beach S. Sch) kwa mahudhurio yake ya shule asingeweza kufanya uchafu huu, m1 wa mawakili wa Jaamhuri alisema si jukumu la mahakama kwenda shule kufuatilia mahudhurio ya mwanafunzi! Kwa kifupi, ktk zile siku nilizokuwa pale na nikifuatilia APPEAL series ya Babu seya, nilikuwa naona namna mawakili wa Jaamhuri wanavomshinda Mabere ktk maswali na majibu (sijasema ktk sheria, maana nina ufahamu mdogo wa mambo ya sheria)
Kama hakuna wa kuthibitisha rumours za mtaani, mm naendelea kuiamini mahakama na hukumu yake na rufaa zake!
 
WAKILI maarufu nchini, Mabere Nyaucho Marando amesema mwanamuziki Nguza Viking ‘Babu Seya' na watoto wake watatu walimbambikiwa kesi.

Mabere Nyaucho Marando akiongea na waandishi wa Global Publishers (hawapo pichani).

Akizungumza na waandishi wa habari wa Global Publishers katika ofisi zao zilizopo Mwenge Bamaga mwishoni mwa wiki iliyopita, Marando alisema alipitia jalada la kesi hiyo lenye kurasa 1,362 na kugundua kuwa hakuna hata sehemu moja inayomhusisha kigogo mmoja wa nchi, lakini kesi walikuwa wamebambikiwa.
Hakutaja waliombambikia. Baadhi ya mahojiano ya Marando na waandishi wetu yalikuwa kama ifuatavyo:
Mwandishi: Wewe uliwatetea Babu Seya na watoto wake, unaweza kutueleza ilikuwaje ukatafutwa wewe kuwatetea?

Nguza Vicking ‘Babu Seya' na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha'.
Marando: Kuna rafiki yangu alikuja kuniomba nifanye kazi ile, nilikataa hasa kwa kuwa nami nina watoto wa kike. Baadaye nilikubali kwanza kusoma jalada la kesi lenye kurasa 1,362 nikaona hawakufanya makosa waliyoshitakiwa, walibambikiwa nikaamua kuwatetea katika ngazi ya rufaa, niliwatetea bure kabisa.
Mwandishi: Kama hivyo ndivyo, ina maana makosa walibambikiwa?

Marando: Ndiyo, naamini makosa yale walibambikiwa lakini siyo na kigogo yeyote wa serikali katika nchi hii. Lakini Mahakama ya Rufaa haina makosa, Babu Seya na wanawe walikuwa wamehukumiwa na magazeti. Nyinyi waandishi mlimhukumu kwa hii fabricated case (kesi ya kutunga) na sababu zipo.
Mwandishi: Je, kuna njia yoyote iliyobaki ya kumtoa Babu Seya na mwanaye?

Marando: Mimi kama wakili, hapo ndiyo mwisho wangu, nimenyoosha mikono. Nimeshindwa nusu, nimeshinda nusu (Kwa kuwatoa jela Mbangu na mdogo wake Francis Nguza na kubaki jela Nguza na Papii.)
Mwandishi: Umekuwa Chadema na kuna habari kuwa uliondolewa kuwa mwanasheria wa chama akapewa Tundu Lissu,pia kuna habari kuwa umekosana na mwenyekiti wako, Freeman Mbowe, Je, kuna ukweli wowote juu ya hayo?
Marando: Sijawahi kuwa mwanasheria wa Chadema isipokuwa wanapokuwa na tatizo la kisheria huwa nawapa ushauri wakihitaji. Mheshimiwa Mbowe sijakosana naye isipokuwa katika vikao tunaweza kutofautiana na hivyo ndivyo chama makini kilivyo. Wote hamuwezi kuwa na wazo moja katika hoja, baadaye inapigwa kura, upande unaoshinda na unaoshindwa huwa kitu kimoja. Hakuna ugomvi hapo, mimi ni Makamu Mwenyekiti Kanda ya Pwani na Mjumbe wa Kamati Kuu.
Mwandishi: Lipo suala kuwa wewe ni usalama wa taifa na ulihusika na mauaji ya Komandoo Tamim, Je, hilo unaweza kulifafanua?
Marando: Mimi nilijiunga na usalama wa taifa na nilikuwa kitengo cha mambo ya nje hasa kuhusu vyama vya ukombozi enzi hizo. Niliacha kazi hiyo kwa kukabidhi barua kwa aliyekuwa mkurugenzi wake, Dk. Hansy Kitime baada ya kulazimishwa kujiunga na TANU kwani sikuwa mwanachama. Kuhusu Tamim aliuawa mwaka 1983 wakati huo mimi nilikuwa nimeshaacha kazi.
Hili la kuua walikuwa wakinipakazia watu wa usalama wa taifa bila shaka kwa sababu niliacha kazi kijeuri nikawa jobless (sina kazi).
Baadaye nikaajiriwa Shirika la Sheria Tanzania kabla ya kuanzisha kampuni yangu ya uwakili mwaka 1984. Nimefafanua hili mara nyingi sana, nadhani leo mmenielewa na Watanzania watanielewa.



chanzo, GPL
 
mambo ya babu seya,serikali iawezi kuepuka lawama
 
sawa sasa hao vijana wawili walitokaje?swali la kufikirisha kidogo
 
money stunna hii inaonyesha kuwa kama jamii nayo ina nafasi kubwa kwenye maamuzi ya jaji,sasa tunashangaa mtu kama ridhiwani hata ahojiwi kwa kutajwatajwa kujihusisha na biashara ya madwa ya kulevya
 
Huyu nae kaona hasikiki mda umepita sasa anatafuta single
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…