Kesi ya Babu Seya na wanae - Ukweli ni upi haswa?

Kesi ya Babu Seya na wanae - Ukweli ni upi haswa?

Hii kesi mpaka sasa ipo kwenye mahakama ya haki za binadam Afrika,jamaa walikata rufani huko.
Sasa watu wamemtonya, mhusika wa kale kwamba amshtue jamaa awatoe kwa msamaha. Sababu kule ilipo hawana figisu wataangalia kila hatua za kesi ilivyo kuanzia mwanzo bila upendeleo.
 
Ushahidi wote uliopo ni kwamba ni kweli hao Nguza na wanawe walifanya huo ufirauni. Sijui sababu yao ya kufanya hivyo ilikuwa nini. Wanaharakati wa haki za watoto na za binadamu walishiriki pia kwenye hiyo kesi, na kuna mafaili ya kutisha sana. Watoto waliofanyiwa hivyo wapo na walitoa ushahidi, ambao kisheria ili kulinda haki za mtoto aliyelawitiwa na kumkinga dhidi ya unyanyapaa, haipaswi kufanywa hadharani na wala majina yao hayatolewi kwenye vyombo vya habari. Mafaili ya Muhimbili walikopimiwa hao watoto na ripoti za madaktari zipo. Yaani hii ilikuwa soo, hawakuwa na jinsi ya kukwepa.

Na huy si wa kwanza. Miaka ya mwisho ya 1980's alitokea fundi mshona nguo akiitwa Ali Maumba, alikuwa akiwafanyia watoto mchezo huohuo, na alilawiti zaidi ya 100, ila wengine wazazi wao waliwazuia wasijitokeze ili kukwepa aibu kwa familia zao. Ile kesi Maumba alihukumiwa kifungo, lakini alipokata rufaa alishinda kutokana na ushahidi "dhaifu" wa madaktari. Na ile kesi ya Maumba hadi leo inatumika kama reference ya kuwakumbusha madaktari umuhimu wa "ushahidi wa kitaaluma" (expert witness) kuandikwa vizuri. Rafiki zangu wanaharakati wamei-cite mara nyingi sana kwenye papers zao.

Hii ya kina Babu Seya, wanasheria walijaribu sana wakakosa pa kutokea. Na hata wakati wa rufaa, haikuwezekana, akaendelea kubaki hatiani.

Hizo habari za kuwasingizia kina nani sijui ni uvumi tu, kungekuwa na ukweli tungeshapata japo chembe ya ushahidi. Hao mnaowataja wakati huo hawakuwa na mamlaka yoyote dhidi ya mahakama, na hata katika kesi hakuna wakili au yeyote aliyeleta ushahidi wa kuwahusisha. Kama ni rushwa, sijui ni rushwa gani watu wangetembeza kila mahali kuanzia kwa watoto wa shule ya msingi, walimu wao, wenyeviti wa serikali za mitaa, askari polisi kwenye posts hadi kwa waendesha mashtaka, wanaharakati wa haki za watoto, mawakili, wafanyakazi wa idara za hospitali (wauguzi, watu wa records, maabara,madaktari, ili ati wote wafoji habari zinazoendana), hakimu mkazi kisutu, majaji wa mahakama kuu, majaji waheshimiwa sana wa mahakama ya rufaa, woote hao utawahonga vipi? Kazi ya ku-organize na ku-stage plot kama hii ni kubwa na haiwezi kuwa siri, lazima ziwepo flaws, hata kama ni fiction unatunga wasomaji wataona tu uongo ulipo!

Kwa hiyo sioni cha kujadili kuhusu Babu Seya na wanawe, alipata haki yake ya fair trial, akawa convicted, na sheria ikachukua mkondo wake. Akatumia pia haki yake ya appeal, nako hatukusikia malalamiko ya unfair trial, akabakia guilty as charged. Basi.
Hao watoto kwa sasa ni watu wazima, waitwe wahojiwe kiutu uzima kama ni kweli au walishinikizwa kumsingizia mzee wa watu
 
Assalam aleykum ndg zanguni,leo nimekaa na kutafakali sana jinsi nchi yetu inavyokwenda,kuanzia uongozi wa chini(tawi) mpaka huko juu,kuna mambo mengi sana ya vioja yanayofanyika na serikali kukaa kimya ama kwa makusudi au kwa kujifanya hawaoni kwa kujua kwamba watanzania ni wepesi wa kusahau.na kitu hicho kipo hapa JF,

Kitu ambacho kinaniuma siku zote na kitaendelea kuniuma ingawa kimetokea kitambo ni jinsi babu seya (nguza viking) na wanawe (papii kocha,nguza mbangu na francis) jinsi walivyohukumiwa kifungo kikubwa kwa sababu tu kesi ilikuwa imetengenezwa na kusimamiwa kidete na mabwana wakubwa wa serikali(mahita na wenzake),haiingii akilini mpaka leo kwa mtu ambaye anaitwa ALHAJI kumwadhibu mtu na familia yake tena kwa SABABU anataka kuilalisha DHINAA(kadhulumiwa kimada wake),

hili jambo ingawa limetokea kitambo lakini lazima tufahamu kuwa wale ni viumbe ambao wanateseka gerezani kwa kesi ya kubambikwa hivyo wanaJF lazima tuwe na utaratibu wa kuyakumbushia na kuendelea kuyakemea mabaya yote ya serikali bila kujali kuwa ni muda gani umepita!
Yule Mahita tulieambiwa kwenye magazeti ya udaku kwamba alizaa na house girl wake?
 
Article 45 ya Katiba bado iko LIVE..Tuendelee kuiheshimu hii katiba mpaka pale tutakapokuwa tayari kuibadilisha,sasa hivi siyo kipaumbele na pia pesa hatuna....BUNGENI
 
Guys ninarudia nimesoma faili zima. Jamaa walikuwa na hatia au niseme walikuwa wapumbavu kui9ngia kwenye mtego.

Kama ni mchongo waliingia kisawasawa. Naweza kuandika facts zaidi ila inategemea wewe una mtazamo upi.

Kumbuka hakimu anaangalia FACTS presented before him/her!!!! kuwa focused itakusaidia
Vipi kuhusu yule mwalimu aliyekuwa anawapeleka, iweje akaachiwa bila hatia?
 
Rafiki ukijua ukweli kuhusu hiyo kesi, utaogopa hata kuishi Tanzania. Hii nchi mwenye nguvu akitaka ufungwe utafungwa tu.
Kama hii kesi ingekuwa na ukweli yule mwalimu aliyekuwa akipeleka watoto kulawitiwa asingeachiwa kwasababu yeye ni mbakaji pia kasababisha watoto waharibike
 
Sawa kabisa, hivyo dhana ya kuwa in taifa la wasiojitambua inapata mashiko. Msamaha wa Rais hauna shida kwani anaweza kumsamehe yeyote lakini kama tuna hakika mahakama zilitenda haki basi hakukuwa na sababu ya kushangilia kuachiwa kwao bali ilitakiwa mambo hayo yaende kimya kwa ajili ya wahanga wa vitendo vile!
Je mahakama za Tanzania zipo huru?
 
watoto kumi kubakwa kwa siku tofuti tofauti na familia moja baba, mtoto ,mtoto harafu watu yaani majirani na watu wanaowazunguka {marafiki} wasijue mpaka serikali ijue duuuuuuh
Haya maajabu yapo tz tu halafu mwl kowadi akaachiwa na kupewa ukubwa wa cwt kagera
 
nilipata kuongea na mwanamuziki mmoja wa kikongo akaniambia kuwa vipimo vya daktari vilionesha kuwa hakuna mtoto aliyekuwa ameonesha ameingiliwa ,ila kuna mmoja alionekana ana uchafu sehemu za siri(na hii ni kutokana na kutojua jinsi ya kujiweka safi)
So ukaamini sio?
 
me nilisikia ni anga za huyo mtalii muungwana dats why pia yasemwa jamaa kutoka may be awe anavyoomba kwa Mungu kuwa atoke pia awe anamuombea mtalii atoke madarakani either kwa kusinda uchaguzi au lolote baya else angalau wasubirie mpaka 2015
Uliona Mbali Mkubwa
 
Kutokana na utata huu mi nabaki njia panda siendi kulia wala kushoto nachoshukuru wametoka tu.Mambo ambayo hukuwepo ni vigumu kuwa na uhakika nayo kwenye kila amuzi lililotolewa
 
  • Thanks
Reactions: 454
Kutokana na utata huu mi nabaki njia panda siendi kulia wala kushoto nachoshukuru wametoka tu.Mambo ambayo hukuwepo ni vigumu kuwa na uhakika nayo kwenye kila amuzi lililotolewa

Hakuna utata wowote Rafiki. Hii kesi ilitengenezwa studio. Mmoja wa wale watoto alimfungisha Jamaa mmoja naye kwa kesi ya ubakaji. Baadae alimwibia Salma Kikwete. Salma hakutaka fuatilia sana sababu Ingemuharibia
 
Ukweli unajulikana... Ila kama ni kweli walibaka na wakawalawiti watoto wadogo.... Mh. Rais itakua hakuzitendea haki familia za watoto hao. Aidha vyovyote iwavo, mimi cungi mkono kabisa wananchi kuwafanyia shangwe watu hao wakati wakitoka gerezan.... Maana ni iman yangu kua hakuna mwananchi anaeufaham ukweli wa suala hili... Kushangilia kuachiwa huru kwa watu hawani kutojitambua kuliko chupa mipaka.
Hayupon Rais duniani anayeweza kutoa msamaha kwa mtu aliyebaka, tena watoto. Jamami tuwe tunajiongeza, za kwako chnanganya na za mwenzio. Za kwako chnaganya na za yule aliyetoa msamah!
 
Moderator kuunganisha huu uzi ni kuficha ukweli na kutokutenda HaKi kwa Walengwa!!!!!!!


Ninamshukuru mungu kupata jukwaa hili maana sina pengine pa kufikisha ujumbe wangu kwenu maana sina namba zenu za simu kama zipo na mna wageni wengi sana muda huu.
Pia sifa na Pongezi ziende kwa Rais wetu Mh. Dct John Pombe Magufuli kwa uamuzi wake thabiti wa huruma na upendo kwa taifa letu hususan kuwaachia wafungwa kwenye sherehe za miaka 56 ya uhuru wa nchi yetu, Ahsante mheshimiwa Rais, Mwenyezi mungu akujalie maisha marefu na Nguvu zaidi ili kutusogeza watanzania kwenye hatua nyingi zaidi.

Nimeandika haya baada ya kuongea na wazazi wa binti mmoja ambaye kwa sasa ni binti mkubwa japo hakuendelea vizuri kimasomo lakini wazazi wake waliwasamehe baada ya kuhukumiwa na mahakama kifungo cha maisha bado anawalaumu sana ninyi kutokana na kuharibika kwa binti yao wakisema ilikuwa ni haribiko la kisaikolojia . Mzee Nguza Vicking Na vijana wako hali iliyopo kwa baadhi ya Wazazi wa mabinti hawa waliofika MAHAKAMANI hata na wale ambao kwa kuogopa kufedheheka hawakufika mahakamani sio nzuri kwa sasa ...maana wanaona kuachiwa kwenu ni upendeleo uliokithiri ,nimejaribu kuwaelimisha kwa namna zote kuwa Rais ana mamlaka hayo kisheria kwa ibara ya 45 ya katiba yete pendwa ila bado kunielewa wananiuliza kwa nini nyie tu.

Ni ukweli uliowazi kwamba Msamaha wa Rais kwa wafungwa chini ya sura 45 ya katiba haumpi mamlaka ya kuwaondolea hatia mliyokutwa nayo na mahakama zote bali imewaondolea ADHABU ya kifungo ninyi pamoja na wafungwa wenzenu.Kwa hiyo bado ninaweza kuwaita WABAKAJI NA WALAWITI japo nitalinda heshima ya rais sitafanya hivyo KAMWE, MAANA KAMA YEYE HAKUWAITA MIMI NI NANI BASI KUFANYA HIVYO,

Bahati mliyonaayo ni kuwa kesi yenu ilionekana ya kisiasa haswa mbele ya jamii na uzushi mbali mbali ulifunika Ukweli lakini sina uhakika kama kuna influence kwenye siasa what i am sure NI KWAMBA MLITIWA HATIANI PASIPO SHAKA kwa makosa mliyoshtakiwa nayo na mimi ni mmoja wa watu niliyebahatika kuwajua Baadhi ya victim/Wathirika wa moja kwa moja wa matendo yenu.

Kingine mimi naamini ni Kumtegemea Mungu,juhudi kali, nguvu ya kazi, nidhamu ya kiwango cha juu na maarifa ya kutoa kazi nzuri tu ndizo zinazoweza kumfanya mtu ang'ae zaidi kwenye kazi yake yoyote na kukubalika sio kuoshwa nyota na yoyote au kufanya tendo lolote kwa nguvu za giza ..Najua mmenielewa ili msirudi kwenye sababu zilizofanya mkatenda kosa la aibu familia nzima jao wengine walipona kupata adhabu iliyopata wengine. ni watoto 10 walienda mahakamani ila nyie mnajua ni idadi ya wa toto wangapi walipaswa kuwa mashahidi wa kesi yenu.

Kiuhalisia ni upendo wa Rais wetu na moyo wake wa huruma aliamua bila kuombwa wala kushurutishwa kuwaachia ninyi na wengine ili kuwapa nafasi ya pili kwenye maisha ya Uhuru...sasa je kwa Upendo na Uamuzi huo wa Rais mna wajibu gani kwa nafsi zenu,kwa waathirika ,washabiki wenu na Taifa kwa ujumla?


Mzee Nguza Viking(BABU SEYA ) na Johnson Nguza(Papii Kocha) Biblia inasema “huenda mwadilifu akaanguka hata mara saba,naye atasimama” (Methali 24:16) pia wazee wetu walipata kusema Kuteleza si kuanguka basi NAFIKIRI mna wajibu wa kujisafisha kidhati ili kuondoa mioyo ya visasi na kinyongo kwa waathirika, wazazi na ndugu zao pia kuweka uhusiano mzuri na jamii ya watu wachache inayowazunguka na inayojua ukweli jambo hili.Naamini mlishajuta na kumuombaq mungu awasamehe ili muwe nje ya zile kuta ndefu sasa mungu amewajibu Maombi yenu. Je mnawezaje KUREKEBISHA?

Mna njia 2 kubwa ya kwanza (1) ni kuzunguka kwa familia zote za waathirika sio wale waliotoa ushahidi tu na kuomba msamaha kwa yaliyotokea kwa kuwa walishasamehe na kuridhika baada ya ninyi kufungwa hawatasita kusamehe tena kiwa mmeonyesha uungwana sio lazima muende na kitu maana wanajua hali yenu baada ya kuachiwa , bahati mbaya sio Wazazi wa watoto wote wapo duniani leo.(kwa hili najua mnajua pa kuanzia kuwapata waliopo dar maana wengine walihama .


Njia ya pili kulizungumzia hili kwenye vyombo vya habari na kuwaomba msamaha kwa jumla japo kwa lugha tofauti ..ata kwa kusema tumejifunza kuwa kufanya makosa ni kitu kibaya tunawaomba msamaha sisi na wenzetu waliopo magerezani kwa makosa tuliyoyafanya bila kuwataja

MSIJARIBU KUJISAFISHA KWA NAMNA YOYOTE kwenye vyombo vya habari kuwa hamkuhusika italeta chuki zaidi ikishindikana kabisa mkae kimya kuhusu hili japo Najua watu wa Media wameanza kuwabuku kwa ahadi ya pesa nyingi kwa ajili ya interview ..sana sana ongeleeni maisha ya Gerezani kuhusu kilichowaweka ndani semeni yameshapita mmsamehe na msamehewe mnamshukuru mungu kwa kumtuma Mtumishi wake Dr John Pombe Magufuli kuwaachia.Msiwe mtaji wa Media au Wanasiasa maana hamjatolewa kwa ajili ya hayo.

Zaidi mimi ni mmoja wa washabiki wa nyimbo zenu tulieni mtupe burudani kwa juhudi tu tutawaelewa ...Mengine nimetoa kama ushauri kutoka karibu sana na waathirika ..
KARIBUNI URAIANI TUIJENGE NCHI YETU

Asanteni..

13th Dec 2017
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Mmmmmh ngoja nisitie neno lakini kama kusoma nimesoma ulichoandika kuelewa ngoja niachie ubongo
 
Back
Top Bottom