GE2025 Kesi ya Dk Malisa dhidi ya CCM yasogezwa hadi Agosti 19

GE2025 Kesi ya Dk Malisa dhidi ya CCM yasogezwa hadi Agosti 19

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Elias Msuya

Platinum Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
267
Reaction score
1,014
Kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na aliyekuwa kada wa CCM, Mchungaji Dkt. Godfrey Malisa iliyokuwa isikilizwe Agosti 14, sasa imesogezwa hadi Agosti 19, 2025.

Katika shauri hilo linalosikilizwa na jopo la mawakili watatu, Dkt Malisa anaiomba mahakama kutoa tafasri na uamuzi wa usahihi katika mchakato wa kumpata mgombea wa CCM, Samia Suluhu Hassan na mgombea mwenza Dr Emmanuel Nchimbi.

Kesi hiyo inayosikilizwa katika Mahakama Kuu Kanda ilianza kusikilizwa Agosti 5,2025, ambapo kwa mujibu wa Dkt. Malissa Mahakama iliwapa siku saba mawakili upande wa CCM kutoa maelezo ya utetezi, kabla mahakama haijatoa uamuzi wa shauri hilo. Ikumbukwe kuwa shauri hilo limewasilishwa mbele ya mahakama kuu kwa hati ya dharula.

Dkt Malisa alipotafutwa kwa simu, amesema shauri hilo limesogezwa hadi Agosti 19, ambapo mawakili wa CCM watatoa utetezi wao.
 
Watapogiwa simu tu hao majaji.
Kuna mambo hata ukipigiwa simu lazima utembelee kwenye uongo unaofanana na ukweli.

Majaji watatoa uamuzi baada ya kusikiliza hoja za pande zote. Upande gani utakuwa na hoja zenye mashiko, tuupe nafasi muda.
 
Wewe utarajie maamuzi ya ajabu ajabu kama tunavyoona kwenye kesi ya Lissu.

Nina wasiwasi hii kesi itatumika kuhalalisha uhuni uliofanyika January 19.
 
hii itapigwa kalenda hadi itajifia
 
Wewe utarajie maamuzi ya ajabu ajabu kama tunavyoona kwenye kesi ya Lissu.

Nina wasiwasi hii kesi itatumika kuhalalisha uhuni uliofanyika January 19.
Kwenye hili nawapa benefit of doubt majaji wanaosikiliza kesi hii.
 
Kwenye hili nawapa benefit of doubt majaji wanaosikiliza kesi hii.
Mimi nina ''machale'' mengine. Je, CCM baada ya kuona ilifanya fyongo baya sana, inataka kumtumia Malisa (huku najua au bila kujua) kufuta kosa lililotokea? 1. Kwa kuhalalisha mchakato wake ili wawe na sababu ya kujitetea kuwa hata mahakama imepitisha? 2. Kufuta mchakato mzima ili kupata nafasi ya kumpitisha baada ya mkakati mpya? All in all, ule mchakato ulikuwa haramu.
 
Di pi pii wetu hajaiona hii aifutilie mbali?
 
Wewe utarajie maamuzi ya ajabu ajabu kama tunavyoona kwenye kesi ya Lissu.

Nina wasiwasi hii kesi itatumika kuhalalisha uhuni uliofanyika January 19.

Shinda ya inch Kila sehem n lazima waepo wana ccm.. hapo atapigwa karenda mpaka apangawe mwenyee
 
Mchakato ukifutwa ccm hawataweza tena kumpata mgombea urais. Watakuwa nje ya ratiba ya tume.

Let's keep our fingers crossed.
Labda Wataitisha mkutano wa dharura siku hiyo hiyo Kwa njia ya mtandao na kukamilisha taratibu zote…ngoja tuone drama zao
 
Mahakama ya mama, majaji wa mama, wanasikiliza kesi dhidi ya mama!
patamu hapo! wacha tuone
 
Back
Top Bottom