Kesi ya Dkt. Abdi Warsame anayeshutumiwa kwa wizi wa mabilioni yasikilizwa kisiri Kisutu, Waandishi wazuiwa

Kesi ya Dkt. Abdi Warsame anayeshutumiwa kwa wizi wa mabilioni yasikilizwa kisiri Kisutu, Waandishi wazuiwa

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Kesi inayomkabili Dkt. Abdi Warsame, anayeshutumiwa kwa kujipatia mamilioni ya shilingi kwa njia ya udanganyifu kutoka kwa kampuni ya bima ya afya AAR (sasa Assemble), imesikilizwa kwa siri katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

1739450826667.png
Waandishi wa habari na umma wamezuiwa kuhudhuria vikao vya kesi hiyo, huku kukiwa hakuna maelezo ya wazi kuhusu sababu za hatua hiyo. Hakimu Mkazi Mwandamizi Gwantwa Mwankuga, anayesimamia kesi hiyo, alieleza kuwa alirithi kesi hiyo kutoka kwa hakimu mwingine na hawezi kutoa maelezo zaidi.

Juhudi za Daily News kupata ufafanuzi kutoka kwa waendesha mashtaka nazo hazikufua dafu, kwani mwendesha mashtaka wa serikali alithibitisha tu kuwa "kesi inasikilizwa kwa siri," bila kueleza sababu za uamuzi huo. Waandishi wa habari waliambiwa wawasiliane na mkuu wa mashtaka wa Kanda ya Dar es Salaam kwa maelezo zaidi.
 
Back
Top Bottom