Manyanza
Platinum Member
- Nov 4, 2010
- 22,269
- 58,563
Shauri la Kikatiba namba 7300 la mwaka 2026 linalohusu madai ya kunyimwa faragha kwa Mawakili wa Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, limeahirisha hadi Septamba 16, 2026 kwa ajili ya kutajwa.
Shauri hilo liliendea leo Alhamisi Julai 23, 2026 katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu Dodoma inayoketi Masjala Ndogo ya Dar es Salaam mbele ya Jopo la Majaji watatu wakiongozwa na Jaji Amir Mruma ambapo ushahidi wa leo ulitokewa na Mkuu wa Gereza Ukonga, ACP Andrew Shaban N’tamamiro.
ACP Andrew Shaban alikamilisha kujibu maswali ya dodoso kutoka kwa Mawakili wa waleta maombi na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) ambapo katika ushahidi wake ambapo alikiri kuwa amewahi kuwachungulia Mawakili wa Tundu Lissu walipokuwa wakifanya mazungumzo na Mteja wao gerezani, lakini akasisitiza kuwa hakuwahi kusikiliza mazungumzo hayo.
Pia alieleza kuwa mlango wa chumba cha mazungumzo ulikuwa wazi ili askari waweze kuwaona waliokuwemo ndani, si kusikia walichokuwa wakizungumza.
Shahidi huyo pia alisema hafahamu kuwa Tundu Lissu aliwahi kuwa Rais wa TLS mwaka 2017/18, ingawa alikubali kuwafahamu Mawakili Nashon Nkung na Paul Kisabo kwa kuwa wamekuwa wakimtembelea Lissu gerezani mara kwa mara.
Baada ya upande wa Jamhuri kumaliza maswali ya ufafanuzi (re-examination), Mahakama imeahirisha shauri hilo hadi Septemba 16, 2026 litakapoitwa tena kwa hatua nyingine.