Kesi ya Kabendera dhidi ya Vodacom yaanza rasmi leo

Kesi ya Kabendera dhidi ya Vodacom yaanza rasmi leo

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Kama ulidhani jambo hili ni utani, basi ulijidanganya, mambo tayari yako Mahakamani.

Kesi hii yaweza kuwa fundisho kwa mitandao mingine ya simu inayoshirikiana na Watekaji na Wauaji, hata kama watekaji hao ni Watu wa Serikali

Taarifa kamili hii hapa

Screenshot_2024-07-09-09-44-19-1.png

---
Mchakato wa usikilizwaji wa kesi inavyohusiana na kukamatwa kwa mwanahabari Erick Kabendera, aliyoifungua mwanahabari huyo dhidi ya kampuni ya huduma za Mawasiliano Kwa simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Ltd unaanza leo.

Katika kesi hiyo Kabendera anaoimba mahakama hiyo iiamuru kampuni hiyo imlipe fidia ya Dola za Marekani 10 milioni (sawa na Sh28 bilioni) akiituhumu kuwa ndio iliyofanikishwa kukamatwa kwake na askari Polisi, tukio analoliita kutekwa, na kisha kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi, mwaka 2019.

Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa na Jaji Mfawidhi Salma Maghimbi na pande zote zimeitwa kufika mahakamani hapo leo Julai 9, 2024.

Kwa mujibu wa hati ya wito wa mahakama kwa wadaawa (pande zote) kufika mahakamani, kesi hiyo namba 12799/2024 imepangwa kutajwa asubuhi hii, huku ikiitaka kampuni hiyo kufika bila kukosa na kuwasilisha nyaraka zake ambazo inatarajia kuzitumia katika utetezi wake.

PIA SOMA
- Mwandishi Eric Kabendera aelezea jinsi Vodacom Tanzania ilivyomkamatisha kwa vyombo vya Usalama

- Madai ya fidia ya dola milioni Moja ya Erick Kabendera dhidi ya Vodacom yakienda mahakamani tutarajie nini?

- Erick Kabendera aitaka Vodacom imlipe Dola Milioni 1 kwa kufanikisha kutekwa kwake 2019
 
Kama ulidhani jambo hili ni utani, basi ulijidanganya, mambo tayari yako Mahakamani.

Kesi hii yaweza kuwa fundisho kwa mitandao mingine ya simu inayoshirikiana na Watekaji na Wauaji, hata kama watekaji hao ni Watu wa Serikali

Taarifa kamili hii hapa

View attachment 3037324View attachment 3037325
Kama amemlipa jaji atashinda lakini kavu kavu tutarudi tena kuupitia huu uzi!
 
Hamna kesi hapo,ni takwa la kisheria kwa watoa huduma za mitandao kutoa ushirikiano kwa vyombo vya Dola katika kufanikisha Upelelezi yaani wamiliki wa mitandao ya simu au huduma za mawasiliano au mtoa huduma yeyote hawaruhusiwa kutoa taarifa ya mteja isipokuwa katika kufanikisha Upelelezi.
 
Back
Top Bottom