Kesi ya kikatiba dhidi ya Pinda yaendelea

Kesi ya kikatiba dhidi ya Pinda yaendelea

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
jaji-fkahi-jundu-nov9-2013.jpg

Jaji Kiongozi Fakhi Jundu


Kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kwa kushirikiana na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) dhidi ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda imeendelea kusikilizwa, huku upande wa waleta maombi wakijibu hoja za pingamizi zilizowasilishwa awali na serikali.

Wanaosikiliza shauri hilo hilo ni jopo la Majaji watatu likiongozwa na Jaji Kiongozi Fakhi Jundu Majaji wengine ni Dokta Fauz Twaib na Augustine Mwarija ambapo awali upande wa serikali ulikuwa na hoja tano ambazo mawaliki wa LHRC na TLS walitakiwa kuzitolea majibu.

Wakili kutoka upande wa waleta maombi, Jeremia Mtobesya akijibu maombi hayo alisema kuizungumzia hoja hiyo ni sawa na kuifanya mahakama kuingia katika msingi wa shauri lenyewe.

Miongoni mwa hoja ni ile iliyosema kuwa mahakama hiyo haiwezi kutolea maamuzi maombi ya LHRC na TLS.

Wakili huyo alidai hatua ya serikali kusema kuwa mahakama hiyo haiwezi kusikiliza na kutolea uamuzi maombi yao ni sawa na kuongelea suala la maombi ambayo yanatokana na kesi ya msingi katika hatua za awali.

Aidha, kutokana na sababu hiyo, Mtobesya aliiomba mahakama hiyo itupilie mbali hoja hiyo ya serikali kwa kuwa haina msingi wowote.

Katika pingamizi lao la awali, upande wa serikali unadai kuwa kesi hiyo ni batili Kikatiba kwa sababu inakiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Sheria ya Haki, Mamlaka na Kinga za Bunge ambazo zinakataa suala lililotokea wakati wa shughuli za Bunge kutohojiwa au kujadiliwa na chombo chochote.

Kesi hiyo imehairishwa na itaendelea kwa siku tatu mfululizo kuanzia Desemba 11, mwaka huu ambapo upande wa waleta maombi utaendelea kujibu hoja za pingamizi la tatu na la nne lililotolewa na serikali.




CHANZO: NIPASHE

 
Nimesikia Dr. Mvungi kandei south africa alipoenda kutibia baada ya kuvamiwa!
 
Mahakama, bunge na serikali ni watoto wa katiba, bunge sio kichaka cha kuvunjia katiba et kwa kigezo cha kinga, kinga ni kwa masuala yanayoendana na katiba, katiba haisemi piga tu bali imesema mtu ataadhibiwa baada ya mahakama kumpata na hatia
 
jaji-fkahi-jundu-nov9-2013.jpg

Jaji Kiongozi Fakhi Jundu




Kesi hiyo imehairishwa na itaendelea kwa siku tatu mfululizo kuanzia Desemba 11, mwaka huu ambapo upande wa waleta maombi utaendelea kujibu hoja za pingamizi la tatu na la nne lililotolewa na serikali.




CHANZO: NIPASHE


Mkuu MziziMkavu nimekugongea like lakini naona haitoshi labda niongezee na asante.
Tunataka wanasiasa na watendaji wote wa taasisi kuu tatu inayojenga mamlaka/Dola kutambua kuwa hakuna kitu kitakachoitwa Nchi kama hatuwezi kuheshimu KATIBA.

Nawaomba wanasheria wasiishie hapo maana kuna madudu mengi yako kinyume na Katiba iliyopo hivyo makelele haya ya Katiba Mpya hayatatusaidia maana kama hii mbofu tunashindwa kuiheshimu je hiyo tunayoihangaikia tuna hakikika gani kuwa mamlaka/dola itaiheshimu.
 
Last edited by a moderator:
jaji-fkahi-jundu-nov9-2013.jpg

Jaji Kiongozi Fakhi Jundu


Kesi hiyo imehairishwa na itaendelea kwa siku tatu mfululizo kuanzia Desemba 11, mwaka huu ambapo upande wa waleta maombi utaendelea kujibu hoja za pingamizi la tatu na la nne lililotolewa na serikali.




CHANZO: NIPASHE


Jamani Kesi hii imezimwa kiaina au !
Mwenye taarifa atubandikie
 
Mahakama, bunge na serikali ni watoto wa katiba, bunge sio kichaka cha kuvunjia katiba et kwa kigezo cha kinga, kinga ni kwa masuala yanayoendana na katiba, katiba haisemi piga tu bali imesema mtu ataadhibiwa baada ya mahakama kumpata na hatia

Hiyo mifisadi itamininize hiyo kesi hata kama wamekosea kweli.
 
Jamani Kesi hii imezimwa kiaina au !
Mwenye taarifa atubandikie



Nimefarijika Kiasi fulani na Kesi hii. Gazeti la Mwananchi hongereni sana kuifanya habari kuu.

LHRC na TLS hakuna wa kuweza kuwalipa na huu ndiyo uwe mwanzo maana kuna lundo la Mashitaka yanayo faa kufikishwa mbele ya Mahakama kwa msaada mwenu.

Hata baada ya hukumu hii ,natumai mtakaa chini na kujipanga kukata Rufaa,kwenye maeneo muhimu yenye kuleta ukakasi kwenye hukumu hii.

Mtazamo wangu kuna haja ya kupanua wigo wa maamuzi ya Mahakama.

Huu uamuzi kwa mtazamo wangu unaonekana kukuweka msisitizo kwenye Wabunge.Kuna Wabunge lakini hawaishi kuwa Wabunge tu!

Nadhani katika kupanua Wingo huu kwenye Kesi hii kuna haja ya Kujumuisha Ofisi ya Spika na Serikali.
Kwanini na fikia mtazamo huu; Suala la kulinda Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni la kila Mtu na kila Taasisi.

Hivyo Spika na ofisi yake hawawezi kuepuka uwajibishaji ,hivyo hivyo Mbunge Mmoja Mmoja na Serikali kupitia waliopewa Dhamana.

Na hii ndiyo Utawala wa Sheria.
 
Hongera Mch.Mtikila kwa kazi hii ambayo mpaka dakika hii hakuna Mtanzania anaweza kufikia Rekodi yako.

Tanzania Daima ya leo Toleo Na.3480 inadodoso kuhusu uamauzi wa Mahakama ya Africa;


[h=3]Mtikila aibwaga tena Serikali[/h]

Ikiwa ni mrejesho wa tangazo hii;
[h=2] Delivery of Ruling in respect of Rev. Christopher R. Mtikila v. United Republic of Tanzania[/h] Details Created on Tuesday, 10 June 2014 07:58 Published Date Category: frontpage Hits: 288
On Friday 13 June 2014, the African Court on Human and Peoples’ Rights (the Court) will deliver a Ruling at its seat in Arusha (Tanzania), in respect of an Application for reparations relating to the matter of Rev. Christopher R. Mtikila v. United Republic of Tanzania – Application 011/2011.
 
Back
Top Bottom