Kesi ya kupinga matokeo ya Rais wa Kenya sasa inarushwa mubashara

Kesi ya kupinga matokeo ya Rais wa Kenya sasa inarushwa mubashara

Thubutu! Tanzania tumezoea giza, hii ya kesi kuendeshwa mubashara kwa kweli wanazidi tu kutudhalilisha tulivyo nyuma katika dunia ya uwazi!

Halafu kama vile kuongeza chumvi kwenye kidonda, kesi yenyewe inaendeshwa kwa lugha ileeee! Kwa Mtanzania, lugha lileee ni usiku wa giza.

Cha kufurahisha nasikia aliyewahi kuwa Jaji wetu Mkuu, Jaji Mohamed Chande Othman, yuko ndani ukumbini anafuatilia, labda atatupa mrejesho!
 
Wapenda demokrasia mnaweza kufuatilia kupitia Citizen TV. Tofauti na kesi hii ya Halima Mdee na wenzake MMM anasikiliza halafu ndio anatusimulia!

Mungu wa mbinguni awabariki.
Mkuu Yohana Mbatizaji, johnthebaptist, kwanza asante kwa taarifa hii.

Baada tuu ya kuipokea hii, mimi mbio the Citizen Kenya nikashuhudie!.

Nikaamua kabla ya kwenda Kenya, nikaamua kupita mahali..., kwani Kenya kuliendeka!. Nilikutana na "jicho ona", safari yangu ikaishia pale!.

Tupe feedback, nini kilijiri, maana ...

P
 
..Ccm watapinga hata hili..
Hilo likitokea halitashangaza hata kidogo kwani kwa akili zao fupi wanaweza kudai kuruhusu kitu kama hicho ni kuhatarisha amani.

Kwa kweli wanachodai ni amani si amani, ni uoga...penye amani hakuna uoga. Watanzania wenzangu, lini tutazinduka? CCM inaogopa ukweli kama ukoma.

..Wanapenda mambo yafanyike kwa kificho ili waweze kudhulumu haki za wananchi.
Wahalifu waoga lazima wafanye mambo yao gizani. Adui wa taifa hili ni CCM na ndio maana mchana hutumulika ili usiku watuchome. Gizani CCM hupata ujasiri wa ajabu!

Nafuatilia kwa karibu yanayojiri mahakami kwa majirani leo na kesi ya msingi inaanza kesho. Kuona jambo kama hili likitendeka Afrika ni kama ndoto. Tuache utani, Kenya wako mbali!
 
Hilo likitokea halitashangaza hata kidogo kwani kwa akili zao fupi wanaweza kudai kuruhusu kitu kama hicho ni kuhatarisha amani.

Kwa kweli wanachodai ni amani si amani, ni uoga...penye amani hakuna uoga. Watanzania wenzangu, lini tutazinduka? CCM inaogopa ukweli kama ukoma.


Wahalifu waoga lazima wafanye mambo yao gizani. Adui wa taifa hili ni CCM na ndio maana mchana hutumulika ili usiku watuchome. Gizani CCM hupata ujasiri wa ajabu!

Nafuatilia kwa karibu yanayojiri mahakami kwa majirani leo na kesi ya msingi inaanza kesho. Kuona jambo kama hili likitendeka Afrika ni kama ndoto. Kenya wako mbali!
Naonga mkono hoja
 
Alafu anakuja mpuuzi mmoja akiandika kutoka kijijini 'thithi tunawathinda, Dar ni dhaidi ya Nailobi na...' kwa lipi? Si kwa uhuru wa raia, si kwa elimu, si kwa quality of life, na wala si kwa GDP....ingawaje tuna mimali chungu nzima ya kutupwa kuliko wao!
 
Any updates plz....
Leo ilikuwa inatajwa tu, kesho ndio kesi rasmi inaanza ikiongozwa na Jaji Mkuu, mwanamama Lady Justice Martha Koome. Kazi ipo!

1661854888674.png
 
Mpaka hadi SAsa wakenya wametulia means wamesharidhika bora amani tu hata akiingia mwingine Hakuna mabadiliko
 
Mkuu sio muda wa kazi kwa kila mtu.
Kila mtu ana majira yake ya kazi.
Hebu muulize hao watakaofuatilia kinachoendelea huko Kenya kwa lugha ya malkia ni asilimia ngapi ya Watanzania?
CCM wananuna Sana kwa kile kinachoendelea Kenya. Sijui kwann?
Kwa nini wasinune?

Hebu fukiria kama mwendazake Magufuli baada ya kutangazwa mshindi angefunguliwa kesi mahakani kupinga ushindi wake!

Hebu fikiria kama mtuhumiwa wa kwanza kwenye kesi hiyo angekuwa ni yeye ibilisi na mshtakiwa wa pili Tume Ya CCM ikiongozwa na Mahera!

Nakuapia hakungelalika wala hakungekalika!
Alichokisema kwenye Space juzi mzee Wasira ndiyo mawazo ya wanaccm wailo wengi.
Ha ha haaa! Usinichekeshe ndugu yangu...heri hata maiti anayetembea anaweza kuwa na mawazo mapya?
Kesi ya mbowe Tu hapa watu walikuwa wanafukuzwa wasione yanayoendelea, CCM ni Kansa
Shetani hutenda gizani. Jaribu kummulika fisi usiku akiwa mawindoni kwa tochi, halafu urudi hapa utusimulie.
 
Back
Top Bottom