GE2025 Kesi ya Lissu Oktoba 8, 2025: Mchuano wa Maswali kati ya Lissu na Shahidi wa Jamhuri

GE2025 Kesi ya Lissu Oktoba 8, 2025: Mchuano wa Maswali kati ya Lissu na Shahidi wa Jamhuri

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,040
LISSU MAHAKAMANI ⚖️​

Lissu: Kwa ufahamu wako kwanini unasema maneno niliyoyasema siku ile ya kuita waandishi wa habari, yalikuwa ni kosa la uhaini? 🤔
ACP Bagyemu: Ni kosa.

Lissu: Hata wewe kuita waandishi wa habari wakusikilize ni kosa la uhaini?
ACP Bagyemu: Inategemea.

Lissu: Soma PGO na useme, kwenye kifungu 8 kama kuna maneno niliyosema kuita waandishi wa habari ni kosa?
ACP Bagyemu: Sijasema.

Lissu: Kuna mahali ambapo umeandika katika maelezo yako kuwa umeita waandishi wa habari, yapo?
ACP Bagyemu: Hayapo.

Lissu: Lengo la uhaini lazima lionekane kwa matendo au kitendo cha dhahiri.
ACP Bagyemu: Ni sahihi.

Lissu: Naomba uwasomee majaji, maana ya neno Publish.
ACP Bagyemu: Akasoma.

Lissu: Aliyepeleka hayo maneno kwenye mtandao wa Jambo TV ni shahidi P?
ACP Bagyemu: Sio kweli.

Lissu: Aliyerusha maneno hayo kwenye mtandao ni P2?
ACP Bagyemu: Ni P na Tundu Lissu.

Lissu: Sasa kwanini P (shahidi fichwa) hajashtakiwa?
ACP Bagyemu: Hajashtakiwa kwa sababu ni mwandishi wa habari na hakuja kwako kwenye mkutano wako ili taarifa akaweke jikoni kwake. 📰

ACP Bagyemu: Huyo P alitueleza kuwa baada ya mkutano wa Mwenyekiti wa Chadema, waandishi walitolewa nje ya ukumbi.

Lissu: Wewe ofisa mzima wa Polisi hujui mkutano ulifanyika wapi?
ACP Bagyemu: Hamkutualika.

Lissu: Ulimhoji John Mnyika, Afisa Habari wa Chadema, Brenda Rupia kuhusu utaratibu wa juu ya kualika waandishi wa habari?
ACP Bagyemu: Sikumhoji.

Lissu: Waeleze majaji, kama mlihoji viongozi wengine wa chama kuhusiana na utaratibu wa kualika waandishi wa habari.
ACP Bagyemu: Sikumhoji.

Lissu: Ila mimi ndiyo umenishikilia?
ACP Bagyemu: ...

Lissu: Waeleze majaji kama mimi ni mmoja wa wakurugenzi wa Jambo TV.
ACP Bagyemu: Sina uhakika nalo.

Lissu: Waeleze kama mimi Tundu Lissu nina password ya mtandao wa Jambo TV.
ACP Bagyemu: Siwezi kufahamu. 🔐

Lissu: Kama unajua nina password, waeleze majaji jinsi nilivyoingia kwenye mtandao wa Kamno TV na kuweka hizo picha mjongeo.
ACP Bagyemu: Sijui.

Lissu: Hizo picha zilikuwepo kwenye mitandao mingine?
ACP Bagyemu: Siwezi kujua, ila shahidi P alieleza hiyo.

Chanzo: Nipashe Digital

1759904185260.png
 
Huyu George ni takataka na mavi kabisa...

Afadhali hata kina Ramadhani Kingai na wenzake wakati wa kesi ya ugaidi wa Freeman Mbowe mwaka 2021 - 2022 walikuwa na akili kidogo...

Huyu George anasukumwa na wakili Tundu Lissu kisha anaingia ndani sufuria la kukaangia na kuanza kujikaanga kwa mafuta yake yeye mwenyewe...

Polisi waongo sana aisee...
 
Part 65

Mhe. Lissu : Matukio ya tarehe 07/04 ulisema Andrew Churu alitoka Makao Makuu ya polisi Dodoma na kuja Dar es Salaam kukuletea vifaa kadhaa na maelezo ya shahidi P?

George: NI KWELI VYOTE ALIKUJA NAVYO. NILIPOKEA.

Mhe. Lissu: Ulimuelekeza akabidhi vitu hivyo kwa Peter Malugala.

George: Ni sahihi kabisa.

Mhe. Lissu: Ulimwambia pia aandike maelezo yake yeye Mwenyewe?

George: Nilisema aandike maelezo.

Mhe. Lissu: Ulisema maelekezo yaandikwe na nani?

George: Sikujali nilisema tu aandike maelezo.

Mhe. Lissu : Kwahiyo hukujali kama anaaandika mwenyewe?

George: Yes sikujali.

Mhe. Lissu : Andrew Churu alijiandikia Mwenyewe?

George: Sikusoma maelezo yake.

Mhe. Lissu : Alijiandikia na kujionya mwenyewe?

George: Mimi sikusoma kiukweli.

Mhe. Lissu: Kesi ya ugaidi husomi mashahidi?

George: Mahamba ndio alisoma hilo sio mimi.

Mhe. Lissu : Baada ya kuwa umeletewa memory card na maelezo ya P ulisema umefahamu kuwa ile video ilikuwa picha halisi?

George: Yes ni kweli nilisema hivyo.

Mhe. Lissu : Je wakati unafikia hiyo conclusion je ulikuwa umeshapata taarifa ya kitaalamu ya Kaaya ambae ni mtaalamu wa forensic?

George: Nilikuwa sijapata hiyo taarifa kabisa.

Mhe. Lissu : Waeleze majaji kulikuwa na sababu gani ya wewe ulishajua hiyo video ya kweli kwanini ulimpa Kaaya aende akachunguze hiyo video wakati ulishajua ni halisia?

Grorge: Sababu ya meta data lakini kuona kwa macho huwezi kugundua kama video ni halisi. 😂

Mhe. Lissu : Umeiwasilisha hiyo video hapa mahakamani?

George: Sijaiwasilisha mimi kiukweli, niliiona ile siku.

Mhe. Lissu : Kwahiyo kama uliona wewe na majaji wameshaona?

George: Watakuja kuiona huko mbele.

Mhe. Lissu : Je wewe sasa umeleta?

George: Sijaleta.

Mhe. Lissu : Je umesoma report ya hiyo video kutoka kwa mtaalamu?

Grorge: Mimi sikuisoma.

Mhe. Lissu : Je maelezo ya Kaaya ulisoma?

George: Nilisoma ndio.

Mhe. Lissu : Je Inspector Kaaya alisema kwamba walioingiza mtandaoni ni P?

George: Si kweli hakusema hivyo.

Mhe. Lissu anasema ngoja twende kwenye statement yako hapa.

Naomba nimsomee yafuatayo kutoka kwenye maelezo yako wewe mwenyewe. "Mnamo tarehe 06 nilimtafuta kiongozi wa Jambo nikimtaka anipatie picha halisi aliniambia muhusika na kifaa viko Dodoma" haya ni yako?

George: Yes niliandika mimi hapo.

Mhe. Lissu : Haya twendeleee kama unayatambua.

Mhe. Lissu : “baada ya kuletwa memory card na maelezo ya shahidi kwamba nj yeye aliyerekodi na kuchapisha mtandaoni nilijiridhisha ni video halisi" haya maneno ni ya kwako au sio ya kwako?

George: Ni ya kwangu kabisa.

Mhe. Lissu : Haya ni maneno uliyoandika tar. 08/04/2025 ?

George: Ni kweli kabisa.

Mhe. Lissu : Sasa tuzungumze kuhusiana na Uhaini.

Ulisema kwamba nilielekeza uchunguzi wa uhaini kwasababu Lissu alisema atahamasisha uasi?

George: Ni kweli kabisa.

Mhe. Lissu : Mheshimiwa nimekosea we sio mheshimiwa sasa kuna mahali kokote umetafsiri neno uasi?

George : Kuzuia uchaguzi, vitisho kwa serikali basi sikusema neno moja moja. kwahiyo sikutoa tafsiri ya neno uasi.

Mhe. Lissu : Je katika hati ya mashitaka ninayoshtakiwa nayo kuna ufafanuzi wa neno tutahamasisha uasi?

George: Huo ufafanuzi upo.

Mhe. Lissu : Sasa tuambie upo wapi? Hapo kwenye hati ya mashitaka? Nakusomea hati ya mashitaka ilivyosema? Neno uasi limetajwa mara mbili. Je kuna mahali kokote imeandikwa?

George: Uasi ilitafsiriwa.

Mhe. Lissu : Una akili timamu wewe afisa wa polisi?

George: Nina akili timamu ndio maana ni afisa wa Polisi.

Mhe. Lissu : unaweza kuwa afisa wa polisi nchi hii na ukawa huna akili timamu.

Part 67 itaendelea kwenye post inayofuata

Naomba repost yako kwenye tweet hii
 
LISSU MAHAKAMANI ⚖️​

Lissu: Kwa ufahamu wako kwanini unasema maneno niliyoyasema siku ile ya kuita waandishi wa habari, yalikuwa ni kosa la uhaini? 🤔
ACP Bagyemu: Ni kosa.

Lissu: Hata wewe kuita waandishi wa habari wakusikilize ni kosa la uhaini?
ACP Bagyemu: Inategemea.

Lissu: Soma PGO na useme, kwenye kifungu 8 kama kuna maneno niliyosema kuita waandishi wa habari ni kosa?
ACP Bagyemu: Sijasema.

Lissu: Kuna mahali ambapo umeandika katika maelezo yako kuwa umeita waandishi wa habari, yapo?
ACP Bagyemu: Hayapo.

Lissu: Lengo la uhaini lazima lionekane kwa matendo au kitendo cha dhahiri.
ACP Bagyemu: Ni sahihi.

Lissu: Naomba uwasomee majaji, maana ya neno Publish.
ACP Bagyemu: Akasoma.

Lissu: Aliyepeleka hayo maneno kwenye mtandao wa Jambo TV ni shahidi P?
ACP Bagyemu: Sio kweli.

Lissu: Aliyerusha maneno hayo kwenye mtandao ni P2?
ACP Bagyemu: Ni P na Tundu Lissu.

Lissu: Sasa kwanini P (shahidi fichwa) hajashtakiwa?
ACP Bagyemu: Hajashtakiwa kwa sababu ni mwandishi wa habari na hakuja kwako kwenye mkutano wako ili taarifa akaweke jikoni kwake. 📰

ACP Bagyemu: Huyo P alitueleza kuwa baada ya mkutano wa Mwenyekiti wa Chadema, waandishi walitolewa nje ya ukumbi.

Lissu: Wewe ofisa mzima wa Polisi hujui mkutano ulifanyika wapi?
ACP Bagyemu: Hamkutualika.

Lissu: Ulimhoji John Mnyika, Afisa Habari wa Chadema, Brenda Rupia kuhusu utaratibu wa juu ya kualika waandishi wa habari?
ACP Bagyemu: Sikumhoji.

Lissu: Waeleze majaji, kama mlihoji viongozi wengine wa chama kuhusiana na utaratibu wa kualika waandishi wa habari.
ACP Bagyemu: Sikumhoji.

Lissu: Ila mimi ndiyo umenishikilia?
ACP Bagyemu: ...

Lissu: Waeleze majaji kama mimi ni mmoja wa wakurugenzi wa Jambo TV.
ACP Bagyemu: Sina uhakika nalo.

Lissu: Waeleze kama mimi Tundu Lissu nina password ya mtandao wa Jambo TV.
ACP Bagyemu: Siwezi kufahamu. 🔐

Lissu: Kama unajua nina password, waeleze majaji jinsi nilivyoingia kwenye mtandao wa Kamno TV na kuweka hizo picha mjongeo.
ACP Bagyemu: Sijui.

Lissu: Hizo picha zilikuwepo kwenye mitandao mingine?
ACP Bagyemu: Siwezi kujua, ila shahidi P alieleza hiyo.

Chanzo: Nipashe Digital

View attachment 3485306
Huyu George ni muhaya ?
 
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI

Part 71

Mhe. Lissu : Jaji Themistocles Kaijage, Jaji lubuva hao wote walikuwa wenyeviti wa tume ya Uchaguzi?

George: Ni kweli kabisa.

Mhe. Lissu: Na waliteuliwa na Rais?

George: Ni sahihi.

Mhe. Lissu : Je kuhusu Jaji Nyalali na Jaji Kisanga aliteuliwa na Rais kuwa wenyeviti wa tume za Rais?

George: Ni kweli.

Mhe. Lissu : Wanalipwa hela za serikali na umma wakateuliwa hao wote majaji nilowataja?

George: Sijui kwakweli.

Mhe. Lissu : Mohamed Chande Othamn amekuwa akiteuliwa kuwa Mwneyekiti wa Kikosi Kazi cha haki jinai?

George: Ni sahihi.

Mhe. Lissu : Sasa nikisema Majaji wanapenda kuteuliwa kwenye tume nakosea wapi?

George: Huna unalokosea.

Mhe. Lissu : Nakosea nini nikisema wanapenda kupandishwa vyeo hao majaji ni dhambi hiyo?

George: Sio dhambi.

Mhe. Lissu ; Unasema nilisema kuwa mahakamani hakuendeki majaji hawatendi Haki?

George: Ni haki ulisema.

Mhe. Lissu : Sasa ngoja nikusomee Tume ya Warioba ilisema nini kuhusu utendaji wa Majaji. Ukurasa wa 85 wa utafiti wa tume. Inasema hivi. "JAJI BILA KULAZIMISHWA ANAWEZA KUWA NA TAMAA KUWA JAJI MKUU AU APEWE CHEO KINGINE"

Ukurasa wa 90 Jaji mkuu Nyalali aliwahi kusema tatizo la mahakama kuu ni rushwa. Tume ya Warioba ilisema majaji "Ingawa Mahakama kuu hufanya maamuzi isiyozingatia maamuzi ya kimsingi ila ni mahakama ya rufani isiyotenda maamuzi yakiufundi yanayoweza kutenda haki ya kimsingi.

Mhe. Lissu : Sasa je mimi nikisema mahahkamani hakuendeki linakuwaje kosa la uhaini?

George : Hilo sio kosa na hujakosea hapa. Hilo lipo Kisutu.

Mhe. Lissu : Mlisema kuwa maneno yangu yalikuwa Jambo TV YouTube, Clouds na Mwanzo TV kwa mujibu wa Kaaya?

George: Ni sahihi tulisema hivyo.

Mhe. Lissu : Sasa kwanini wewe na wenzako mliamua kwenda Jambo TV peke yake?

George:Tulienda kote.

Mhe. Lissu : Je kwenye maelezo yako uliandika hilo?

George: Sikuandika.

Mhe. Lissu : Sasa kama mlienda huko kote Jambo TV na kwingine kote kwanini hujaandika?

George: Niliandika kabla sijaenda ila watu walienda.

Mhe. Lissu : Sasa tuambie shahidi gani alienda huko kwingine?

George: Simjui aliyeenda.

Mhe. Lissu : Sasa je ulikuwa objective kwenye police action zako?

George: Nilikuwa sahihi.

Mhe. Lissu: Ni kweli P alisema tulikuwa tunazingumzia matatizo ya uchaguzi?

George; Ni sahihi P alisema.

Mhe. Lissu :Sasa je kuzungumzia hayo matatizo ya Uchaguzi ni makosa ya uhaini?

George: Yeye alielewa hivyo.

Mhe. Lissu. Kwahiyo ni uhaini?

George; Sio Uhaini.

Mhe. Lissu : Haya maneno ulikuwa unayafahamu ulipoletewa Tar. 07/04?

George: Ndio sahihi.

Mhe. Lissu : Na tarehe 08/04 ndio uliamua kufungua makosa ya Uhaini?

George: Ni kweli kwa maelekezo yangu nilielekeza kufungua Uhaini.

Mhe. Lissu : Hadi tarehe 08/04 unahamishia jalada kwa Mahamba ulikuwa umemjulisha DPP kuhusu Uhaini?

George : Ndio nilikuwa sijamwambia DPP.

Mhe. Lissu : Mpaka unanfungua tarehe 08 si DPP wala maafisa wake aliyekuwa na taarifa yoyote kwamba kuna uchunguzi?

George: Mimi sikumjulisha ila Mahamba asingekuja ningemjulisha.

Mhe. Lissu : Sikiliza wewe POLISI acha kiherehere.

Jaji Nduguru anasema anaomba tupate health break angalau ya lisaa limoja.

Mahakama imeahirishwa baada ya lisaa limoja.

Part 72 itaendelea baada ya Break

Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali.
 
Naona Jaji kampa nafasi ya kwenda kujipanga,
 
Hii nchi wenye elimu ndio wanaharibu sana kuliko wasio na elimu.
Nakubaliana na wewe. Mafisadi papa wana elimu. Uharibifu mkubwa unaofanywa na wengi wa wale wasiokuwa na elimu ni kukubali kutumiwa na wahuni.
 
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI

Part 72

Mhe. Lissu anaendelea na Maswali ya Dodoso kwa Shahidi namba 1 wa Jamhuri George Bagyemu

Karani anasoma shauri na mawakili wa serikali wanajitambulisha hapa.

Tunaendelea muda huu.

Mhe. Lissu : Kesi ya Uhaini kwa haiba yake ni kesi ya usalama wa taifa ni kweli au si kweli?

George : ni kweli kabisa.

Mhe. Lissu : Mamlaka nyingine yenye mamlaka ya kuhusika na usalama wa taifa ni TISS?

Grorge : Ni sahihi.

Mhe. Lissu : Sasa waeleze majaji kama uliwahi mjulisha RSO?

George: SIJAWAHI. RSO ni mkuu wa usalama Dar es salaam.

Mhe. Lissu : Je ulimwambia mkurugenzi mkuu wa usalama wa Taifa?

George: Sijawahi kabisa.

Mhe. Lissu : Je unafahamu kama kiongozi mwingine wa Polisi aliwahi kutoa taarifa kwa idara ya Polisi?

George: Sijui kabisa.

Mhe. Lissu : Je hii ni kesi ambayo ilikuwa na umuhimu mkubwa kwa umma?

George: Ni sahihi ilikuwa hivyo.

Mhe. Lissu : Na hii ni kesi inayomuhusu mtu muhimu kisiasa?

George: Si kweli umuhimu huo siuoni.

Mhe. Lissu : Huyu Mshitakiwa ni Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Upinzani nchi hii?

George: Si kweli.

Mhe. Lissu : Je unafahamu ni Makamu Mwenyekiti na Mjumbe wa Kamati ya halmashauri kuu ya IDU international Democratic Union?

George: Ndio nasikia kwako.

Mhe. Lissu : Waeleze waheshimiwa majaji kama unafahamu au hufahamu amekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema 2019 hadi 2025?

George: Hilo ni sahihi kabisa.

Mhe. Lissu : Je unafahamu Mshitakiwa kwenye kesi hii aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Chadema 2011 hadi 2017 na alishambuliwa kwa risasi?

George: Hilo nalifahamu ila kuhusu risasi sijui.

Mhe. Lissu : Sawa Afisa wa polisi mkubwa kama wewe hujui kama nilishambuliwa na risasi.

Je mshitakiwa huyu amekuwa Mkurugenzi wa Sheria, Katiba na haki za Binadamu wa Chadema tangu 2004 hadi 2010.

Kama unafahamu kwamba mshitakiwa huyu aliwahi kuwa Mbunge wa Kuchaguliwa kati ya 2010 hadi 2019 alipovuliwa ubunge?

George: la kuwa Mbunge nafahamu ila la kuvuliwa sifahamu.

Mwanasheria Mkuu kivuli 2010 hadi 2017 nilipopigwa risasi?

George: Hilo ni sahihi ila kwenye risasi sina uhakika nalo.

Mhe. Lissu : Je unafahamu mshitakiwa huyu alishambuliwa na risasi tar. 07/09/2025?

George: Nafahamu lakini sijui kuhusu wasiojulikana.

Mhe. Lissu : Je unafahamu aliyekuwa Waziri wa mambo ya ndani mwezi September mwaka 2017?

George: Sikumbuki.

Mhe. Lissu Je nikukumbushe?

George: Naomba unikumbushe.

Mhe. Lissu: Alikuwa ni Mwigulu.

Mhe. Lissu : Sasa baada ya kushambuliwa nilisafirishwa kwenda Nairobi?

George: Ni sahihi ila muda sijui ilikuwa saa ngapi.

Mhe. Lissu : Je unafahamu au hufahamu kwa wakati huo uwanja wa Ndege wa Dodoma ulikuwa hauruhusu ndege kutua baada ya saa 12 jioni?

George: Hilo nafahamu kabisa.

Mhe. Lissu : Eleza kwa vile kulikuwa na hilo zuio ilibidi ruhusa maalumu itolewe na mamlaka ya ndege Tanzania?

George: Hilo sijui.

Mhe. Lissu: Je unafahamu Waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba ndie aliyetoa maelekezo?

George: Hilo sijui.

Mhe. Lissu : Je unafahamu ni Waziri Mwigulu Nchemba Dodoma wawepo saa sita ili niweze kusafirishwa kwenda Hospitali?

George: Sifahamu.

Mhe. Lissu : Waeleze kama unajua kama Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan alikuja kunitembelea Nairobi?

George: Nafahamu alikuja ndio.

Mhe. Lissu : Rais Mwinyi na mkewe pia walikuja. Hilo je?

George: Hao sifahamu kama waliokuja.

Mhe. Lissu : Je unafahamu Warioba, Jaji Chande Othman nao walikuja kunitembelea.

George: Kimya

Mhe. Lissu : SASA NAKUULIZA TENA.

Je hii ni kesi yenye umuhimu mkubwa wa kisiasa na umma?

George : Sio, kwasababu sio kesi ya kisiasa.

Mhe. Lissu : Je mshitakiwa huyu ni mtu muhimu kisiasa ndani ya JMT?

George: Sio mtu muhimu.
 
Back
Top Bottom