tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,040
Tutake radhi form 4 failures.Form four failures wameanza kudhalilika kwa mara nyingine tena kutokana na ujinga wao wa kutumiwa na wahuni. Hadi aibu.
Form 4 failure wenye akili hawakubali kutumiwa na wahuni.Tutake radhi form 4 failures.
Sio kila aliefeli hana akili yakupambanua mambo.
Huyu George ni muhaya ?LISSU MAHAKAMANI ⚖️
Lissu: Kwa ufahamu wako kwanini unasema maneno niliyoyasema siku ile ya kuita waandishi wa habari, yalikuwa ni kosa la uhaini? 🤔
ACP Bagyemu: Ni kosa.
Lissu: Hata wewe kuita waandishi wa habari wakusikilize ni kosa la uhaini?
ACP Bagyemu: Inategemea.
Lissu: Soma PGO na useme, kwenye kifungu 8 kama kuna maneno niliyosema kuita waandishi wa habari ni kosa?
ACP Bagyemu: Sijasema.
Lissu: Kuna mahali ambapo umeandika katika maelezo yako kuwa umeita waandishi wa habari, yapo?
ACP Bagyemu: Hayapo.
Lissu: Lengo la uhaini lazima lionekane kwa matendo au kitendo cha dhahiri.
ACP Bagyemu: Ni sahihi.
Lissu: Naomba uwasomee majaji, maana ya neno Publish.
ACP Bagyemu: Akasoma.
Lissu: Aliyepeleka hayo maneno kwenye mtandao wa Jambo TV ni shahidi P?
ACP Bagyemu: Sio kweli.
Lissu: Aliyerusha maneno hayo kwenye mtandao ni P2?
ACP Bagyemu: Ni P na Tundu Lissu.
Lissu: Sasa kwanini P (shahidi fichwa) hajashtakiwa?
ACP Bagyemu: Hajashtakiwa kwa sababu ni mwandishi wa habari na hakuja kwako kwenye mkutano wako ili taarifa akaweke jikoni kwake. 📰
ACP Bagyemu: Huyo P alitueleza kuwa baada ya mkutano wa Mwenyekiti wa Chadema, waandishi walitolewa nje ya ukumbi.
Lissu: Wewe ofisa mzima wa Polisi hujui mkutano ulifanyika wapi?
ACP Bagyemu: Hamkutualika.
Lissu: Ulimhoji John Mnyika, Afisa Habari wa Chadema, Brenda Rupia kuhusu utaratibu wa juu ya kualika waandishi wa habari?
ACP Bagyemu: Sikumhoji.
Lissu: Waeleze majaji, kama mlihoji viongozi wengine wa chama kuhusiana na utaratibu wa kualika waandishi wa habari.
ACP Bagyemu: Sikumhoji.
Lissu: Ila mimi ndiyo umenishikilia?
ACP Bagyemu: ...
Lissu: Waeleze majaji kama mimi ni mmoja wa wakurugenzi wa Jambo TV.
ACP Bagyemu: Sina uhakika nalo.
Lissu: Waeleze kama mimi Tundu Lissu nina password ya mtandao wa Jambo TV.
ACP Bagyemu: Siwezi kufahamu. 🔐
Lissu: Kama unajua nina password, waeleze majaji jinsi nilivyoingia kwenye mtandao wa Kamno TV na kuweka hizo picha mjongeo.
ACP Bagyemu: Sijui.
Lissu: Hizo picha zilikuwepo kwenye mitandao mingine?
ACP Bagyemu: Siwezi kujua, ila shahidi P alieleza hiyo.
Chanzo: Nipashe Digital
View attachment 3485306
Naona Jaji kampa nafasi ya kwenda kujipanga,#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 71
Mhe. Lissu : Jaji Themistocles Kaijage, Jaji lubuva hao wote walikuwa wenyeviti wa tume ya Uchaguzi?
George: Ni kweli kabisa.
Mhe. Lissu: Na waliteuliwa na Rais?
George: Ni sahihi.
Mhe. Lissu : Je kuhusu Jaji Nyalali na Jaji Kisanga aliteuliwa na Rais kuwa wenyeviti wa tume za Rais?
George: Ni kweli.
Mhe. Lissu : Wanalipwa hela za serikali na umma wakateuliwa hao wote majaji nilowataja?
George: Sijui kwakweli.
Mhe. Lissu : Mohamed Chande Othamn amekuwa akiteuliwa kuwa Mwneyekiti wa Kikosi Kazi cha haki jinai?
George: Ni sahihi.
Mhe. Lissu : Sasa nikisema Majaji wanapenda kuteuliwa kwenye tume nakosea wapi?
George: Huna unalokosea.
Mhe. Lissu : Nakosea nini nikisema wanapenda kupandishwa vyeo hao majaji ni dhambi hiyo?
George: Sio dhambi.
Mhe. Lissu ; Unasema nilisema kuwa mahakamani hakuendeki majaji hawatendi Haki?
George: Ni haki ulisema.
Mhe. Lissu : Sasa ngoja nikusomee Tume ya Warioba ilisema nini kuhusu utendaji wa Majaji. Ukurasa wa 85 wa utafiti wa tume. Inasema hivi. "JAJI BILA KULAZIMISHWA ANAWEZA KUWA NA TAMAA KUWA JAJI MKUU AU APEWE CHEO KINGINE"
Ukurasa wa 90 Jaji mkuu Nyalali aliwahi kusema tatizo la mahakama kuu ni rushwa. Tume ya Warioba ilisema majaji "Ingawa Mahakama kuu hufanya maamuzi isiyozingatia maamuzi ya kimsingi ila ni mahakama ya rufani isiyotenda maamuzi yakiufundi yanayoweza kutenda haki ya kimsingi.
Mhe. Lissu : Sasa je mimi nikisema mahahkamani hakuendeki linakuwaje kosa la uhaini?
George : Hilo sio kosa na hujakosea hapa. Hilo lipo Kisutu.
Mhe. Lissu : Mlisema kuwa maneno yangu yalikuwa Jambo TV YouTube, Clouds na Mwanzo TV kwa mujibu wa Kaaya?
George: Ni sahihi tulisema hivyo.
Mhe. Lissu : Sasa kwanini wewe na wenzako mliamua kwenda Jambo TV peke yake?
George:Tulienda kote.
Mhe. Lissu : Je kwenye maelezo yako uliandika hilo?
George: Sikuandika.
Mhe. Lissu : Sasa kama mlienda huko kote Jambo TV na kwingine kote kwanini hujaandika?
George: Niliandika kabla sijaenda ila watu walienda.
Mhe. Lissu : Sasa tuambie shahidi gani alienda huko kwingine?
George: Simjui aliyeenda.
Mhe. Lissu : Sasa je ulikuwa objective kwenye police action zako?
George: Nilikuwa sahihi.
Mhe. Lissu: Ni kweli P alisema tulikuwa tunazingumzia matatizo ya uchaguzi?
George; Ni sahihi P alisema.
Mhe. Lissu :Sasa je kuzungumzia hayo matatizo ya Uchaguzi ni makosa ya uhaini?
George: Yeye alielewa hivyo.
Mhe. Lissu. Kwahiyo ni uhaini?
George; Sio Uhaini.
Mhe. Lissu : Haya maneno ulikuwa unayafahamu ulipoletewa Tar. 07/04?
George: Ndio sahihi.
Mhe. Lissu : Na tarehe 08/04 ndio uliamua kufungua makosa ya Uhaini?
George: Ni kweli kwa maelekezo yangu nilielekeza kufungua Uhaini.
Mhe. Lissu : Hadi tarehe 08/04 unahamishia jalada kwa Mahamba ulikuwa umemjulisha DPP kuhusu Uhaini?
George : Ndio nilikuwa sijamwambia DPP.
Mhe. Lissu : Mpaka unanfungua tarehe 08 si DPP wala maafisa wake aliyekuwa na taarifa yoyote kwamba kuna uchunguzi?
George: Mimi sikumjulisha ila Mahamba asingekuja ningemjulisha.
Mhe. Lissu : Sikiliza wewe POLISI acha kiherehere.
Jaji Nduguru anasema anaomba tupate health break angalau ya lisaa limoja.
Mahakama imeahirishwa baada ya lisaa limoja.
Part 72 itaendelea baada ya Break
Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali.
Form IV mwenye akili hawezi kukubali kufanya kazi ya polisi hata siku moja.Tutake radhi form 4 failures.
Sio kila aliefeli hana akili yakupambanua mambo.
Hii nchi wenye elimu ndio wanaharibu sana kuliko wasio na elimu.Form 4 failure wenye akili hawakubali kutumiwa na wahuni.
Nakubaliana na wewe. Mafisadi papa wana elimu. Uharibifu mkubwa unaofanywa na wengi wa wale wasiokuwa na elimu ni kukubali kutumiwa na wahuni.Hii nchi wenye elimu ndio wanaharibu sana kuliko wasio na elimu.