Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Baada ya jana Septemba 9, 2026 Makamu Mwenyeekiti wa CHADEMA Bara, Joun Heche kupanda Kizimbani na kuanza kutoa ushahidi wake katika Kesi ya Uhaini inayomkabili Mwenyeekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu na leo tena anaendelea.
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam leo Septemba 10, 2026, huenda ikatoa uamuzi kuhusu pingamizi la Serikali katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu.
Pingamizi hilo linahusu ombi la Lissu la kuwaita viongozi na maafisa mbalimbali wa Serikali, wakiwemo Rais Samia Suluhu Hassan, kuwa mashahidi wa utetezi.
Miongoni mwa wanaosubiriwa ni Rais Samia, Makamu wa Rais Mstaafu Philip Mpango, Waziri Mkuu Mstaafu Kassim Majaliwa, CDF Jenerali Jacob John Mkunda, IGP Camilius Wambura na viongozi wa vyombo vya usalama.
Kinachoendelea kutoka Mahakamani - Shahidi John Heche akisalimiana na Dada yake Tundu Lissu.
Tundu Lissu ameshafika Mahakamani tayari kwa mwendelezo wa kesi inayomkabili, kwa ajili ya kuendelea kutoa utetezi wake katika kesi ya uhaini namba 19605/2025.
Leo, Septemba 10, 2026, tunaendelea na Part 387 ya kesi inayomkabili Mwenyekiti wetu wa Chama, Mhe. Lissu, ambapo shahidi wa tano wa utetezi, John Wegesa Heche, anaendelea kutoa ushahidi. Makamu Mwenyekiti amefika mapema katika viunga vya Mahakama, huku tukisubiri Majaji kuingia.
Wasaidizi wa Majaji kitaaluma ni Mahakimu wakazi wa Mahakama za wilaya au Mahakama za Hakimu Mkazi walioteuliwa kufanya kazi hiyo ya usaidizi kwa Majaji kwa maana ya kuwafanyia research za mambo mbalimbali ya Kisheria.
Kwahiyo kwa vile Majaji ni watatu na wasaidizi wa majaji wapo watatu hawa Mahakimu. Sasa hao mahakimu walishaingia na karani alikwisha ingia.
Kumbukeni jana Majaji walisema wataanza na uamuzi wa kwamba je wale mashahihidi wa Mhe. Tundu Lissu ambao ni Samia Suluhusu Hassan, Philip Mpango na Kassim Majaliwa wataitwa kuja kutoa ushahidi au hawataitwa? Ndo tutaanza nacho kabla ya John Heche kuendelea na ushahidi wake.
Majaji wameshaingia na Mwenyekiti Lissu pia ameingia.
Tunasubiri mambo kuanza na kuendelea. Mawakili wa serikali na wao wameingia.
Ajuaye wakili wa Serikali Mkuu amesimama na kutambulisho jopo lake.
Amesema shauri limekuja kwaajili ya kusikilizwa na Upande wa Jamhuri tupo tayari kuendelea.
Jaji Ndunguru anamuuliza Mshtakiwa kwamba unasemaje?
Mhe. Lissu anajibu kwamba yupo tayari
Jaji Ndunguru anamwambia Shahidi kwamba Mahakama inakukumbusha kuwa bado uko chini ya kiapo.
Lissu: Shahidi habari yako, habari za toka jana
Heche: Salama Mwenyekiti
Lissu: Waeleze majaji matukio mengine ya mauaji nyakati za uchaguzi ambayo hukuyataja jana
Heche: Waheshimiwa majaji tukio jingine lilitokea kwenye Uchaguzi mdogo Igunga aliuwawa Mbwana Masudi mwaka 2011 baada ya aliyekuwa Mbunge wa Igunga kujiuzulu na ilifanyika By-Election.
Lissu: Huyu Mbwana Masudi alikuwa nani aliuwawa namna gani na nani alihusika?
Heche: Mbwana Masudi alikuwa kiongozi wa CHADEMA kutoka Ubungo ambapo alienda kushiriki kampeni za uchaguzi Igunga, aliuwawa na viongozi na wanachama wa CCM na hakuna hatua zozote za kisheria zilizochukuliwa dhidi ya wale watu waliomuua
Lissu: Waeleze Majaji ufahamu wako iwapo kuna wanachadema walikamatwa kwenye uchaguzi huo wa Igunga
Heche: Kabla na wakati wa uchaguzi walikamatwa mojawapo ni Mwenyekiti wa Chama wa Kinondoni wakati huo Henry Kileo na Mkurugenzi wa Ulinzi wakati huo Wilfred Lwakatare walishtakiwa wote kwa kesi kubwa ya ugaidi. Kileo alishtakiwa Tabora na Mahakama baadae ilitupilia mbali hiyo kesi na kumuachia huru. Wilfred Lwakatare alishtakiwa mahakamani hapa Dar es Salaam na baadae Mahakama ilimuachia huru baada ya kuwa wamekaa gerezani muda mrefu maana kesi hizo hazina dhamana.
Lissu: Endelea na matukio mengine ya mauaji wakati wa Uchaguzi mdogo na Uchaguzi mkuu
Heche: Matukio ya mauaji yanayotokana na uchaguzi ni mengi mno. Mwaka 2020 kiongozi wa CHADEMA Tunduma aliuwawa, Mwanza aliuwawa kiongozi wa BAVICHA jimbo la Nyamagana
Lissu: Waeleze majaji kama kuna mauaji mengine yanayohusisha wananchi na sio viongozi wa chadema
Heche: Kuna mauaji yanayohusisha wananchi nimeyasoma kwenye vyombo vya habari wakati wa chaguzi za Serikali za mitaa, kuna maeneo ambayo yalitokea Shinyanga, Tunduma.
Lissu: Waeleze majaji juu ya mauaji Pemba na Zanzibar
Katuga: Mshtakiwa anauliza shahidi aelezee mauaji Pemba maana yake ana suggest jibu
Lissu: Shahidi kama anajua atasema anajua na kama hajui atasema hajui
Sehemu ya 388
Makam Mwenyekiti upande wa Bara, John Heche anaendelea kutoa Ushahidi wake
Jaji Ndunguru anasema nadhani hilo swali liondoe au muulize tu kama anakumbuka mauaji mengine
Lissu: Waeleze majaji mauaji mengine yaliyofanyika nyakati za uchaguzi
Heche: Waheshimiwa majaji nakumbuka mauaji makubwa wakati wa Uchaguzi wa mwaka jana yaliyofanywa na vyombo vya Dola na Polisi, mamia ya watu waliuwawa hasa Dar es Salaam, Mbeya, Arusha, Mwanza, Geita, Tarime na maeneo mengine.
Lissu: Waeleze majaji matukio mengine ya uonevu dhidi ya raia tofauti na mauaji
Heche: Matukio mengine ya uonevu ni pamoja na watu kutekwa, kupotezwa, ripoti ya TLS inasema kuna watu 718 wametekwa na kupotezwa, kati ya hao kuna Wanachama wa CHADEMA, viongozi wa CHADEMA, viongozi wengine wa Vyama vya siasa kama CCM ambao wameonyesha msimamo wao dhidi ya Serikali hii.
Lissu: Ripoti ya TLS ni ya mwaka gani, matukio yalitokea lini
Heche: Ripoti ni ya Mwaka 2026 ila matukio hayo ni ya muda mrefu, yapo ya mwaka huu, mwaka jana, mwaka juzi na mengine ni ya tangu 2016, 2017, 2018 na miaka mingine.
Lissu: Waeleze majaji kuhusu matukio ya watu kutekwa na kupotezwa unayoyafamu hasa 2016, 2017
Heche: Waheshimiwa Majaji matukio ya 2016 na 2017 ni pamoja na Kutekwa kwa Ben Saanane aliyekuwa Msaidizi wa Mwenyekiti Freeman Mbowe, Azori Gwanda aliyekuwa Mwandishi wa habari wa Mwananchi, Kanguye aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri mojawapo ya Wilaya huko Kigoma.
Lissu: Waeleze Majaji ufahamu wako kuhusu hawa watu endapo walipatikana au vipi
Heche: Mpaka leo hawajawahi kupatikana; familia ya Ben Saanane hawajawahi kuambiwa alipo Ben, vile Azori Gwanda na Kanguye vilevile
Lissu: Waeleze matukio mengine ya watu kutekwa
Heche: Waheshimiwa Majaji matukio mengine ni kutekwa kwa Balozi Humphrey Polepole alikuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, alikuwa Balozi, Mbunge, Mkuu wa Wilaya. Kutekwa kwa Mdude Nyagali mwanachama wa CHADEMA kutoka Mbozi tangu 2024 mpaka leo hajulikani alipo.
Kutekwa kwa Deusdedith Soka Mwenyekiti wa Bavicha Temeke, Jacob Mlay alikuwa Katibu wa CHADEMA Temeke, Daniel Chonchori anatokea Jimbo la Tarime na alikuwa Mjumbe wa Halimashauri Kuu ya CCM Taifa, Sinda Geteba huyu alikuwa mgombea wa Uchaguzi Kata ya Tarime kwenye uchafuzi wa mwaka jana na familia yake ilisema alichukuliwa na RCO wa Tarime, Bhurure Tall alikuwa Mwanachama wa CHADEMA, Amani Manengelo alikuwa Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Mwanza, Nyangoko Kina anatoka Sirari Tarime ni Mwananchi tu wa jimbo la Tarime, Dionizi Kipanya alikuwa Kiongozi wa CHADEMA Sumbawanga mjini, Siza Keheta kutoka Tarime. Waheshimiwa majaji orodha ni ndefu kwasasa naomba niseme hao
Lissu: Shahidi jana wakati unatoa ushahidi ulielezea kesi iliyokuhusu wewe na aliyekuwa Mwenyekiti Mbowe na viongozi wengine, naomba uwaeleze majaji ukiachia hiyo kesi, eleza zingine unazozifahamu za aina hiyo zinazokuhusu wewe au viongozi wenzako wa chama
Heche: Kuna kesi ya Ugaidi iliyomuhusu Freeman Mbowe kesi ya Mwaka 2021 na baadae aliachiwa na tukaona picha yake ya kwanza wakati huo akiwa Ikulu na Rais Samia Suluhu, msemo maarufu ni kuwa “kutoka Ukonga mpaka Ikulu”
Lissu: Alikaa gerezani muda gani?
Heche: Miezi 8 waheshimiwa majaji. Siku hiyo mwenyekiti anakamatwa tulikamatwa nae tulikuwa Mwanza.
Tulikuwa pia na viongozi wa dini na wazee; Dkt. Azaveli Lwaitama kwasasa ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Chama na Mwanachama wa CHADEMA, tulikamatwa na Mzee Masinde alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini CHADEMA, John Pambalu Mwenyekiti wa BAVICHA wakati huo na kwasasa ni Mkurugenzi wa Organization na Mafunzo Makao Makuu ya CHADEMA, Baba Askofu Emmaus Mwamakula, Mwenyekiti wa Njombe ambaye kwasasa ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema Dada Rose Mayemba.
Sehemu ya 389
Lissu: Shahidi umesema mlikamatwa wewe na Mwenyekiti na hao wengine, ila Mwenyekiti pekee ndio alifunguliwa kesi ya Ugaidi. Nyie wengine nini kiliwatokea?
Heche: Tulishikiliwa vituo mbalimbali vya Polisi ikiwemo Nyakato, Central Police Mwanza.
Tulikaa kwa siku kadhaa mimi nilikaa central Police Mwanza, Police walipekua nyumbani kwangu na baadae nikaambiwa niwe naripoti kituo cha Polisi, wengine walipelekwa Majumbani kwao kama Rose alipelekwa Njombe, Mzee Lwaitama alipelekwa Dar es Salaam.
Lissu: Endelea uwepo wa kesi zingine za aina hiyo
Heche: Oktoba 22, 2025 nilikamatwa hapo nje ya Mahakama hii, Nilikuwa nakuja kwenye kesi hii, nikaambiwa nina tuhuma za kuvuka mpaka kinyume cha sheria na nilishikiliwa Central Police Dar es Salaam na niliambiwa nasafirishwa kwenda Tarime na nilianza safari mpaka tulipofika Dodoma usiku, nikapelekwa kituo cha Polisi Mtumba Dodoma ambapo nilikiwekwa kwenye selo ya peke yangu mpaka nilipokuja kutolewa tarehe 4/11/2025 na kusafirishwa kurudishwa Dar es Salaam.
Waheshimiwa Majaji nilipokuwa kituoni ndugu zangu hawakujulishwa na wala hawakuruhusiwa kuniona mpaka nilipogomea kula na kunywa maji kwa siku tatu:
Lissu: Waeleze Majaji nini kilitokea uliporudishwa Dar es Salaam.
Heche: Niliporudishwa Dar es Salaam nilipelekwa kituo cha Polisi Oysterbay na niliwakuta Nassoro Katuga, Thawabu Issa, Job Mrema.
Lissu: Waeleze Majaji kitu gani kilitokea
Heche: Niliwakuta Mawakili wa Serikali Wakuu na pale kulikuwa na watu wengi siku hiyo wakiwa na majeraha na wengine wameumizwa sana na kukikuwa na watu wengi sana mpaka pale kwenye vyumba vya kwenye korido na hawa mawakili walikuwa na George Bagyemu Deputy ZCO na baadae waliingia kwenye chumba fulani.
Lissu: Waeleze majaji Nini kilitokea ?
Heche: Nilipelekwa kwenye chumba ghorofa ya kwanza, nikasomewa charge ya Ugaidi ya kuchoma vituo vya mwendokasi kutoka Kimara mpaka Ubungo, na hadi Magomeni. Alinisomea askari ambaye aliletwa na DZCO George Bagyemu.
Lissu: Ilikuwaje baadae ya kusomewa hiyo charge?
Heche: Sikuwa tayari kutoa maelezo yangu niliandika tu particulars zangu na nilipelekwa kituo cha Polisi Mburahati.
Lissu: Ulikaa muda gani Oysterbay Police?
Heche: Nilikaa hadi saa nne usiku lakini badae nilipelekwa Kituo cha Polisi Kijitonyama wakasema kimejaa ndio nikapelekwa Mburahati Police.
Lissu: Ulipofika Mburahati kitu gani kilitokea?
Heche: Nilikaa Mburahati kutoka tarehe 4 October mpaka tarehe 10 Mwezi wa 11, 2025.
Lissu: Ilipofika Novemba 10 nini kilitokea? Waeleze Majaji
Heche: Waheshimiwa Majaji nilirudishwa kituo cha Polisi Oysterbay na nilikutana na Naibu Katibu Mkuu Amani Golugwa ambaye alikuwa amekamatwa huko Arusha, Godbless Lema Mjumbe wa Kamati Kuu, Boniface Jacob nae Mjumbe wa Kamati Kuu., nao walikuwa wamekamatwa. Tulimkuta ZCO Mafwele alikuwepo pale, alituambia tudhaminiwe tuondoke na kesho yake tukaripoti central Police Dar es Salaam na baada ya hapo tuliambiwa tuendelee na shughuli zetu mpaka leo.
Sehemu ya 390
Lissu: Ulisema umekuwa Kiongozi wa Chama toka mwaka 2008 umekuwa diwani na baadae 2011 ukawa Mwenyekiti wa BAVICHA miaka yote hii, kuna kiongozi yoyote Mkuu wa Chama ambae hakukamatwa kwa sababu moja ama nyingine?
Heche: Sina Kumbukumbu ya Kiongozi yeyote ambae hajawai kukamatwa hadi leo.
Dr. Wilbroad Slaa, Wabunge akina Lema, Msigwa, Mwenyekiti Mbowe Mwenyewe.
Lissu: Kwenye kesi hii mimi nimekamatwa Tarehe 09/04 Je unafahamu kesi nyingine ya kwangu?
Heche: Hii sio kesi pekeee ambayo naifahamu uliwahi kukamatwa Tarime maeneo ya Nyamongo miaka ya 2013 na tulipokuwa Bungeni umekamatwa mara nyingi sana.
Na kati ya mwaka 2015 na 2020 umekamatwa mara kadhaa kwa kesi za Uchochezi na vitu kama hivyo.
Lissu: Nilipokamatwa Tarime tuhuma ilikuwa nini na nini kilitokea?
Heche: Nakumbuka kuna watu waliuwawa mgodini na Mhe. Tundu Lissu alikuja pale kwasababu kulikuwa na msuguano kati ya Polisi na familia zilizopoteza ndugu, Mhe. Lissu alikuja kama mtetezi wao hivyo alikakatwa na kufunguliwa kesi.
Lissu: Nilikuwa nani kipindi hicho?
Heche: Waheshimiwa Majaji alikuwa ni Mbunge na Mkurugenzi wa Sheria wa Chama.
Lissu: Hiyo kesi ya Uchochezi Tarime iliyokuwa inanikabili iliishaje?
Heche: Iliisha kama kesi hizi zingine kwenye vituo vya Polisi haikuendelea.
Lissu: Hizo kesi zingine ulizoziita za Uchochezi nazo ziliishaje?
Heche: Hizo kesi ziliisha hivyo hivyo na zingine tuliambiwa Serikali imezifuta kwasababu haikuwa na interest ya kuendelea nazo.
Lissu: Kwa ufahamu wako je nimewahi kutiwa hatiani na Mahakama yoyote nchini?
Heche: Hakuna kesi hata moja amewahi kukutwa na hatia katika kesi hizi nilizosema.
Lissu: Waeleze kwa ufahamu wako wa kesi za Wanachama wa Chadema waliofungwa na kukutwa na hatia?
Heche: Ukiachilia na ile kesi yetu ya Kisutu sina kumbukumbu na viongozi wakuu ambao wamewahi kukutwa na hatia hata mmoja.
Lissu: Waeleze Majaji kwa unavyofahamu wewe kama kuna chama kingine chochote ambacho wapo viongozi wake wanakamatwa kama Chadema?
Heche: Sina kumbukumbu za viongozi wa Chama kingine wamewahi kukamatwa.
Lissu: Hivi vitendo vya kukamata Viongozi na Wanachama na kuwapoteza. Lengo la haya mambo haya kutokea ni nini???
Heche: Waheshimiwa majaji lengo la kukamata kwao ni kuwatisha viongozi hao wa Chadema na wengine, kuwakatisha tamaa kusimamia Misimamo ya Chama mbalimbali ambayo wanakuwa wameichukua.
Lissu: Waeleze Majaji kwa ufahamu wako uhalali wa vitendo hivyo kwa kuwatisha na kuwakamata?
Heche: Hakuna uhalali wowote wa kuyafanya hayo, hakuna uhalali wa kisheria wala ki utu wa kukamata watu na kuwanyanyasa. Ninachokiona ni kile alichokisema Katibu Mkuu wa CCM wa Wakati huo kuwa unatumia Dola kuendelea kubaki kwenye dola kwa CCM.
Lissu: Nini kiliendelea Tarehe 07/09/2017 Dodoma Bungeni?
Heche: Mchana wa Tar. 07/09/20217 mchana akiwa ameenda kula Chakula cha mchana nyumbani kwake, alivamiwa na watu wasiojuliana, aliumizwa vibaya sana kwa risasi za moto. Alishambuliwa kwa risasi mchana kweupe.
Lissu: Wewe ulikuwa wapi siku hiyo?
Heche: Siku hiyo nilikuwa Bungeni Dodoma na tulikuwa na Mhe. Tundu Lissu.
Lissu: Kitu gani kilitokea kabla ya hilo tukio na baada ya hilo tukio?
Heche: Kabla ya hilo Shambulio tulikuwa Bungeni tulikuwa tunajadili Mkataba wa River Songwe Basin na nakumbuka Mhe. Lissu alichangia siku hiyo.
Sehemu ya 391
Makam Mwenyekiti upande wa Bara John Heche anaendelea kutoa Ushahidi wake.
Heche anaendelea kusema baada ya Mhe. Lissu kuchangia Bungeni, mchana alienda nyumbani kwake lakini akiwa njiani kuna gari ilikuwa ikimfuatilia nyuma mpaka maeneo ya nyumbani kwake kwenye eneo ambalo mimi nalifahamu ni eneo ambalo Viongozi wengine wa Bunge na Serikali walikuwa pia wanakaa hapo kwenye Compound moja na mara zote hata ukitaka kuingia kwenye hilo eneo, ukifika pale getini kulikuwa na maaskari ambao watakuuliza unaenda wapi? Nyumba namba ngapi? na kulikuwa na kitabu cha kusaini pale Getini. Alishambuliwa kwa risasi na baadae alisafirishwa kwenda Nairobi kwa ajili ya Matibabu ambapo alitibiwa kwa muda mrefu na baadae Ubelgiji.
Lissu: Ulijuaje hizo taarifa zote?
Heche: Nilikuwa Bungeni nilikuwa nae. Na pia nilimtembelea Nairobi Hospitali mara kadhaa na vilevile Spika wa Bunge kipindi hicho Job Ndugai alitutangazia Bungeni.
Lissu: Sasa Shahidi waeleze Majaji utaratibu wa Mbunge anapougua au kuumwa kupata matibabu huwa ukoje?
Heche: Mbunge anapopata matatizo ya kiafya ikiwa ni ndani ya Nchi anatibiwa kwa Bima ambayo ni kubwa kwa maana unapewa wewe na watoto wako. Na kama ni nje ya nchi, Ofisi ya Katibu wa Bunge inachukua jukumu la kukulipia matibabu eneo unalofikia pamoja na msaidizi wako unayekuwa nae.
Lissu: Sasa eleza Majaji kama utaratibu huo ulitumika kwa matibabu yangu?
Heche: Utaratibu huo haukutumika kwa Mh. Tundu Lissu. Hakulipiwa matibabu wala matumizi wala eneo alilokuwa anafikia alipokuwa anajiuguza.
Lissu: Kwahiyo nilitibiwaje?
Heche: Chama kililipia sehemu ya matibabu, michango ya matibabu na TLS Chama cha Mawakili Tanganyika ndo waligharamia pamoja na wananchi kwa ujumla.
Lissu: Hivi huo ubunge nini kilitokea baada ya mimi kuwa kwenye matibabu?
Heche: Mheshimiwa Tundu Lissu alivuliwa ubunge kwa sababu zilizoelezwa kuwa ni utoro wakati huo Mhe. Lissu alikuwa bado yuko Ubelgiji kwenye matibabu kati ya mwaka 2018 na 2019, nakumbuka jimbo lake alilokuwa Mbunge alichaguliwa mtu anaitwa Mtaturu.
Lissu: Waliokuja kunitembelea ni pamoja na nani?
Heche: Alikuja Makamu wa Rais wa Wakati huo Samia Suluhu ambae alikuja kukuangalia hapo Hospitali.
Lissu: Vipi kuhusu Rais Mwinyi?
Heche: Nakumbuka Rais mstaafu Mwinyi na mke wake Mama Siti Mwinyi walimtembelea Hospitali Nairobi.
Lissu: Je kuhusu Edward Lowasa, Fredrick Sumaye na Vuai kunitembelea Hospitalini Nairobi?
Heche: Nina kumbukumbu ya Edward Lowasa na Fredrick Sumaye Mawaziri Wakuu wastaafu kumtembelea Mwenyekiti hapo Hospitali. Sina kumbukumbu kuhusu Mzee Warioba na Vuai.
Lissu: Je ufahamu wako kuhusu Mohamed Chande Othman kunitembelea hospitali Nairobi?
Heche: Nina kumbukumbu hiyo ya Jaji Chande kumtembelea Mh. Lissu Hospitalini Nairobi.
Lissu: Kuhusu Pindi Hazara Chana Mh. Balozi wa Tanzania Kenya kunitembelea Kenya?
Heche: Mh. PINDI CHANA alimtembelea Mhe. Lissu kule Nairobi Hospitalini alipokuwa amelazwa.
Lissu: Wewe ulikuja Nairobi mara ngapi na ulitumia muda gani?
Heche: Waheshimiwa majaji nimeenda Nairobi mara kadhaa wakati mwingine nilikuwa nakaa week mbili au week moja.
Lissu: Kwa kukadiria utakuwa umekaa muda gani?
Heche: Ukiziunganisha ni mwezi mmoja na nusu hivi.
Lissu: Sasa turudi kwenye kesi ya Uhaini kwenye Tarehe 03/04/2025 kwenye ushahidi wako ulisema nia ya kuwaita ni kuwaita na kuwaelimisha watia nia juu ya msimamo wa Chama. Je mabadiliko gani mlikuwa mnayataka.
Heche: Ni mabadiliko ya Kikatiba na kisheria, Sheria zinazoongoza uchaguzi. namna zinavyopatikana tume za Uchaguzi, Kifungu cha 74 kinachounda hiyo Tume ya Uchaguzi na kuwepo kwa tume huru itakayotoa haki na usawa kwa watu wote.
Sehemu ya 392
Makam Mwenyekiti upande wa Tanganyika John Heche anaendelea kutoa Ushahidi wake.
Lissu: Waeleze Majaji baada ya Kamati Kuu hiyo ya 03/12/2025 kuchukua msimamo huo nini kiliendelea?
Heche: Msimamo huo ulitangazwa hadharani baada ya yalitotokea kudhulumu na kuwaonea watu Mheshimiwa Mbowe alitangaza na kusema Bila Mabadiliko, Hakuna Uchaguzi kwamba uchaguzi hauwezekani tena kwenye nchi hii kwa njia hizi za kawaida haziwezekani.
Lissu: Tamko hilo lilikuwa la tarehe ngapi?
Heche: Lilikuwa Tarehe 10/12/2024.
Lissu: Nini kiliendelea baada ya tamko hilo?
Heche: Tulikuwa tunaenda kwenye Baraza Kuu la Chama Chama mwezi January. Kamati kuu ilikutana Tarehe 19/01/2025 tulipitisha msimamo wa No reforms, No Election na kupelekwa kama agenda kwenye Baraza Kuu la Chama.
Tarehe 20/01/2025 katika Kikao cha Baraza Kuu la Chama lilipokea agenda hii na kuiunga mkono na baadae ilipelekwa siku iliyofuata kwenye Mkutano Mkuu wa Chama ambao ulikuwa ni Tarehe 21/01/2025.
Lissu: Kitu gani kilitokea kwenye mkutano huo mkuu?
Heche: Vilevile huo Mkutano huo ulikuwa ni mkutano wa Uchaguzi ambao ulimchagua Mwenyekiti Mpya wa Chama yaani Tundu Lissu na Makamu Mwenyekiti wa Chama Zanzibar Said Mzee na Makamu Mwenyekiti Bara John Heche.
Lissu: Mkutano Mkuu ulisema nini kuhusu No Reforms, No Election?
Heche: Mkutano Mkuu uliazimia kwamba Kamati Kuu ya Chama iandae mpango wa namna ya kuwafikia wadau na wananchi, Viongozi mbalimbali, wakiwemo Viongozi wa dini kuwaelimisha kuhusu msimamo wa No Reforms, No Election.
Lissu: Baada ya Mkutano Mkuu kuamua hivyo Kamati ikafanya nini?
Heche: Kamati Kuu ya Chama ilikutana kwenye Retreat iliyofanyika Bagamoyo na ikaazimia kwamba maazimio ya Mkutano Mkuu yakatekelezwe kwa maana ya kwamba Viongozi wa Chama, Mwenyekiti Tundu Lissu na Makamu Wenyeviti kutoka Bara na Zanzibar, John Mnyika Katibu Mkuu na Manaibu Katibu wakuu tulikubaliana kuwa tupeleke ujumbe wa No Reforms, No Election kwa wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa Dini, Wazee Maarufu, NGO's Asasi za Kiraia kwamba waunge mkono msimamo huo ili Uchaguzi ufanyike ambao utakuwa ni huru, haki na wawazi.
Lissu: Sasa shitaka linalonikabili nilisema maneno yenye maudhui ya kihaini mbele ya waandishi wa kihabari na kuhusu waandishi wa habari?
Heche: Tulikutana pia na Jukwaa la Wahariri kama wadau muhimu wa Habari na wao pia tulikutana nao kujadili kuhusu msimamo huu na Jukwaa la Wahariri.
Lissu: Mikutano gani mimi na wewe tulishiriki tulipowatembelea hao wadau uliosema?
Heche: Tulitembelea Ubalozi wa Marekani, Tulimtembelea Mzee Joseph Sinde Warioba na Mzee Butiku tulikutana nae.
Lissu: Ngoja ngoja huyu Mzee Butiku ni nani?
Heche: Mzee Butiku ni Mwenyekiti wa Mwalimu Nyerere Fiundation, wengine tulizungumza Jukwaa la Wahariri Makao Makuu ya Chama chetu, Tulimtembelea Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Ask. Pissa, Tuliwatembelea Legal and Human Right Centre.
Lissu: Huko kote tulipokwenda ulikosema na tulipoenda kwa Askofu Pissa. Waeleze Majaji huko kote nani alikuwa kiongozi na msemaji mkuu wa ujumbe wetu?
Heche: Kiongozi na Msemaji mkuu alikuwa ni Mwenyekiti Tundu Lissu, ambae ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Lissu: Katika Mazungumzo na wadau wote hawa ufahamu wako au kumbukumbu zako kuhusu mimi kuzungumzia kuhusu matatizo yetu ya mfumo wetu wa kisiasa na Kikatiba?
Jaji Ndunguru: Tuishie hapo. Tutarudi saa nane na nusu so hilo swali litakuja kujibiwa baadae.
Sehemu ya 393
Mawakili wa Serikali wameshaingia tayari Mahakamani.
Wasaidizi wa Majaji nao wameingia.
Hapa tunasubili Majaji na Mhe. Lissu then tuendelee tulipoishia.
Mahakama imerejea
Majaji wameingia na kuketi kwenye nafasi zao, wapo watatu kama kawaida yao.
Mhe. Lissu na yeye tayari keshaingia.
Jaji Ndunguru anasema tuendelee anauliza upande wa mashtaka kama wapi tayari?
Ajuaye wakili wa Serikali anasema Waheshimiwa Majaji sisi corum ipo kama ilivyokuwa awali na tupo tayari kuendelea:
Jaji Ndunguru anamuuliza Mshtakiwa kama yupo tayari?
Mhe. Lissu anasema Waheshimiwa Majaji nipo tayari, tuendelee.

Heche anasema sawa Waheshimiwa Majaji
Mhe.Lissu anaanza kumuongoza Heche
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji mazungumzo yangu kuhusu Tume ya Uchaguzi ya nchi hii kutawaliwa na Rais
Heche: Waheshimiwa Majaji kote tulikopita kwa maana ya kwamba tulizungumza na Wahariri, Viongozi Wastaafu kama Mzee Warioba, Askofu Pisa na wengine niliowataja ujumbe wetu ukiongozwa na Mwenyekiti wetu Tundu Lissu alieleza namna ambavyo Uongozi wa Tume ya Uchaguzi unaoteuliwa na Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, jinsi inavyovuruga Uchaguzi, kuonea wapinzani hasa Chadema, kufanya upendeleo wa wazi hasa kwa wagombea wa CCM, kuvunja sheria za uchaguzi kwa uwazi.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kuhusu kushiriki kwetu kwenye chaguzi hizo.
Heche: Tundu Lissu aliweka msimamo wetu wa CHADEMA kuwa hatuko tayari kushiriki kwenye chaguzi za namna hii ambayo matokeo yake ni mauaji, kuengua wagombea na watu kupotezwa.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji nilichowaeleza wadau hao juu ya kuhamasisha watanzania kupinga Uchaguzi wa 2025.
Heche: Mwenyekiti Tundu Lissu aliwaeleza wadau hao kuwa msimamo wetu wa chama kuhusu No reforms, No election tutazungumza na wananchi kwenye mikutano ya hadhara ili kupinga uchaguzi wa namna hii kufanyika katika nchi yetu.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji juu ya kuhamasisha uasi wa Watanzania kupinga mfumo huu wa uchaguzi.
Heche: Hakuna maneno exactly ya uasi ila kwa ujumla alilenga kupinga mifumo mibovu ya uchaguzi ili tuwe na chaguzi huru na za haki
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kuhusu maneno tutahamasisha umma kuzuia uchaguzi.
Heche: Ndio alisema waheshimiwa majaji
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kuhusu maneno tutavuruga uchaguzi huu
Heche: Ndio alisema uchaguzi huu tutauvuruga
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji katika mazungumzo yetu na wadau kuhusu kutumia neno tutakinukisha.
Heche: Sikumbuki mahali ambapo ulitumia neno tutakinukisha.
Mhe. Lissu: Katika mazungumzo na wadau, waeleze majaji kuhusu utengenezaji wa majimbo ya uchaguzi.
Heche: Tundu Lissu alizungumza kuhusu matatizo ya ugawaji wa majimbo ya uchaguzi na viongozi kujigawia majimbo bila kufuata idadi ya watu.
Mhe. Lissu: Shahidi nilisema nini kwenye mikutano na wadau kuhusu uteuzi wa wagombea?
Heche : Mhe. Tundu Lissu alieleza kuhusu namna ambayo wagombea wetu walienguliwa kwa wingi akitolea mfano kwa uchaguzi wa 2020 ambao ulivunja rekodi kwa wagombea wetu kuenguliwa.
Alitolea Mfano Jimbo la Mlimba alikokuwa anagombea Suzani Kiwanga na alizungumzia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji nilizungumzia nini kuhusu utaratibu wa kampeni za uchaguzi?
Heche: Tundu Lissu alieleza namna ambavyo kampeni za Uchaguzi hasa za Chadema zinavyoingiliwa na kuvurugwa, wagombea kusimamishwa kwa muda, vyombo vya habari kutokutoa habari sawa kwa wagombea kwa maana ya kufanya upendeleo kwa CCM.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji nilisema nini juu ya kamati za maadili ya uchaguzi?
Heche: Alisema zinatumika kuzuia wagombea wa upinzani hasa Chadema kufanya kampeni zao kwa uhuru, hii ni kuanzia ngazi ya Udiwani, Ubunge na Urais.
Sehemu ya 394
John Heche anaendelea kutoa ushahidi wake.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji nilisema nini juu ya mawakala na wagombea
Heche: Waheshimiwa Majaji, Tundu Lissu alieleza namna ambavyo mawakala na wagombea wamekuwa wakipata usumbufu kwenye process ya kuapisha, kupata fomu lakini pia hata kuingia kwenye vituo vya kupigiwa kura huwa wanazuiwa huku zoezi la kupiga kura likiendelea mpaka wagombea wanajiwakilisha wenyewe.
Alisema pia utaratibu wa Mawakala ni mbovu hasa unaolenga kuzuia Vyama vya upinzani hasa Chadema kushinda uchaguzi
Mhe. Lissu: Waeleze majaji nilisema nini juu ya yanayotokea siku ya uchaguzi
Heche: Tundu Lissu alieleza kuhusu namna uchaguzi unavovurugwa, kura zisizo halali kuingizwa kwenye mabox ya kura, kutangazwa wagombea ambao hawakushinda.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji nilisema nini kuhusu utaratibu wa kupinga matokeonya uchaguzi Mahakamani.
Heche: Tundu Lissu alieleza ni vingumu kupinga matokeo ya uchaguzi Mahakamani namna ilivyongumu kwenda Mahakamani,
Ukienguliwa na Tume unaanza kwanza kulalamika kwenye Tume iliyokuengua, hata kama umeenguliwa kimakosa haki yako yote unakuwa umeipoteza, vilevile kama ulikuwa mgombea lazima uweke deposit ya hela kwahiyo kama huna hela unapoteza haki ya kupinga matokeo ya uchaguzi.
Kama huna kiasi hicho cha fedha huwezi kufungua kesi hata kama umeonewa, Ushahidi unakuwa umevurugwa kwa kunyimwa fomu.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji nilisema nini juu ya kupinga matokeo ya Rais Mahakamani.
Heche: Tundu Lissu alisema Huwezi kupinga Matokeo ya Urais kwenye Mahakama yoyote katika nchi hii hata kama hakuchaguliwa.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji nilisema nini juu ya wananchi wasio na vyama kugombea Uongozi?
Heche: Katika nchi hii huwezi kugombea kama huna Uanachama wa Chama cha Siasa hata kama wananchi wanakuhitaji, lazima uwe kwenye Chama cha Siasa.
Alieleza namna ambavyo Mchungaji Christopher Mtikila alivyopambana kudai hiyo haki ya mgombea huru akafungua kesi mbalimbali mpaka Mahakama ya Afrika akashinda lakini Hukumu haijawahi kutekelezwa mpaka leo tangu mwaka 2011.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji nilisema nini juu ya harakati mbalimbali juu ya kubadilisha mfumo huu wa uchaguzi.
Heche: Tundu Lissu alieleza juu ya harakati mbalimbali ambazo zimekuwepo tangu 1993 lakini zimekuwa zikizuiliwa na CCM kwasababu ni wanufaika, Harakati za Tume ya Jaji Nyalali, Tume ya Jaji Kisanga, Tume ya Mark Bomani na Tume ya Jaji Joseph Sinde Warioba ambazo zote zilikuwa na mapendekezo kuhusu kubadili mfumo wa Uchaguzi kuruhusu mfumo wa kidemokrasia na kuondoa mfumo wa chama kimoja, kuwapa wananchi nguvu ya wao kuamua nani awe kiongozi wao.
Mhe. Lissu: Naomba ufafanue unaposema mfumo wa Chama kimoja una maana gani licha ya kwanza nchi ni ya vyama vingi???
Heche: Nina maana ya kwamba mfumo uliopo sasa wa uchaguzi umehodhiwa na CCM, ambapo Mgombea wa CCM ndio anaamua nani awe Mwenyekiti wa Tume, Makamu Mwenyekiti, Mkurugenzi wa Tume, nani awe kamishna kwenye Tume na hata ngazi za Wilayani wote wanaofanya kazi ni wateule wake au wanafanya kazi chini ya wateule wake, kama vile watendaji wa kata na wengi wao kama sio wote ni wanachama wa CCM mmoja wapo ni Wilson Mahera aliyekuwa Mkurugenzi wa Tume mwaka 2020 alisema Lissu hawezi kushindana na Magufuli na Mwaka 2025 amekuwa Mbunge wa Jimbo la Butiama kupitia CCM.
Heche anaendelea anasema kwenye Uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 aliyekuwa Mkurugenzi wa Tume Ramadhan Kailima aliondolewa katikati ya kampeni akaletwa Mkurugenzi mpya (yaani katikati ya match unaleta refa mpya) na aliteuliwa Kipilimba na baadae Kailima alirudishwa na ndo Mkurugenzi wa sasa.
Vilevile Katibu wa zamani wa CCM Bw. Omari Mapuli ni miongoni mwa makamishna wa Tume na hiyo inaonyesha namna ambayo mfumo wa Uchaguzi umehodhiwa na CCM.
Sehemu ya 395
Makam Mwenyekiti Bara John Heche anaendelea kutoa ushahidi wake.
Mhe. Lissu: Katika Ushahidi wako umemtaja Mchungaji Mtikila, kuna ushahidi ulitolewa hapa kuwa Mahakama ndio yenye kauli ya mwisho, hebu elezea.
Heche: Waheshimiwa Majaji tuna mikataba ya kimataifa ambayo tumesaini na tunapaswa kuizingatia, lakini kuna kesi katika Mahakama ya Afrika Mashariki mfano kesi ya Bob Cha Wangwe, Kesi ya Freeman Mbowe, Maalim Seif, Zitto Kabwe na wengine kuhusu mfumo wetu wa uchaguzi.
Mhe.Lissu: Waambie Majaji kuhusu mazungumzo yangu na wadau kuhusu kwenda Mahakama za Kikanda au Kimataifa.
Heche: Tundu Lissu alizungumzia kwamba kumekuwa na attempts nyingi za wadau kwenda Mahakamani kudai mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi lakini Serikali imekuwa ikipuuza kutekeleza maamuzi na ndio maana alisema Mahakamani hakuendeki hivyo alisema yanahitajika mabadiliko ya kisiasa ili kuwe na total overwhole ya mabadiliko katika mfumo wa kisiasa.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji nilizungumza nini juu ya haja ya kuahirisha uchaguzi wa 2025.
Heche: Alisema kwamba kwasababu Uchaguzi huu una matatizo, unaleta mauaji , hauleti matokea wanayotarajiwa na Wananchi hivyo alisema tuko tayari uchaguzi usogezwe mbele na tuzungumze na wananchi na wadau wote ili yafanyike mabadiliko ambayo yanaruhusu Uchaguzi huru na wa haki kuepusha maafa ambayo yangeweza kujitokeza kama uchaguzi ungeendeshwa kwa njia zilezile ambazo zimetumika miaka yote ili kuepusha maafa.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji jitihada za kuwashirikisha wadau wa nje kuhusu msimamo wetu.
Heche: Tulisafiri mimi, Tundu Lissu na Godbless Lema ambapo tulikutana na Waziri Mkuu wa Zamani wa Kenya Raila Amolo Odinga tulimueleza pia msimamo wetu kama mzee maarufu naye atoe kauli kuhusiana na mambo yaliyokuwa yanaendelea Tanzania kuhusu uchaguzi.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji ilikuwa tarehe ngapi
Heche: Sikumbuki tarehe exactly ila ilikuwa March 2025
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji sasa mkakati wa kwenda kwa wananchi tuliutekeleza namna gani.
Heche: Tuliutekeleza kwa kufanya mikutano ya hadhara, tulianza na Kanda ya Nyasa yenye Mikoa ya Njombe, Iringa, Mbeya, Songwe na Rukwa. Huko kote tulizungumza na wananchi kwamba ni muhimu mabadiliko kwanza yafanyike ya kuwapa wananchi uhuru wa kuchagua viongozi wanaowataka.
Mhe. Lissu: Mikutano ya Nyasa ilianza lini na kuisha lini?
Heche: Sikumbuki tarehe lakini ilikuwa mwezi wa tatu na kuisha mwanzoni mwa mwezi wa nne then tukarudi Dar es Salaam na baadae tukaenda Kanda ya kusini.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji mikutano tuliyofanya pamoja mimi na wewe
Heche: Mikutano ya pamoja tulifanya Iringa Mjini na Mbeya mjini.
Mhe. Lissu: ilikuwaje baada ya hiyo mikutano ya pamoja?
Heche: Tuligawanyika team mimi nilienda Njombe na baadhi ya maeneo ya Iringa na Mbeya, Tundu Lissu alienda Rukwa, Songwe, Tunduma na baadae tukaenda Iringa mjini.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kwenye hiyo mikutano tuliyokuwa pamoja nilizungumza nini tofauti yake na mikutano ya wadau.
Heche: Waheshimiwa Majaji ni mambo yale yale hakukuwa na utofauti inaweza kuwa lugha tu lakini content ni ileile kama aliyozungumza na wadau.
Sehemu ya 396

Mhe. Lissu: Waeleze Majaji wewe ulipataje habari ya mkutano wa tarehe 03/04/2025 ambao ndio nashtakiwa nao.
Heche: Nilipigiwa simu na Naibu Katibu Mkuu Bara wa CHADEMA anaitwa Amani Gokugwa.
Jaji Ndunguru: Mshtakiwa naomba kwa leo tuishie hapa
Jaji Ndunguru: Shahidi kwa leo tunaishia hapa tutaendelea kesho ila bado haujamaliza kutoa ushahidi wako.
Jaji Ndunguru mtakumbuka jana tulisema tutatoa uamuzi mdogo kuhusu mashahidi wa Lissu ambao ni watumishi wa Serikali.
Mtakumbuka kuwa tarehe 21/08/2025 baada ya Mahakama kutoa uamuzi kuwa mshtakiwa ana kesi ya kujibu, mshtakiwa aliwataja mashahidi 11 na shahidi wa kwanza ni Samia Suluhu Hassan, Philip Isdori Mpango, Kassim Majaliwa, Camillius Wambura ambaye ni IGP, John Mkunda ambaye ni CDF, Mkurugenzi wa TISS, Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai na wengine ni viongozi wa CHADEMA ambao wameshatoa ushahidi akiwemo John Heche anayeendelea kutoa ushahidi.
Tundu Lissu aliomba Mahakama itoe summons kuwaita kama mashahidi.
Upande wa mashtaka ulipinga juu ya maombi ya kuwaita mashahidi kwa mujibu wa kifungu cha 218 (1) na 314(2) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai
Hoja za upande wa mashtaka zilikuwa sita. Hoja ya kwanza ilitokana na kifungu cha 218(1) cha CPA kwakuwa mshtakiwa hakuwataja hao mashahidi wakati wa mwenendo wa ukabidhi hivyo hawezi kuwataja sasahivi ingawa aliwataja wakati wa hatua ya hoja za awali (PH) hiyo haitibu hoja ya kutowataja wakati wa mwenendo wa ukabidhi.
Hoja nyingine ni kwamba ushahidi wa Samia Suluhu na Kassim Majaliwa hauna relevance katika shauri hili, Pia walisema kuna mashahidi tayari ambao wameshatoa ushahidi ambao ni watumishi wa umma, pia waliendeleza kuialika Mahakama kwamba kuwaalika mashahidi hao ni sawa na kuja kuwafanyia maswali ya Dodoso kuhusu ushahidi ambao umeshatolewa kwasababu alisema mshtakiwa kuwa anataka waje waeleze kama walitishika au hawakutishika na hayo maneno.
Hoja nyingine ilihusiana na kifungu cha 9 cha Presidential Affairs Act kuwa Rais sio shahidi anayelazimika kutoa ushahidi au kuitwa kwenye proceedings ambazo ziko mahakamani na upande wa mashtaka pia walitaka kifungu cha 24 cha Sheria ya Usalama wa Taifa kuwa kinazuia kutoa taarifa zilizopo kwenye chombo cha usalama.
Mshtakiwa alijibu hoja hizo na alieleza kwamba mahakama iweze kutoa wito kwa mashahidi wote kwasababu ni haki yake kikatiba na kwamba hiyo ndio maana ya fair trial. Alieleza kwamba wakati wa committal Proceedings aliwataja mashahidi ila Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilikataa kuwaandika. Alieleza kuwa ndio maana aliwataja mashahidi hao katika mahakama kuu wakati wa usikilizwaji wa hoja za awali (PH).
Mshtakiwa alisema kila mtu ni compelable witness isipokuwa kama sheria imezuia. Alisema pia hakuna sheria inayozuia Rais kupewa wito wa kufika mahakamani na hao mashahidi wengine. Presidential Affairs Act imeeleza namna ya kumpatia wito Rais ambao ni kupitia kwa Katibu Mkuu Kiongozi au Msaidizi wake Binafasi (Kifungu cha 9 na cha 10).
Mshtakiwa alisema kwasbaabu shtaka linahusu kuitishia Serikali hivyo ushahidi wao ni muhimu sana katika shauri hili na wataisaidia mahakama katika kufikia kutenda haki. Mshtakiwa alisema pia hata kifungu cha 24 cha Sheria ya Usalama wa Taifa kinazuia shahidi kutoa chanzo cha taarifa na alitoa mfano hata katika kesi ya Khatibu Ghandi aliyekuwa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa Augustine Mahiga alitoa ushahidi.
Sehemu ya 396
Jaji Ndunguru anaendelea kusoma uamuzi,
anasema Mahakama imejiuliza endapo pingamizi ni la msingi.
Kifungu cha 281 cha CPA kinaeleza kuwa msajili atatoa summons kwa mashahidi waliotajwa wakati wa committal na tumeangalia ni kweli kwenye proceedings hakuna orodha ya mashahidi. Kutoorodheshwa mashahidi hakuwezi kutibiwa wakati wa usikilizwaji wa hoja za awali.
Tunakubaliana na upande wa mashtaka kwamba kutowataja mashahidi wakati wa committal hakutibiwi na kuwataja wakati wa usikilizwaji wa hoja za awali.
Kwa mujibu wa kifungu cha 314 cha CPA kinaipa Mahakama hiari ya kuruhusu mashahidi kuitwa kwa kuangalia umuhimu wa mashahidi hao.
Wakati mshtakiwa anasema anawataka hao mashahidi alisema anawataka waje waeleze kama walitishika au vinginevyo.
Katika kesi za jinai upande wa mashtaka ndio una wajibu wa kuthibitisha jinai na sio upande wa utetezi kuthibitisha utakatifu wake (innocence yake) hivyo Jamhuri ndio walikuwa na wajibu wa kuwaleta wao hao mashahidi kuja kuthibitisha na sio upande wa Jamhuri.
Mahakama inaona kwamba hakuna haja ya kuwaita mashahidi hao na ushahidi wao sio relevant katika kesi hii kwa upande wa utetezi.
Kuhusu Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa aliyetoa ushahidi katika kesi ya Khatibu Ghandi aliitwa na Jamhuri na sio upande wa utetezi na ni msimamo wa kisheria kwamba kila kesi huamuliwa kutokana na mazingira yake.
Katika kesi ya Khatibu Ghandi Sheria hii ya sasa ya Usalama wa Taifa haikuwepo.
Mashahidi ambao hatujawagusa ni DCI, CDF na IGP wao tumeona ushahidi wao ni relevant, hivyo summons zitolewe ili waje kutoa ushahidi upande wa utetezi.
Uamuzi wa Mahakama
Mahakama Kuu kupitia kwa Jaji Dunstan Ndunguru imekataa ombi la mshtakiwa Tundu Lissu la kuwaita baadhi ya mashahidi wa utetezi, ikieleza kuwa ushahidi wao hauna umuhimu kwani wajibu wa kuthibitisha kosa ni wa Jamhuri.
Hata hivyo, Jaji Ndunguru ameagiza kutolewa kwa wito rasmi (summons) kwa Mkuu wa Majeshi (CDF), Mkuu wa Polisi (IGP) na DCI ili wafike Mahakamani kutoa ushahidi upande wa utetezi.
Kesi imeahirishwa hadi Septemba 11, 2026
Updates via: Hilda Newton