Kesi ya Lissu Septemba 10, 2026: IGP Wambura, DCI Kingai na CDF Mkunda waitwa kutoa ushahidi

Kesi ya Lissu Septemba 10, 2026: IGP Wambura, DCI Kingai na CDF Mkunda waitwa kutoa ushahidi

10 September 2026
High Court of Tanzania
Kivukoni Front
Dar es Salaam, Tanzania

The High Court of Tanzania in Dar es Salaam September 10 , 2026.
REPUBLIC Versus TUNDU LISSU Treason case No. 19605 / 2025

1789024041364.png
 
MAHAKAMA IMEANZA TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE


SEHEMU YA 1.

ULE UAMUZI MDOGO WANAUKWEPA KAMA MAITI YA MCHINA.

Mahakama imeanza majaji wameingia

Mawakili wa pande zote wapo.

Jaji Nduguru: Mshtakiwa

Lissu: Nipo tayari

Shahidi John Heche anaoanda kizimbani.

Jaji Nduguru tuendelee UAMUZI MDOGO utasomwa.

Lissu: Sasa Heche elezea mauaji mengine.

Heche: Anaelezea mauaji ya Igunga. Kaulizwa na Lissu, mwaka gani?

Heche: Mwaka 2011, baada ya aliyekuwa Mbunge wa Igunga, Rostam, kujiuzulu. Akauawa Bwana Masoud.

Lissu: Huyo Masoud alikuwa nani na aliuawa na nani?

Heche: Alikuwa Kiongozi wa CHADEMA, anatokea Jimbo la Ubungo, akaenda kushiriki kampeni za uchaguzi.

Heche: Aliuawa na viongozi na wanachama wa CCM, na hakuna hatua zozote za kisheria zilizochukuliwa kwa waliofanya kitendo hicho.

Lissu: Waeleze, kwa ufahamu wako, kama wapo watu wa CHADEMA walikamatwa kwenye uchaguzi huo.

Heche: Ndiyo. Wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi walikamatwa. Mwenyekiti wa Mkoa wa Kichama Kinondoni, Henry Kilewo, na Mkurugenzi wa Ulinzi kipindi hicho, Wilfred Lwakatare.

Heche: Wakapewa kesi kubwa za ugaidi. Henry Kilewo alishtakiwa huko Tabora, baadaye wakamwachia huru, na Wilfred Lwakatare alishtakiwa (nimesahau wapi mimi, Grace), baadaye wakamwachia huru. Hiyo ni baada ya kuwa wamekaa ndani kwa muda mrefu, maana hizo kesi hazina dhamana.

Lissu: Basi endelea na matukio mengine au mauaji sehemu nyingine.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA 2.

Heche: Mwaka 2020, Kiongozi wa CHADEMA aliuawa Tunduma. Mwanza aliuwawa Mwenyekiti wa BAVICHA Nyamagana.

Lissu: Sasa, Shahidi, yote uliyoyaeleza yanahusu wanachama au viongozi wa CHADEMA. Sasa elezea kama kuna mauaji yanayowahusu wananchi wa kawaida ambao sio CHADEMA.

Heche: Waheshimiwa Majaji, kuna mauaji yanayowahusu wananchi ambayo nimeyasoma, kama mauaji yaliyotokea Shinyanga, ...

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji iwapo unafahamu mauaji ya Zanzibar na Pemba.

Katuga: Kaleta objection kwamba Lissu anampa Shahidi leading question, kwamba Heche alikuwa anaelezea mauaji ya uchaguzi. Sasa Lissu anampelekaje Pemba?

Lissu: Anasema yeye kamuuliza Shahidi kama anajua mauaji ya Pemba. Shahidi kama anajua aseme, kama hajui aseme. Haoni shida ya hilo swali.

Jaji: Umemuuliza kuhusu Pemba, ina maana Shahidi ataeleza specific kuhusu Pemba.

Lissu: Kasema amewithdraw hilo swali.

Lissu: Elezea mauaji mengine kama unayafahamu.

Heche: Waheshimiwa Majaji, nakumbuka mauaji yaliyotokea mwaka jana katika uchaguzi mkuu, ambapo mamia ya watu waliuawa. Mauaji hayo yalifanywa na vyombo vya Dola na polisi wa nchi hii.

Heche: Mauaji makubwa yalifanyika Dar, Mwanza, Mbeya, Arusha, Tarime, Geita na maeneo mengine mengi, mauaji ambayo hayakupaswa kutokea kwa kweli.

Lissu: Tutakuja huko. Unataka kutangulia peke yako. Waeleze Waheshimiwa Majaji kuhusu utekaji nyara wa viongozi na wanachama wa CHADEMA.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA 3.

Katuga: Ka-raise objection. Huu ulizaji maswali unapendekeza majibu, kwa sababu Shahidi katoka kwenye masuala ya mauaji, anamuhamisha.

Lissu: Nimeshaondoka kwenye masuala ya mauaji. Sasa Wakili wa Serikali anasema huu ulizaji unapendekeza majibu. Unapendekeza majibu gani? Kama kipo, Shahidi atasema kipo; kama hakipo, atasema hakipo. Issue ya utekaji nyara na upotezaji wa watu ni suala kubwa nchini hii. Sasa nasuggest nini? Hii ni leading question vipi? Basi vinginevyo, Waheshimiwa Majaji, nita-introduce new way ya jinsi ya kumuuliza maswali Shahidi yangu.

Majaji: Wanadebate hapa.

Ndunguru: Tunasisitiza tu mjikite kwenye zile kanuni za examination in chief. Maswali unayomuuliza Shahidi yasiwe yanamfanya Shahidi akujibu kama unavyotaka wewe.

Lissu: Basi, Waheshimiwa, naomba nirephrase. Shahidi, naomba uwaelezee Majaji matukio mengine ya uonevu mbali na hayo ya mauaji.

Heche: Waheshimiwa Majaji, matukio ya uonevu ni mengi, pamoja na utekaji na upotezaji wa watu. Nitaeleza ambayo nayafahamu.

Heche: Report ya TLS inasema watu 718 wametekwa na kupotezwa, ikiwemo viongozi wa CHADEMA, wanachama, na wanachama wa CCM ambao wameonyesha msimamo wa wazi wa kupinga Serikali hii.

Lissu: Simama hapo hapo, Shahidi.

Lissu: Swali langu ni kuhusu hiyo report ya TLS ni ya mwaka gani? Na hao waliodaiwa kutekwa ni kipindi gani? Tupe ushahidi uliokamilika.

Heche: Waheshimiwa Majaji, hiyo report ni ya mwaka huu, lakini haya matukio ni ya muda. Yapo ya mwaka jana, juzi, na mengine ya 2017, 2018. Kwa hiyo, yapo ya muda mrefu.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji matukio ya mwaka 2016.


WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
LEO MAHAKAMA ITATOA UAMUZI KAMA HAWA WAFUATAO WATAFIKA MAHAKAMANI KUTOA USHAHIDI AU LAA.


MASHAHIDI WA TUNDU LISSU

The key witnesses of Tundu Lissu in his defence against bogus charges:

Samia Suluhu Hassan — popote alipo, apelekewe summons. Mwenyekiti wa Baraza la Usalama wa Taifa na Mkuu wa Baraza la Usalama wa Taifa.

Philip Isdor Mpango — aliyekuwa Makamu wa Rais na Mjumbe wa Baraza la Usalama wa Taifa.

Kassim Majaliwa — aliyekuwa Waziri Mkuu, Kiongozi wa Shughuli za Serikali na Mjumbe wa Baraza la Usalama wa Taifa.

IGP Camillius Wambura — Inspector General of Police.

General Jacob John Mkunda — CDF.

Suleiman Mombo — Director General of Tanzania Intelligence and Security Services
Manyanza,shusha vitu!
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA 4.

Lissu: Tuanze na matukio ya mwaka 2017 ya utekaji na upotevu wa watu unayoyafahamu.

Heche: Kutekwa kwa Ben Saanane, aliyekuwa msaidizi wa Mwenyekiti wa wakati huo.

Azory Gwanda, aliyekuwa mwandishi wa habari wa Mwananchi.

Kanguye, aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri moja ya Mkoa wa Kigoma.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kwa ufahamu wako, hawa watu walipatikana ama vipi?

Heche: Mpaka leo, familia ya Ben Saanane haijawahi kumpata ndugu yao, na vyombo vya ulinzi na usalama viko kimya hivyo hivyo kuhusu Azory Gwanda.

Lissu: Na Kanguye?

Heche: Hivyo hivyo.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kuhusu utekaji mwingine unaoufahamu.

Heche: Waheshimiwa Majaji, kuna tukio la kutekwa kwa aliyekuwa Katibu Mwenezi wa CCM, Humphrey Polepole. Alikuwa Mbunge, Balozi na Mkuu wa Wilaya (DC).

Kuna pia matukio ya kutekwa kwa Mdude Nyangali, mwanachama wa CHADEMA kutoka Mbozi, ambaye mpaka sasa haijulikani alipo tangu mwaka 2024.

Pia kuna Deudedith Soka, Mwenyekiti wa Vijana wa CHADEMA kutoka Temeke.


WEKA EMOJI KAMA UNASOMA SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA 5.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, ufahamu wako, hao watu walipatikana au vipi?

Heche: Waheshimiwa Majaji, familia ya Ben Saa Nane haijawahi kumpata ndugu yao, na vyombo vya ulinzi havijawahi kuwaambia ndugu yao yupo wapi.

Hivyo hivyo kwa Azory Gwanda.

Lissu: Na Kanguye je?

Heche: Hivyo hivyo kwa Kanguye, Waheshimiwa Majaji.

Lissu: Tueleze matukio mengine.

Heche: Matukio mengine ni kutekwa kwa Humphrey Polepole, ambaye amekuwa Mbunge, amekuwa DC.

Matukio ya kutekwa ya Mdude Nyagali, mwanachama kutoka Mbozi. Mpaka sasa hafahamiki alipo.

Deusdedith Soka, Mwenyekiti wa Vijana CHADEMA kutoka Temeke.

Jacob Mray, alikuwa Katibu wa CHADEMA Temeke.

Daniel Chonchori, huyu Waheshimiwa Majaji anatokea Jimboni Tarime na alikuwa ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa.

Sinda Geteba, huyu alikuwa mgombea udiwani wa CCM Kata ya Sirari. Alikuwa ameshapitishwa kwenye uchaguzi wa mwaka jana.

Alichukuliwa na RCO Kanda Maalum ya Mara.

Kuna Bhurure Tall kutoka Tarime, alikuwa mwanachama wa CHADEMA.

Kuna Amani Manengero, Mwenyekiti wa Vijana kutoka Misungwi, Mkoa wa Mwanza.

Kuna Nyangoko Kina, huyu anatoka Tarime, Sirari. Alikuwa mwananchi wa kawaida kutoka Tarime.

Deonizse Kupanya alikuwa kiongozi wa CHADEMA kutoka Sumbawanga Mjini.

Kuna Siza Keheta kutoka Tarime.

Waheshimiwa Majaji, hao ni wachache ninaowakumbuka waliotekwa na kupotea.

Lissu: Asante.

Sasa Shahidi, jana wakati unatoa ushahidi ulielezea kesi iliyokuwa inakuhusu wewe na Freeman Mbowe na wabunge wengine.

Ukiacha kesi hii, eleza kesi nyingine zinazokuhusu wewe au viongozi wenzako.

Heche: Waheshimiwa Majaji, kuna kesi inayomhusu Mbowe ya ugaidi, ya kupanga kuua viongozi.

Lissu: Ilikuwa mwaka gani?

Heche: Ilikuwa mwaka 2021, na baada ya hapo tukaona picha akiwa Ikulu.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, hiyo kesi ilimuweka Mwenyekiti kwa muda gani?

Heche: Kwa miezi 8.

Na Waheshimiwa Majaji, siku hiyo Mwenyekiti anakamatwa nilikuwa naye.

Tulikamatwa pamoja, na hata viongozi tuliokuwa nao na wazee.

Naweza kuwakumbuka kama Dr. Azavery Rwaitama.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, huyu Dr. Azavery Rwaitama ni nani?

Heche: Huyu Dr. Azavery Rwaitama ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini.

Tulikamatwa na Mzee Sylvester Masinde.

Tulikamatwa na John Pambalu akiwa Mwenyekiti wa Vijana na sasa ni Mkurugenzi wa Organization na Uchaguzi.

Pamoja na Baba Askofu Emmaus Mwamakula.

Lissu: Baba Askofu Emmaus Mwamakula ni nani?

Heche: Sikumbuki vizuri.

Lissu: Katika ushahidi wako ulisema wewe na Mwenyekiti mlikamatwa na Mwenyekiti akafunguliwa kesi ya ugaidi.

Heche: Tulishikiliwa vituo mbalimbali vya polisi. Wengine walikuwa Kirumba, wengine Nyakato, na mimi na wenzangu tulikuwa Central, kituo kikuu cha Polisi Mwanza.

Tulikaa kituoni kwa siku tano. Mimi nilikaa siku tano. Tukaenda nyumbani kwangu kufanya upekuzi.

Baada ya hapo tukaachiliwa, tukatakiwa kuripoti polisi.

Na wengine walisafirishwa kwenda Dar es Salaam, kama Rose Mayemba na Askofu Mwamakula.

Lissu: Kesi gani nyingine umeshawahi kushitakiwa?

Heche: Tarehe 22 October mwaka jana nilikamatwa hapa hapa nje ya Mahakama.

Kwa tuhuma ya kuvuka nje ya mpaka.

Kwa hiyo nilichukuliwa hapa, Waheshimiwa Majaji, nikaambiwa nasafirishwa kwenda nilipofanyia kosa, kwa maana ya Tarime.

Lissu: Uliposema nje ya Mahakama, ni Mahakama ipi? Nchi hii ina Mahakama lukuki.

Heche: Nje ya Mahakama Kuu hii hii. Nilikuwa nakuja kwenye kesi.

Lissu: Endelea.

Heche: Waheshimiwa Majaji, niliambiwa napelekwa Tarime nilipofanyia kosa.

Mpaka nilipofika Dodoma usiku, nikapelekwa Kituo cha Polisi Mtumba.

Mtumba ipo ule mji wa Serikali.

Niliwekwa Kituo cha Polisi peke yangu mpaka nilipotolewa tarehe 04 November, kusafirishwa kurudishwa Dar es Salaam.

Waheshimiwa Majaji, nilipokuwa mle kituo cha polisi familia yangu haikujulishwa mpaka nilipogomea kula na kunywa maji.

Ndipo ndugu yangu akatafutwa na kuruhusiwa kuja kuniona Kituo cha Polisi Mtumba.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, hiyo siku ya tarehe 04 ulipofika Dar es Salaam kituoni kilitokea nini?

Heche: Nilifika Dar es Salaam, Kituo cha Oysterbay.

Nikawakuta hawa mabwana Katuga, Tawabu, Job Mrema na yule Bwana wa mwisho.

Lissu: Cuthbert Mbilinyi.

Nassoro Katuga: Hiyo Cuthbert Mbilinyi iondolewe, hajamtaja shahidi.

Lissu: Sawa.

Waeleze Waheshimiwa Majaji nini kilitokea.

Heche: Niliwakuta hawa mabwana—

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA 6.

Lissu: Siyo mabwana, wanaitwa Mawakili wa Serikali Wakuu.

Heche: Niliwakuta na watu wengi siku ile wakiwa wamejeruhiwa. Nikaambiwa ni sababu ya siku ya uchaguzi.

Na mimi siku ya uchaguzi nilikuwa Mtumba.

Hadi vyumba vya kwenye corridor palikuwa na watu wengine sana.

Hawa mawakili walikuwa na Bwana George Byagemu, Deputy ZCO.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kitu gani kiliendelea?

Heche: Nilipelekwa ghorofa ya kwanza kwenye chumba kimoja.

Nikasomewa charge ya ugaidi, kuanzia Ubungo, Msewe mpaka Magomeni, kwamba mimi nilihusika kuchoma vituo vya Mwendo Kasi.

Lissu: Nani alikusomea hiyo charge?

Heche: Simkumbuki nani alinisomea. Alikuwa ni askari ambaye aliletwa na George Byagemu.

Lissu: Nini kiliendelea?

Heche: Siku taa maelezo baada ya kusomewa charge.

Nilijaza particulars zangu tu, basi. Na baada ya hapo wakanipeleka Kituo cha Polisi Mburahati.

Lissu: Ulikaa muda gani pale Oysterbay?

Heche: Ni masaa tu. Siku hiyo hiyo nilipelekwa Mburahati.

Kwanza tulipita Kijitonyama, pakawa pamejaa. Wakasema wanipeleke Mburahati, katika kituo cha peke yangu.

Lissu: Kitu gani kiliendelea?

Heche: Nilikaa pale kituoni kutoka tarehe 04 hadi 10 November.

Lissu: Ilipofika tarehe 10, kitu gani kilitokea?

Heche: Nilichukuliwa pale kituoni, nikapelekwa Oysterbay.

Ambapo pale nilikutana na Naibu Katibu Mkuu ambaye alikamatwa kutoka Arusha.

Nilikutana na Mheshimiwa Godbless Lema, Mjumbe wa Kamati Kuu.

Boniface Jacob, Mjumbe wa Kamati Kuu.

Waheshimiwa Majaji, wote kwa pamoja walikuwa wamekamatwa na kuletwa kutoka walipokuwa.

Tukakutana na ZCO Mafwele.

Lissu: ZCO Mafwele wa wapi?

Heche: Wa Dar es Salaam.

Kwa hiyo tulikutana naye, akatuambia tudhaminiwe tuondoke.

Na baada ya hapo tuliambiwa tuondoke.

Lissu: Siku ya kuachiwa ni tarehe ngapi?

Heche: Tarehe 11 November.

Lissu: Mlipoenda kuripoti ilikuwaje?

Heche: Tulienda kuripoti kwa ZCO Mafwele. Akatuambia tuendelee tu na shughuli zetu.

Lissu: Hii tuhuma ya ugaidi iliyokuweka ndani kuanzia tarehe 22 October hadi tarehe 11, iliishia wapi?

Heche: Mimi sikukamatwa kwa ugaidi, bali kwa makosa ya kuvuka mpaka.

Ugaidi nilikuja kuona tarehe 04.

Lissu: Sasa hizi tuhuma za kuvuka mpaka na ugaidi ziliishaje?

Heche: Ziliisha tu, Waheshimiwa Majaji.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA 7.

Lissu: Kwa miaka yote hii, nani ambaye amepona kukamatwa na kufunguliwa kesi, kisha kuisha juu juu?

Heche: Hakuna ambaye amepona tangu niwe katika Kamati Kuu ya chama, kuanzia kina Dr. Slaa, Freeman Mbowe, Godbless Lema.

Lissu: Una kumbukumbu ya mtu ambaye hajakamatwa?

Heche: Sina kumbukumbu ya mtu ambaye hajakamatwa.

Lissu: Sasa Shahidi, mimi nimekamatwa tarehe 09 April na tarehe 10 April nikafunguliwa mashitaka.

Waeleze Waheshimiwa Majaji kama hii ni kesi yangu pekee unayoifahamu.

Heche: Waheshimiwa Majaji, hii siyo kesi pekee ya Mheshimiwa Lissu.

Kati ya mwaka 2012 au 2013 alikamatwa maeneo ya Nyamongo, Tarime.

Nakumbuka tukiwa Bungeni amekamatwa mara kadhaa.

Mimi nikiwa Bungeni karibu naye, amekamatwa mara nyingi sana, kesi mbalimbali kama za uchochezi.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, nilipokamatwa Tarime tukio lilikuwa ni nini?

Heche: Kuna watu wameuawa pale mgodini.

Palikuwa na msuguano kati ya ndugu na polisi walikuwepo.

Kwa hiyo alikuja Nyamongo, akapewa kesi ya uchochezi.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, wakati huo nilikuwa na nafasi gani ndani ya chama?

Heche: Waheshimiwa Majaji, wakati huo Lissu alikuwa Mwanasheria na Mkurugenzi wa Haki za Binadamu.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, hiyo kesi ya uchochezi Tarime iliishia wapi?

Heche: Waheshimiwa Majaji, hiyo kesi kama zilivyo kesi zingine, ziliishia vituo vya polisi.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, hizo kesi ulizoita za uchochezi ziliishaje?

Heche: Kesi nyingine ambazo Lissu alifunguliwa nazo ziliisha hivyo hivyo.

Lissu: Sasa Shahidi, naomba uwaeleze Waheshimiwa Majaji, kwa hizi kesi ambazo nilikamatwa na zikaisha hivi hivi, waeleze Waheshimiwa Majaji iwapo nimewahi kutiwa hatiani.

Heche: Waheshimiwa Majaji, katika kesi ambazo nazifahamu, Lissu ameshitakiwa, hakuna kesi ambayo ametiwa hatiani.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA 8.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji ufahamu wako wa kiongozi au mwanachama wa CHADEMA ambaye alipatikana na hati, akafungwa mahakamani au akalipa faini.

Heche: Sina kumbukumbu ya kesi zozote ambazo kiongozi au mwanachama amewahi kushitakiwa na kutiwa hatiani.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama unafahamu kuna kinga kwa viongozi wa CHADEMA ya kukamatwa na kushitakiwa.

Heche: Hakuna kiongozi wa CHADEMA mwenye kinga ya kushitakiwa.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama una kumbukumbu ya chama kingine chochote na wajumbe wake wa Kamati Kuu wamekamatwa na kushitakiwa, na kesi kuisha juu.

Heche: Sina kumbukumbu ya chama kingine chochote na wajumbe wake wa Kamati Kuu wamekamatwa na kushitakiwa, na kesi kuisha juu.

Lissu: Lengo la viongozi na wanachama wa CHADEMA kukamatwa na kuwekwa mahabusu na kuwafungulia kesi ni nini?

Heche: Kuwatisha, kuwakatisha tamaa na kuwarudisha nyuma katika misimamo mbalimbali ambayo chama kinapaswa kusimamia.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, uhalali wa vitendo hivyo vya kuwakamata viongozi na wanachama upo, kwa unavyofahamu wewe?

Heche: Hakuna uhalali wa kisheria wala kiutu wa kukamata watu na kuwanyanyasa.

Ni kama alivyosema aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa CCM, Dr. Bashiru Ally, kutumia dola kuendelea kubaki kwenye madaraka kwa CCM.

Lissu: Umesema ulikuwa na mimi Bungeni kuanzia 2015 hadi 2020. Waeleze Waheshimiwa Majaji, kitu gani kilitokea tarehe 07 September 2017?

Heche: Nilisema kwamba tulikuwa Bungeni 2015 hadi 2020, lakini yeye alishambuliwa kwa risasi alipokuwa anaenda kula chakula cha mchana kweupe nyumbani kwake siku ya tarehe 07 September 2017.

Lissu: Siku ya tukio wewe ulikuwa wapi?

Heche: Nilikuwa Bungeni Dodoma.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kitu gani kilitokea kabla ya shambulio na baada ya hilo shambulio?

Heche: Kabla ya hilo shambulio, siku hiyo tulikuwa Bungeni katika mjadala wa River Songwe Basin.

Baadaye mchana alienda nyumbani kwake, ambapo alifuatiliwa na gari mpaka maeneo ya nyumbani kwake, ambapo mimi ninapafahamu.

Na viongozi wa Serikali na Bunge walikuwa wanakaa kwenye hiyo compound hiyo moja.

Mara zote pale getini kulikuwa na walinzi.

Akafuatiliwa na akashambuliwa pale nyumbani kwake.

Hao washambuliaji walimfuatilia hadi nyumbani kwake.


WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
Back
Top Bottom