Kesi ya Lisu jinsi inavyowapa CHADEMA jukwaa la kupelela madai Yao mazito duniani

Kesi ya Lisu jinsi inavyowapa CHADEMA jukwaa la kupelela madai Yao mazito duniani

Lee Van free

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2024
Posts
2,833
Reaction score
8,777
Kupitia kesi ya Lisu CHADEMA wamepata nafasi sahihi kabisa ya kueleza mateso Yao,kudai haki za wananchi,kupelela hoja zao za msingi kabisa Kwa MAHAKAMA na Dunia nzima.

Kupitia kesi hii ya kijinga CHADEMA wamepata uwanja mzuri sana wa kuifahamisha Dunia rangi Halisi ya Tanzania ya CCM.

Kupitia kesi hii CHADEMA watafanikiwa kuua ndege wengi sana Kwa jiwe moja.

Ama kweli CCM ni kubwa jinga.Mara nyingi hua wanajikaanga kwa mafuta Yao wenyewe,na ndio maana kesi nyingi za kisiasa hua wanaangukia pua,ama kuachana na kesi hizo bila kujali hasara ya muda na fedha.

Kumbuka kesi za mpenda kesi na mpenda mahakama Mtikila.
Nchi ya ajabu sana hii.

Kupitia kesi hii MAHAKAMA ya Tanzania itaweka kumbukumbu zote ambazo Seriali ya CCM imewatendea wapinzani na hasa CHADEMA .

Mfano, uonevu wa CCM dhidi ya upinzani wakati wa kurudisha fomu,kampeni,wizi wa kura,kupika matokeo ya Urais,ubunge na udiwani na uchaguzi wa serikali za mitaa.

Matumizi ya Vyombo vya Dola nyakati za uchaguzi,na kukandamiza upinzani kwa manufaa ya CCM.

Jinsi serikali inavyoshutumiwa kubambikia kesi wapinzani,kuteka,kutesa na kuua

Matumizi ya MAHAKAMA,kukandamiza upinzanikwa manufaa ya CCM.

Mapungufu ya katiba yetu hususan Tume ya Taifa ya plUchaguzi kua haiko huru na SI ya haki kwa sababu inaundwa na wateule wa Raisa aliyepo madarakani ambae ni Mwenyekiti wa CCM na ni mgombea wa CCM.

PKwa kifupi KESI hii inaifaidisha sana CHADEMA kuliko serikali ya CCM.

Kesi hii inaifunua CCM Hadi Dunia imeweza kujua nguo ya ndani za CCM kua imetoboka

Yale ambayo CHADEMA ingechukua mwaka mzima kuzunguka Tanzania mzima kuwaeleza wananchi jinsi wanavyonyimwa haki zao za kisiasa,CHADEMA wanatumia muda mfupi kuwaeleza Majaji kupitia MAHAKAMA.

Ijapokua MAHAKAMA haitaamua juu ya mapungufu ya katiba na uonevu wa Vyombo vya Dola lkn kumbukumbu zitaandikwa na Dunia inasikia kwa haraka zaidi.

Dunia imeweza kujua matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2015,2020 na 2026 kua yalikua ya kimazingaombwe.

Uwanja huu wa kumwaga Radhi CHADEMA hata kama wangekua bungeni wasingeweza kuupata,lkn imekua kama zali Kila kitu kinamwagwa mahakamani.

Pengine kubwa jinga CCM wangeogopa CHADEMA wsiongee bungeni kwa kuhofia hoja zao zitaingia kwenye Hansadi,Sasa zinaingia kwenye kumbukumbu za MAHAKAMA za Dunia.

Haya maelezo ya mashahidi wa tundu Lisu yanaweza kuja kutumika kama ushahidi wa kesi za siku zijazo.

Ama kweli kumpiga teke chura ni kumfupishia safari.
 
Aliye juu mngoje chini.
Unaweza ukadhani unatamba sana huko juu ila wahalisia wanakusubiri hapa chini.
Hakuna jambo la huku chini linaloamuliwa huko juu katika dunia huru ya leo.
Kesi hii ni fursa ya kuonesha UHURU WA KWELI WA SHERIA ZETU ZENYE KUUZINGATIA UTAMADUNI WETU na sio mapokeo tu ya wakoloni.
mashtaka na hukumu yalikuwako hata kabla ya kuingia kwa ukoloni...hii ni rejea sahihi kwa majaji waliosoma uhakimu au ujaji wa nje ya nchi kwamba hata mababu zetu wa kihistoria (masokwe) waliamua na kuhukumu ...na inawezekana wazungu waliiga kutoka traditions zetu za hukumu...kwa vyovyote vile weledi,utashi ,uzoefu na historia vinawasimamia majaji wetu hadi sasa
 
Watulisema hii kesi ya kipumbavu tunachafuka kimataifa haina maslahi kwa umma mnataka kututeka tukisema maneno kama aya
 
Hii inatudhihirishia ule ukweli kuwa shetani hufanya hadaa ili uone kuwa umeshinda, lakini ushindi wa shetani kamwe siyo wa kudumu, kwa sababu lengo ni kukuangamiza.

CCM na viongozi wake walipoweza kutengeneza makundi ya watekaji, wauaji, wafiraji na waporaji wa mamlaka ya wananchi kupitia kura; na walipoona wameua maelfu ya watanganyika, kisha kujipachika rasmi madarakani, waliona wamepata ushindi wa kudumu, wakati kiuhalisia ni kuwa kila tukio ovu wanalolifanya linazidi kuwaangamiza. Lakini kwa vile inabidi CCM ipotee, wahusika wote wamenyimwa akili na hekima ii waendelee kufanya makosa mpaka kwa kiwango cha kutotibika.
 
Back
Top Bottom