Kesi ya Liyumba, Utata na Maendeleo yake

Status
Not open for further replies.
Ndio hapo tunajiuliza ni kazi gani hiyo ya mahakama yenye kuruhusu vitambulisho vilivyokwisha muda? Kwanini tusiulizie procedures za kuhakiki ili tujuwe ilikuwa vipi? Huyo mtu aliyeiangalia hiyo passport lazima kuna document alizosaini kuwa document hizo ni halali na pia hazijapitwa na wakati,wote na hakimu lazima wanajuwa.
 

- Kwenye hili ninakuelewa sana, lakini bado hujajibu swali langu linalotokana na hoja yako mwenyewe, eti hii ishu nzima inahusika vipi na JK kuwa serious au kutokuwa na vita vya ufisadi?
 

Kwenye highlight nyekundu, rejea pointi yangu kuhusu inavalid document kukubalika kisheria.

Kuhusu JK ni kwamba nyie mnasema inakuwa vipi tulitegema something different kwenye kesi hii, sasa na mimi nikasema ni kwanini mlimsifia JK mara baada ya kesi hizi kuanza? Kusema kuwa sasa anafanya kweli?
Sasa hapo siyo politics kusema wanapelekwa mahakamani na wakati huo huo wanatoweka chini ya sheria za utawala wako huo? Enzi hizo waliita makida makida, yani mnawachezesha masikini wa Tanzania makida.
 
Mtajadili weeeeeee lakini hapa ni changa la macho tokea za EPA yaani wizi mtupu.
 
- Kwenye hili ninakuelewa sana, lakini bado hujajibu swali langu linalotokana na hoja yako mwenyewe, eti hii ishu nzima inahusika vipi na JK kuwa serious au kutokuwa na vita vya ufisadi?

Hopefully posting yangu iliyopita imekupatia jibu.
 
Hapo pia mimi nimechoka kabisa. How do we elevate AL to such a status kwamba dhamana yake mpaka mkulu ahusike????? Bongo kweli kuna mambo!

Usiparamie issue kwa ushabiki.
Rejea posting zilizopita na utajuwa kuwa issue hii ni muunganiko wa issues....Hii kashfa ya twin towers unaijuwa wewe?
 
Hivi mfano Liyumba angetoroka jela nani tungemuona amezembea akam si magereza? Au angetoroka kituo cha polisi ingeelewekaje? Kwa sasa ni kwamba ametoroka katk mikono ya mahakama tena akiwa hakukwalifai hata hiyo bail. Hapa moja kwa moja ni uzembe wa mahakama!!!!!!

Sasa hili la kuhusika kwa JK nadhani kama nimekuelewa mkuu Jmushi ni kwamba watu kibao walianza kutoa credits kwa kukamatwa kwa hawa baadhi ya mafisadi!!! And JK seems alipendezewa na hizo sifa sasa basi kama kuna uzembe the very same people waliosifia JK wanapaswa kum-descredit. Maana isiwe sifa kwangu ok, uzembe am not responsible.
 
Usiparamie issue kwa ushabiki.
Rejea posting zilizopita na utajuwa kuwa issue hii ni muunganiko wa issues....Hii kashfa ya twin towers unaijuwa wewe?

Wewe dogo acha hizo mimi naweza kuwa naijua kuliko wewe maana niliwahi kufanya pale na inter-consult kwa miezi mitano!!
 
Wewe dogo acha hizo mimi naweza kuwa naijua kuliko wewe maana niliwahi kufanya pale na inter-consult kwa miezi mitano!!


And mind you unachokiona pale ni version ya 12 + variations zenye zaidi ya 30%
 

Jasusi,

Kesi zote za rushwa kubwakubwa hazitaleta neema kwa watanzania bali machungu na vilio ndio matarajio!

Ndiyo sababu mimi nilimuunga mkono Mh. Sitta pale alipomunyoshea kidole Jaji Mkuu pamoja na watumishi wa idara zake zote za mahakama.

Jasusi, pamoja na kwamba tatizo kubwa la nchi yetu ni lile la uongozi mbovu wa serikali yetu lakini kuna hili jingine la Idara ya mahakama hasa hawa ndugu zetu mahakimu na ma-advocates. Kwa kifupi ni kwamba hawa jamaa wameshindwa kabisa na hawawezi tena kufuata maadili ya kazi zao. Wamegeuza idara yao kuwa biashara chafu. Hawawezi tena kusimamia ile kitu inaitwa HAKI! Wanakula rushwa asubuhi, mchana na usiku bila hata aibu. Mishipa yao ya aibu imekatika. Ila siku yaja, pale watakapolia na kusaga meno!

Mungu wasaidie watz waweze kujinasua kutoka kwenye makucha ya hawa wala rushwa wakubwa akina Jaji, mahakimu na ma-advocates! Amen!
 
Last edited:
Mimi naona tatizo hapa ni
kuchukulia dhana ya kwamba mahakama na serikali ni vitu viwili tofauti.
Harafu dhana nyingine ni kwamba mtu kama Liumba ama Balali anaweza kuzitia kwapani bilioni 200 peke yake .

Ushauri
Haya mambo ya EPA sijui BOT yaachane kama yalivyo tukubalini kushindwa saizi tuelekezeni nguvu kuwanyang'anya hizo nafasi tukiweza hilo hapo baadae ndipo yataibuliwa haya ya EPA na BOT ,tukishindwa hilo bora tukae kimya.

Hivi kunafaida gani kumtuhumu mtu wizi wa EPA wa sh bilion 10 harafu akaundiwa kamati ika cost bilion 2.harafu akatoroshwa?? Harafu fedha hizo akaenda kuzitumia huko aliko?? Mim naona bora waacheni wajenge majumba yao hapo bongo kwa kutumia wizi wao na mda ukifika tutayarudisha majumba yetu maana yapo kwetu.
 

na hii inaonyesha ni kiasi gani hawa mafisadi wanaweza kuichezea hii nchi viganjwani mwao wapendavo
 
Wewe dogo acha hizo mimi naweza kuwa naijua kuliko wewe maana niliwahi kufanya pale na inter-consult kwa miezi mitano!!

Una maana ulishiriki kuwa consult ama?
Pointi yangu ni kwamba ccm imeingiza politics kwenye issue hii nyeti ya vita dhidi ya ufisadi na kwahiyo politics hizo ni lazima ziwacost. Wananchi kwa wingi wao wanaweza kupotoshwa lakini hapa JF ni NO.
 
Kuhusu JK ni kwamba nyie mnasema inakuwa vipi tulitegema something different kwenye kesi hii, sasa na mimi nikasema ni kwanini mlimsifia JK mara baada ya kesi hizi kuanza? Kusema kuwa sasa anafanya kweli?

- Bado ninamsifu JK kwa kitendo cha kuwafikisha mafisadi kwenye sheria, maana ndio kazi ya Chief Law Enforcement, yaani ku-enforce the law na kwa hili unless kutatokea rais mwingine huko mbele kama yeye, so far he stands tall kuliko marais wengine wote,

- What happens kwenye mahakama, hapana he has nothing to do with unless unashauri aziinglie mahakama, ili haki isitendeke kwa washitakiwa, eti unashauri Tanzania tuanze kwua taifa la namna hiyo? Kwani wale wahaini kina Uncle Tom Lugakingira, walipotoroka Jela kule Ukonga, inaamaanisha kwamba Mwalimu hakuwa serious na sheria?

Mushi bado sijakuelewa point yako, yaani JK anahusika vipi na dhamana ya huyu Liyumba na kutoroka kwake?
 

Mkamap hapo umenena..Ndio maana nikasema ccm sasa iwekwe kando, na kama wanacheza politics, basi reflection ya ubovu wa uongozi inaweza ikawaletea siasa chungu...Trust me, muda ni mfupi sana kuelekea uchaguzi mkuu na karata hazitachangika.
 
Mimi naona tatizo hapa ni
kuchukulia dhana ya kwamba mahakama na serikali ni vitu viwili tofauti.

- Hapana, mahakama ni moja ya vyombo vitatu muhimu vya serikali, ambavyo vinatakiwa ku-function independent of each other for the good of the people, sasa kama hili halifanyiki Tanzania, ni muhimu kujua sababu na kujaribu kurekebisha sababu,

Lakini ya kwamba rais wa jamhuri ahusike tena na mahubusu waliko mikononi mwa mahakama, itakuwa ni more than Banana Republic!
 

FMES Unaweza kuona hapo juu maelezo ya Mkandara, ccm waliizima ile issue ya Chenge kule bungeni na inawezekana ule unga unga ulikuwa ni mifupa ya albino kwani ukweli haujawekwa wazi na kitendo cha sakata lile kwisha labda kilihusishwa na uwezo wa kufanya kazi wa dawa hizo za kichawi...Ikapelekea viungo hivyo vya albino kuwa dili na ndio maana wenye kuhitaji viungo hivyo ni watu wenye uwezo ama madaraka. Kama issue ya unga unga ingeshughulikiwa ipasavyo basi labda albino wasingekumbwa na dhahma hii na waziri mkuu asingekuwa na haja ya kulia lia.

Hata hivyo pointi yangu inarudi pale pale, wewe na Mkandara mlisema JK anafanya kweli na bado unasisitiza kuwa thats the case,kwasababu mlijuwa kuwa sheria ni mbovu kama alivyosema Mkandara hapo juu na huku mkimsifia Mh Rais kwa kuwafikisha watuhumiwa hao kunako sheria mbovu.
 
Hakuna uwezekano hata kidogo wa CCM kukaa kando kwenye suala la Ufisadi Tanzania, ndio maana Makamba anajaribu kila leo kulibananga. Iwe ni EPA, Richmonduli, Radar etc. Maamuzi yote yaliyokuwa yanafanyika yalikuwa na baraka za chama. Kama mwenyekiti wa chama alikuwa anafahamu nini serikali ya chama chake inafanya "kutekeleza" ilani ya uchaguzi na kutatua matatizo yaliyokuwepo, na kama katibu mkuu alikubali kupokea fedha za wizi kwa ajili ya kampeni za chama na wagombea wake, basi chama hakiwezi kukwepa. Unaweza kusema huwezi kukihukumu chama kwa vitendo vya mwanachma wake, lakini how do you separate the two? Hasa pale anapokitumia chama na dhamana aliyopewa na chama kufanya ufisadi wake.
Lakini ni lazima tukubali kuwa Muungwana amefanya jambo la maana. Japokuwa waliofikishwa mahakamani wamefikishwa kutokana na shinikizo, na wamefikishwa kwa shingo upande, still hiyo ni hatua kubwa inayostahili heshima. Kufikishwa mahakamani ni hatua moja, na haki kutendeka ni hatua nyingine. Inaweza kuwa ni yale yale ya Brother Ditto, unaweza kusikia mtuhumiwa amekufa na faili lake limefungwa. Tunapaswa kuwa na subira kuona dhamira halisi ya serikali.
 
...ina maana bado hakuna taarifa inayoeleweka mpaka sasa? mliopo karibu na source mtujuze basi kuhusu hii episode na ijayo ikibidi.🙄
 
Una maana ulishiriki kuwa consult ama?
Pointi yangu ni kwamba ccm imeingiza politics kwenye issue hii nyeti ya vita dhidi ya ufisadi na kwahiyo politics hizo ni lazima ziwacost. Wananchi kwa wingi wao wanaweza kupotoshwa lakini hapa JF ni NO.

Nope nilikuwa nabeba zege!

Ok let's now get back to the topic. Kuhusu kupoliticize issues nadhani ni kaugonjwa ka viongozi wa kitanzania. And I especially smell a rat hasa pale uchaguzi unapokuwa ukikaribia. My point is and still is........ Not necessarily kwamba JK anahusika ( Well I am not ruling out completely maana Bongo kila kitu kinawezekana) Lakini katika jamii iliyomomonyoka maadili kiasi hiki je Liyumba hawezi kucheza faulo na hakimu pale Kisutu akatoka kwa staili aliyotokea??
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…