jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 26,329
- 25,263
Nadhani kijichuki hicho binafsi kipo...
Jamani inabidi nirudi tena kuweka wazi kuhusu Masha. Inaonekana huyu waziri haeleweki na watu japo anafanya kazi zake kwa mipangilio maalum. Katika hili, Takukuru iko chini ya Ikulu, Police iko chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani. Kesi imepelekwa mahakamani na Takukuru. Baada ya jamaa Liyumba kukitoa, waliopeleka kesi mahakamani ndio waliopewa jukumu la kumsaka. Sasa hii ni operation. Lazima Takukuru iwe na stratergy zake za kumnasa, zikiwemo kama ilivyoelezwa katika taarifa zao, matumizi ya resources zote zilizo chini yao, i.e. fedha, watu na vifaa.
Sasa niniyi mnataka wakati huo huo, Polisi nao waweke stratergy na kutumia resources zake kwa kazi ambayo tayari inafnywa na chombo kingine cha serikali. Hii italeta confusion ya hali ya juu.
Kitu kinachotakiwa hapa na alicho dai Masha ni kuwa, iwapo Takukuru inaona uwezo wake ni mdogo na inataka msaaada wa Polisi basi waseme hivyo na baadaye wakae na kuweka stratergy ya pamoja. Kwa mtindo huo wa kuunganisha nguvu, wanaweza kumnasa.
Hivyo ndio utaratibu wa kazi. Sio kuvamia tu kazi za watu wengine. Endapo itatokea katika utekelezaji wa kazi zake za kawaida, Polisi ikamuona mtuhumiwa Liyumba, hapo inaweza kumkamata kama mtuhumiwa mwingine yeyote.
Kama Masha angekurupuka tu na kwaambia Mapolisi wake wamtafute Liyumba, ninyi ndio mngekuwa wa kwanza kulalamika kuwa anaingilia kazi za Takukuru. Ama sivyo?
Nadhani hapo kwenye highlights panaweza kutusaidia zaidi kuona kwamba ikulu itachukuwa hatua gani kumtafuta Liyumba, Wakati Masha ana offer msaada kwa mkuu wa nchi(technically) Liyumba yeye ana ambaa ambaa.