Kesi ya Liyumba, Utata na Maendeleo yake

Kesi ya Liyumba, Utata na Maendeleo yake

Status
Not open for further replies.
Hii sinema kama ya kiarabu,nashindwa kabisa kuyaunganisha matukio duuh! sijui nini mwisho wake?
 
Ametoroka au ametoroshwa?

Yaani kama ni kweli hajulikani alipo mie kabla haijafika jioni naombea laana kwa viongozi waliobaki.Haiwezekani kabisa hawa watu wanaofanya kazi BOT wakawa wanapotea potea tu!

Where is Balali.Siko tayari kabisa,i have lot of question to ask
 
Duh!!! Kama ni kweli hii basi mafisadi wote warudishwe rumande haraka sana wakiwamo wale wa EPA na akina Mramba.
Kwa kweli Bubu uliyoyasema hapa yafaa kutekelezwa maana kama huyo bwana amekimbia tumeanza kuingiwa na hofu juu ya wengine iwapo nao hawatakimbia, lakini kakimbilia wapi passport yake si alikabidhi?
 
Tunatakiwa tuamini hivyo, tunatakiwa tumnyoshee vidole hakimu, tunatakiwa tumlaani Liumba, tunatakiwa ....... ndiyo ndivyo walivyopanga.

Tulitakiwa tuamini Balali anaumwa, tulitakiwa tuamini kapewa sumu, tulitakiwa tuamini serikali haijui yuko hospitali gani, tulitakiwa tuamini amekufa, tulitakiwa......ndiyo ndivyo walivyopanga.

Tutatakiwa tuamini makubwa zaidi ya haya, tutatakiwa tuamini tunapaa, tutatakiwa tuamini tunaelekea Kanaani nchi ya maziwa na asali, tutatakiwa ....... ndiyo ndivyo wanavyopanga.

OOh masikini Tanzania, nchi iliyojaaliwa neema, nchi inayojengwa na wenye moyo lakini inaliwa na wenye meno, nchi inayeondeshwa kwa usanii na ulaghai, nchi ambayo .....ndiyo ndivyo tulivyo - tumewaruhusu, tunawaruhusu na tutazidi kuwaruhusu wenyewe.
 
Kwamba Hakimu aliweka masharti magumu ya dhamana,
Kwamba Hakimu akayalegeza,
Kwamba Hakimu akapokea nyaraka zenye utata,
Kwamba hata hati ya kusafiria ya zamani,
Kwamba ile mpya sasa anayo mikononi mwake,

Duh kali, kwamba yuko bado nchini kwa mmoja wa wale vimwana na kwamba alijisahau tu akawa amelala fofofooooo

.... na kwamba sasa anatakiwa kesho aende mwenyewe mahakamani!!!! Je, ataweza ama ndio safari na muziki!!!!!

USIKOSE SEHEMU YA PILI YA FILAMU HII YA AJABU
 
kwa kweli hii ni zaidi ya movie, kweli hii ni "tanzania zaidi ya uijuavyo"
 
Kwamba Hakimu aliweka masharti magumu ya dhamana,
Kwamba Hakimu akayalegeza,
Kwamba Hakimu akapokea nyaraka zenye utata,
Kwamba hata hati ya kusafiria ya zamani,
Kwamba ile mpya sasa anayo mikononi mwake,

Duh kali, kwamba yuko bado nchini kwa mmoja wa wale vimwana na kwamba alijisahau tu akawa amelala fofofooooo

.... na kwamba sasa anatakiwa kesho aende mwenyewe mahakamani!!!! Je, ataweza ama ndio safari na muziki!!!!!

USIKOSE SEHEMU YA PILI YA FILAMU HII YA AJABU ILIYOREKODIWA BONGOWOOD
 
.... ametoraka na alionekana alijifunika kanga au buibui?..... interval sinema yenyewe inakuja baada ya muda mfupi
 
Liyumba atoweka?
Neema Mgonja
Daily News; Thursday,February 19, 2009 @18:56​

Dhamana aliyopewa mtuhumiwa wa matumizi mabaya ya madaraka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba, imeingia dosari baada ya mahakama kutoa amri ya kukamatwa pamoja na wadhamini wake.

Hata hivyo, amri hiyo leo ilionekana kugonga mwamba, baada ya mtuhumiwa huyo kusakwa na maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) bila mafanikio. Alitakiwa apandishwe kizimbani jana, lakini badala yake maofisa wa Takukuru waliambulia kuwakamata wadhamini na wakakiri mahakamani hapo kuwa Liyumba haonekani.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam juzi ilitoa hati ya kukamatwa kwa Liyumba ikiwa ni siku moja tu, baada ya kupewa dhamana na mahakama hiyo katika mazingira ambayo hayakuuridhisha upande wa mashitaka. Hakimu Hadija Msongo alikiri kuwa mahakama hiyo ilitoa hati ya kukamatwa kwa mshitakiwa huyo na wadhamini wake.

Lakini hakueleza sababu ya mahakama kutoa hati hiyo, kwa kile alichodai kuwa jalada la kesi hiyo tayari limepelekwa Mahakama Kuu ya Tanzania. Liyumba alipewa dhamana baada ya kuwasilisha mahakamani hapo hati ya mali yenye thamani ya Sh milioni 882 wakati alitakiwa kuwasilisha fedha taslimu Sh bilioni 55 au hati za mali zenye thamani ya kiasi hicho cha fedha.

Aliwasilisha mahakamani hapo hati ya kusafiria ambayo muda wake wa kutumika umekwisha. Pia wadhamini wake wawili ambao walijitambulisha kuwa wanafanya kazi BoT, hawakuwa na barua kutoka kwa mwajiri wao zaidi ya vitambulisho vyao vya kazi. Licha ya Liyumba kutokamatwa na Takukuru, maofisa wa Taasisi hiyo waliwakamata wadhamini wake wawili ambao jana waliwekwa katika mahabusu ya mahakama hiyo kuanzia asubuhi hadi saa 10 jioni.

Wadhamini hao ni Otto Agatuangelus ambaye ni Ofisa Usalama wa Ndani BoT na Mhasibu wa Benki hiyo, Benjamini Nguluguni. Baadaye wadhamini hao walifikishwa mahakamani na Hakimu Msongo anayesikiliza kesi hiyo, akasema mahakama hiyo ilitoa amri ya kukamatwa kwa mshitakiwa na wadhamini wake, ila kwa bahati mbaya jalada la kesi hiyo limepelekwa Mahakama Kuu.

Kwa hali hiyo, Hakimu alilazimika kuahirisha kesi hiyo hadi leo, kusubiri jalada hilo litoke Mahakama Kuu na kurudishwa katika mahakama hiyo, ili kuendelea na shauri hilo. Aliwaamuru wadhamini hao kwenda mahakamani hapo leo kuelezwa kinachoendelea. Hakimu Msongo hakusema sababu ya kutoa amri ya kukamatwa kwa Liyumba, kwani wakati akitoa dhamana kwa mshitakiwa huyo, alipanga tarehe ya kurudi mahakamani kuwa ni Februari 24 mwaka huu.

Hata upande wa mashitaka haukueleza sababu ya kutolewa kwa hati hiyo ya kukamatwa mshitakiwa huyo na wadhamini wake. Hata hivyo, wakati mahakama ikitoa dhamana kwa mshitakiwa huyo, waendesha mashitaka wa serikali walidai kutoridhika na hatua hiyo, kutokana na upungufu kadhaa katika hati alizowasilisha na hati yake ya kusafiria.

Juzi mawakili wa Liyumba walizungumza na waandishi wa habari na kueleza kuwa uamuzi wa mahakama kutoa dhamana kwa mteja wao, ulikuwa halali kwa vile mteja alitimiza masharti ndiyo maana akaachiwa. Masharti ya dhamana yaliyowekwa na mahakama hiyo ni mshitakiwa huyo kujidhamini kwa fedha taslimu au hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya Sh bilioni 55.

Masharti mengine ni kuwasilisha mahakamani hati yake ya kusafiria, kuzuiwa kusafiri nje ya mkoa wa Dar es Salaam bila kibali cha mahakama, na kuwa na wadhamini wawili wanaofanya kazi katika taasisi inayotambulika. Wakati akiwa katika harakati za kudhaminiwa, mawakili wake ambao wanaongozwa na Profesa Mgongo Fimbo, waliwasilisha hati 11 za mali tofauti na kuwapeleka mahakamani wamiliki wanane wa hati hizo.

Baada ya kuwasilishwa kwa hati hizo za dhamana, upande wa mashitaka ulipinga kupokewa kwa madai kuwa hazikuwa zimepitiwa na kufanyiwa uhakiki. Pia walidai hati hizo zina makosa yanayotakiwa kurekebishwa na ndipo walipoikubali hati moja ya nyumba iliyoko Mbezi, Dar es Salaam, ambayo inamilikiwa na mshitakiwa yenye thamani ya Sh milioni 882.

Mawakili wa Liyumba pia waliwasilisha hati ya kusafiria ya mshitakiwa huyo yenye namba A0320091 ambayo muda wake wa kutumika ulimalizika tangu Februari 12, mwaka juzi. Baada ya mahakama kutoa dhamana hiyo, waendesha mashitaka ambao hawakuridhika na uamuzi huo, waliahidi kufanya kikao ili kujadili mwenendo wa suala hilo. Liyumba ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala, katika kesi hiyo anashitakiwa pamoja na Deogratius Kweka ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Miradi BoT.
 
hapa nasubiri breaking news nyingine ya ....lyumba is no more.....mchezo uishe....
 
Nimejifunza kitu hapa kumbe sitakiwi kuharibu passport ilo kwisha muda nikipata zali nawapa hiyo ili nitoroke na yahalali
 
Kama ni kweli itathibitishwa Liyumba ametoroka, kwa mujibu wa mwenendo wa kesi za jinai, kesi hiyo kesho inafutwa rasmi na mtuhumiwa anaachiwa huru.
Hivi ndivyo ilivyofanyika wakati wa Kesi ya Pili ya Uhaini Tanzania, Mwaka 1983, baada ya kutoroka gereza la Ukonga, Mshtakiwa wa kwanza, Father Tom na mshtakiwa wa pili, Hatty McGhee, kesi hiyo ilifutwa rasmi na washtakiwa wengine wote 29 waliachiwa huru. Hata hivyo, washtakiwa wote walikamatwa mara tuu baada ya kutoka mahakani na kesho yake walifikishwa tena mahakamani kusomewa mashitaka mapya.
Kwa hiyo kesi ya Liyumba itafutwa kesho, mshtakiwa mwenza ataachiwa huru, labda serikali ikiamua kumkamata tena na kumfungulia kesi mpya.

Pamoja na jamaa kutoroka, serikali ilikurupuka kufungua mashtaka ya thamani yote ya majengo pacha kana kwamba mradi mzima ni mradi batili.
Angetokea mwanasheria wa John Cochram type, angemwambia Liyummba na mwenzake wakubali kosa, wairudishie serikali hizo
Bilioni 200 na majengo pacha yawe ya mwekezaji mpya.

The-proper charge ya kuitia hasara serikali, ilikuwa ifanyike baada ya valuation ya Twin Towers. Then unacompare value halisi na value iliyozidishwa, ndipo unawafungulia kesi ya kusababisha hasara ya kile kiasi tuu kilichozidi.

Pamoja na hasira zetu zote kuhusiana na hivi vitendo vya ufisadi,
Waliovitenda ni binadamu, hivyo ubinadamu uko pale pale kama Mkapa anavyoheshimiwa pamoja na madudu yote yaliyofanyika wakati wa utawala wake.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom