Kesi ya Liyumba, Utata na Maendeleo yake

Kesi ya Liyumba, Utata na Maendeleo yake

Status
Not open for further replies.
Akitimiza masharti ya hiyo dhamana mimi nita kana uraia wangu!!!!!!!

ha ha ha! Kwasababu hiyo dhamna inakaribia bajeti ya wizara ama? Mkuu upo right kwa mtazamo wako maana itashangaza wengi na wengine ndio tunachokisubiri sasa kuona hela zetu zinavyochezewa na watu wanaojidai wana mapenzi na nchi yao.
 
Navyosikia huyu jamaa sii mzima hivyo inawezekana yupo ktk matibabu maalum kusetiriwa siri kubwa inayoweza kuvunja ndoa za watu wakubwa! picha zake za keko zinaonyesha wazi jamaa alianza kuonyesha mkorogo haufanyi kazi!..kwi kwi kwi!
 
Kama kweli atakuwa bado yuko yuko ina maanisha pccb haina ushirikiano wa karibu na mahakama yaani vyombo vyetu vya usalama haviaminiani na havina ushirikiano wa karibu mpaka pccb waamue kutoa donge nono wakati hawana uhakika na kinachoendelea

si ajabu kesho tukasikia mtu kapewa hilo donge nono

Cha ajabu ni kuwa leo jumapili Masha ansema wizara yake haina habari rasmi kuwa huyu jamaa kapotea na kama wangeambiwa kumpata ni mara moja.
We ca read between the lines, hakuna ushirikiano vyombo vyetu vya ulinzi na usalama!
 
dah kama huyu jamaa atawasilishe hizo hati za bilion 55 inabidi ashtakiwe, anamshahara wakuweza kua na hizo mali au hela... kweli analipa kodi, inabid watu wa Tax wafatilie and takukuru pia iangalie hili, au wana JF mnasemaje?
 
Mimi nilitaka Liyumba otoroke na asipatikane ili tuzibe matundu yanayovuja kwenye paa la sheria yetu ya dhamana kwa kesi za jinai.
The truth is 50 Billion bail is absurb!.
Nilisema tangu mwanzo, mwache atoroke, Jumanne kesi ifutwe, halafu mchawi atafutwe.
Ukweli ni kuwa, pamoja na ufisadi, piga ua, bado washtakiwa ni binadamu, wanastahili kutendewa haki. Dhamana ya nusu ya gharama sio halali wala sio haki.
Naomba nieleweke vizuri, sitetei ufisadi bali natetea haki itendeke hata kwa watuhumiwa.
Hao PCCB hawana lolote, ni papara za kulinda kibarua cha Hosea na kupandisha chati ya JK.
Mashitaka halisi yalikuwa kufanya tathmini ya thamani halisi ya Twin Towers na kutoa from the expenditure. The diference ndiyo hasara waliyosababisha.
Jamani hata normal common sense inathibitisha sio Lyumba wala Kweka ambaye angeithinisha matumizi hayo bila baraka za bodi. Bodi ya BOT ni very peculiar, Gavana ndio kila kitu, hivyo Balali ndio alikuwa kila kitu na serikali inaujua ukweli wote kama kilivyo kiini macho cha Kagoda.







.
 
Jmushi1,
Kweli kabisa mkuu wangu nipo nawe na nazungumza yote haya kwa sababu nafahamu fika kwamba Tanzania hakuna sheria isipokuwa ktk majarida na makabrasha..Huyu Masha hafai kabisa, hata elimu yake naanza kuiwekea mashaka kwa sababu wapo watu husoma kushinda ili mitihani...
Just imagine PCCB kwanza hawakutaka washtakiwa wapewe dhamana isipokuwa ni sheria inayompa haki mtuhumiwa kupewa dhamana, leo mahakama itoe hukumu kukubali dhamana nje ya matakwa ya PCCB, kisha mtu atoroke halafu mshitaka (PCCB) tena liwe jukumu lake kumtafuta mtu aliyetoroka kwa dhamana waliyokuwa wakiipinga.. hii kweli inaingia akilini..
 
N uukane kweli usije ukatuambie eti mliniquote vibaya, unadhani billion 50 za mdhamana kwa liyumba ni nyingi?

Mkuu hesima mbele sasa wewe unaziona kidogo hizo, Hiyo nyumba kufika 800 million walihesabu kilia kitu kuanzia mapazia, Kuku ng'ombe mbuzi na kondoo (wakaandika ship) Wanasheria wetu Kaazi kweli kweli.

Kumbuka bilion 40 za ndege tuu mpaka leo Mramba hana msamaha kuwaambia watu wale nyasi kwa hizo pesa.

Hiyo rada imecost Bilion 28.

Labda kidogo unayosema wewe ni kwa kuandika
 
Mkuu hesima mbele sasa wewe unaziona kidogo hizo, Hiyo nyumba kufika 800 million walihesabu kilia kitu kuanzia mapazia, Kuku ng'ombe mbuzi na kondoo (wakaandika ship) Wanasheria wetu Kaazi kweli kweli.

Kumbuka bilion 40 za ndege tuu mpaka leo Mramba hana msamaha kuwaambia watu wale nyasi kwa hizo pesa.

Hiyo rada imecost Bilion 28.

Labda kidogo unayosema wewe ni kwa kuandika
Kumbuka hizo Mali zenye thamani ya kufikia Bil 55 sio lazima ziwe zake. Hata wewe kama unampenda na kumwamini unaweza kumpa hati ya nyumba yako aiweke kama sehemu ya dhamana.
 
Ya Liyumba ni mkorogo

2009-02-23 10:05:32
Na Joseph Mwendapole


Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa Nchini (Takukuru), imesema imefanya jitihada zote, lakini imeshindwa kumpata aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba, ambaye ameshitakiwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu katika kesi ya kuisababishia serikali hasara ya Sh. 221, 197,299,200.95 ya mradi wa maghorofa pacha ya benki hiyo.

Ofisa Uhusiano wa Takukuru, Doreen Kapwani, aliiambia Nipashe jana kwamba taasisi yake imetafuta, lakini bado haijaweza kumpata.

``Mpaka sasa hajapatikana na tunaendelea na jitihada za kumtafuta, tunaomba mtu yeyote mwenye taarifa za alipo atupatie, atapewa donge nono,`` alisema

Liyumba alipewa dhamana tata na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam Jumanne wiki iliyopita, baada ya kuwasilisha hati ya nyumba yenye thamani ya Sh. 800,820,000 kati ya masharti ya dhamana ya kuwasilisha mali yenye thamani ya Sh bilioni 55.

Yeye na mwenzake, Deogratius Dawson Kweka, aliyekuwa meneja wa mradi wa ujenzi wa maghorofa pacha ya BoT, wanashitakiwa kwa makosa tofauti, yakiwemo matumizi mabaya ya ofisi na kuisababishia serikali hasara hiyo.

Katika masharti ya awali, kila mshitakiwa alitakiwa kutoa hati yenye thamani ya Sh. Bilioni 55, hivyo thamani ya hati aliyowasilisha na kupata dhamana wiki iliyopita, ilikuwa sawa na asilimia 1.4 ya kiasi kilichostahili.

Hata hivyo, siku moja baada ya kupewa dhamana, Jamhuri ilitoa notisi ya kukamatwa Liyumba na wadhamini wake, Benjamin Ngurugulu na Otto Agatuangelus, ili warejeshwe mahakamani hapo.

Wadhamini wake walishikwa na kuwekwa maabusu kwa saa tatu kisha kuachiwa.

Vyanzo mbalimbali vimedokeza Nipashe kwamba tangu kutolewa kwa hati ya kukamatwa kwa Liyumba, maofisa wa Takukuru wamefanya uchunguzi katika viwanja vingi vya ndege hapa nchini, lakini hakuna sehemu iliyoonyesha kwamba amesafiri nje ya nchi kupitia viwanja hivyo.

Habari zilisema kuwa hata kamera zilizoko Viwanja vya Ndege vya Julius Nyerere, Kilimanjaro na Zanzibar zimeangaliwa, lakini hazionyeshi Liyumba akipita.

``Tumeangalia katika viwanja vyote vya ndege, kumbukumbu, na hata kamera, lakini hakuna sehemu ambayo Liyumba anaonekana,`` kilisema vyanzo kimojawapo kutoka Takukuru.

Habari zinadai maafisa wa Takukuru wanadai kama atakuwa ametoroka basi atakuwa ametumia usafiri wa barabara, hivyo nguvu sasa imeelekezwa sehemu za mipakani.

``Sasa tunafanya jitihada kuangalia maeneo ya mipakani ili kuweza kubaini kama alitumia njia hizo au la,`` alisema mtoa habari mmoja ndani ya Takukuru.

Wakati Takukuru wakidai hivyo, kumekuwa na tetesi kwamba huenda Liyumba yuko hapa nchini na amejichimbia mafichoni kwa ajili ya kukusanya ushahidi wa kwenda mahakamani kesho ambayo ni siku ya kesi yake.

Tetesi hizo ambazo jana zilikuwa zimezagaa nchini, zilidai kuwa kuna taarifa kwamba Liyumba ambaye sasa anatajwa kwamba ametoroka na hajulikani aliko, hajatoroka na kwamba alikuwa amejipumzikia akiangalia afya yake huku akijipanga kutimiza masharti ya dhamana.

Tetesi hizo zilidai huenda Liyumba akaibuka tena mahakamani kesho kuwasilisha hati za ziada za dhamana zenye thamani sawa ama zaidi ya Sh Bilioni 54 .

Hadi sasa si Takukuru wala Mahakama ambao wamekuwa tayari kueleza sababu za kutolewa kwa hati ya kukamatwa Liyumba.

Wiki iliyopita mwanasheria wa Takukuru, Tabu Mzee, alisema tangu kutolewa kwa hati ya kukamatwa na kufikishwa mahakamani hapo, Liyumba hayajaonekana na hakuna taarifa zinazohusu mahali alipo.

Baada ya jitihada za kumnasa Liyumba kugomba mwamba, wadhamini wa mshitakiwa huyo Ijumaa waliachiwa huru baada ya Hakimu Mkazi Khadija Msongo kuahirisha shauri hilo.

Akitoa uamuzi wa dhamana kwa Liyumba Jumatatu iliyopita, Hakimu Mkazi Msongo alieleza kuridhishwa na hati iliyowasilishwa, huku pasi yake (Liyumba) ya kusafiria yenye namba A0320091 ikishikiliwa.

Pasi hiyo iliyoonyesha kumalizika muda wake Februari 12, mwaka huu, ilibaki mahakamani hapo kwa uchunguzi zaidi.

Kwa upande mwingine, hati iliyowasilishwa mahakamani hapo na kusababisha Liyumba kupata dhamana, ilisajiliwa kwa kitalu namba 6233 kilichopo Mbezi Juu jijini hapa.

Aidha, hati nyingine zilizowasilishwa mahakamani hapo, zilikataliwa baada ya kubainika kwa na mapungufu kadhaa.

Shitaka la kwanza linalomkabili Liyumba ni matumizi mabaya ya ofisi ya umma, kwamba kati ya mwaka 2001-2006 akiwa mwajiriwa wa serikali, aliidhinisha ujenzi wa ghorofa pacha bila baraka za uongozi wa juu wa benki hiyo.

Katika shtaka la pili, mshtakiwa huyo anatuhumiwa kuidhinisha malipo ya ujenzi huo bila kibali cha Bodi ya Wakurugenzi wa BoT na shitaka la tatu linalowakabili washitakiwa wote, ni kuisababishia serikali hasara ya Sh. bilioni 221.

Wanadaiwa kutenda kosa hilo kati ya mwaka 2001 hadi 2006, wakiwa ni watumishi wa umma, kwa makusudi au kwa kushindwa kuwa makini na kazi yao.

SOURCE: Nipashe

Kweli JF kiboko, tazama hawa Nipashe yaani wamecopy na kupaste hii post ya Halisi, halafu hawataki kucredit JF kama chanzo cha habari zao. Mkuu Halisi ama kweli wewe uko mbele hatua kadhaa kuliko media zetu. Ndo maana huwa natumia muda mwingi hapa jamvini kuliko kusoma habari za waandishi wetu.
 
Baada ya kuona wamechemka nahisi wameamua kumficha Liumba ili wajipange upya au ndo hivyo tena wazime kila kitu.....duh Bongo mfilisi.
Hii inadhihilisha jamaa hakula peke yake wapo wengi sana nyuma yake....haingii akilini eti wameshindwa kumkamata Liumba wapi na wapi jamani tunazugana tu.
 
Liyumba shows up: Set for court appearance tomorrow

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

FORMER Bank of Tanzania (BoT) senior official Amatus Liyumba, the subject of a comprehensive manhunt on suspicion of jumping bail on charges of occasioning a 221bn/- loss to the Government through the infamous Twin Towers construction project, has at last been found, it was learnt yesterday.

Reliable sources told THISDAY that Liyumba was on Saturday evening traced to an undisclosed location within Dar es Salaam, and will appear in court tomorrow.

The sources did not confirm or deny whether the former BoT director of personnel and administration had been formally re-arrested or not, but asserted that he would be present when his case comes up for its next scheduled mention at the Kisutu Resident Magistrate’s Court tomorrow.

’’He was not in hiding as has been suggested in some quarters, but was only resting...looking after his health,’’ the sources said.

Details of the circumstances behind Liyumba’s resurfacing remain sketchy, along with his present whereabouts as he awaits tomorrow’s case mention at the Kisutu court, including whether he is in the custody of any Government law enforcement body or not.

Efforts to contact officials of the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB), which is overseeing prosecution matters in the case, for comment proved futile over the weekend.

The Bureau on Saturday issued a public notice promising a ’big reward’ for anybody coming forward with information that would help bring the hunt for Liyumba to a successful conclusion.

At the same time, Home Affairs Minister Lawrence Masha was quoted as saying although the police are willing to help PCCB in the hunt, it can only do so on the basis of a formal request from the Government anti-corruption watchdog body.

The minister’s statement appears to have raised questions about the extent of cooperation between Government agencies on such matters, with one prominent city lawyer who requested anonymity noting that it is the police which is primarily responsible for following up on all court arrest warrants - whether by request or not.

A Kisutu court magistrate on Wednesday issued a fresh arrest warrant against Liyumba on the back of rising fears that he may have jumped bail, which had been granted to him in questionable circumstances by the same magistrate only the previous day.

Liyumba and his co-accused in the same case, former BoT project officer Deogratius Kweka, had been required to deposit with the court at least 55bn/- in cash each, or produce title deeds for property worth that amount, as part of their bail conditions.

They were also required to secure two reliable sureties each, employed by the Government or any other reputable institution, who should sign a 50m/- bond with the court; and to surrender their passports to the court, along with a restriction to leave the city without the court’s express permission.

Last Tuesday, advocates representing Liyumba produced title deeds of several immovable properties, which they said were of a value equivalent to the required amount.

However, only one of the title deeds - for plot number 2232 located in Mbezi Juu on the outskirts of the city, with a stated value of just 882m/- - was approved by the court.

At the same time, the passport that he surrendered showed a long-past expiry date of February 12, 2007.

While Liyumba was nevertheless granted the bail, his co-accused Kweka was also allowed out of remand custody, but immediately handed over to PCCB officials to assist in further investigations.

In asking the court to hand Kweka over to the PCCB, prosecuting State Attorney Justus Mulokozi offered an assurance of the accused’s continued security.

In the case, the duo is charged with abuse of office, disobedience, and occasioning a loss totaling $53,077,715 (about 221.1bn/-) to the Government.

It is alleged that in the period between 2001 and 2006, the two abused their respective positions within the central bank to make and implement major decisions related to the extension of the BoT Twin Towers headquarters construction project, without the approval of the bank’s board of directors.

They are said to have, amongst other things, failed to scrutinize the legitimacy of various payments to be made in respect of the Twin Towers extension project, and furthermore misled the board into authorizing the payments, thereby causing the said loss.

Liyumba is facing all the counts in the joint charge sheet, while Kweka is charged with only one count of occasioning monetary loss to a specified authority.
 
"Wakati Takukuru ikifikia maamuzi hayo Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imesema kama Takukuru itahitaji msaada wa Wizara hiyo kumtafuta Liyumba iko tayari kutoa msaada huo.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili Waziri wa Wizara hiyo, Lawrance Masha alisema wakipewa maombi ya kumtafuta Liyumba, watasaidia kumtafuta kwa kuwa wote ni Serikali."

"Juzi nilitoa tamko kuwa hatujaletewa maombi ya kumtafuta, lakini Takukuru wakituletea tutafanya hivyo, kwa kuwa sisi ni Serikali," alisema Masha.

Source: Mwananchi


Wakuu hii mi naona kali. Hivi fugitive anapokata kamba kwenye mkono wa sheria polisi inabidi waandikiwe barua kuombwa wamkamate? i thought ilikua ni automatic duty yao kumkamata.... Nilikua sijui!

Now you know!
Kumbuka hadithi ya George Orwel " Animal Farm" - Usijethubutu ndugu! Yatakukuta makubwa. Some are more equal than others remember that!
 
Nadhani kijichuki hicho binafsi kipo...

Jamani inabidi nirudi tena kuweka wazi kuhusu Masha. Inaonekana huyu waziri haeleweki na watu japo anafanya kazi zake kwa mipangilio maalum. Katika hili, Takukuru iko chini ya Ikulu, Police iko chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani. Kesi imepelekwa mahakamani na Takukuru. Baada ya jamaa Liyumba kukitoa, waliopeleka kesi mahakamani ndio waliopewa jukumu la kumsaka. Sasa hii ni operation. Lazima Takukuru iwe na stratergy zake za kumnasa, zikiwemo kama ilivyoelezwa katika taarifa zao, matumizi ya resources zote zilizo chini yao, i.e. fedha, watu na vifaa.

Sasa niniyi mnataka wakati huo huo, Polisi nao waweke stratergy na kutumia resources zake kwa kazi ambayo tayari inafnywa na chombo kingine cha serikali. Hii italeta confusion ya hali ya juu.

Kitu kinachotakiwa hapa na alicho dai Masha ni kuwa, iwapo Takukuru inaona uwezo wake ni mdogo na inataka msaaada wa Polisi basi waseme hivyo na baadaye wakae na kuweka stratergy ya pamoja. Kwa mtindo huo wa kuunganisha nguvu, wanaweza kumnasa.

Hivyo ndio utaratibu wa kazi. Sio kuvamia tu kazi za watu wengine. Endapo itatokea katika utekelezaji wa kazi zake za kawaida, Polisi ikamuona mtuhumiwa Liyumba, hapo inaweza kumkamata kama mtuhumiwa mwingine yeyote.

Kama Masha angekurupuka tu na kwaambia Mapolisi wake wamtafute Liyumba, ninyi ndio mngekuwa wa kwanza kulalamika kuwa anaingilia kazi za Takukuru. Ama sivyo?

Mkuu pamoja na good reasoning on how to use reasources prudently bado ukweli unabaki kuwa suala la kuhakikisha law and order ni kazi ya police.Isitoshe ndiyo maana kesi hii ni Republic verses Liumba and others... na siyo TAKUKURU VS LIUMBA! Kwa msingi huu ni wajibu wa vyombo vyote vya dola kuvuta nguvu pamoja na kushughulikia ukiukwaji wa sheria na hakuna suala la compartmentalisation hapa! Hivyo basi Masha kusema wanasubiri "waombwe" kumsaka na kumkamata Liyumba ni understatement ya mwaka hasa ukizingatia kuwa Masha is a " learned brother"!
Sijui mkuu kama ulishaona ama kusikia jinsi watuhumiwa wanaojaribu kutoroka mahakamani ( wengine wamewahi hata kujipaka vinyesi mwili mzima na kutimua kwa speed ya radi ) lakini polisi wanawakimbiza na kuwakamata bila kujali hali. Liyumba ni nani hadi polisi wajiweke pembeni??
 
Liyumba shows up: Set for court appearance tomorrow

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

FORMER Bank of Tanzania (BoT) senior official Amatus Liyumba, the subject of a comprehensive manhunt on suspicion of jumping bail on charges of occasioning a 221bn/- loss to the Government through the infamous Twin Towers construction project, has at last been found, it was learnt yesterday.

Reliable sources told THISDAY that Liyumba was on Saturday evening traced to an undisclosed location within Dar es Salaam, and will appear in court tomorrow.

The sources did not confirm or deny whether the former BoT director of personnel and administration had been formally re-arrested or not, but asserted that he would be present when his case comes up for its next scheduled mention at the Kisutu Resident Magistrate’s Court tomorrow.

’’He was not in hiding as has been suggested in some quarters, but was only resting...looking after his health,’’ the sources said.

Details of the circumstances behind Liyumba’s resurfacing remain sketchy, along with his present whereabouts as he awaits tomorrow’s case mention at the Kisutu court, including whether he is in the custody of any Government law enforcement body or not.

Mkuu Mtanzania,

Hii ni kali ya mwaka. Nilitegemea kusikia kama amekamatwa basi lile gari la kimulimuli la polisi linamrudisha keko. Au tena atasomewa tena kurudi keko leo??? Au tena hiyo dhamana ya over 800 mil ndo imetosha?? Sheria za tanzania ni utata mtupu!!!! Na wenye kufanya maamuzi yasheria ni utata mpupu!!!! It is a shame. Bravo Liyumba, umezitumia feza zako vizuri!!! Na umewapata!!!! Nasubiri kwa hamu kupata yatakayojiri leo mahakamani if at all he will appear before Hon Hadija!!!! Kwiki kwiki.
 
Liyumba shows up: Set for court appearance tomorrow

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

FORMER Bank of Tanzania (BoT) senior official Amatus Liyumba, the subject of a comprehensive manhunt on suspicion of jumping bail on charges of occasioning a 221bn/- loss to the Government through the infamous Twin Towers construction project, has at last been found, it was learnt yesterday.

Reliable sources told THISDAY that Liyumba was on Saturday evening traced to an undisclosed location within Dar es Salaam, and will appear in court tomorrow.

The sources did not confirm or deny whether the former BoT director of personnel and administration had been formally re-arrested or not, but asserted that he would be present when his case comes up for its next scheduled mention at the Kisutu Resident Magistrate’s Court tomorrow.

’’He was not in hiding as has been suggested in some quarters, but was only resting...looking after his health,’’ the sources said.

Kwenye bold: Wanataka kutuambia nini-has he been traced au he has shown up kama inavyoelezwa kwenye headline?
Kwenye italics: Why have they decided to contradict their story?
And the quote: Anajipumzisha! Why didnt he come out wakati anafatafutwa (Ingawa wanaomtafuta hawajasema wanamtafutia nini)?
 
Kwenye bold: Wanataka kutuambia nini-has he been traced au he has shown up kama inavyoelezwa kwenye headline?
Kwenye italics: Why have they decided to contradict their story?
And the quote: Anajipumzisha! Why didnt he come out wakati anafatafutwa (Ingawa wanaomtafuta hawajasema wanamtafutia nini)?

Kaka uko sahihi, hii ni dalili kwamba hii story inaficha mambo mengi ambayo yatajulikana kesho mahakamani. Nadhani ni katika mambo ya "Protection of Source" ndio unakuta "kujikanganya huko" ila ujumbe umefika. Jambo la HATARI na kubwa zaidi ni WAPI ALIPOKUWAPO? Kwanini kuna KIGUGUMIZI?
 
waacheni hawa bado wamelala..... kukurupuka kwao ni faida kwetu ya kupata info zaidi
 
Jamani, tulisema walikuwa na Liyumba tangu ijumaa ile, hakupotea popote wala kutoroka. Illi michezo mingine mibaya sana.. ninaowaonea huruma ni watu wa PCCB!
 
Jamani, tulisema walikuwa na Liyumba tangu ijumaa ile, hakupotea popote wala kutoroka. Illi michezo mingine mibaya sana.. ninaowaonea huruma ni watu wa PCCB!


PCCB wanatufanyia usanii mchana kweupe unawahurumia wa nini mkuu.

Mimi wameniudhi sana; hawa waliomba msaada wa wananchi kumtafuta. Sasa wamempata hawasemi kitu kwa Wananchi maana yake nini..!!??Grrrrrr...ningekuwa Dar es salaam kesho mapema asubihi ningefika Kisutu kusubiri; Liyumba akitoea hata kama akiletwa na hao hao PCCB mimi naenda kuwadai donge nono..!! Nasema nimemuona Liyumba Kisutu, nasikia mnamtafuta..!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom