Kesi ya Magoma dhidi ya Yanga imedhihirisha umbumbumbu wa wanasheria wa Tanzania

Kesi ya Magoma dhidi ya Yanga imedhihirisha umbumbumbu wa wanasheria wa Tanzania

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
18,037
Reaction score
33,681
Mwanasheria/ Jaji mzuri ni yule anae paswa kutazama sheria kama inavyo paswa kuwa na sio kama ilivyo andikwa.

Lakini hii haipo kwa wanasheria wa Tanzania. Wengi hawana busara. Wanakariri vifungu vya sheria na procedures tu.

KWA mfano:

Kwa mujibu wa sheria za Tanzania. Mtu mzima ananzia miaka 18. Chini ya hapo ni mtoto.

Kijana wa kiume mwenye umri wa miaka kumi na saba akimnajisi mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja anahukumiwa kifungo cha nje cha mwaka mmoja au miwili na faini ya shilingi laki moja au laki 2..

Kijana wa miaka 18 akimpa mimba binti wa miaka 17, anafungwa miaka 30 au maisha..

Umeona jinsi nchi yetu ilivyo na wanasheria wasio na uwezo kichwani.

Kesi ya Magoma sasa. Yani kashindwa kabisa kujua outcome za maamuzi yake katika nchi na katika jamii nzima ya watanzania.

Kashindwa kufanya fact analysis.

Kaamua kwa kufuata vifungu vya sheria na sio busara..
 
Sisi hatuja soma sheria ila Huwa sielewi.
Yaani mahakama zinakosa busara Kwa maamizi ya ajabu
 
Yaani waache kufuata sheria waanze kutumia busara? Tukifika hapo tutakuwa taifa la ovyo kabisa
Kwako ni sahihi kijana wa miaka kumi na saba alie mnajisi mtoto wa mwaka mmoja kupewa adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja nje ya gereza kwa sababu sheria inamtambua kama mtoto?
 
Sheria ni msumeno. Mmezoea mambo ya kuchekeana matokeo yake nchi imefikia mahali wanaoiba kuku wanafungwa au kuchomwa moto, ila wanaoiba mabilioni na rasilimali za nchi wanaachiwa eti kwa kutumia busara waendelee kuneemeka. Utasikia "wakichukuliwa hatua nchi itatikisika!"
 
Sisi hatuja soma sheria ila Huwa sielewi.
Yaani mahakama zinakosa busara Kwa maamizi ya ajabu
Sana yani hawa watu ni weupe kweli kichwani wamekariri tu
 
Mwanasheria/ Jaji mzuri ni yule anae paswa kutazama sheria kama inavyo paswa kuwa na sio kama ilivyo andikwa...

Mnamchelewesha Mzee Magoma....!

Mkabidhini Funguo za Jengo aanze kupiga Kazi...!

Mahakamani nendeni nyie , Yeye Kashashinda..!
 
Sheria ni msumeno. Mmezoea mambo ya kuchekeana matokeo yake nchi imefikia mahali wanaoiba kuku wanafungwa au kuchomwa moto, ila wanaoiba mabilioni na rasilimali za nchi wanaachiwa eti kwa kutumia busara waendelee kuneemeka. Utasikia "wakichukuliwa hatua nchi itatikisika!"
umewaza kama wanasheria wa Tanzania
 
Andiko lako umenifilisi, nilitaka kuandika kama wewe, ni aibu kwa wanasheria kushindwa kesi na Magoma Shaaban, tena kwa mwanasheria kama Alex Mgongolwa
 
Muhimu tu kama wameghushi saini za watu wengine, basi sheria na yenyewe ifuate mkondo wake. Na kama huyo Magoma hana kadi ya uanachaama wa klabu, basi ni jambo la kushangaza sana kushinda hiyo kesi.
 
Muhimu tu kama wameghushi saini za watu wengine, basi sheria na yenyewe ifuate mkondo wake. Na kama huyo Magoma hana kadi ya uanachaama wa klabu, basi ni jambo la kushangaza sana kushinda hiyo kesi.
ndio maana nimesema wanasheria wa Tanzania ni mbumbumbu
 
Back
Top Bottom