Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Kesi ya uchochezi inayomkabili Mwanaharakati na Mkurugenzi wa GH Foundation, Godlisten Malisa imezua sintofahamu baada ya kufika mahakamani leo, Julai 18, 2024 mkoani Kilimanjaro na kukuta kesi hiyo bado haijasajiliwa.
Pia soma: Kilimanjaro: Godlisten Malissa afikishwa Mahakamani
Malisa akiongozana na mawakili wake watatu kati ya saba, wakiwamo Dickson Matata, Hekima Mwasipu na Peter Kidumbuo, walifika mahakamani hapo saa tatu asubuhi kama alivyotakiwa na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Kilimanjaro (RCO) kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo inayomkabili.
Pia soma: Malisa aripoti Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi, ajulishwa kuwa upelelezi haujakamilika
Wengine waliofika mahakamani hapo ni wafanyakazi wa taasisi yake, akiwamo James Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro, Michael Kilawila na marafiki zake wa karibu.
Mwananchi