GE2025 Kesi ya Malisa: Mahakama kutoa uamuzi mapingamizi ya CCM Agosti 22

GE2025 Kesi ya Malisa: Mahakama kutoa uamuzi mapingamizi ya CCM Agosti 22

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Hii kesi angefungua kama raia wa kawaida sio mwanachama wa ccm, maana naona kuna utaratibu akufuata hadi kufungua kesi, wanasheria mnasemaje?
 
Hii kesi angefungua kama raia wa kawaida sio mwanachama wa ccm, maana naona kuna utaratibu akufuata hadi kufungua kesi, wanasheria mnasemaje?
Kuvunja katiba ya nchi kunahusiana vipi na uanachama wa ccm!
 
Kuvunja katiba ya nchi kunahusiana vipi na uanachama wa ccm!
Hakuna uhusiano wowote, ila mawakili wa ccm wamekuja na mapingamizi kwamba Malisa akufuata utaratibu kumuandikia barua katibu mkuu wa chama na yeye kajibu akufanya hivyo kwasababu katibu mkuu ni mtuhumiwa pia ila Malisa anakiri alimwandikia mwenyekiti barua.
 
Ngoja tusubiri hiyo tr 22 tuone mahakama itaamua vipi.
 
19 August 2025
Dodoma, Tanzania

Mchungaji Dkt Godfrey Malisa: Tumevunja Misingi ya Haki na Demokrasia​

View: https://m.youtube.com/watch?v=OJ6z5GakMp4
Mchungaji Dkt Godfrey Malisa Asema Taifa Letu Limeiacha Haki na Demokrasia. Atoa Wito Mkubwa kwa Viongozi na Wananchi Kushikamana, Kulikomboa Taifa Linalopitia Kipindi Kigumu Ambacho Hakijawahi Kuonekana, Ili Kuweka Msingi Imara wa Maendeleo na Ukombozi wa Tanzania...

Mkae chini na kutumia simu janja ya jirani yako mkiwa 2 au 3 kwa wale wasio na simu janja msikilize ujumbe huu kuwa kama nchi tunapoelekea siyo salama maana mgombea urais kupitia tiketi ya CCM amezunja katiba..

Ukiwa na viongozi wa chama na nchi wasiojali katika ya chama na nchi, mbaya zaidi ambao wapo katika serikali na ikulu ya nchi yetu hii ni hatari sana ..

Hivyo ni lazima katiba ya nchi lazima iheshimiwe ...sasa naongea yale ya ndani ya Chama cha Mapinduzi kutekwa nyara ,kuburuzwa maana yake mali za Tanzania na haki za raia zinapunjwa ...

Rasilimali za taifa zitakuwa chini ya genge la wachache na wale waliokinunua chama cha mapinduzi CCM kwa harambee ya bilioni 87 huku mmoja wao kwa kujipiga kifua ametoa bilioni 10 kama bei ya kukidhibiti chama tawala kongwe tawala CCM..

Natoa wito ukaguzi wa mali za viongozi ikiwemo za Rais Samia Hassan, Makamu wa Rais wa Tanzania Dr. Philip Isidori Nzabhayanga Mpango, waziri mkuu Kassim Majaliwa, waziri wa fedha Mwigulu Nchemba .... na ripoti hizo zitolewe hadharani ndani ya wiki 3 kutoka leo mwezi agosti 19, 2025 ..

Wananchi wasusie bidhaa za mabepari waliokiteka nyara chama siku ya Harambee ya bilioni 87, raia wasusie energy drinks, cola na bidhaa za madalali hawa wa mali zetu za taifa ...

Mzee ana hoja ajibiwe🤣🤣🤣
 
Lazima majaji watajificha katika kichaka cha kusema utaratibu haukufuatwa
 
Back
Top Bottom